Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Februari 9, 1927🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Februari 9, 1927🖋📃📖📔


Nilikuwa nikionja kutotaka kuandika, kwa vile, nilijiona kuwa sina uwezo wowote. Si hivyo tu, bali nguvu zangu zilizidi kupunguka kwa haraka hivi hata nikaonja kuwa sitaweza kabisa. Ndipo nikawa nawaza moyoni mwangu: ‘Labda siyo mapenzi ya Mungu tena kwamba mimi niwe ninaandika, vinginevyo Yeye angenipa msaada zaidi na nguvu zaidi. Aidha, kama kweli Yesu anataka, basi anaweza akaandika Yeye Mwenyewe - akaandika bila mimi’. Ndipo Yesu Wangu Mpendevu, akiingia pale ndani mwangu aliniambia:

“Binti Yangu, jua huwa linatoa mwanga daima, na kamwe huwa linachoka kuzingatia njia na safari yake ya kwenda kuufunika uso wa ardhi kwa mwanga wake. Na ushindi wake mkuu ni pale unapoikuta mbegu kwa ajili ya kuiwezesha kuota na kuchipuka, na kuikuza ili lenyewe liweze kuirudufu. Ushindi wake ni pale linapolikuta ua ili kulipatia rangi na harufu nzuri. Fahari yake ni kulikuta tunda ili kulipatia utamu na ladha. Kwa kushirikisha matokeo yake, jua, kwa matendo halisi, hudhihirisha kwamba, lenyewe ni mfalme halisi wa ardhi, na kwa hiyo linapata fahari pale linapomkuta yule ambaye litamshirikisha na kumgawia matokeo yake, na hivyo linatekeleza zoezi la jukumu lake la kifalme juu ya viumbe vyote.

Kwa upande mwingine, katika nchi fulani fulani, ambako halizikuti mbegu, wala maua, wala mimea, wala matunda, jua huwa haliwezi kushirikisha na kugawia matokeo yake. Badala yake, linayahifadhi hayo yote ndani yake lenyewe, na kwa hiyo linajionja kukosa fahari. Hapo jua linakuwa ni kama mfalme asiyekuwa na raia, mfalme asiyeweza kutekeleza jukumu lake. Basi, jua, katika kuchukia na kusikitika kwa vile linashindwa kushirikisha matokeo yake, huwa linaichoma na kuiunguza ardhi hiyo kiasi cha kuifanya iwe tasa na jangwa lisiloweza kamwe kuzalisha hata unyasi moja.

Kwa hiyo, Binti Yangu, jua ni picha mfano ya Utashi Wangu, na, kwa asili yake wenyewe, Utashi Wangu huwa unapenda kufuata mwendo wa mwanga ndani ya mtu yule ambamo unatawala. Na maadam mwanga wake unabeba idadi ya matokeo mengi yasiyohesabika, jua huwa halifikii kuchoka, wala huwa halijimalizi, na kwa hiyo huwa linapenda kushirikisha matokeo yake, na fahari yake ni pale linapoona utayari na uhiari ndani yako. Basi, hapo huwa linashirikisha matokeo yake kwako zaidi kuliko linavyoshirikisha kwenye mbegu, kwenye ua, na au kwenye tunda - linashirikisha ile harufu nzuri, linashirikisha rangi, linashirikisha utamu wake, ambao, kwa kuubadilisha kuwa maarifa yake mbalimbali, huleta ule uvutio wa bustani yake. Na FIAT Yangu ya Kimungu, zaidi kupita jua, huonja kuwa kama mfalme, ambaye, anaweza kutekeleza jukumu lake la kifalme. Inaonja kuwa inao siyo raia wake tu, bali inaye hata Binti yake, ambaye kwake, pale inaposhirikisha matokeo yake na maelezo yake, yenyewe FIAT papo hapo inaweza kumshirikisha ufanano wa malkia. Na fahari yake yote ni hii - kuweza kumgeuza mtu awe malkia, na hatimaye kumvika mavazi ya kifalme.

Na maadam maelezo Yangu yote juu ya FIAT Kuu ya Juu yataleta ile bustani mpya ya watoto wa Ufalme Wangu, FIAT inataka daima kuingiza ndani yako wewe, matokeo yake pamoja na ule mwanga wake, ili, kuitajirisha hiyo bustani na kuifanya ijae anasa za aina zote za maua ya Mbinguni, anasa za matunda na mimea, kwa jinsi kwamba, wanadamu wote watakapokuwa wamevutwa na hizo tofautitofauti za hayo mambo mazuri na yapendezayo, wote waweze kuonja kana kwamba wanavutiwa, na ndipo watajitahidi sana na kupigania kuja kuishi ndani ya Ufalme Wangu.

Sasa, kama wewe ungekuwa unakosa ule uhiari na utayari wa kupokea ule ushirikisho mbalimbali wa yale matokeo ya Jua la Utashi Wangu, na kama ungekosa uhiari na utayari wa kuyatoa nje hayo matokeo kwa ajili ya kuyaandika, ili kulijulisha jema lile lililoko ndani ya huo Utashi, na pia kuijulisha ile miujiza isiyowahi kusikika, Utashi Wangu, hapo, ungetenda sawa kama jua - yaani, ungekuchoma na kukuunguza wewe, kiasi kwamba ungekuja kuwa kama nchi iliyo tasa na jangwa isiyo na rutuba yoyote.

Halafu tena, itawezekanaje Mimi niandike peke Yangu bila wewe?

Maelezo Yangu budi yawe yanagusika na kuonjeka, na yasiwe katika hali ya kutokuonekana. Ni budi yatue juu ya vionjo vya wanadamu. Jicho la kibinadamu halina nguvu ya kutazama na kuona vitu visivyoonekana.

Ni sawa kama vile ningekuwa nimekuambia wewe: ‘Andika bila wino, bila peni na bila karatasi yoyote’. Je hilo lisingekuwa ni kichekesho na ujinga?

Kwa hiyo basi, kwa vile maelezo Yangu budi yawe kwa matumizi ya wanadamu, ambao wametengenezwa kwa roho na mwili, Mimi ninahitaji kitu kinachoonekana kwa ajili ya kuandikia - na ni wewe ndiye mwenye kuniazimisha kitu hicho.

Kwa hiyo basi wewe utatumika kama wino, kama peni, na kama karatasi kwa ajili Yangu Mimi, na kwa njia hiyo, Mimi ninaweza kutengeneza herufi Zangu. Na wewe, utakapokuwa unazionja hizo herufi ndani yako, uwe unazitoa nje na kuzifanya ziwe zinagusika na kuonjeka kwa njia ya kuziandika karatasini. Kwa hiyo basi, huwezi ukaandika bila Mimi, kwa vile, ungekuwa unakosa kichwa cha kuandika, ungekosa mada, na ungekosa pia imla ya kuweza kunakili, na kwa hiyo, usingeweza kusema chochote kile. Na Mimi siwezi nikaandika bila wewe, kwani ningekosa kuwa na mambo muhimu ya kuniwezesha kuandika: karatasi ya roho yako, wino wa pendo lako, na peni ya utashi wako. Basi, hiyo ni kazi ambayo Sisi sote wawili budi tuitende kwa pamoja na kwa kuelewana kati Yetu”.

Ndipo, nilipokuwa nikiandika, nikawa nawaza moyoni mwangu: ‘Kabla ya kuandika mambo fulani madogo madogo ambayo Yesu ananieleza, kwangu mimi ninayaona kuwa ni mambo yenye umuhimu mdogo sana, na kwa hiyo nisingedhani kuwa ni lazima kuyaweka hayo katika maandishi. Lakini sasa, maadam nipo tayari katika tendo la kuyaaandika, mtindo anaotumia Yesu kuamrisha mambo hayo ndani mwangu unabadili kabisa mazingira. Ingawa kama ni madogo kwa kuonekana, inaelekea kuwa na umuhimu mkubwa sana katika kiini chao. Kutokana na hayo yote, ni maelezo gani watakayoyatoa mbele ya Mungu, wale viongozi wote waliowahi kuwa na mamlaka juu yangu mimi, na wale ambao bado wana mamlaka hayo, kama wao hawakutumia mamlaka yao kunishinikiza, ili mimi, chini ya utii, niwe ninaandika? Ni mambo mangapi nimekuwa ninayazembea wakati nilipokuwa sipokei uamrisho wowote?’. Ndipo Yesu, akiingia pale ndani mwangu, aliniambia:

“Binti, ni kweli kabisa, hao watapasika kunipatia Mimi ripoti. Kama wanasadiki kuwa ni Mimi, basi, ripoti itakuwa ni kali kabisa, kwa vile, kwa kusadiki kwamba ni Mimi wakati wao hawakuandika ripoti yoyote hata ya neno moja, ni sawa na kutaka kuziba pumzi ya bahari ya lile jema lenye manufaa kwa wanadamu, kwa vile neno Langu huwa linaanza daima kutokana na nguvu ya Maweza ya Uumbaji. Ndiyo maana, Mimi, nilikuwa nimetamka FIAT moja tu katika Uumbwa, na mara nikawa nimepanua na kueneza anga iliyojaa na kupambwa na mamilioni yasiyo na idadi ya nyota mbalimbali. Nilitamka FIAT nyingine na ndipo nikatengeneza jua. Sikuwa nimeyasema maneno ishirini kwa ajili ya kutengeneza hivyo vitu vingi katika Uumbwa, bali FIAT moja tu ilitosha Kwangu Mimi. Neno Langu bado linayo nguvu yake ya Uumbaji, na wewe au watu wengine, hamwezi mkajua iwapo neno Langu linalenga kutengeneza anga, kutengeneza nyota, bahari, au jua kwa ajili ya watu. Kwa hiyo, kwa kosa la kutolizingatia na kutolionyesha wazi kwa ajili ya wanadamu, hawa wanadamu wameweza kufikia kukataa hiyo anga, hilo jua, hizo nyota, na hiyo bahari, na hata wamenigomea vyote na kuvirudisha ndani Mwangu Mimi, wakati vitu hivyo vingeweza kuleta faida kubwa kabisa kwa wanadamu. Na athari yote ambayo inaweza ikatokea, itaelekezwa kwa yule ambaye, kwa kosa la kutozingatia neno Langu, amelibana lisipumue na kulizuia ndani Mwangu ili lisitoke.

Kinyume chake, endapo wanadamu hawasadiki, hapo mambo huweza kuwa ni mabaya zaidi. Hapo wanakuwa ni vipofu sana hivi kwamba wanakosa kuwa na macho ya kuweza kuliona Jua la neno Langu. Na utovu wa imani huleta ukaidi na kiburi, na pia ugumu wa moyo. Lakini kumbe, imani huwa inaulainisha moyo, na huweza kuuandaa huo moyo uweze kutiishwa na neema, na uweze kupokea macho kwa ajili ya kuweza kuzielewa zile kweli Zangu”.

Juzuu na. 20 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page