Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 19 - Aprili 25, 1926🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 19 - Aprili 25, 1926🖋📄📖📔


Ninapita katika kipindi kigumu na cha mateso makali sababu ya kukosekana kwa Yesu Wangu Mtamu. Ninaonja kana kwamba ninavuta hewa chafu yenye sumu inayotosha kunisababishia, siyo kifo kimoja, bali vifo elfu na elfu. Na wakati ninapokaribia kudondoka kutokana na pigo hili la kifo, ninaionja pia hewa ya uhai na ya uponyaji ya ule Utashi Mkuu wa Juu ambao kwangu mimi ni kama dawa ya kinga dhidi ya sumu ili nisife. Utashi huo unanishikilia niendelee kuishi ili nivikabili hivyo vifo endelevu chini ya uzito usioweza kukadiriwa wa kumkosa Yeye aliye ni Chema Changu pekee na cha juu kabisa. Oh! Kumkosa Yesu Wangu, kunanitesa ilioje! Wewe ndiwe ushahidi wa kweli wa roho yangu duni! Oh, ewe Utashi Mkuu wa juu, ni jinsi gani ulivyo na nguvu na maweza - kwa kuendelea kunipatia mimi uhai, unazuia mruko wangu kuelekea kwenye makao ya Mbinguni, kwenda kumwona Yule ambaye ninamchuchumia na ninamtamani. O tafadhali sana! unionee huruma mimi katika huu uhamisho wangu wa uchungu - unihurumie mimi ninayeishi bila uwepo wa Yule ambaye pekee anaweza akanipatia uhai.

Hata hivyo, wakati nikijiona kuwa nimepondeka kabisa chini ya uzito huo wa kumkosa, Yesu Mpendevu Wangu aliingia ndani mwangu na akaanza kunitazama kwa kunikazia macho Yake. Kwa yale macho Yake ya huruma, nikaanza kuonja kuwa nimeokolewa toka hali ile ya kifo na kurejea kwenye uhai. Na vile nilikuwa nikitekeleza matendo yangu ya siku zote ndani ya Utashi Mkuu wa Juu, Yeye aliniambia:

“Binti Yangu, wakati ulipokuwa ukigonga mihuri yako ya ‘Ninakupenda’ juu ya viumbe pale ndani ya Utashi Wangu, Uumbwa wote ulikuwa ukionja kuwa lile Pendo la Muumba Wake likiwa linaongezeka mara dufu. Na kwa vile viumbe hawana hoja ya akili, lile Pendo likawa linatiririka kwa kasi kabisa kuelekea kwa Yule aliyekuwa amewaumba. Na Baba wa Mbinguni, alipoona lile Pendo alilokuwa amelitoa wakati wa Uumbaji likiwa limerudufiwa na yule mzaliwa mpya mdogo wa Utashi Wake, ili asipitwe katika upendo, Naye anarudufu Pendo Lake na kulifanya lifurikie kwenye viumbe vyote na likafuate mkondo ule ule aliofuata Binti Yake Mdogo. Kishapo Yeye Baba akakusanya na kujaza Pendo hilo lote ndani ya yule ambaye alimfikishia Pendo Lake likiwa sasa limerudufiwa. Na kwa ulaini wa kibaba Yeye anasubiri ashitushwe na mambo mengine mapya - kwamba yule mzaliwa Wake mpya atarudufu tena lile Pendo Lake.

Oh! Kama ungeifahamu ile mikondo na yale mawimbi ya pendo yanayokuja na kwenda kutoka duniani hadi Mbinguni, na kutoka Mbinguni kuja duniani - kama ungefahamu jinsi viumbe vyote, licha ya kuwa katika lugha yao bubu, na licha ya kuwa bila akili, wanavyoonja hilo Pendo lililorudufiwa la Yule aliyewaumba na la yule ambaye kwaye walikuwa wameumbwa. Na viumbe hao wote wanavaa uso wa tabasamu, wa sherehe, uso wa kuachilia mambo yafurikie nje, uso wa ukarimu, wanatiririsha hayo matokeo ya kwao kwenda kwa wanadamu.

Kuishi ndani ya Utashi Wangu, kunafanya mambo yote yaanze kujimudu, kunagusa kila jambo na kunahitimisha ile kazi ya Muumba ndani ya Uumbwa. Ile FIAT hapa duniani kama ilivyo kule Mbinguni ina muujiza wake, ina noti ya muziki yenye harmonia zaidi, inaleta tabia nzuri zaidi, ambayo hata kule Mbinguni huwa haiifaidi wala haiibebi. Kwa kweli, kule Mbinguni inabeba muujiza wa FIAT ya ushindi mkuu, ambao hamna mtu yeyote awezaye kuuzuia. Na kila aina ya burudani katika yale maeneo ya Mbinguni huwa inatoka kwa FIAT kuu ya juu. Lakini hapa uhamishoni, katika kina cha mtu, FIAT hapa duniani kama ilivyo kule Mbinguni, ina muujiza wa FIAT iliyo katika kushinda na katika kujipatia mateka mapya. Kumbe lakini, kule Mbinguni hakuna mateka mapya, kwa vile mambo yote ni mali ya kwake. Ndani ya mtu anayehiji hapa duniani FIAT Yangu haitumii mamlaka ya imla, bali huwa inataka iwe pamoja na mtu fulani katika kazi yake yenyewe. Kwa sababu hiyo huwa inafurahia kujionyesha na kujieleza yenyewe, inafurahia kuamrisha, na hata hufurahia kumwomba mtu atende kazi pamoja nayo. Mtu anapoitikia na kukubali kujazwa na FIAT kuu ya juu, huwa kunatokea noti za muziki zenye harmonia nzuri kutokea pande zote mbili. Hizo harmonia huwa ni nzuri hivi kwamba Muumba Mwenyewe anaonja kufurahishwa na noti za muziki za kimungu za Kwake Mwenyewe lakini zikiwa zinamfikia toka kwa mwanadamu. Noti hizo hazipatikani kule Mbinguni, kwani Mbingu siyo makao ya kazi, bali ni makao ya burudani mbalimbali. Kwa hiyo, FIAT Yangu hapa duniani inayo tabia hii nzuri kabisa ya kugonga mhuri wa utendaji wa kimungu wa kwake wenyewe ndani ya mtu, na inayo pia tabia ya kumfanya mtu huyo awe ni maikrofoni au kipaza sauti cha kazi zake.

Basi, kule Mbinguni FIAT Yangu ni yenye ushindi, na hakuna yeyote kule katika maeneo ya Mbinguni anayeweza akasema: ‘Hapa nimetenda kazi fulani ya kuonyesha pendo langu, na sadaka yangu kwa FIAT Kuu ya juu’. Hapa duniani, FIAT ipo katika kushinda. Na kama mtu anapenda kupata kiti cha kifalme, basi mtu huyo atakuwa anapenda zaidi kujipatia ushindi mbalimbali mpya. Na kweli kabisa, kwani FIAT Yangu ingeacha kutenda nini kwa ajili ya kumshinda na kumteka mtu mmoja ili kumfanya awe anatenda ndani ya Utashi wake? Kwani ni mangapi ambayo haijakutendea wewe na ni mangapi ambayo haikutendei wewe sasa hivi?”

Halafu, baadaye, Yesu Wangu Mtamu, alijitokeza na kujionyesha akiwa kama Msulibiwa na alikuwa katika mateso makali sana sana. Mimi sikuwa nikielewe nifanye nini ili nimpunguzie ukali wa mateso. Nikawa ninajikuta kuhinishwa sana kutokana na kutokuonekana kwa Yesu, kitu kilichonitesa sana sana. Ndipo Yesu, akawa anaivuta na kuichomoa ile misumari toka pale Msalabani. Alijitupa Mwenyewe mikononi mwangu akawa ananiambia: “Naomba unisaidie kuituliza ile Haki ya Hukumu ya Mungu. Kwani inataka kuwapiga wanadamu”. Kishapo tukawa tunaonja tetemeko kali la ardhi, ni tetemeko lililoharibu  miji mbalimbali. Mimi nilibaki nikiogopa na kutetemeka. Halafu Yesu alififia na mimi nikajiona nipo tena ndani yangu mwenyewe.

Juzuu na. 19 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

Swahili - Telegram Channel: Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaîne Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaîne Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page