Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 11 - Oktoba 20, 1916🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 11 - Oktoba 20, 1916🖋📄📖📔


Nilikuwa nikijiyeyushia mwenyewe ndani ya Utashi wa Mungu. Ndipo likanijia wazo la kuwaombea, na kwa namna ya pekee, kuwakabidhi watu kadhaa, kwa Utashi wa Mungu. Ndipo Yesu Mbarikiwa aliniambia:

“Binti Yangu, hata usipoweka nia maalum yoyote ile, inatosha ile hali ya kutambulika kuwa ni jambo la pekee kabisa.

Katika mpangilio wa Haki ya Hukumu ya Mungu huwa inatokea sawa kama inavyokuwa katika mpangilio wa maumbile: Yaani, jua huwa linatoa mwanga kwa watu wote hata kama siyo watu wote wanafikia kufaidi matunda yenyewe.

Hali hiyo lakini, haitokani na jua bali hutokana na hali ya wanadamu. 

Kuna mwanadamu anayeufaidi mwanga wa jua kwa ajili ya kutendea kazi, kwa ajili ya kujituma katika mambo mbalimbali, kwa ajili ya kuvitambua na kuvielewa vitu, na kwa ajili ya kuvithamini na kuvifurahia vitu: huyo mwanadamu ataweza kujitajirisha, atajijenga na kujiunda, na wala hazungukizunguki kwa watu kwenda kuomba omba mkate toka kwa wengine.

Mwanadamu mwingine, lakini, yeye hupenda kula raha tu, hapandi kujishughulisha na chochote.  

Ingawa kama mwanga wa jua unamwangaza popote mtu huyo, lakini kwake huyo huwa yote ni kazi bure tu.

Hapendi kabisa kutenda lolote lile: huyo anabaki kuwa fukara na mwenye maradhi maradhi – kwa vile uvivu huleta mabaya mengi, yawe ya kimwili au yale ya kimaadili - na huyo mtu, kila anapoonja njaa, analazimika kwenda kuombaomba mkate kwa kwa wengine. 

Sasa, ili kutokee hali iliyo kinyume kabisa na hiyo hali ya sasa, je, litakuwa ni suala litakalosababishwa eti na mwanga wa jua?

Au je ni jua ndilo labda linatoa mwanga mwingi zaidi kwa huyu na mwanga mdogo zaidi kwa yule?  

La hasha kabisa kabisa!

Tofauti iliyopo ni hii tu, kwamba mwanadamu mmoja anaufaidi mwanga kwa kiasi cha pekee zaidi na yule mwingine haufaidi kwa lolote. 

Basi ndivyo inavyokuwa katika mpangilio wa Neema ambayo, zaidi zaidi ya mwanga wa jua, huwa inawajaza na kuwafunika watu. 

Yaani, wakati fulani Neema huwa inatoa sauti yote ili kuwaita wanadamu, ili kuwafundisha, na ili kuwaonya.  

Wakati mwingine Neema huwa inaleta moto, ili, kwa ajili ya wanadamu, kuchomelea mbali mambo ya hapa chini duniani, na kwa miali yake moto huo huwa unawasaidia wanadamu kufukuzia mbali matamaa mbalimbali.  

Moto huo, kwa ukali wake wa kuunguza, huwa unaleta mateso, na pia unaleta misalaba, ili kumletea mtu ule mtindo wa utakatifu ambao Neema inautaka toka kwake.

Wakati fulani Neema hutengeneza maji ili kumsafisha mtu, ili kumpamba na kumremba na ili kumziriba kwa Neema.

Lakini, ni nani hapa huwa makini kutosha ili aweze kuipokea hiyo mitiririko ya Neema? 

Ni nani huyo anayeambatana Nami daima? 

Ah, Ni wachache mno mno! Lakini halafu, wanapotaka kunilaumu Mimi, huwa wanazoea kusema eti kwamba Mimi huwa ninapendelea kutoa Neema kwa akina fulani hawa ili wawe watakatifu na kwa wengine wale siwapatii Neema yoyote! 

Wao hao wanafurahia kupitisha maisha katika raha za uvivu eti kana kwamba mwanga wa Neema haupo kwa ajili yao pia”. 

Kishapo aliongeza kusema: 

“Binti Yangu, Mimi ninampenda sana mwanadamu hata nimejiweka Mimi mwenyewe mbele ya kila moyo ili kuilinda, ili kuitetea, na nimejiweka pale ili, kwa mikono Yangu yenyewe, niweze kuwa nafanya kazi ya kuwatakatifuza wao.  

Lakini, ni kwa masikitiko sana sana gani, wao hawapendi kujikabidhi Kwangu na kunitii?

Utamwona yule akinisukumia pembeni, yule asiyenijali kabisa, na yule akinidharau, yule akilalamikia shughuli Yangu ya kuwalinda na kuwaangalia, na mwingine utamwona akifunga mlango wa moyo wake mbele ya macho Yangu ili nisiingie, na hivyo wanafanya kazi Yangu yote isiweze kuwaletea matunda yoyote yale.

Aidha, si tu kwamba Mimi nimejiweka kuwa mlinzi wao, lakini, kwa watu hao wanaouishi Utashi Wangu, Mimi nimewachagulia nafasi nzuri kweli. Kwa vile wanajikuta wenyewe wapo katika kila sehemu Yangu, Mimi ninawaketisha pamoja Nami wawe kama walinzi wa pili kwa kila moyo. 

Hawa walinzi wa pili ndio wanaonifariji, ndio wanaonilipa madeni badala ya wanadamu na ndio hawa wanaokesha pamoja Nami katika upweke ambao mioyo mingi sana imenilazimisha niukabili.

Hao wananisukuma na kunilazimisha nisiachane nao kamwe. 

Mimi nisingeweza kuwapatia wanadamu Neema kubwa isipokuwa hiyo ya kuwaletea hao watu ambao wanaishi ndani ya Utashi Wangu, watu hawa ambao ndiyo muujiza mkuu wa miujiza yote!”.

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe


Report Page