Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Agosti 6, 1922🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Agosti 6, 1922🖋📃📖📔


Nilijikuta nimezama katika kina cha Utashi Mtakatifu wa Mungu, na ndipo Yesu Wangu Mtamu alikuja na kuniambia:

“Binti Yangu, Kwangu Mimi, vitu vyote vina uzito ulio sawa. Mbingu ina uzito ule ule sawa kama ilivyo dunia. Utashi Wangu Mimi unabeba mizani kamilifu ya uuwiano. Uuwiano huleta mpangilio na taratibu, huleta utawala, huleta mambo yafaayo na huleta harmonia. Mambo yote, kwa pamoja, yanaingia katika harmonia kana kwamba pangekuwa na kitu kimoja. Na mpangilio na utaratibu huleta usawa, na usawa huleta ufanano. Ndiyo maana unaweza kuona harmonia kubwa, mpangilio na taratibu na ufanano ndani ya Nafsi Tatu za Mungu. Na vitu vyote vilivyoumbwa vipo katika harmonia kamili: kitu kimoja huwa ni tegemezo, nguvu na uhai wa kitu cha pili. Kama kitu kimoja pekee kilichoumbwa kingevunja harmonia, vitu vyote vingine vingevunjika na vingeharibika kabisa. Ni binadamu peke yake ndiye aliyejing’oa toka Kwetu, na toka kwenye mizani ya uuwiano ya Utashi Wetu. Oh, ni jinsi gani alivyovunjikana binadamu, na kutoka mahali pake kule juu kabisa, akaporomokea kilindini mwa lile shimo kuu! Na hata kwa ule Ukombozi Wangu wote, siyo familia nzima ya binadamu imeweza kurejea kwenye hali yake ile ya mwanzoni. Hiyo inaonyesha kwamba, jambo lililo kubwa zaidi ni kuwa binadamu alikuwa amejiondoa toka kwenye mizani ya uuwiano ya Utashi Wetu, na hii ina maana ya kujibwaga ndani ya vurumai, ndani ya vurugu, ndani ya genge la maovu yote.

Sasa, Binti Yangu, ni kwa minajili hiyo Mimi nimekuita wewe, kwa namna ya pekee, uingie katika mizani hiyo ya uuwiano ya Utashi Wangu, ili, kwa wewe kuishi ndani yake, ufikie kuwa mizani ya utendaji wote wa kizazi cha binadamu kilichovurugika. Kwa kuishi ndani ya Utashi Wangu, utakuwa ni mizani kwako wewe mwenyewe, utasimama katika mpangilio na katika harmonia kamili kabisa kati Yetu Sisi na vitu vyote vilivyoumbwa na Sisi. Kwa jinsi hiyo, wakati utakapokuwa unaleta harmonia kwa kila jambo, Sisi tutakuwa tukikuonja wewe ukitiririka ndani ya anga la Utashi Wetu, ukipita kutupatia mpangilio, na harmonia ya akili zote, ya maneno yote, ya kazi zote, na ya hatua zote za watu wote. Matendo yako ndani ya Utashi Wetu, Sisi tutayaweka yawe ni matendo tawala juu ya matendo mengine yote ya watu wote. Na hivyo tutarekebisha lile vurumai ya kizazi cha binadamu kilichokuwa kimeingia katika mkasa. Kila moja ya matendo yako wewe yatakuwa ndiyo alama ya mpangilio tutakaokuwa tunapokea kwa niaba ya watu wengine wote. Ndani ya Utashi Wetu, wewe unayo mambo mengi sana ya kutekeleza. Utakuwa kama Malkia atakayekuwa anatuletea Sisi matunda yote ya ushindi wetu na harmonia zetu zote. Utashi Wetu utakuwa unakuletea wewe kila kitu kilicho cha lazima ili wewe uweze kulipa fidia za watu wote mbele Yetu Sisi, ili wewe uweze kujaza ile ombwe ya mizani iliyoletwa na utashi wa kibinadamu. Utashi uliokuwa umeathirika kabisa kabisa pale ulipojiondoa kutoka kwenye mizani ya uuwiano iliyopo katika Utashi Wetu”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page