Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Novemba 3, 1919🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Novemba 3, 1919🖋📄📖📔


Mimi nilikuwa nimepata wasiwasi mwingi sana juu ya hali yangu dhaifu. Pia wakati huo huo yale maumivu ya kumkosa Yesu yanaendelea kuniletea hali ya ganzi hata kama nimebaki nikiwa nimetulia huku nikiwa nimejikabidhi na kujiachia ndani ya Yesu Wangu Mtamu. Mbingu ni kana kwamba imefungwa kwa ajili ya mimi. Na kuhusu dunia, ni tangu muda mrefu sana mimi siijui bado. Na kama siijui, nitawezaje mimi kutegemea kupata msaada wowote? Ndiyo maana sinayo hata yale matumaini matamu ya kutegemea kupata msaada kutoka kwa watu wa dunia hii masikini. Kama mimi nisingelikuwa na tumaini tamu katika Yesu Wangu, katika huyu aliye ni Uhai Wangu, aliye ni Chote Changu, aliye ndiye tegemeo langu pekee, mimi sielewi ningefanya nini’.

Halafu, Yesu Wangu Mpendevu wa daima, alipotambua kuwa siwezi kuvumilia zaidi, alinijongea, akiweka mkono Wake mtakatifu juu ya panda langu la uso ili kuniimarisha, aliniambia:

“Masikini Binti, ewe Binti wa Moyo Wangu na wa maumivu Yangu, shime, jipe moyo, usikate tamaa. Kwa wewe, hakuna jambo ambalo limekwisha kupita. Kinyume chake, wakati jambo fulani linapoonekana kana kwamba limepita tayari kumbe kwa kweli ndipo linapoanza. Mambo hayo yote unayoyafikiria hamna lililo ni la ukweli. Kinyume chake, hiyo hali yako ya sasa hivi siyo kitu kingine, isipokuwa ni sehemu moja tu ya ile hali ya mhanga ya Ubinadamu Wangu. Oh! Ni mara ngapi  Ubinadamu Wangu ulikuwa unajikuta ukibanwa na mateso ya maumivu haya. Ulikuwa daima umeunganishwa na kuoanishwa na Umungu Wangu - na zaidi zaidi, ulikuwa ni kitu kimoja nao. Hata hivyo, Umungu Wangu, uliokuwa ukishika mamlaka yote juu ya Ubinadamu Wangu, na uliokuwa ukiudai uwe unalipa malipizi kwa ajili ya familia nzima ya binadamu, ulikuwa unanifanya Mimi niwe ninaonja kule kusalitiwa, kule kusahaulika, yale mapigo, na kule kukosekana kwa mambo yale yote ambayo hulka ya kibinadamu ilikuwa inastahili kuyapata. Maumivu hayo ndiyo yaliyokuwa makali na machungu mno Kwangu Mimi. Na kadiri nilivyokuwa ninaoanishwa zaidi na Umungu, ndivyo nilivyozidi kuteseka wakati wa kuonja utengano wakati nikiwa bado vimeungana. Yatakiwa kupendwa wakati ukionja unasahauliwa. Yutakiwa kuheshimiwa wakati unakumbana na usaliti. Yatakiwa kuwa mtakatifu wakati unajiona na kuonja kuwa umefunikwa na madhambi yote. Ni mgongano gani uliopo! Ni mateso yalioje! Imekuwa ni mgongano na mateso kwa jinsi hii kwamba, ili niweze kuyapokea na kuyakubalia hayo yote, palitendeka muujiza wa maweza Yangu juu ya mambo yote.

Sasa, ile Haki Yangu huwa inataka marudio ya maumivu hayo ya Ubinadamu Wangu. Je ni nani sasa angeweza kuyaonja hayo yote, kama siyo mtu yule niliyemchagua, kumfananisha na kumwoanisha na Mimi Mwenyewe - yaani, yule niliyekuwa nimemheshimu mno hivi hata kufikia kumwita aje kuishi katika kilele cha Utashi Wangu. Na kutoka ndani hapo, kutoka katikati kabisa, mtu huyo huwa anaweza kutwaa sehemu zote za vizazi vyote, anaziunganisha pamoja, na anaweza kunilipa Mimi fidia, anaweza kunipenda Mimi na anaweza kuwa ni mbadala kwa wanadamu wote. Na wakati anapokuwa akitekeleza hilo, yeye huyo anakuwa akionja kusahaulika, kusalitiwa, na kujitenga kwa Yule ambaye ndiye huwa anatengeneza Uhai wake. Hayo ni yale maumivu ambayo Yesu Wako pekee ndiye anaweza akayakadiria na kuyahesabia. Lakini katika mazingira fulani fulani maumivu haya huwa ni ya lazima kabisa Kwangu. Ni ya lazima hivi kwamba huwa ninalazimika kukuficha wewe zaidi ndani Yangu ili nisikuache wewe ukapata machungu yale yote ya maumivu. Na pindi ninapokuficha, huwa ninayarudia yale yote ambayo Ubinadamu Wangu ulitenda na kuteseka.

Kwa hiyo basi, wewe tulia. Hiyo hali yako itakwisha siku moja ili kukupitisha ukaingie hatua nyingine za Ubinadamu Wangu. Utakapoonja kuwa huwezi kuvumilia zaidi, wewe ujitoe na kujiachilia zaidi na zaidi ndani Yangu, na hapo utakuwa ukimwonja Yesu Wako akisali, akiteseka, na akilipa fidia. Na wewe - ebu nifuate. Mimi nitakuwa ndiye mtendaji na wewe uwe ndiye mtazamaji. Na baada ya kufurahishwa, wewe utakuja na kushika nafasi ya mtendaji mkuu, na  Mimi nitakuwa ndiye mtazamaji. Basi tutakuwa tunabadilishana kati yetu”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here



Report Page