Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 15 - Mei 2, 1923🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 15 - Mei 2, 1923🖋📃📖📔


Ni siku ambapo nilikuwa nikionja akili yangu duni, ikiwa kana kwamba imepotea kabisa pale ndani ya ile bahari kuu ya Utashi wa Milele, na ndipo Yesu Wangu Mtamu, alirejea kwangu kuja kuzungumzia juu ya Utashi Mtukufu wa Mungu. Aliniambia hivi:

“Binti Yangu, lo! Ni jinsi gani hayo matendo yako uliyoyatekeleza ndani ya Utashi Wangu yanavyoendana vizuri kabisa. Tena yanaendana vizuri sana na matendo ya Kwangu Mimi, yanaendana na yale ya Mama Yangu Mpendwa, na kila tendo huingia na kupotea ndani ya lile jingine hata kutengeneza tendo moja tu pekee - inaonekana ni kama vile ni Mbingu ya hapa duniani na ni dunia ya kule Mbinguni. Na ni mwangwi wa mtu mmoja ndani ya wale Watatu na papo hapo ni mwangwi wa wale Watatu ndani ya huyu mmoja, yaani ndani ya Utatu Mtakatifu.  Lo, ni jinsi gani, unavyosikika utamu wa mwangwi huo hapa kwenye masikio Yetu. Ni jinsi gani unavyotuteka Sisi. Na unatuteka kwa nguvu sana, kiasi kwamba, unauteka hata Utashi Wetu kuja kutoka pale Mbinguni hadi kufika hapa duniani! Na pale ambapo hii Mapenzi Yako Yatimizwe ya Kwangu itakapofikia kupata utimilifu wake, iwe kule Mbinguni na kama hapa duniani, basi, ndipo utakapofika na ule utimilifu kamili wa ile sehemu ya pili ya sala ya Baba Yetu, yaani: utupe leo mkate wetu wa kila siku. 

Mimi nilikuwa nikisema kwa Baba: ’Ewe Baba Yetu, kwa jina la watu wote, Mimi ninakuomba utupatie kila siku aina tatu za mkate: ule mkate wa Utashi Wako, au tuseme, ni zaidi ya mkate, kwani, kama mkate huhitajika mara mbili au mara tatu kila siku, huu mkate ninaoomba ni wa lazima kwa kila nukta na kwa mazingira yote. Na hata zaidi,  lazima uwe siyo mkate tu, bali uwe ni kama hewa ya uponyaji ambayo inaleta uhai - yaani, uwe unaleta ule mzunguko wa Uhai wa Kimungu ndani ya mwanadamu. Ee Baba, kama huo mkate wa Utashi Wako hautatolewa, basi Mimi sitaweza kamwe kuyapokea yale matunda yote ya Uhai Wangu wa ki-Sakramenti, uhai ambao ndio mkate wa pili ambao huwa tunauomba Kwako kila siku. Lo! Ni jinsi gani Uhai Wangu wa ki-Sakramenti unavyojionja kukosa raha, kwa vile ule mkate wa Utashi Wako hauwalishi wale wanadamu. Kumbe kinyume chake, Uhai Wangu wa ki-Sakramenti unaukuta pale mkate ulioharibika wa utashi wa kibinadamu. Lo! Ni jinsi gani unavyonilete Mimi kinyaa! Ni jinsi gani ninavyoukimbia! Na ingawa kama huwa ninakwenda kwa wanadamu, hata hivyo, huwa siwezi kuwapatia yale matunda, siwezi kuwapa yale mema, yale matokeo, wala ule utakatifu, kwa vile huwa siwezi kuuona ule mkate Wetu pale ndani yao. Na ikitokea ninawapatia chochote, basi huwa ni kibaba kidogo sana kulingana na mitazamo yao, na wala siwapatii mema yote ninayokuwa ninayo ndani Yangu. Na uhai Wangu wa ki-Sakramenti upo ukimngojea kwa saburi sana yule binadamu akubali kutwaa ule mkate wa Utashi Mkuu wa Juu, ili kusudi, niweze hatimaye kutoa lile jema lote la Uhai Wangu wa ki-Sakramenti’.  

Basi unaweza kuona jinsi Sakramenti ya Ekaristi Takatifu - na wala siyo hiyo tu, bali hata Sakramenti zote, ambazo nililiachia Kanisa Langu na ambazo zilikuwa zimewekwa na Mimi Mwenyewe - zitakuja kutoa matunda yote yaliyomo pale ndani yao na zitakuja kutoa utimilifu wao kamili, pale tu ambapo Mkate Wetu, yaani, yale Mapenzi ya Mungu, yatakapokuwa yametimizwa hapa duniani kama kule Mbinguni.

Kishapo, nilikuwa nikiomba kupata ule mkate wa tatu - yaani ule mkate wa ngano. Kwani Mimi ningewezaje kusema: ’Utupe leo mkate wetu?’. Kama ukizingatia kwamba binadamu, alipopasika kutekeleza Utashi Wetu, chochote kilichokuwa ni cha Kwetu kilikuwa papo hapo ni cha kwake, na wala Baba hakupasika kutoa tena - ule Mkate wa Utashi Wake, ule Mkate wa Uhai Wangu wa ki-Sakramenti, na ule mkate wa kila siku wa uhai wa kawaida - kwa wale watoto haramu, watoto waporaji na wabaya, bali angepasika kutoa kwa wale watoto halali, watoto wema, ambao watayashikilia yale mema ya Baba katika ushirika wao. Kwa minajili hiyo, nilikuwa nikisema: ’Utupe mkate wetu’. Basi, hao watakuja kula ule mkate uliobarikiwa, na ndipo viumbe vyote yanavyowazunguka vitakuwa vinawachekelea kuwafurahia, na dunia na Mbingu vitaleta ule mhuri wa harmonia ya Muumba Wao.

Halafu, baada ya kitambo, nikawa nimeongezea kusema: ’Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea’. Kwa jinsi hiyo, hata upendo na ukarimu utakuja kuwa kamili. Ndivyo msamaha utakuwa kamili kwa kujipatia ule mhuri wa ushujaa - sawa kama ule msamaha niliokuwa nao Mimi pale Msalabani - pale binadamu atakapokuwa amekula ule mkate wa Utashi Wangu, yaani, ule mkate ambao Ubinadamu Wangu ulikuwa ukila. Hapo ndipo fadhila mbalimbali zitakuwa zimemezwa na kuingizwa ndani ya Utashi Wangu, na zote zitapokea ule mhuri wa ushujaa halisi, na ule mhuri wa fadhila za kimungu. Fadhila hizo zitakuja kuwa kama vijito vingi sana vinavyoibuka kutoka tumboni mwa ile bahari kuu ya Utashi Wangu.

Na halafu, kama Mimi niliongezea kusema: ’Usitutie katika kishawishi’.....hivi ingewezekanaje Mola aweze kumtia binadamu katika kishawishi? Ilikuwa ni kwa vile binadamu ni daima binadamu, na ni huru kabisa ndani yake mwenyewe - kwa vile Mimi huwa simwondolei kamwe zile haki nilizokuwa nimempatia wakati nilipomuumba - na yeye mwenyewe, anapokuwa ametishika mno na anapokuwa ameingiwa na hofu juu yake mwenyewe, huwa anapiga kelele za kimyakimya, na huwa anasali na kuomba bila kutoa maneno, huwa analia akisema: ’Utupe Mkate wa Utashi Wako, ili kusudi tuweze kuvifukuzia mbali vishawishi vyote, na kwa nguvu ya Mkate huo,  utuopoe na maovu yote. Amina’.

Basi, unaweza kuona kwamba, mema yote ya binadamu yanaweza kuvikuta tena vile vishina vyao, yanaweza kuviona vile vifungo imara vinavyoyabana kabisa, vifungo vya tumfanye mtu kwa mfano na sura Yetu. Mema yote hupata tena ule uhalali wa kila tendo lao, hupata marejesho ya yale mema yaliyokuwa yamepotea, hupata na sahihi ya uthibitisho na bima yao kwamba ile heri yao ya duniani na mbinguni, iliyokuwa imepotea, itakuja kurejeshwa kwa mtu husika. Ndiyo maana, ilikuwa ni lazima kabisa kwamba, Mapenzi Yangu yatimizwe hapa duniani kama kule Mbinguni, kwamba Mimi sikuwa na mpango Wangu mwingine, na wala Mimi sikufundisha sala nyingine, isipokuwa hii Baba Yetu. Na Kanisa, mtekelezaji mwaminifu na mhifadhi mwaminifu wa mafundisho Yangu limekuwa na sala hiyo daima mdomoni pake, katika mazingira yote, na watu wake wote, wasomi na wasiosoma, wadogo na wakubwa, wakleri na walei, wafalme na raia, wote huwa wananiomba kwamba huu Utashi Wangu utimizwe hapa duniani kama kule Mbinguni.

Je, kwani wewe hupendi kwamba Utashi Wangu ushuke kuja hapa duniani? Lakini, kama vile Ukombozi ulivyokuwa na mwanzo wake ndani ya Bikira - kwa vile Mimi sikutungwa mimba ndani ya watu wote ili kuwakomboa, hata kama yeyote yule anayeutaka ukombozi, anaweza akaingiza ile faida ya Ukombozi, na kwamba, katika Sakramenti, yeyote yule anaweza akanipokea Mimi kwa ajili yake mwenyewe - hali kadhalika, sasa, Utashi Wangu budi uwe na mwanzo wake, uwe na hati miliki, uwe na makuzi yake na maendeleo yake ndani ya mwanadamu mmoja bikira. Kishapo, Yeyote yule anayejiweka sawa na anayetaka, anaweza akayatwaa na kuyaingiza ndani yake mwenyewe, yale mema yatokanayo na kule kuishi ndani ya Utashi Wangu. Kama Mimi nisingekuwa nimetungwa mimba katika tumbo la Mama Yangu mpendwa, kamwe Ukombozi usingeweza kufika. Hali kadhalika, kama Mimi sitatenda ule muujiza wa kumfanya mtu mmoja aishi ndani ya Utashi Wangu Mkuu wa Juu, basi, ile Mapenzi Yako yatimizwe duniani kama Mbinguni, haitaweza kamwe kutokea katika vizazi vyote vya binadamu.

Juzuu na. 15 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here



Report Page