Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Septemba 27, 1922🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Septemba 27, 1922🖋📃📖📔


Nikawa napata mateso makali kweli kweli kutokana na kumkosa Yesu Wangu Mtamu, na maumivu yalikuwa makali hivi hata nikafikia kutamka mambo ya upuuziupuuzi, hadi kufikia kusema kuwa Yeye hanipendi mimi, kwamba alikuwa hanitaki tena, na kwamba mimi ndiye niliyekuwa ninampenda zaidi. Ya kwamba, ni kweli kuwa pendo langu ni dogo, yaani ni kivuli tu, ni kitone tu, ni kasenti tu. Ni kwa vile nafsi yangu mimi imetengenezwa hivi kwa jinsi kwamba ni finyu, ni ndogo, lakini, licha ya udogo wake huo, nafsi nzima ni kwa ajili tu ya kumpenda.......Kwani lakini atakuwa nani mwenye kueleza ujinga wote niliokuwa nikisema? Ilikuwa ni ile homa kali iliyotokana na kukosekana Kwake ndiyo iliyonifanya niwe ninazungumza upuuzi ule wote. Halafu, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu, yule Yesu Wangu Mtamu alinijia na akaniambia: “Binti Yangu, Mimi nataka nione kama unanipenda zaidi”.

Wakati akisema hilo, kiwiliwili cha Yesu kikawa kinajirudufu, kwa jinsi kwamba nikawa nikimwona Yesu upande wa kulia, Yesu upande wa kushoto, na Yesu moyoni mwangu. Hapakuwa tena na sehemu yoyote ya nafsi yangu au kona yoyote ambamo sikuweza kumwona Yesu. Na hawa ma-Yesu wote wakawa wakisema kwa pamoja: ‘Ninakupenda, ninakupenda”. Hata hivyo, hilo halikuwa ni chochote. Kwa vile Yesu anabeba maweza ya kiuumbaji, viumbe vyote vikawa vikirudia kwa pamoja kusema: ‘Ninakupenda’. Mbingu na dunia, wanaosafiri bado duniani na roho zote zenye heri, wote kwa pamoja, kama kwaya moja, na kama vile mwangwi mmoja tu, wakawa wanarudia kusema: ‘Sisi tunakupenda sawa kwa pendo lile analokupendea Yesu’. Mimi nilibaki nimeduwaa na kuvurugika mbele ya pendo hilo kubwa. Ndipo Yesu akaongeza kusema:

 “Ebu sema, na urudie kusema kuwa Unanipenda zaidi! Ebu ujirudufu mwenyewe ili uweze kunipa Mimi pendo kubwa kulingana na hilo ninalokupatia wewe!”.

Hapo mimi nikasema: ‘Ewe Yesu Wangu, unisamehe, mimi sijui namna ya kujirudufu, mimi sina maweza hayo ya kiuumbaji, na kwa hiyo, sina lolote chini ya uwezo wangu. Nitawezaje kukupatia Wewe pendo kubwa kama lile unalonipatia mimi? Hata mimi mwenyewe ninafahamu kuwa pendo langu ni kivuli tu mbele ya Pendo Lako, lakini yale maumivu ya kukosekana Kwako, ndilo linalonipatia mahangaiko na ndilo linanifanya niwe nikizungumza ujinga mwingi. Kwa hiyo basi, nakuomba usiniache tena peke yangu bila Wewe, kama hutaki mimi niwe ninazungumza ujinga’. Na Yesu, huku akikatisha mazungumzo yangu, aliongeza kusema:

“Ah, Binti Yangu, wewe hujatambua bado Mimi sasa hivi nipo katika hali gani ya mapigano! Pendo Langu linanisukuma sana hata linanifanyia ukatili kunilazimisha Mimi nifike kwako. Hukumu Yangu ya Haki karibu ingenikataza, kwa vile binadamu sasa anafikia maovu kupindukia, na wala asingestahili tena kupata ile huruma ambayo inatiririka juu yao wakati ule ninapokuja kwako na wakati ninapokushirikisha wewe yale maumivu Yangu, ambayo wao wenyewe wamenibebesha. Ni budi ujue kuwa wakuu wa mataifa mbalimbali wapo wakifanya njama za maovu dhidi ya Kanisa Langu. Na ili waweze kutekeleza nia yao hiyo, wao wanataka kutumia msaada wa nguvu za kigeni toka nje. Inatisha kweli, Dakika ambapo dunia imefikia. Basi uwe unasali sana na uwe na subira”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page