Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Februari 19, 1927🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Februari 19, 1927🖋📃📖📔


Nilikuwa nikiendelea na mruko wangu pale ndani ya FIAT ya Kimungu, na Yesu Wangu Mtamu alijitokeza akinijia kutoka pale ndani mwangu huku akinyosha mikono Yake kuishika mikono yangu, na hivyo kuitikisa, ili kunialika niwe ninapigana Naye. Mimi nilikuwa ni kadogo kweli, na wala sikuonja kuwa na uwezo wala na nguvu za kupigana na Yesu. Zaidi zaidi, ni kwa vile nilikuwa nikisikia sauti inayotoka katika mwanga, iliyokuwa ikisema: ‘Ni kadogo mno hako - katawezaje kushinda mapigano hayo?’ Ndipo Yesu alijibu akisema: “Ni kinyume chake. Kwa vile yeye ni kadogo, basi, ndiye yeye atakayeweza kushinda, kwani nguvu zote zipo katika huo udogo”. Nikawa nimekatishwa tamaa, na wala sikuthubutu kupigana na Yesu. Na Yeye, akiendelea kunichokoza mimi kupigana Naye, aliniambia:

“Binti Yangu, jipe moyo - ebu jaribu. Kama utashinda, basi utajipatia ule Ufalme wa Utashi Wangu. Na wala usisitishe mapigano kwa vile u mdogo, kwani, Mimi nimekuwekea nguvu zote za viumbe. Kwa hiyo, pamoja na wewe inapigana nguvu yote iliyopo katika anga mbalimbali, nguvu iliyo ndani ya jua, ndani ya maji, ndani ya upepo, na ile ndani ya bahari. Hivyo vyote sasa hivi vinanipiga vita Mimi. Vinanipiga vita Mimi ili kunifanya nitoe na kukabidhi Ufalme wa FIAT ya Kimungu. Vinawapiga vita hiyo wanadamu, kwa kutumia silaha zile ambazo kila kiumbe kinazo chini ya uwezo wake, ili kuwafanya walegee na kukubali kuutambua Utashi Wangu, ili kusudi wanadamu waruhusu Utashi Wangu kutawala kama vile viumbe vyenyewe vinavyouruhusu uwe unavitawala. Na kwa vile vinataka kushinda vita, vyote vimejipanga kwa utaratibu wa kivita. Na wanapotambua kuwa wanadamu wanagoma na kuizuia vita, na kwa vile vyenyewe vinataka kwa vyovyote vile vishinde hiyo vita, na kwa vile vinayo ile nguvu ya ule Utashi unaovirohoisha na unaoviamrisha, kwa silaha zile vinazokuwa nazo, viumbe hivyo vinawatwanga mataifa na majiji, kwa mamlaka yote, hata hakuna mtu anayeweza akavizuia. Wewe huwezi ukaielewa ile nguvu yote na maweza ambayo sayari zote zinabeba. Ni kubwa hivi kwamba, kama Utashi Wangu usingevishikilia na kuvizuia, vita ingepamba moto kabisa hata vingefanya dunia nzima kuwa kifusi tu.

Sasa, hiyo nguvu ya viumbe ndiyo ni ya kwako. Basi, wewe - nenda zungukia kati ya viumbe ili ukavipange kwa ajili ya vita. Acha hayo matendo yako, yale matendo endelevu ya kuomba kuupata Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu, yauite ule Uumbwa mzima usimame na kusikiliza. Na Utashi Wangu, kwa kujimudu ndani ya huo Uumbwa, utaweka matendo yake yote katika jukumu la kifame ili kusudi kuutoa, na kujipatia Ufalme wake pale kati ya wanadamu. Kwa hiyo basi, ni Utashi Wangu wenyewe ndio unaopigana - unaopiga vita dhidi ya Utashi Wangu ule ule kwa ajili ya ushindi wa kifahari wa Ufalme wake. Basi, mapigano yako yanarohoishwa na Utashi Wangu ambao una nguvu ya kutosha na isiyozuilika kwa ajili ya kuweza kushinda. Kwa hiyo, wewe endelea kupigana, kwa vile utashinda tu. Aidha, kupigana kwa lengo la kushinda ule Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu, ni mapigano matakatifu kabisa ambayo yanaweza kutokea. Ni mapigano ya haki kabisa, na yafaayo ambayo mtu anaweza akayakabili. Hilo ni kweli kabisa hivi kwamba, Utashi Wangu wenyewe, ndio uliokuwa umeanzisha vita hii, na mapigano haya, pale ulipokuwa unautengeneza Uumbwa. Na ni pale tu wakati Utashi Wangu utakaposhinda kitimilifu, ndipo utaweza kutulia.

Lakini je, wewe ungependa kufahamu ni wakati gani unapopigana na Mimi na Mimi ninapopigana na wewe? Mimi huwa ninapigana na wewe pale ninapokufundisha yale maarifa juu ya FIAT ya Milele. Basi, kila kauli, kila aina ya maarifa, kila mfano juu ya FIAT, huwa ni pigano moja na ni vita moja ninayofanya na wewe kwa ajili ya Mimi kujipatia utashi wako, kwa ajili ya kuuweka huo mahali pake, pale ulipokuwa umeumbwa na Sisi, kwa ajili ya kuuita, na kwa kukaribia kupigana nao, nauita uingie katika utaratibu wa Ufalme wa Utashi Wangu wa Kimungu. Na kama vile ninavyotenda na wewe kwa ajili ya kutiisha utashi wako, ndivyo ninavyoanza vita pale kati ya wanadamu. Ninapigana na wewe wakati ninapokufundisha wewe njia unayopasika kuifuata, ninakufundisha nini utende ili uweze kuishi ndani ya Ufalme Wangu, na ninakufundisha ile heri, na zile furaha ambazo utakuja kuwa nazo. Kwa kijumla, Mimi ninapiga vita kwa nguvu ya ule memetuko wa mwanga ule ambao upo katika yale maarifa Yangu. Ninapigana kwa ule memetuko wa pendo na kwa ile mifano inayogusa sana mioyo, kwa jinsi kwamba, wewe huwezi ukagoma mapigano na Mimi. Mimi ninapigana kwa njia ya zile ahadi za heri na furaha isiyo na mwisho. Mapigano Yangu ni endelevu kwa kudumu, na wala huwa sichoki - lakini huwa napigana ili nipate nini? Ili niupate utashi wako, na ndani ya utashi wako niwapate wale watakaoutambua na kuukiri Utashi Wangu kwa ajili ya kuishi ndani ya Ufalme Wangu. Na wewe unapigana na Mimi pale unapoyapokea maarifa Yangu mbalimbali, na pale unapoujenga Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu ndani yako mwenyewe, kwa kuyapanga hayo maarifa kwa utaratibu na mpangilio ndani ya roho yako. Na kwa kupigana na Mimi, wewe unajaribu kujipatia Ufalme Wangu. Kila moja ya matendo yako unayoyatekeleza ndani ya Utashi Wangu ni mapigano unayoyafanya na Mimi. Katika kila mzunguko unaofanya kupitia viumbe vyote kwa ajili ya wewe kujiunganisha na matendo yote ambayo Utashi Wangu unayatekeleza ndani ya Uumbwa mzima, wewe unauita Uumbwa mzima kuja kupiga vita kwa ajili ya kujipatia Ufalme Wangu. Hivyo unaugusa ule Utashi Wangu wenyewe ambao unatawala na unaamrisha ndani ya viumbe vyote, hata uweze kuanza kupiga vita dhidi ya Utashi Wangu wenyewe, ili uweze kuujenga Ufalme wake. Ndiyo maana, katika nyakati hizi, iwe upepo, iwe maji, iwe bahari, iwe ardhi na hata iwe zile anga mbalimbali, vyote vipo katika ujimudu zaidi zaidi kabisa kuliko nyakati nyingine zote, vyote vikipiga vita dhidi ya wanadamu, kadiri matukio mapya yanavyojitokeza - na kwa kweli, ni matukio mengi mapya mangapi zaidi yatakayojitokeza - matukio ya kuja kuangamiza mataifa na majiji: Ni kwa vile, katika mapigano mbalimbali, ni lazima kujiweka tayari kukabili hasara fulani fulani, na mara nyingi sana, hata kwa ule upande wa yule anayeshinda. Kamwe hapajawahi kutokea ushindi wa kuteka himaya mbalimbali bila mapigano, na kama ushindi umewahi kutokea, basi, huo ushindi haujawahi kuwa ni wa kudumu. Wewe unapigana na Mimi wakati ule ambapo wewe unafunika chochote kile nilichokuwa nimetenda na kuteseka katika Ubinadamu Wangu - yaani, yale machozi Yangu, yale maumivu Yangu ya ndani kabisa, zile sala Zangu, zile hatua Zangu, yale maneno Yangu, na hata yale matone ya Damu Yangu - wewe unagonga, juu ya matendo hayo yote, ule mhuri wako wa ‘Ninakupenda’ yako, na kwa kila moja ya matendo Yangu, wewe unaendelea kuomba ujio wa ule Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu. Kuna nani awezaye kuelezea mapigano unayoyafanya dhidi ya Mimi? Wewe unayaamsha na kuyatikisa hata yale matendo ya Kwangu yenyewe yaanze kunipiga vita Mimi, ili hata Mimi nitetereke na nitoe na kukupatia wewe Ufalme Wangu.

Kwa hiyo, ninapigana nawe, na wewe unapigana na Mimi. Mapigano haya ni ya lazima - iwe kwako wewe kwa ajili ya kujipatia Ufalme, iwe na Kwangu Mimi kwa ajili ya kujipatia huo utashi wako na kwa ajili ya kuanza mapigano kati ya wanadamu ili kuujenga Ufalme wa Utashi Wangu Mkuu wa Juu. Mimi ninao Utashi wa Kwangu Mwenyewe, na ninayo Maweza yake yale yale yote, Nguvu yake yote, na Ukubwa wake wote kwa ajili ya kushinda. Wewe unao Utashi Wangu wenyewe kwa ajili yako, unao Uumbwa wote, na pia yale mema yote niliyotekeleza katika Ukombozi. Unayo hayo yote ili kukusaidia kuzindua kikosi kikali kabisa cha jeshi kwa ajili ya mapigano ya vita ili ushinde na kujipatia Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu. Ebu angalia, kila neno unaloliandika ni pia mapigano unayoyafanya dhidi ya Mimi - Ni kama askari moja zaidi ambaye anajiunga na jeshi, ambalo ni lazima lishinde ili kujipatia Ufalme wa Utashi Wangu. Kwa hyo basi, uwe makini, Binti Yangu, kwa vile hizi ni nyakati za mapigano, na ni lazima kutumia kila mbinu kwa ajili ya kuweza kushinda”.

Juzuu na. 20 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

Swahili - Telegram Channel - Bikira Maria Katika Ufalme wa Utashi wa Mungu

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page