Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Desemba 25, 1920🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Desemba 25, 1920🖋📄📖📔


Wakati nilipokuwa bado katika hali yangu ya siku zote, nikajikuta nipo nje ya nafsi yangu, lakini nikiwa pamoja na Yesu. Nilijikuta nipo safarini nikitembea katika njia ndefu sana. Wakati mwingine nilijikuta natembea pamoja na Yesu, na halafu mara nilijikuta nipo na Mama Malkia. Kama Yesu alififia, hapo nikawa najikuta nipo na Mama. Katika safari hiyo walikuwa wakiniambia mambo mengi sana. Yesu na Mama walinionyesha upendo sana, walikuwa na utamu unaovutia sana. Mimi nikawa nimesahau kila kitu - nilisahau uchungu wangu mbalimbali, nikasahau hata kule kukosekana kwa machungu hayo. Nikawa nafikiri kwamba, kamwe nisingeweza. Nikadhani kwamba sitaweza kuyapoteza tena maumivu hayo. Oh! Ni jinsi gani ilivyo ni rahisi kusahau ubaya mbele ya mambo mema na mazuri. 

Halafu, mwishoni mwa safari ile, Mama wa Mbinguni alinichukua mikononi mwake. Mimi nilikuwa kadogo sana sana. Akaniambia:  

“Binti Yangu, Mimi nataka kukuimarisha wewe katika kila kitu”. 

Na ikaonekana kana kwamba, kwa mkono wake mtakatifu alikuwa akichora alama fulani usoni pangu. Alikuwa anaonekana kana kwamba anaandika na kutia mhuri pale. Halafu akaonekana kana kwamba anaandika kitu na hatimaye anagonga mhuri juu yake. Kishapo alionekana kana kwamba akiandika juu ya macho yangu, mdomoni mwangu, katika moyo wangu, na hata katika mikono yangu na katika miguu yangu. Mwisho aligonga mhuri juu ya hivyo vyote. 

Mimi nilikuwa nikitamani kuona kile alichokiandika ndani yangu, lakini nikawa nashindwa kusoma ule mwandiko. 

Ni pale mdomoni pangu tu ndipo nilipoweza kuziona herufi mbili zilizosema: ‘Kufutilia mbali kila aina ya kionjo’. 

Nami nilijibu mara moja: ‘Asante, Oh! Mama - Kumbe wewe unanifutilia mbali kila aina ya kionjo kisichomhusu Yesu’.  

Mimi nikawa natamani kujua mambo zaidi. Lakini Mama akaniambia: 

“Si jambo la lazima kwa wewe kuyafahamu hayo. Uniamini Mimi, nimekutendea wewe kila kitu kilichohitajika”. 

Alinibariki na akafifia. Ndipo nilipojikuta nimerudi ndani ya nafsi yangu.

Halafu, baada ya muda, Yesu Wangu Mtamu alirejea akaja kwangu. Alikuwa ni mtoto mchanga na laini sana. Alikuwa akilalamika, akilia, na kutetemeka kwa baridi. Alijitupa mikononi mwangu ili nimpashe joto. Mimi nilimkumbatia na kumbana sana sana. 

Na kama kawaida yangu, nilijiyeyushia nafsi yangu ndani ya Utashi Wake, ili niweze kuyakuta pale mawazo ya watu wote pamoja na ya kwangu, na pia, katika uabudu mbalimbali wa akili zote zilizoumbwa, niweze kumzungushia huyu Yesu anayetetemeka kwa baridi. Ningemzungushia pia katika mitazamo ya watu wote ili wawe wanamwangalia wote, na kwa njia hiyo wayashitue macho ya huyo mtoto hata aweze kuacha kulia. Ningeweza kumzungushia midomo, maneno, na hata sauti za wanadamu wote ili kusudi wote hao wawe wakimbusu, na hivyo kumfanya asiwe analia na kulalamika na kwa pumzi zao wawe wanaendelea kumpasha joto.

Na kweli, wakati nilipokuwa nikifanya hilo, Mtoto Yesu akawa ameacha kupiga makelele. Aliacha kulia, na huku akionekana kuwa amepata joto kidogo, akawa ameniambia: 

“Binti Yangu, je umetambua ni kitu gani kilichonifanya niwe ninatetemeka, niwe ninalia na niwe ninapiga makelele? Ni tatizo langu la kule kuachika na wanadamu. Lakini halafu wewe uliwaleta na kuwapanga kunizunguka Mimi; ndipo nilianza kuona kuwa ninatunzwa, ninapata busu la wote, na ndipo niliweza kutulia na kuacha kulia.

Lakini ni vema ukumbuke kwamba mkasa Wangu wa kwenye Sakramenti ni mkasa mbovu na mkali zaidi kuliko hata mkasa huu wa utotoni Mwangu. 

Lile pango, hata kama lilikuwa ni baridi, lakini walau lilikuwa na nafasi ya kutosha, na pia lilikuwa na hewa kutosha ya kuweza kuvuta. Hostia ina baridi pia, lakini pia ni ndogo mno hivi hata sipati hewa ya kuvuta.

Pale pangoni angalau nilikuwa na lile hori lililokuwa limetandikwa nyasi kidogo kama kitanda changu. Lakini pale katika maisha Yangu ya Sakramenti ninakosa hata nyasi za kulalia, na wala sina kitu chochote pale isipokuwa yale mabati baridi ya chuma cha chiborio ninayolalia.

 Pale pangoni nilikuwa na Mama Yangu mpenzi ambaye mara nyingi sana alikuwa akinichukua katika ile mikono yake safi mno, alikuwa ananifunika kwa mabusu motomoto ili kunipasha joto. Na alikuwa akituliza kilio Changu kwa kuninyonyesha maziwa yake matamu kabisa. Lakini, kinyume chake, katika maisha Yangu yale ya Sakramenti: sina Mama pale, pale wanaponichukua huwa ninaonja kuguswa na mikono isiyostahili - yaani mikono inayonuka kama matope na mavi. Oh! Ni jinsi gani ninavyoonja ile harufu chafu - harufu chafu zaidi kuliko hata ile ya mbolea niliyokuwa nikinusa pale pangoni. Badala ya kunifunika Mimi kwa mabusu, wao wananigusa Mimi kwa matendo yao yenye kunidhalilisha. Na badala ya kunipatia maziwa ninywe, wao wananipatia nyongo ya makufuru, ya kutokujali, na ya ubaridi. 

Pale pangoni Mtakatifu Yosefu hakuniacha kamwe bila mwanga angalau wa koroboi ndogo ya usiku. Lakini, hapa katika Sakramenti, ni mara ngapi huwa ninaachwa gizani usiku wote! 

Oh! Ni jinsi gani mkasa Wangu wa Sakramenti unavyoniletea maumivu. 

Ni machozi mengi mangapi yaliyofichikana ambayo hayaonekani kwa mtu mwingine yeyote. 

Ni malalamiko mangapi ambayo hayasikilizwi na yeyote yule.  

Kama mkasa Wangu ule wa utotoni ulikushitua wewe hata ukawa unanihurumia, basi mkasa Wangu huu wa Sakramenti ndio ukusukume wewe zaidi kunionea huruma!”

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page