Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 14 - Novemba 20, 1922🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 14 - Novemba 20, 1922🖋📄📖📔


Nilikuwa nikitafakari jinsi Yesu Wangu Mtamu, alipokuwa pale Bustanini, alivyoyakabili maumivu mengi kabisa, lakini, siyo hasa kutoka kwa upande wa wanadamu, kwa vile pale alikuwa peke Yake, na kwa kweli alikuwa ameachwa na watu wote, bali aliyakabili kutoka upande wa Baba Yake wa Milele. 

Palikuwa na mikondo ya Pendo kati Yake Mwenyewe na Baba wa Mbinguni. 

Na wanadamu wote, walikuwa wameingizwa ndani ya mikondo ile, ambayo, ndanimo mlikuwa na Pendo lote la Mungu kwa ajili ya kila mmoja wao, na pia kulikuwa na pendo lile lote ambalo kila mmoja wa wanadamu alikuwa akimwia Mungu. Na kwa vile pendo hilo lilikosekana, Yeye alifikia hatua ya kuteseka na kuyakabili maumivu kama hayo yaliyokuwa makali kushinda maumivu mengine yote, na aliteseka hadi kufikia kutoa jasho la Damu hai. 

Ndipo Yesu Wangu Mtamu alinishika na kunibana kwenye Moyo Wake akitafuta kitulizo na huku akawa ananiambia:

“Binti Yangu, maumivu ya Pendo ndiyo yanayoumiza na kutesa kupita yote. Angalia na uone hapa ndani ya mikondo hii ya Pendo kati Yangu na Baba Yangu lipo pendo lote lile ambalo wanadamu waliniwia Mimi, na kwa hiyo ni pendo lililosalitika, pendo lililokataliwa, pendo lisilojulikana, pendo lililokanyagwa, nk.. Oh! Ni jinsi gani linavyouchoma Moyo Wangu, linanichoma hadi naonja Mwenyewe ninakufa.

Uelewe ya kwamba, pale nilipomwumba binadamu, nilikuwa nimeweka mikondo mingi ya pendo kati Yangu Mimi naye binadamu. 

Ya kwamba nilimwumba binadamu, Kwangu Mimi haikutosha, hapana. Nilihitaji bado kuweka mikondo mingi ya pendo kiasi kile kati Yangu na yeye, kwa jinsi kwamba, pasingalikuwepo na kiungo chake chochote ambamo mikondo hiyo isingetiririka. 

Yaani, katika nguvu ya uelewa wa binadamu kulipita ukikimbia mkondo wa pendo wa hekima Yangu. Katika macho yake kulipita mkondo wa pendo wa mwanga Wangu. Katika kinywa chake, mkondo wa pendo wa neno Langu. Katika mikono yake, mkondo wa pendo wa utakatifu wa kazi Zangu. Na katika utashi wake, mkondo wa pendo wa Utashi Wangu - na ndivyo hivyo kwa viungo vingine vyote vilivyobaki. 

Binadamu aliumbwa ili adumu katika mawasiliano endelevu na Muumba Wake, Na angewezaje kuingia na kudumu katika mawasiliano Na Mimi kama ile mikondo Yangu isingekuwa inapita ikitiririka katika ile ya kwake? 

Kutokana na dhambi, binadamu alivunja na kubomoa mikondo hiyo yote, na akabaki ametenganishwa na Mimi. 

Je wajua ilivyotokea? 

Ebu liangalie jua: mwanga wake wote unaipiga ardhi na unaifunika kiasi kwamba ardhi inaonja joto lake - ni joto hai na halisia hata linaleta nguvu ya kuotesha na uhai kwa kila kitu ambacho ardhi huzalisha. Ni hivyo, hata twaweza kusema kuwa, jua na ardhi vipo katika mawasiliano kati yao. Oh! Ni karibu mno jinsi gani yalivyo yale mawasiliano kati ya binadamu na Mimi Mwenyewe, niliye ni Jua la Milele la kweli. 

Sasa, kama mwanadamu angeweza kuwa na uwezo wa kuvunja, baina ya ile ardhi na lile jua, ule mkondo wa mwanga ambao unapiga uso wa ile ardhi, je, ni maafa gani angeyaleta? 

Jua lingeondoa mkondo wote wa mwanga na kuurudishia ndani yake lenyewe. Ardhi ingebaki katika giza tupu, bila nguvu yoyote ya kuotesha na bila uhai wowote. 

Huyo binadamu angestahili adhabu gani? 

Binadamu alitenda hilo lote katika Uumbaji, na Mimi niliteremka toka Mbinguni hadi duniani kwa ajili ya kuja kuunganisha tena hiyo mikondo yote ya pendo, lakini - oh! Ni makubwa mangapi yaliyonigharimu.  

Na huyu binadamu, anaendelea bado kuwa katika utovu wake wa shukrani, na anarudia bado kwenda kuvunja na kubomoa ile mikondo iliyokuwa imekarabatiwa na Mimi!”

Juzuu na. 14 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page