Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Novemba 22, 1921🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Novemba 22, 1921🖋📄📖📔


Wakati nikiendelea kuwa katika hali yangu ya siku zote, na baada ya kukesha karibu usiku mzima, mawazo yangu yakawa yanaruka daima kwenda kwa Yesu Wangu Mfungwa. Yeye, akiwa ndani ya giza totoro, alijitokeza na kunijia, kwa jinsi kwamba niliweza kuonja pumzi Yake ya kuhema, na nilionja hata mguso wa Nafsi Yake. Lakini, sikuweza kumwona. Basi nikajaribu kujiyeyusha nafsi yangu ndani ya Utashi Wake Mtukufu huku nikitekeleza yale matendo yangu ya daima ya kumhurumia, na matendo ya kulipa fidia. Ndipo mwonzi wa mwanga mkali kuliko ule wa jua, ulijitokeza toka ndani mwangu, na ukawa unang’aa juu ya uso wa Yesu. Mbele ya mwonzi ule, Uso Wake Mtukufu uliangazwa, na kadiri kulivyozidi kupambazuka, giza lilifukuzwa, na ndipo mimi niliweza kukumbatia magoti ya Yesu. Na Yeye aliniambia:

“Binti Yangu, matendo yale yanayotekelezwa ndani ya Utashi Wangu huwa ni mwanga wa mchana kwa Mimi. Na endapo binadamu, katika dhambi zake, atanizungushia Mimi katika giza, matendo hayo, zaidi kupita hata mionzi ya jua, huwa yananitetea na kunikinga Mimi dhidi ya giza, yananizungushia Mimi ndani ya mwanga, na hatimaye huwa yananichukua Mimi mkononi ili kwenda kuwafahamisha wanadamu Mimi ni nani. 

Ndiyo maana Mimi nampenda sana mtu yule anayeishi ndani ya Utashi Wangu - ni kwa vile ndani ya Utashi Wangu mtu huyo huweza kunipatia Mimi kila kitu, anaweza kunitetea dhidi ya mambo yote, na mbele yake Mimi naonja kama vile ninampatia kila kitu na ninafungilia ndani yake mema yale yote ambayo napenda kuwapatia watu wengine wote.  

Ebu fikiria, kwamba jua lingekuwa na nguvu ya hoja, na tujali kama mimea ingekuwa nayo na uwezo wa hoja, na kwa hoja hiyo, ikawa inaukataa mwanga na joto kutoka kwa jua, na tujali hiyo mimea iwe inachukia kuchanua na kuzaa matunda. Na tujali mmea mmoja peke yake ukawa ndio unapokea mwanga wa jua kwa upendo, na hatimaye, huo mmea ukawa unapenda kutoa kwa jua matunda yale yote ambayo ile mimea mingine kakataa kuzaa. 

Sasa je, isingekuwa ni vema na haki kwa jua kuuondoa mwanga wake kutoka kwa ile mimea mingine yote, na kishapo likamwaga mwanga wake wote na joto lake lote juu ya ule mmea moja? Ninasadiki kwamba ndivyo lingefanya. 

Sasa kile ambacho hakitendeki katika jua kwa vile halina nguvu ya hoja, hilo linaweza kutokea kati ya mtu na Mimi”. 

Baada ya kuyasema hayo, Yeye alififia. Halafu, baadaye alirejea kwangu na akaongeza kusema:

“Binti Yangu, maumivu yaliyonichoma Mimi kupita yote wakati wa Mateso Yangu yalikuwa ni ule unafiki wa Mafarisayo. 

Walijizingizia kutafuta haki, lakini ndio wao waliokuwa wanaovunja haki kupita wote.

Walijizingizia kutafuta utakatifu, kushika uthabiti, kuzingatia taratibu, kumbe lakini, ni wao waliokuwa wapotovu, nje ya kila aina ya sheria, na ni wao waliojaa vurugu kabisa.

Na kwa jinsi walivyokuwa wanajizingizia kumheshimu Mungu, ndivyo walivyokuwa wanatafuta kujiheshimu wao wenyewe, masilahi yao wenyewe, na raha zao. 

Kwa hiyo, mwanga haukuweza kuingia ndani yao kwa vile hizo hulka za kujipenda wenyewe zilikuwa zinaziba milango mwanga usiweze kuingia. 

Unafiki na kujisingizia vilikuwa ndiyo ufunguo ambao, kwa kufuli mbili, ulikuwa unawafungilia kifoni. 

Katika ukaidi wao, walifungiliwa hivi, kiasi kwamba, hata mimemetuko fulani ya mwanga haikuweza kupenya kuwafikia.  

Ilitokea hivyo kiasi kwamba hata yule Pilato, mpagani anayeabudu miungu, aliambulia angalau mwanga zaidi kuliko wale Wafarisayo wenyewe, kwa vile, chochote kile alichosema na kutenda Pilato, kilikuwa hakitoki kwa kujisingizia, bali angalau kilitoka katika hofu. 

Na Mimi huwa ninaelekea kuvutwa zaidi na mdhambi potofu asiyekuwa mwongo na mnafiki, kuliko kuvutwa na wale walio wema, lakini waongo na wanafiki.

Oh! Ni jinsi gani ninavyochukizwa Mimi na mtu yule ambaye kwa nje hutenda mema, anajisingizia kuwa mwema, anasali, na lakini, kwa ndani, anafuga ubaya na uovu, na ubinafsi. Na wakati midomo yake inasali, moyo wake huwa mbali sana kutoka Kwangu Mimi. 

Na katika lile lile tendo lake jema, huwa anafikiria namna ya kutimiza matamaa yake machafu. 

Aidha, mtu yule ambaye ni mwongo katika lile jema ambalo anajisingizia kutenda na kusema, huwa anashindwa kutoa mwanga kwa wengine kwa vile huwa amefunga milango ya mwanga huo. 

Hao watu hutenda kama mashetani waliomwilishwa, ambao mara nyingi sana huwa wanawavuta watu kwa sura na mavazi ya wema.  

Na watu wanapouona huo wema, huwa wanadiriki kuvutwa na kuingia katika matendo hayo mema. Lakini, wanapokuwa tayari katikati ya mwendo, watu wale wanawatumbukiza katika madhambi makubwa zaidi. 

Oh! Ni jinsi gani vishawishi vyenye sura ya dhambi ni salama zaidi kuliko vishawishi vile vyenye sura ya wema.  

Kadhalika, ni salama zaidi kushughulika na watu potofu, kuliko kushughulika na watu wema ambao ni wanafiki. 

Hawa ni sumu nyingi ngapi wanazozificha ndani yao? Ni watu wengi wangapi ambao wanawasumisha?  

Kama isingekuwa kwa ajili ya unafiki na kujisingizia, na kama watu wote wangejulikana kwa hali ile waliyo nayo, hakika paa la uovu lingekuwa limeondolewa kutoka uso wa dunia, na ndipo watu wote wangekombolewa kutoka kila aina ya udanganyifu”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page