Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 11 - Mei 25, 1916🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 11 - Mei 25, 1916🖋📄📖📔


Wakati nikiendelea katika hali yangu ya siku zote, nilikuwa nimejaa maumivu kabisa, hasa kwa vile katika siku za karibuni Yesu Mbarikiwa alikuwa amenionyesha jinsi maaskari wapiganaji wa mataifa mageni walivyokuwa wakiishambulia Italia, mauaji makubwa ya maaskari wetu, na yale mabwawa ya damu, ambayo hata Yesu Mwenyewe alikuwa ametishika sana kuyatazama. Nilikuwa naonja moyo wangu duni ukipasuka kwa uchungu. Basi nilimwambia Yesu: ‘Okoa ndugu zangu kutoka bwawa hili la damu. Ni sura na mfano Wako. Usiruhusu hata roho mojawapo itumbukie motoni’. Na kwa kutambua kuwa Hukumu ya Haki ya Mungu itaendelea kuwasha hasira Yake zaidi na zaidi dhidi ya masikini wanadamu, mimi nilikuwa nikionja kuwa ninakufa. Ili kutaka kuniondoa katika fikra hizo zinazotisha sana, Yesu aliniambia:

“Binti Yangu, pendo ambalo kwalo huwa nawapenda watu, ni kali hivi kwamba, mara mtu anapoamua tu kujitoa nafsi yake Kwangu, Mimi huwa ninamjia na kumzungushia neema nyingi mno, ninampapasa, ninamshitua, ninamnyakua, na ninamjaza kwa neema nyingi zionekanazo na zinazoonjeka, namjaza upendeleo, namjaza uangazo na ninaukumbatia moyo wake.

Kwa hiyo, yeye anapojitambua kuwa amejazwa neema nyingi vile, mtu huanza kunipenda Mimi, anatengeneza msingi wa sala mbalimbali na mazoezi mbalimbali ya uchaji na ibada ndani ya moyo wake, na anaanza kuzitekeleza fadhila fulani fulani. Hayo yote yanatengeneza namna ya bustani yenye maua ndani ya roho ya mtu. Pendo Langu lakini, huwa haliridhiki kwa hayo maua tu kwani linataka kuona matunda.

Basi roho hiyo huanza kuangusha chini maua yaliyopo – yaani, inauondoa polepole ule upendo wa vionjo, inauondoa upendo wa hamaki, upendo wa mambo mengine yote – ili kuruhusu matunda yaanze kuzaliwa. Kama mtu ni mwaminifu, yeye huendelea na mazoezi yake, na fadhila zake, anaacha kabisa kuchuchumia mambo ya kibinadamu, anaacha kujifikiria yeye mwenyewe, anabaki kunifikiria Mimi pekee. Kwa imani yake juu Yangu Mimi, huyu mtu anakuwa akitoa utamu na ladha kwa matunda, kwa uaminifu wake atayawezesha matunda kukomaa. Na kwa ujasiri wake, uvumilivu wake, utulivu wake, matunda yake yanakua na kutajirika sana.

Na Mimi, niliye ndiye Mkulima Mkuu wa Mbinguni, nitakuwa ninayachuma matunda haya na kuyafanya yawe ni lishe Yangu, nitapanda shamba lingine, shamba lenye rutuba na udongo mzuri zaidi, ambamo, matunda ya kijasiri zaidi yatasitawi hata kuweza kuvuta toka Moyoni Mwangu neema nyingi sana za ziada ambazo hazijawahi kusikika.

Lakini kama mtu huyo siyo mwaminifu, na haaminiki, kama hatulii, kama ana tamaa za mambo ya kibinadamu, nk., matunda haya, kwa kawaida, hayatakomaa wala kuiva. Badala yake yanakuwa mabichi, machachu, machungu, yamechafuka na matope. Hayo yatakuwa yakiniletea Mimi uchungu na uchachu zaidi. Yatanifanya Mimi niwe ninamwepuka mtu huyo na hivyo kujitenga naye”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page