Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 25 - Februari 27, 1929🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 25 - Februari 27, 1929🖋📄📖📔


Zoezi langu la kujiachia mimi mwenyewe ndani ya FIAT Kuu ya Juu ni endelevu. Na pindi nikijaribu kufuatilia matendo ya Utashi wa Mungu kwa jinsi nilivyoweza, pindi nikipita kukumbatia kila kitu na kila mtu, ndipo Yesu Wangu Mtamu alinijia akitokea pale ndani mwangu, na aliniambia:

“Ewe Binti Yangu, Uumbwa mzima na hata wale Watakatifu wote, si kitu cha pekee isipokuwa ni matokeo ya Utashi Wangu wa Kimungu.

Kama Utashi Wangu unazungumza, hapo huwa unaumba na kutengeneza kazi zililizo nzuri kabisa.

Kila ujimudu mdogo tu wa Utashi Wangu huwa ni marashi ya yale matendo makuu ambayo huwa unayarashia juu ya wanadamu.

Pumzi ya Utashi Wangu, hata ile ndogo kabisa, huwa inatupia aina mbalimbali za uzuri upendezao juu ya mtu yule anayeupokea.

Kielelezo halisi cha jambo hili ni lile jua ambalo, kwa kuifunika ardhi tu na kwa mguso wake wa mwanga, huwa linaleta, juu ya mimea yote, aina nyingi kabisa za rangi mbalimbali, linaleta pia ladha na utamu wa aina mbalimbali.

Hata mtu mmoja hawezi akagoma kwamba, kwa kule kuguswa tu na mwanga wa lile jua, pale pale huwa amekwisha kujipatia yale manufaa yaliyopo ndani ya hilo jua. Utashi Wangu wa Kimungu ni zaidi kabisa ya jua.

Hata kama mtu atakubali aguswe na huo Utashi, basi, ule mguso wa kimuujiza wa huo Utashi ni budi kabisa umletee manufaa ambayo, kwa kumwachia harufu ya marashi yake, na kwa kumtia joto la mwanga wake, utamfanya mtu huyo awe anaonja matokeo yake yenye manufaa ya utakatifu, manufaa ya mwanga na ya upendo. 

Basi, matokeo ya FIAT Yangu huwa yanatolewa na kuwafikia wale wanaotekeleza Utashi Wangu wa Kimungu, wale wanaoyaabudu maelekezo Yake, na wale wanaoyapokea kwa saburi na uvumilivu mambo yale unayoyataka.

Kwa kutenda hivyo, mwanadamu atakuwa anakiri na kutambua kuwa Utashi Mkuu wa Juu upo.

Nao Utashi Mkuu unapofahamu tu kuwa wenyewe unatambulikana, hapo na wenyewe hautaweza kumnyima mtu huyo yale matokeo yake staajabivu.

Hata hivyo, yule anayepasika kuishi ndani ya Utashi Wangu, ni budi kabisa awe anabeba ndanimo ule uhai wote, na wala siyo yale matokeo peke yake - bali aubebe ule uhai pamoja na yale matokeo yote ya FIAT Yangu ya Kimungu.

Na maadam hakuna utakatifu wowote, wa kale, wa sasa, au wa baadaye, ambao chanzo chake cha kwanza kabisa siyo Utashi Wangu wa Kimungu, katika kujenga aina zote za utakatifu uliopo, Utashi Wangu, kwa hiyo, huwa unabeba ndanimo, yale mema yote na matokeo yote ya utakatifu ambayo ni wenyewe ndio ulioyaleta.

Kwa minajili hiyo, mtu yule atakayeishi ndani ya Utashi Wangu, kwa kuubeba uhai Wake, pamoja na matokeo Yake yote, atakuja kuona pale ndani yake, kwa pamoja na kwa wakati ule ule, zile aina zote za utakatifu ambazo zimewahi kutolewa.

Huyo mtu ataweza kufikia kusema hivi:

‘Baadhi wametekeleza sehemu mojawapo ya utakatifu, wakati mimi nimetekeleza mambo yote, mimi nimebeba ndani mwangu mambo yote, nimebeba kila kitu ambacho kila Mtakatifu amewahi kukitenda’.

Kwa hiyo basi, ule utakatifu wa mababu, ule utakatifu wa manabii, ule wa wale mashahidi, utakuwa ukionekana ndani ya mtu huyo.

Ule utakatifu wa wale waliolipa malipizi, zile aina kubwakubwa za utakatifu, sawa kama zile aina ndogondogo za utakatifu, zote zitaonekana pale ndani ya mtu huyo. Siyo hilo tu, bali, Uumbwa mzima utakuja kuonekana umekusanyika kwenye maonyesho pale ndani yake mtu huyo.

Na kwa kweli, Utashi Wangu wa Kimungu, huwa haupotezi chochote pale unapozitoa kazi Zake.

Kinyume chake, wakati unapotoa kazi Zake, huwa bado unaendelea kuzishikilia pale ndani Mwake wenyewe ukiwa kama ni chimbuko la awali la kazi hizo.

Kwa hiyo basi, kwa yule anayeishi ndani ya Utashi Wangu, hakuna chochote kile ambacho Utashi Wangu wa Kimungu umekitenda au utakachokitenda, ambacho hatimaye hakitakuja kubebwa Nao.

Ebu fikiri, kama mwanadamu fulani, angefikia kuweza kubeba ndanimo lile tufe lote la jua pamoja na ule mwanga wake, huyo mtu angekuwa ni kivutio na mshangao ulioje?

Je ni nani asingefikia kusema kwamba huyo mtu anabeba ndani yake matokeo yote, rangi zote mbalimbali, ule utamu wote, ule mwanga wote, yaani, vile vyote ambavyo jua limewahi kuvitoa, na ambavyo litakuja kulitoa bado kwa ardhi yote, na kwa mimea yote mbalimbali, iwe mikubwa au midogo?

Kama hilo lingekuja kutokea, hakika Mbingu na dunia vingekuja kuduwaa, na vyote hivyo vingekuja kukiri na kutambua kwamba, kila moja ya yale mambo ambayo vimeyabeba, kumbe yamekwisha kubebwa tayari na yule mwanadamu, anayelibeba lile tufe la jua, jua ambalo ndilo uhai wake yule mtu na jua linalobeba matokeo yale yote.

Kumbe lakini, kwa mtazamo wa kibinadamu, jambo hilo lisingeweza kutokea.

Ni kwa vile yule mwanadamu asingeweza kabisa kubeba, iwe ile nguvu ya ule mwanga wote wa jua, na wala asingeweza kuibeba ile nguvu ya lile joto lake lote.

Mbona angeungua kabisa, na wala jua lisingeweza kuwa na nguvu ya kujizuia kumwunguza huyo mtu.

Kwa upande mwingine, Utashi Wangu unayo nguvu ya kujibeba ndani Yake wenyewe, unayo nguvu ya kujifanya kuwa kadogo zaidi, na pia unayo nguvu ya kujipanua wenyewe - yaani, katika mtindo au jinsi yoyote ile unayotaka uwe, ndivyo wenyewe huweza kujifanya uwe hivyo.

Pindi Utashi Wangu unapomgeuza mwanadamu awe kama wenyewe, Utashi Wangu huwa unamhifadhi mtu huyo abaki kuwa hai, na papo hapo huwa unampatia madoido yote ya ule uzuri Wake wenyewe, na pia huwa unamfanya huyo mtu kuwa ndiye mtawala na mbebaji wa zile himaya Zake za kimungu.

Kwa hiyo basi, wewe uwe makini, Binti Yangu - uwe unayatambua yale manufaa makubwa ya ule Uhai wa FIAT Yangu hapo ndani yako.

FIAT hiyo, wakati inapokubeba wewe, huwa inataka kukufanya wewe uwe mmiliki wa kila jambo ambalo ni la Kwake”.

Halafu aliongezea kusema:

“Binti Yangu, yule anayeishi ndani ya Utashi Wangu wa Kimungu, huwa hahami kamwe na kuziacha njia za Muumba Wake, na wala huwa haachi kamwe kuwa maikrofoni Yetu - yaani, kwamba, ingawa kama kiini Chetu ni kimoja tu na ingawa kama Utashi ni mmoja, uhai ni mmoja, pendo ni moja tu, na uwezo ni mmoja tu, hata hivyo, Sisi, hata hivyo, ni Nafsi Tatu zilizo ni tofauti.

Hali kadhalika, kwa mtu anayeishi ndani ya Utashi Wetu, pigo lake la moyo ni moja tu, na katika kila pigo la moyo , yeye huwa anatenda matendo matatu: tendo moja linamkumbatia Mungu, tendo la pili linawakumbatia wanadamu wote, na tendo la tatu linamkumbatia yeye mwenyewe binafsi.

Basi, iwapo huyo mtu anazungumza, iwapo anatenda kitu fulani, katika kila kitendo anachotekeleza, hapo huwa anatengeneza hayo matendo matatu ambayo, kwa kutoa mwangwi wa Uwezo, mwangwi wa Hekima na mwangwi wa Pendo wa Yule aliyemwumba, hayo matendo hukumbatia kila kitu na kila mtu”.

Juzuu na. 25 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page