Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 21 - Machi 31, 1927🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 21 - Machi 31, 1927🖋📃📖📔


Nilikuwa nimezama kabisa, nimeachwa peke yangu katika Utashi wa Mungu, na nikawa nikifuatilia matendo yangu ndani ya huo Utashi. Yesu Wangu Mtamu alikuja ndani mwangu na kusema:

“Binti Yangu, mtu anayeishi katika Utashi Wangu wa kimungu, huyo ni ushindi wa Utashi huo. Kama vile mtu anapofanya matendo yake ndani ya Utashi, ndivyo na Utashi Wangu huwa unatoa nje nguvu na uwezo Wake wa kuwepo mahali mbalimbali kwa wakati mmoja, na kwa nguvu hiyo hupita ukiruka juu ya Uumbwa wote na kusambaza Uhai Wake wa kimungu. Utashi Wangu huwa anampatia fursa ya kugawia Uhai Wangu kwa matendo yale yote anayotenda huyo mtu ndani ya Utashi. Kwa hiyo, huo siyo tu ni ushindi wa Utashi Wangu, bali Utashi unapata Heshima kubwa zaidi toka kwa huyo mtu anayefanya matendo ndani yake kuliko unavyopata toka kwa Uumbwa wote kijumla. Ni hivyo kwa vile ndani ya kila kitu kilichoumbwa, Mwenyezi, wakati alipokuwa akikiumba, aliweka ndani ya kimoja, kivuli cha mwanga Wake, ndani ya kingine kaweka noti za musiki wa Pendo Lake, ndani ya kitu kingine tena aliweka mfano wa uwezo na nguvu Zake, na katika vingine aliweka mapambo na urembo wa uzuri Wake. Kwa jinsi hiyo, wakati kila kitu kilichoumbwa kinashika ndani yake jambo fulani lililo ni la Muumba Wake, lakini katika mtu anayeishi ndani ya FIAT ya kimungu, Muumba anajiweka Yeye Mwenyewe mzima, anajaza ndani hapo Uwepo Wake wote. Kwa nguvu Yake ya kuwepo mahali mbalimbali kwa wakati moja, Mwenyezi anaujaza Uumbwa wote kwa matendo yale yanayofanywa na mtu huyo katika Utashi Wake Mungu. Kwa namna hiyo, kutoka kwa mtu huyo Mungu anapokea upendo, utukufu, uabudu kwa niaba ya kila kitu kilichokuwa kimetoka katika Mikono Yetu ya uumbaji. Kwa minajili hiyo, mtu anayeishi katika Utashi wa Mungu huingia katika mahusiano na vitu vyote vilivyoumbwa. Halafu mtu huchukua moyoni mwake ile Heshima ya Muumba Wake pamoja na mahusiano yale anayoyapata kwa niaba ya kila kitu kilichoumbwa toka kile kidogo kabisa hadi kile kikubwa kabisa, na mwishowe anapeleka na kufikisha mambo yote kwa viumbe akibadilisha na yale aliyopeleka kwa Muumba. Ndiyo sababu mahusiano yote kati ya mtu na Mungu huwa sasa yamefunguliwa na ni wazi. Mtu anaingia katika mfumo wa kimungu na anaanza kufaidi utulivu na uelewano kamili na Yule aliye Mkuu wa Juu. Huo ndio ushindi halisi wa Utashi Wangu.

Kinyume chake, mtu yule asiyeishi katika Utashi wa Mungu, huwa anaishi katika utashi wa kibinadamu, na kwa hiyo mawasiliano yake yote na Yule aliye Mkuu wa Juu huwa yamefungwa. Mambo yote kwake ni fujo na vurugu na migongano na kutoelewana. Mtu huyu ana mahusiano na tamaa zake, na anaelekeza matendo yake kwenye tamaa. Haelewi lolote wala hashughulikii taarifa mintarafu Muumba Wake; anabaki akitambaa na kujiburuza ardhini vibaya zaidi kuliko nyoka, na anaishi katika vurugu za mambo ya kibinadamu tu. Kwa hiyo, mtu anayeishi kwa utashi wake wa kibinadamu ni kashifa ya Utashi Wangu, na ndiyo kushindwa kwa FIAT ya kimungu katika kazi Yake ya kuumba. Ni Teso lilioje Binti Yangu! Ni Teso lilioje kuona kuwa utashi wa kibinadamu unataka kusababisha na kushuhudia Utashi wa Muumba Wake ukishindwa, Muumba wake anayempenda mno, na ambaye katika ushindi wake bado anataka ushindi wa mwanadamu huyo huyo!”.

Halafu kukafika kipindi nikawa namnung’unikia Yesu kwa tendo la kuniacha wakati fulani fulani kama kipindi hiki. Nafikiri haijawahi kutokea hapo kabla kwamba kaniacha nionje umbali Wake zaidi ya safari hii. Lakini papo hapo anasema eti ananipenda! Nani ajuaye kama hatafikia kuniacha kabisa? Kumbe lakini nilipokuwa nikiwaza hivyo, Yesu Wangu Mtamu alikuja ndani mwangu. Huku akinizungushia mwanga, na katika mwanga huo aliniwezesha kushuhudia vita na mapigano mbalimbali makali ya kiraia dhidi ya wakatoliki. Walionekana watu wa rangi zote wakipigana na wote wakiwa katika hatua ya kujiandaa kwa ajili ya vita nyinginezo. Hapo Yesu aliyevunjika Moyo kwa Mateso aliniambia:

“Binti Yangu, wewe hujui bado jinsi Moyo Wangu unaoungua upendo, unavyotaka kukimbia na Pendo kwenda kufuata wanadamu. Lakini, wakati Moyo huo unapokimbilia kwao, wanadamu wanaugomea na kuusukumia mbali. Badala yake wanakimbilia wao kwangu Mimi, huku wakiwa na makosa machafu mno, na wakiwa pia na udanganyifu na maigizo ya kutisha mno. Ninaposhuhudia Pendo Langu likidhulumiwa na kuhujumiwa namna ile, Haki Yangu hujitokeza mara moja kuja nje uwanjani ili kutetea Pendo Langu. Kwa mijeledi, Haki inawachapa wale ambao wananihujumu. Inafuatilia na kuzigundua hizo hujuma, na inashambulia kila aina ya mazingizio na maigizo wanayotenda, siyo dhidi ya Mimi tu, bali hata wanayotendeana wenyewe kati ya matataifa. Kwa kudanganyana wenyewe wanafikia kuona kuwa badala ya wao kupendana, wanamalizikia kuchukiana vichafu sana. Karne hii mtu anaweza akaiita ni karne ya udanganyifu na maigizo machafu mno. Kwa kweli, kati ya matabaka yote ya watu kunatendeka njama za kuanzisha vita mpya. Kwa sababu hiyo, hawapatani wala kukubaliana kati yao ingawa kama pengine kwa nje huonekana kana kwamba wanataka wapatane. Udanganyifu na maigizo hayajawahi kuleta kamwe faida ya kweli, iwe katika uwanja wa kiraia na hata katika auwanja wa kidini. Ikiwa bahati sana, panaweza kutokea tu kivuli cha faida ya mpito. Kwa sasa, amani ya mdomo wanayoisifia, ambayo si amani ya kweli na ya matendo. Kwa kweli, wanaigeuza na kutumia kama maandalizi kwa vita.

Kama unavyoweza kuona tayari makundi mengi ya watu wa rangi mbali mbali wameungana ili kupigana, huyu kwa kizingizio hiki, yule kwa kizingizio kile. Na wengine zaidi wataungana pamoja bado. Lakini mimi nitatumia huo ushirika mbalimbali wa mataifa hayo ya rangi mbalimbali. Ni kwa vile, kwa minajili ya ujio wa Ufalme wa Utashi Wangu wa kimungu, ni budi ufike muungano au ushirika wa mataifa yote kwa njia ya vita nyingine itakayoenea zaidi kupita vita ile ya mara ya mwisho ambamo Italia ilihusika kwa pesa yake. Kwa njia ya umoja au ushirikiano au muungano wa mataifa hayo, watu watafahamiana na hivyo baada ya vita itakuwa rahisi zaidi kueneza Ufalme wa Utashi Wangu. Basi, uwe na subira katika kuvumilia kipindi hiki ambapo Mimi sionekani na sifiki kwako. Na pia uvumilie ombwe ambalo Haki yangu inataka kutengeneza kwa ajili ya kutetea Pendo Langu lililohujumiwa. Wewe usali na utolee yote ili Ufalme wa FIAT Yangu ufike haraka”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page