Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 25 - Machi 3, 1929🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 25 - Machi 3, 1929🖋📃📖📔


Mimi nikawa ninaendelea na ziara yangu pale ndani ya FIAT ya Kimungu. Nilifika na kusimama kidogo pale Eden, na hapo nikawa ninauabudu ule Utashi Mkuu wa Juu katika lile tendo la kumwumba binadamu. Nilifanya tendo hilo ili mimi mwenyewe nijiunge na ule muungano wa tashi uliokuwepo kati ya Muumba na binadamu wakati ule mwanadamu alipoumbwa. Naye Yesu, Chema Changu Kikuu, alipoingia pale ndani mwangu aliniambia hivi: 

“Binti Yangu, uumbaji wa binadamu ndio uliokuwa mzuri na wa kupendeza mno. 

Ulikuwa ndilo tendo adhimu mno kupita yote katika Uumbwa wote. Katika ujazo wote wa ule motomoto wa Pendo Letu umbaji, FIAT Yetu iliviumba viumbe vingine vyote pale ndani ya Adamu, ilibaki ikiendelea na lile tendo la kuumba na kuupyaisha ndani ya kila mwanadamu kile ambacho Sisi tulikuwa tumekitenda ndani ya yule binadamu wa kwanza. 

Na kwa kweli, ilipasika wazao wake wote wajipatie chanzo chao kutoka kwake yeye. 

Kwa hiyo, Utashi Wetu wa Kimungu uliazimia kuchukua jukumu, kwamba, kadiri wanadamu walivyokuwa wakizaliwa, Wenyewe ulikuwa unaupyaisha yale mafuriko ya Pendo Letu, ulikuwa unaleta nje sifa na maweza Yetu yote ya Kimungu, na pia ulikuwa unaandaa maonyesho mapya ya mambo mazuri yapendezayo, maonyesho ya neema mbalimbali, ya utakatifu, na ya Pendo Letu juu ya kila mmoja wa wanadamu. 

Kwa sababu hiyo, ilitakiwa kila mwanadamu awe ni sherehe mpya kwa ajili Yetu Sisi - yaani kila mwanadamu alikuwa ndiye aliyejitokeza vema zaidi, ndiye aliyekaribishwa, na alikuwa ndiye nyongeza mpya ya furaha katika Familia ya Mbinguni.  

Lo! Ni jinsi gani ile FIAT Yetu ya Kimungu ilivyokuwa ikishangilia inapoingia katika lile tendo la kutoa daima kwa mwanadamu, na lile tendo la kuupyaisha ule utukufu, ukuu, adhama na ule ustadi usiopitwa na yeyote, ustadi ambao ilikuwa inauonyesha juu ya kila mwanadamu.

Lakini, kwa vile Adamu kaasi, akatoka na kwenda nje ya Utashi Wetu wa Kimungu, wale wazao wake wakawa wamepoteza ile njia ya kulifikia lile tendo la kwanza la uumbaji wa binadamu. 

Na hata hivyo, Utashi Wetu wa Kimungu haujasitisha mpango wake. Ni kwa sababu, Sisi tunapoamua kutekeleza tendo fulani, hapo hakuna mtu anayeweza akatubadilisha. Na kwa hiyo, Utashi Wetu huwa unabaki katika kutekeleza zoezi la kuupyaisha yale maajabu ya Uumbaji - lakini, licha ya hilo, kwa sikitiko, huwa haumpati yeyote wa kuweza kumshushia hayo mambo mapya. 

Ndipo Utashi huwa unasubiri kwa uthabiti wa kimungu na kwa saburi hata mwanadamu atakaporejea tena ndani kwenye Utashi. 

Hapo Utashi utaweza kurudia tena lile tendo Lake, na utabaki katika utendaji Wake, yaani, utendaji wa kurudia kile ambacho ulikuwa umetenda wakati wa kumwumba binadamu. 

Na muda huo wote, unapokuwa unamngojea kila mtu, ndipo huwa linamkuta tu yule Binti Yake Mdogo, yule Mzaliwa Mpya wa Utashi Wangu wa Kimungu, ambaye, kila siku, huwa anaingia pale ndani kwenye lile tendo la kwanza la kuumbwa binadamu, yaani, katika muda ule ambapo Nafsi Yetu ya Kimungu, ilifanya yale maonyesho ya sifa na maweza Yetu yote ya Kimungu, kwa ajili ya kumfanya binadamu awe ndiye mfalme mdogo na awe mtoto Wetu asiyeweza kutenganika, na ndipo pale tulipomremba huyo binadamu kwa zile sare Zetu zote za Kimungu, ili kusudi, watu wote waweze kumtambua na kumkiri kuwa ndiye muujiza mkuu kabisa wa lile Pendo Letu.

Binti Yangu, laiti kama ungefahamu ni kwa pendo kuu gani Utashi Wangu unavyokungojea wewe, unavyokungojea wewe ufike kufanya kila siku yale matembezi yako mafupi pale ndani ya bustani ya Eden, pale ambapo FIAT Yetu, ilipokuwa imechukuliwa na ule msukumo wa Pendo, ilipokuwa inachukua mtazamo wa kisherehe, kwa ajili ya kumuumba binadamu….. 

Lo! ni matendo mengi mangapi ambayo FIAT inaendelea kuyafungilia na kuyazuia pale ndani Mwake. 

Ni mitweto mingi mingapi ya pendo inayobanwa pale ndani Mwake. 

Ni furaha nyingi ngapi zinazobebwa pale ndani Mwake. 

Ni mambo mengi mazuri mangapi yaliyofungiliwa pale ndani Mwake. 

Yamefungiliwa pale kwa vile hakuna mtu anayediriki kuingi pale ndani ya lile tendo Lake la uumbaji ili kutwaa yale mema mengi yasiyowahi kusikika, ambayo, Utashi unataka kuyatoa kwa wanadamu. 

Na mara, unapokuona wewe, ambaye, katika Utashi Wake Wenyewe, unayo ile njia ya kufikia kwenye lile tendo la kumwumba binadamu - Lo! ni jinsi gani, unavyoanza kushangilia huo Utashi! 

Na jinsi gani unavyoonja kuvutiwa, mithili ya sumaku kali, kujaribu wenyewe kujitambulisha hata uweze kujulikana kwa wanadamu, ili kusudi, kwa kuufanya Utashi Wangu wa Kimungu utawale kati yao wanadamu, wao hao waweze kuipata njia ya kufikia lile tendo la kwanza la uumbaji wa binadamu, ili kusudi, Utashi usiweze tena kuendelea kushikilia na kubana ndani Yake, yale mema unayotaka kuyatoa na kuwapatia wanadamu.  

Lo! laiti kama wanadamu wangejua ni matendo mengi mangapi mapya ya uumbaji, kila moja likiwa ni zuri zaidi kuliko lile lingine, kama wangejua matendo mengi mangapi ambayo FIAT Yangu ya Kimungu inatarajia kutengeneza na kuyatoa kutoka pale ndani Mwake na tayari kuyamwaga juu ya kila mmoja wao - lo! hakika ni jinsi gani wangekuwa wanaharakisha kwenda kuingia pale ndani ya huo Utashi Wangu wa Kimungu kwa ajili ya kuanza mara kuendesha uhai wao pale ndani Yake na ili kuanza mara kuyapata yale mema Yake yasiyo na ukomo”.

Halafu mimi nikawa naendelea kufuatilia ule Utashi Mtakatifu wa Kimungu, na nikawa ninawaza moyoni mwangu: 

‘Je ni kweli kwamba mimi hapa ninaibeba hii FIAT iliyo ni takatifu kiasi hicho? Ni kweli kabisa kwamba mimi ninajihisi kwamba sina uwezo tena wa kutaka au kutamani chochote kile kingine, na kwamba hiyo FIAT inafurika kama bahari kuu, bahari pale ndani na pale nje ya nafsi yangu, bahari inayonifunika gubigubi kabisa ndani ya hiyo FIAT ya Kimungu, na ninajihisi kwamba vitu vingine vyote si mali yangu tena. Hata hivyo, lakini, ni nani ajuaye kwamba kweli mimi ninayo hiyo FIAT!’. 

Lakini, pindi nilipokuwa nikiwaza juu ya jambo hilo, Yesu Wangu Mpendwa aliongeza kusema:

“Binti Yangu, alama kwamba mtu anao Utashi Wangu huwa ni kule kujihisi kuwa yeye ni mtawala wa nafsi yake mwenyewe, kwa jinsi kwamba, matamaa yake huwa hayathubutu kujiingiza mbele ya ule mwanga wa FIAT Yangu. 

Matamaa yanajionja kukosa nguvu yoyote ile ya kutenda kitu kana kwamba yanakosa uhai kabisa. Na kwa kweli, Nguvu na Utakatifu wa Utashi Wangu huwa vinatwanga na kubomoa kila kitu. 

Na juu ya yale makuruhu yenyewe yote ya utashi wa kibinadamu, FIAT huwa inatandaza ule Mwanga Wake, ule Utakatifu Wake, na yale mauamaua Yake mazuri kabisa, kwa jinsi kwamba, kwa namna ya kushangaza kabisa, inageuza adha zenyewe zote kuwa ni ardhi yenye rutuba na nguvu ya kuzalisha na yenye heri, kuwa ni ardhi isiyoweza kuzaa miba tena, bali, inayozalisha maua ya kimbingu, na inayozalisha matunda matamu na yaliyokomaa. 

Na himaya ya huyo mwanadamu aliyebahatika, huwa ni kubwa hivi kwamba, mwenyewe hujihisi kuwa anammiliki hata Mungu Mwenyewe, anamiliki wanadamu na anamiliki vitu vyote vilivyokwisha kuumbwa. 

Huyo huwa ana nguvu ya kuvutia watu, kwa jinsi kwamba, yeyote yule aliyebahatika kumjua, huwa anajihisi kulazimika mno kufungamana naye, kwa jinsi kwamba, hushindwa kabisa kutoka na kwenda mbali naye. 

Ni ile nguvu ya FIAT Yangu, ambayo, ikiwa imefungiliwa pale ndani yake mtu husika, huwa inamvutia Mungu, ambaye, huanza kuona furaha kabisa kubakia amefungiliwa pale ndani yake. 

Pia FIAT inavutia wanadamu, kwa vile, huwa wanayaonja yale marashi ya uponyaji ya FIAT Yangu ya Kimungu, marashi ambayo huwa yanawaletea amani ya kweli na mema ya kweli pale katika mioyo yao. 

Watu wengine wangefanya nini ili kuweza kujipatia angalau neno moja tu kutoka kwako wewe, neno ambalo, mithili ya uhai, lingeteremka na kuingia katika mioyo yao? 

Kwa hiyo basi, uwe makini sana, na uwe unaendelea daima na hiyo ziara yako hapo ndani ya Utashi Wangu wa Kimungu”.

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

 

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

⬇️⬇️⬇️

Swahili - Telegram Channel: click here Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

English - Telegram Channel: click here Divine Will Divine Love

Français - Chaîne Telegram: click here Divine Volonte Divin Amour

Lingala - Chaîne Telegram: click here Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe


Report Page