Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 29 – Oktoba 8, 1931🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 29 – Oktoba 8, 1931🖋📄📖📔


Akili yangu duni ipo ikichunguza mambo kuzunguka Jua la FIAT Kuu. Nikagundua kuwa imezungukwa na kazi zote za Watakatifu wote wa kale na wa sasa. Aidha imezungukwa na sadaka zao zote, maumivu yao yote na ushujaa wao wote, yaani, imezungukwa na mambo yote mema waliyoyatenda. Kadhalika ilikuwa imezungukwa na matendo yale yote ya Malkia wa Mbingu na pia na yale yote ambayo Yesu Mbarikiwa aliyatenda kwa ajili ya kutupenda sisi. Utashi wa Mungu unahifadhi kila kitu. Kwa vile Utashi ndio uliokuwa ni mtendaji mwanzilishi wa matendo mema hayo yote ya wanadamu, wenyewe unayashika matendo hayo – kwa wivu mkubwa - na inayahifadhi ndani ya Uhai wake wenyewe na baadaye unayatumia matendo hayo katika kujitukuza wenyewe, na kuwatukuza wale walioyatekeleza. Nami, nilipoona kuwa kila kitu ni mali ya Utashi wa Mungu, maadam huo ni Utashi Wangu pia, nikajua kuwa kila kitu kilikuwa ni changu. Niliendelea kuzunguka na kuingia ndani ya kila tendo, ili kulitolea kila moja lao kama tendo langu kwa ajili ya kuutukuza zaidi Utashi wa Milele, huku nikiendelea kuuomba ujio wa Ufalme Wake hapa duniani. Lakini, pindi nikifanya hilo, Yesu Wangu Mpendevu wa daima, alinishitua na kuniambia:

“Binti Yangu, ebu sikiliza siri hizi za ajabu za Utashi Wangu: Endapo mwanadamu anataka aone kila kitu kilicho kizuri, kilicho chema, kipendezacho na kitakatifu, ambacho katika historia yote ya dunia hii kimewahi kufanywa na Mimi na Mama Yangu wa Mbinguni, na kile likichofanywa na Watakatifu wote, basi ni budi aingie katika Utashi wa Mungu. Ndani yake kuna kila kitu kikiwa katika utendaji wake. Wakati ule ulipokuwa unaliangalia na kulichunguza kila tendo, pale ulipokuwa unalikumbuka, ulipokuwa ukilitolea kwa Mungu, yule Mtakatifu aliyekuwa amelifanya tendo lile au aliyeifanya sadaka ile, alionja akiitwa na wewe mhujaji hata akaliona lile tendo lake likihuishwa tena na kutendeka upya duniani. Basi, alipoona hivyo aliongeza mara dufu kutoa Utukufu kwa Muumba Wake na kwake yeye mwenyewe. Na wewe uliyekuwa ukilitolea tendo hilo kwa Mungu, ulikuwa unajazwa na kufunikwa kwa umande wa mema yatokanayo na tendo lile takatifu. Na kutegemeana na nia au lengo unaloweka wakati wa kutolea, ndivyo utukufu utakavyozidi kuwa na nguvu na kuwa mkubwa, na ndivyo mema yanayozaliwa kutokana na tendo hilo, yatazidi kuwa mengi na makubwa pia. Ni utajiri mwingi ulioje uliopo ndani ya Utashi Wangu! Pale ndani yapo matendo Yangu yote, yapo matendo yote ya Malkia mwenye Mamlaka. Yote hayo yapo pale yakingojea yaitwe, yakumbukwe, na yatolewe na mtu kwa ajili ya kuongeza mara dufu mema yenye manufaa kwa wanadamu, na pia kuongeza kutoa mara dufu Utukufu Kwetu Sisi Utatu. Matendo hayo yote yanatamani yakumbukwe na yaitwe, ili yahuishwe na kufanya kazi yao tena kama Uhai mpya kati ya wanadamu. Lakini, kwa kukosekana umakini[1] , kuna wanadamu wanaokufa, wanaopata matatizo ya kudhoofika, wanaokufa kwa baridi, wanaokufa kwa njaa. Mema Yetu, Matendo na Sadaka Zetu, huwa hayatoki pale yalipo, kama hayajaitwa, kwani pale wanadamu wanapoyakumbuka na kuyatolea kwa Mungu ndipo wao wanajiandaa na kujiweka sawa kwa ajili ya kuyajua na kuyapokea yale mema yaliyopo ndani ya matendo hayo. Halafu, hapana Heshima iliyo kuu zaidi unayoweza ukaitoa kwa Mbingu nzima, isipokuwa ile ya kuwatolea matendo yao yale waliyokuwa wameyatenda hapa duniani, kwa lile lengo kubwa na Tukufu la Juu kabisa, yaani kwamba:

Kishapo, nikawa naendelea kuwaza juu ya Utashi wa Mungu, ndipo Yesu Wangu Mpendwa aliendelea kuniambia:

“Binti Yangu, matendo yote, iwe ni kitendo chochote kimoja - iwe ni sala fulani, iwe ni wazo, ni hisia ya upenzi, liwe ni neno - ili yote hayo yaweze kupokelewa, yaweze kuwa makamilifu, yaweze kupangiliwa, ili yaweze kutimia, ni budi kabisa yawe yanainuliwa na kuelekezwa kwenye lengo lile analolitaka Mungu Mwenyewe. Kwa kweli, kama mwanadamu, katika tendo lake, akijiinua na kujielekeza kwenye lengo lile linalotarajiwa na Yule aliye Juu, ndipo anapokumbatia mwanzo wa hilo tendo na anaingiza ndani yake lile lengo ambalo kwalo Mungu alikuwa amemuumba. Hapo, Mungu na mwanadamu wanashikana mikono pamoja, wanatarajia kitu kile kile, na aidha wanatekeleza kitu kile kwa pamoja. Kwa kufanya vile, mpango wa Mungu, tendo la Mungu, na lengo lile lile analotaka Mungu litimie katika tendo husika, hayo yote yanaingia mara ndani ya tendo la huyo mwanadamu. Kwa hiyo basi, mara pale lengo la Mungu linapoingia ndani ya tendo la mwanadamu, hilo tendo la mwanadamu, kwa lenyewe, linajifanya kuwa kamili na kamilifu, linatimilika na kuwa timilifu, linajifanya kuwa takatifu, linakuwa na mpangilio kamilifu. Lile tendo la mwanadamu litageuka kuwa ni la yule aliyeasisi lile lengo lake. Hata hivyo lakini, endapo mwanadamu hajiinui na kujielekeza kwenye lengo lililowekwa na Mungu kuhusu tendo lake, huyo mwanadamu anakuwa akiteremka chini kutoka ule mwanzo wa kuumbwa kwake na kwa hiyo hatakuwa akiuonja Uhai wa tendo la Kimungu ndani ya tendo lake. Anaweza akawa anatenda matendo mengi, lakini yatakuwa hayatimiliki, hayakamiliki, na hayana mpangilio. Yote yatakuwa ni kama matendo yanayokuwa yamepotea kutoka lengo la Muumba wake. Kwa hiyo basi, kitu ambacho kinatupendeza Sisi zaidi, ni kuona lengo Letu lile lile katika kila tendo la mwanadamu. Unaweza ukasema kwamba, mwanadamu kama huyo huwa anaendeleza Uhai Wetu Sisi hapa duniani, na anaendeleza Utashi Wetu tendaji katika matendo yake, katika maneno yake na katika kila kitu”. 


[1] lakini kwa vile hawachukulii umakini juu ya matendo haya yaliyo pale yakingojea yaitwe, yakumbukwe, yatolewe kwa Mungu na mwanadamu, kwa ajili ya kuzalisha mara dufu mema yenye kuleta manufaa kwa watu.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page