KITABU CHA MBINGU katika Telegraph - TAYARI KUSOMWA

KITABU CHA MBINGU katika Telegraph - TAYARI KUSOMWA



Jinsi mtu anavyoweza kushiriki katika mateso ya Mama Malkia.
Juzuu na. 6 - Septemba 17, 1905


Italia itashambuliwa. Kazi ya Yesu ndani ya Mtu. Ili kuzaa matunda makubwa na mazuri ni lazima pawepo na ufanano na uhusiano.
Juzuu na. 11 - Mei 25, 1916


Jinsi muunganiko wa nguvu baina ya mtu na Mungu usivyoweza kuvunjika kamwe.
Juzuu na. 12 - Machi 16, 1917


Yesu hakufanya jambo lolote lingine isipokuwa kujitoa Mwenyewe kama chombo cha Utashi wa Mungu Baba. Tofauti iliyopo kati ya kuishi katika utii kwa Utashi wa Mungu na utakatifu uliopo katika kuishi ndani ya Utashi wa Mungu. Mifano mbalimbali.
Juzuu na. 12 - Agosti 14, 1917


Neema, kama ilivyo kwa mwanga wa jua, huwa inatolewa kwa watu wote, lakini yupo anayeifaidi na yupo asiyeifaidi.

Juzuu na. 11 - Oktoba 20, 1916


Ndani ya kila kitu kilichoumbwa Mungu alikuwa akiweka uhusiano, mfereji wa neema mbalimbali, na pendo la pekee kati ya Utukufu Mkuu na kiumbe.

Juzuu na. 12 - Februari 20, 1919


Kushiriki katika maumivu ya hali ya uhanga wa Yesu.
Juzuu na. 12 - Novemba 3, 1919


Mkasa wa Yesu wa Sakramenti una maumivu zaidi hata kupita ule mkasa Wake wa utotoni.

Juzuu na. 12 - Desemba 25, 1920


Kutoka jukumu lile la Ubinadamu Wake Yesu anampitisha Luisa kwenda kwenye jukumu linaloshikwa na Utashi Wake katika Ubinadamu Wake.
Juzuu na. 12 - Machi 17, 1921


Matendo yanayotekelezwa katika Utashi wa Mungu huwa ni mwanga. Teso lililomchoma Moyo Yesu kupita yote katika Mateso Yake ni unafiki.

Juzuu Na. 13 - Novemba 22, 1921


Ile bahari ya Utashi wa Mungu na ule mtumbwi mdogo wa mwanga.

Juzuu Na. 13 - Novemba 28, 1921


Ukombozi ni wokovu. Utashi wa Mungu ni Utakatifu.
Juzuu na. 13 - Desemba 3, 1921


Lengo pekee la kumpenda Mungu, huwa ni kuiacha wazi mioyo ya watu ili waweze kupokea mkondo wa neema Zake zote. Utashi wa Mungu ndiyo fadhila iliyo kuu kabisa kati ya fadhila zote.
Juzuu na. 13 - Desemba 22, 1921


Utashi wa Mungu ni mizani ya uuwiano na mpangilio.
Juzuu na. 14 - Agosti 6, 1922


Sadaka hubadili hulka ya utashi wa kibinadamu.
Juzuu na. 14 - Agosti 12, 1922


Mungu alipomwumba binadamu alikuwa akijenga ufalme kwa ajili Yake. Raha ya Yesu anapoona, ndani ya mwanadamu, siyo tu sura ya Ubinadamu Wake, bali anapoona kila kitu ambacho Umungu Wake ulikuwa umekitenda ndani ya Ubinadamu huo.
Juzuu na. 14 - Septemba 9, 1922


Tamaa ya Yesu kwamba watu waujue Utashi wa Mungu unaotenda kazi ndani ya mwanadamu.

Juzuu na. 14 - Septemba 15, 1922


Malalamiko, Pendo la Yesu.
Juzuu na. 14 - Septemba 27, 1922


Mpango wa kwanza wa matendo yakibinadamu, yakiwa yamegeuzwa kuwa ya kimungu pale ndani ya Utashi wa Mungu, ulifanyika na Yesu. Luisa: ndiye wa kwanza kuishi ndani ya Utashi wa Mungu.

Juzuu Na. 14 - Oktoba 6, 1922


Utashi wa Mungu humfanya mtu awe johari liangazalo. Ufahamu juu ya ikulu ya Utashi wa Mungu.
Juzuu na. 14 - Novemba 6, 1922


Mikondo ya Pendo kati ya Mungu na binadamu.
Juzuu na. 14 - Novemba 20, 1922


Wakati Mapenzi Yako Yatimizwe, itakapofikia utimilifu wake kule Mbinguni kama hapa duniani, basi, utafika na ule utimilifu kamili wa ile sehemu ya pili ya sala ya Baba Yetu. “Endapo Mimi sitatenda muujiza wa kumfanya mtu akaishi ndani ya Utashi Wangu Mkuu wa Juu, basi Mapenzi Yako Yatimizwe duniani kama kule Mbinguni, halitatokea kwa vizazi vyote vya binadamu.

Juzuu Na. 15 - Mei 2, 1923


Udogo, jinsi gani ulivyo mzuri na wa kupendeza!. Bwana anatenda mambo makuu kabisa kwa kupitia wale walio wadogo kabisa: Kwa ajili ya Ukombozi alitumia ule udogo wa Bikira Mtukufu, na kwa ajili ya Mapenzi Yako yatimizwe anatumia udogo wa Luisa.

Juzuu Na. 16 - Novemba 10, 1923


Anayeishi katika Utashi wa Mungu, kwake huwa daima ni Noeli. Tendo endelevu la kufa hutokea katika Utashi wa Ubinadamu wa Yesu, na linatokea pia katika utashi wa Luisa ili FIAT Voluntas Tua iweze kufika kutawala hapa duniani kama kule Mbinguni.
Juzuu na. 16 - Desemba 26, 1923


Ule utume wa Utashi wa Mungu utatia kivuli juu ya Utatu Mtakatifu hapa duniani, na ndio utamfanya binadamu arejee kule kwenye asilia yake.

Juzuu na. 17 - Mei 4, 1925


Kwa nini ni wajibu wa kwanza wa mwanadamu kumrudishia Mungu upendo kwa ajili ya kila kitu alichokiumba. Utashi wa Mungu umetolewa kama Uhai wa kwanza kabisa wa mwanadamu.
Juzuu na. 18 - Agosti 9, 1925


Vitu vyote vilivyoumbwa hutembea kuelekea kwa binadamu. Sikukuu ya Kutwaliwa Bikira Maria Mbinguni ilitakiwa iwe inaitwa: ‘Sikukuu ya Utashi wa Mungu’.
Juzuu na. 18 - Agosti 15, 1925


Kilio cha malalamiko ya Roho Mtakatifu pale ndani ya Sakramenti mbalimbali. Malipo ya pendo la mtu.

Juzuu na. 18 - Novemba 5, 1925


Adamu, baada ya ile dhambi, alikuwa akitenda matendo yale yale ya kabla yake, lakini, pale alipojiondoa kutoka Utashi Mkuu wa Juu, hayo matendo yake yakawa tupu kabisa kwani yalikosa kuwa na kile kiini cha Uhai wa Kimungu.

Juzuu Na. 18 - Januari 28, 1926


FIAT ya kule Mbinguni ni msherehekeaji, kumbe hapa duniani ni mshindaji.
Juzuu na. 19 - Aprili 25, 1926


Kama Bikira Maria, kwa ajili ya kumpata Mkombozi Mtamaniwa, na ili kumchukua katika mimba, alivyopasika kukumbatia na kubeba mambo yote na kutenda yale matendo ya watu wote, ndivyo yule anayetaka kuipata FIAT kuu ya juu, budi akumbatie na kubeba watu wote na awe anajibu kwa ajili ya watu wote.
Juzuu na. 19 - Mei 18, 1926


Tofauti iliyopo kati ya yule anayeishi ndani ya Utashi wa Mungu na yule aliyejikabidhi kwa Utashi wa Mungu na anayeutii. Yule wa kwanza ndiye jua, na yule mwingine ni ardhi inayofaidi matokeo ya mwanga.
Juzuu na. 19 - Mei 31, 1926


Jinsi uelewa ulivyoleta uhai kwa matunda ya Ukombozi, ndivyo utaleta uhai kwa matunda ya Utashi wa Mungu.
Juzuu na. 19 - Juni 15, 1926


Mtu yule anayebeba ndani yake Ufalme wa Utashi wa Mungu, huyo anatenda kazi katika kiwango cha ulimwengu mzima na kwa hiyo ataupata utukufu wa kila kitu.
Juzuu na. 19 - Juni 26, 1926


Namna Yesu alivyokuwa anaandaa Ufalme wa Utashi Wake katika Ubinadamu Wake, ili aweze kuurejesha kwa Wanadamu. Matamanio yote, yawe ya kimungu au yale ya kibinadamu, yataingia hatarini endapo hatuishi katika Utashi wa Mungu.

Juzuu na. 19 - Julai 14, 1926


Siri ya Yesu. Nguvu na Manufaa ya siri Yake.
Juzuu na. 19 - Agosti 1, 1926


Kadiri mtu anavyozidi kujioanisha na Mungu, ndivyo Mungu anavyozidi kumjali, na ndivyo mtu atakavyoweza kupokea. Mfano wa bahari na kijito kidogo.
Juzuu na. 19 - Agosti 8, 1926


Utashi wa Mungu ndio unaofanya Maisha yote ya Bwana Wetu yawe ni tendo moja pekee pale ndani Yake.

Juzuu na. 19 - Agosti 25, 1926


Nafsi ya Mungu ipo katika mizani. Zawadi ya FIAT ya Kimungu ndiyo inayoweka kila kitu shirika. Katika kutoa, Hukumu ya Haki, inapenda likute egemeo la matendo ya wanadamu.
Juzuu na. 19 - Septemba 13, 1926


Ulinzi na uangalizi wa Yesu wakati Luisa anapoandika. Jinsi Ufalme wa FIAT unavyogharimu sana. Matendo yaliyotekelezwa ndani ya FIAT ni zaidi ya Jua.
Juzuu na. 19 - Septemba 15, 1926


Yule asiyetekeleza Utashi wa Mungu ni sawa na kikosi cha nyota za angani ambacho kinajiondoa toka mahali pake. Ni sawa na kiungo cha mwili kilichochomoka na kudondoka. Ni mchana angavu kwa Yule anayetekeleza Utashi wa Mungu na ni usiku wa giza kwa Yule asiyeutekeleza.
Juzuu na. 20 - Septemba 20, 1926


Faida kuu itakayoletwa na Ufalme wa FIAT ya Kimungu. Jinsi itakavyokinga watu dhidi ya maovu yote. Kama vile Bikira, ingawa kama hakutenda muujiza wowote ule, alitenda ule muujiza mkuu wa kumleta Mungu kwa wanadamu, ndivyo itakavyokuwa kwa yule anayepasika kufanya Ufalme ujulikane: atatenda muujiza mkuu wa kuleta Utashi wa Mungu.
Juzuu na. 20 - Oktoba 22, 1926


Jinsi Utashi wa Mungu unavyopatwa na maumivu makali sana kati ya wanadamu, na jinsi unavyotaka kuondokana na hali hiyo.
Juzuu na. 20 - Novemba 19, 1926


Yule anayeishi katika Utashi wa Mungu ni Mwangwi, ni jua dogo. Jinsi Makala haya yanavyotoka katika Moyo wa Bwana Wetu. Kazi za Bwana Wetu ni mapazia yanayomficha Malkia Mtukufu wa Utashi wa Mungu.
Juzuu na. 20 - Desemba 8, 1926


Jinsi Mtoto Mchanga anayetoka kuzaliwa tu alivyojionyesha kwa Mama Yake. Ule Mwanga alioutoa Mtoto Mchanga ambao ulikuwa ni salamu ya ujio wake hapa duniani. Tofauti kati ya Pango na lile gereza la wakati wa Mateso.
Juzuu na. 20 - Desemba 25, 1926


Utashi wa mtu kama zawadi kwa Mtoto Yesu. Jinsi maisha yake yote yalivyokuwa ni picha mfano na ni wito wa Utashi wa Mungu. Jinsi maarifa mbalimbali yanavyokuwa ni nyenzo za kuharakisha ujio wa Ufalme wa Utashi Wake.
Juzuu na. 20 - Januari 1, 1927


Jinsi Bwana Wetu atakavyokuwa na Ufalme wa aina tatu. Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu utakuwa ndiyo mwangwi wa Uumbwa. Jinsi Ufukara na utovu wa raha vitakavyofutwa. Jinsi pale ndani ya Bwana Wetu na pale ndani ya Bikira kulivyokuwa na ufukara wa hiari na siyo wa kulazimishwa. Jinsi Utashi wa Mungu unavyoshikwa na wivu katika kumtunza Binti yake.
Juzuu na. 20 - Januari 28, 1927


Kushindwa kuandika. Kama vile jua huwa linatoa mwanga daima, ndivyo Utashi Mkuu wa Juu hutaka uwe unatoa daima mwanga wa maelezo yake. Mtu anapozembea kuandika kile asemacho Yesu.
Juzuu na. 20 - Februari 9, 1927


Kama Utashi wa Mungu hautajulikana, na kama utakuwa haujapata Ufalme wake, utukufu wa Mungu ndani ya Uumbwa utakuwa haujakamilika bado. Mfano wa mfalme fulani.
Juzuu na. 20 - Februari 13, 1927


Yesu anamwalika Luisa kupigana Naye. Jinsi Yesu anavyopigana kwa njia ya maarifa Yake mbalimbali, kwa njia ya mifano mbalimbali, kwa njia ya mafundisho mbalimbali, wakati mtu anapigana kwa kuyapokea hayo, na kwa kufuata yale matendo ya Utashi Wake Yesu yaliyomo pale ndani ya Uumbwa na ndani ya Ukombozi.
Juzuu na. 20 - Februari 19, 1927


Jinsi mtu anayeishi katika Utashi wa Mungu anavyokuwa ni ushindi wa huo Utashi. Matishio ya Vita. Watu wa rangi zote.
Juzuu na. 21 - Machi 31, 1927


Jinsi Bikira Maria alivyomiliki Ufalme wa FIAT ya Kimungu. Jinsi mianga ilivyopiga mbizi na jinsi alivyotunga mimba. Jinsi Yesu, akiwa ndani ya pazia la Ubinadamu Wake, alivyotoka kama Jua lipambazukalo akienda kuwatafuta wanadamu wote. Jinsi kila aina ya ufunuo wa Kimungu ni hisani Yake Mungu kwa wanadamu.
Juzuu na. 23 - Desemba 18, 1927


Jinsi Mungu anavyotamani kurejesha zile furaha za nyakati za awali za Uumbwa. Uzuri ambao Utashi wa Mungu utaleta juu ya utashi wa kibinadamu. Mfano wa jua. Ni lini na wapi ilipofungwa ndoa ya Umungu na Uumbwa wa binadamu, na lini ndoa hiyo itafungwa tena?
Juzuu na. 24 - Juni 12, 1928


Mfano wa Mume anayepewa talaka na mkewe mahakamani, ndivyo ilivyo kwa Mungu tangu siku ile mwanadamu alipoanguka katika dhambi ya kwanza.
Juzuu na. 24 - Juni 16, 1928


Bahari ya Pendo katika Pendo-Kupindukia la Yesu. Mfano wa bahari hiyo. Utashi wa Mungu ni mwonzi wa jua unaoleta Uhai wa Mbinguni. Utashi wa Mungu unapotenda kazi yake. Furaha ya Yesu.
Juzuu na. 25 - Desemba 21, 1928


Jinsi Watakatifu wote ni matokeo ya Utashi wa Mungu, wakati wale ambao wanaishi ndanimo ndio watakaoubeba na uhai Wake.

Juzuu na. 25 - Februari 27, 1929


Jinsi Utashi wa Mungu unavyokuwa daima katika tendo la kuupyaisha kile ambacho ulikitenda wakati wa kumwumba binadamu. Jinsi Utashi wa Mungu unavyobeba ile nguvu inayovutia.

Juzuu Na. 25 - Machi 3, 1929


Yale yote aliyoyaeleza Yesu juu ya Utashi Wake Mwabudiwa ni Uzao mbalimbali wa Kimungu. Masikitiko Yake pale anapoona kwamba hizo kweli mbalimbali hazizingatiwi vema.

Juzuu na. 25 - Machi 17, 1929


Jinsi Uumbwa unavyopiga mbio za taabu taabu kwenda kwa Muumba Wake. Yule anayeishi ndani ya Utashi wa Mungu hatenganiki nao. Utaratibu ambao Yesu ameuzingatia wakati anaelezea zile kweli mbalimbali mintarafu Utashi wa Mungu. Uupyaisho wa Uumbwa. Umuhimu wa zile kweli mbalimbali.

Juzuu na. 25 - Machi 25, 1929


Jinsi gani katika Utashi wa Mungu, mtu huwa na kila kitu chini ya mamlaka yake, kwani pale anaipata chemchemi ya chimbuko la kazi za Kimungu, na kutokana na chimbuko hilo, anaweza akawa anazirudia kazi za Kimungu kila anapotaka.
Juzuu na. 27 - Oktoba 24, 1929


Utashi wa Mungu ni hifadhi ya matendo yote ya Watakatifu wote. Jinsi Mungu anavyoshikana mkono na Mwanadamu. Matendo gani yaliyopotea nje ya lengo la Muumba Wetu.
Juzuu na. 29 - Oktoba 8, 1931


Hamu ya Yesu ya kutaka asindikizwe na mwanadamu. Hamu kali kabisa ya Yesu Kichanga kutaka apendwe kwa Pendo la Kimungu la Mama Yake wa Mbinguni.
Juzuu na. 30 - Desemba 25, 1931


Mungu kamwumba binadamu katika ekstasi ya Pendo. Uumbwa: Seti ya Mapaji aliyopata binadamu. Sauti tamu ya Kengele, ekstasi kati ya Muumba na Mwanadamu. Tukio la ajabu la Bikira kutungwa katika mimba.
Juzuu na. 31 - Oktoba 9, 1932


Ubinadamu wa Bwana Wetu, kaburi takatifu na hifadhi ya kazi zote za wanadamu. Jinsi Pendo lisivyoweza likasema ‘inatosha’.
Juzuu na. 32 – Septemba 24, 1933


Maajabu ya Uimmakulata, Mawasiliano ya haki za Kimungu. Jinsi Mungu asivyopenda kutenda lolote bila Mama Yake wa Mbinguni.
Juzuu na. 34 - Desemba 8, 1935


Maonyesho ya Kimungu kwa mtu yule anayeishi katika Utashi Wake. Jinsi Mungu anavyomshirikisha mtu huyo katika kazi Zake. Jinsi anavyokuwa daima na kitu cha kumpatia mwanadamu na jinsi anavyokuwa daima ana shughuli ya kutenda naye.
Juzuu na. 34 - Aprili 21, 1936


Jinsi kilio cha Yesu cha Msalabani, ‘sitio’, kinavyoendelea bado kusikika ndani ya kila moyo: ‘Naona kiu!’ Jinsi ufufuko wa kweli unavyodhihirika katika Utashi wa Mungu. Jinsi yule anayeishi ndani ya Utashi wa Mungu hawezi akanyimwa kitu.
Juzuu na. 36 - Aprili 20, 1938


Anayeishi katika Utashi wa Mungu huwa anabaki katika mawasiliano ya kudumu na endelevu na Mwenyezi Mungu. Kuzaliwa upya na Pendo linaloongezeka. Jinsi mtu anayeishi katika Utashi wa Mungu anaavyowafurahia na anavyowafurahisha watu wote. Jinsi Yesu Mwenyewe atakavyokuwa ndiye mlinzi wa kuhifadhi Makala hizi na jinsi suala zima litakavyokuwa linamhusu Yeye Mwenyewe.
Juzuu na. 36 - Juni 20, 1938

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Sahihi halisi ya mkono wa Luisa mwenyewe


⬆️⬆️⬆️

http://divinewilldivinelove.com/Kiswahili-/-Swahili/

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































Report Page