Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 20 - Desemba 25, 1926🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 20 - Desemba 25, 1926🖋📄📖📔


Mimi nilikuwa nikimngojea kwa hamu kubwa Yesu Kichanga Mdogo. Baada ya mimi kuhema sana, aliwasili mwishowe. Yeye kama Kichanga Mdogo alijitupa mikononi mwangu na kuniambia:

“Binti Yangu, je unapenda kuona jinsi Mama Yangu, asiyetenganika Nami, alivyoniona Mimi dakika ile nilipokuwa natoka tumboni mwake? Ebu uniangalie na uone”.

Nilimwangalia na nikawa namwona akiwa ni Kichanga Mdogo sana mwenye uzuri upendezao wa aina ya pekee, uzuri unaoteka moyo wa yule atazamaye. Kutoka kwenye Ubinadamu Wake Mdogo wote, kutoka kwenye macho Yake, mdomoni Mwake, kutoka mikononi na miguuni Mwake, kulijitokeza mionzi inayong’aa mno ya Mwanga. Mwanga huu ulimfunika kabisa.

Si hivyo tu, bali ulisambaa na kuenea kiasi kwamba ukawa unachoma na kujeruhi kila moyo wa mwanadamu. Hiyo ilikuwa ni kama salamu Yake ya kwanza ya ujio Wake hapa duniani. Yaani, ilikuwa ndiyo hodi ya kwanza; ni kupiga hodi kwa mioyo yote kuitaka ifungue milango yao ili Yeye aweze kuomba nafasi ya kujihifadhi ndani yao.

Ile hodi ilikuwa ni tamu, lakini ikawa inapenya sana mioyoni. Hata hivyo, kwa vile ilikuwa ni hodi ya Mwanga, haikufanya kelele yoyote ya kushitua, ingawa kama ilikuwa inasikika vizuri mno kupita sauti nyingine yeyote.

Ndiyo maana usiku ule watu wote walikuwa wakionja kitu fulani cha pekee moyoni mwao, lakini hata hivyo ni wachache sana waliofungua mioyo yao ili kumpatia angalau nafasi ndogo ya malazi. Yule Kichanga Mdogo, alipoona salamu Yake haijibiwi na alipoona hakuna mtu aliyediriki kumfungulia mlango, alirudiarudia kubisha hodi, na hatimaye Yeye alianza kulia.

Niliona midomo Yake inavimba na ikitetemeka kwa baridi. Alilialia, alilalamika, na alitweta. Wakati Mwanga uliokuwa ukimtoka ulipokuwa ukifanya hayo yote kwa wanadamu, na huku akiwa anagomewa kiasi kile kwa mara Yake ya kwanza kabisa, huku akiwa pamoja na Mama Yake wa Mbinguni, Yeye mara tu alipotoka tumboni mwa Mamae, alijitupa ndani ya mikono yake ya kimama ili akumbatiwe naye kwa mara ya kwanza, na aweze pia kulipata busu la kwanza.

Na kwa vile Tumikono Twake tulikuwa ni tudogo mno kuweza kumfikia Mama na kumkumbatia kabisa, ule Mwanga uliokuwa ukiangaza toka Mikononi Mwake ulimwangaza na kumfunika Mama Yake mzima. Mama na Mtoto wakabaki wamegubikwa na Mwanga uleule mmoja.

Oh! Ni jinsi gani Mama alivyoitikia pendo la Mtoto wake kwa tendo la yeye pia kumkumbatia na kumbusu. Pale wakabaki wamekumbatiana, hata wakawa kama vile wameyeyushiana mmoja ndani ya mwenzake. Kwa pendo lake Mama alilipa fidia ya ule ukatalio alioupata Yesu toka kwa mioyo ya wanadamu.

Ndipo yule Mpendwa Kichanga Mdogo mwenye kuvutia sana, aliingiza na kuweka tendo Lake la kwanza la kuzaliwa ndani ya moyo wa Mama Yake.

Aliweka pale pia neema Zake na Teso Lake la kwanza, ili kusudi chochote kilichowezekana kuonekana ndani ya Mwana, ndicho kikaweze kuonekana ndani ya Mama Yake. Kishapo, Kichanga Mdogo wa kupendeza, alikuja mikononi mwangu, na wakati aliponibana sana kunikumbatia, nikawa naonja anaingia ndani yangu na mimi ndani yake. Halafu, aliniambia:

“Binti Yangu, nilikuwa napenda nikukumbatie wewe sawa kama nilivyomkumbatia Mama Yangu mpenzi siku nilipotoka kuzaliwa. Napenda kufanya hivyo ili na wewe pia uweze kupata tendo Langu la kwanza la kuzaliwa, upate Teso Langu la kwanza, upate machozi Yangu ya kwanza, malalamiko Yangu laini ya kwanza, kusudi nawe uweze kuguswa, hata unionee huruma kwa hali yangu ya uchungu wakati nilipozaliwa.

Kama nisingekuwa nina Mama Yangu, ambaye ndanimo niliweza kuhifadhi hazina yote ya manufaa ya kuzaliwa Kwangu, na pia ambaye ndanimo niliweza kuhifadhi ule Mwanga wa Umungu Wangu, ambao nilikuwa nao Mimi niliye ni Neno la Baba, halafu nisingeweza kumpata mtu ambaye ndanimo ningeweza kuyaweka hayo yote.

Sasa, ebu uone jinsi ilivyokuwa ni lazima kwamba, wakati Yule aliye Mkuu anapoamua jema Kuu litekelezwe kwa manufaa ya wanadamu wote, kwa kawaida huwa Tunamteua mtu fulani mmoja ambaye tunampa neema nyingi sana sana, ili huyo aweze kupokea ndani yake lile jema lote litakalotolewa kwa watu wote.

Kwa kweli, hata kama wengine hawatapokea kabisa jema lile, au hata kama wakiacha kupokea sehemu tu ya jema hilo, kazi Yetu huwa haisitishwi na wala haikosi kuzaa matunda yake, bali yule mtu aliyeteuliwa ndiye anapewa jema lote ndani yake na papo hapo kazi Yetu hiyo inapata kulipwa kwa matunda yake.

Kwa hiyo, Mama Yangu, amekuwa ndiye hifadhi siyo ya Uhai Wangu tu, bali amekuwa ni hifadhi ya matendo Yangu yote. Ndiyo maana, katika matendo Yangu yote, nilikuwa nikitazama kwanza iwapo nitafanikiwa kuyahifadhi ndani yake; baada ya kulijua hilo, ndipo niliyatekeleza. Ndani yake nilihifadhi machozi Yangu, malalamiko Yangu, baridi na Mateso niliyoyaumia. Naye alikuwa analijibu kila mojawapo ya hayo matendo Yangu na kishapo aliyapokea yote katika shukrani zisizokoma. Palikuwa na namna ya mashindano kati Yetu, Mimi Mwanae na yeye Mamangu - Mimi nikiwa ninatoa na yeye akiwa anapokea. Pindi huu Ubinadamu Wangu Mdogo ulipokuwa ukiingia kwa mara ya kwanza duniani, Umungu Wangu ukawa unapenda kujitokeza ili ung’ae nje Yake, na hivyo uweze kufanya mara ziara Yake ya kuzungukia popote, kutembelea Uumbwa wote, kwa jinsi ya kuonekana. Mbingu na dunia – vitu vyote, kasoro binadamu, vilifikiwa na ziara hiyo ya Muumba Wao. Kamwe haikuwahi kutokea kabla yake kwa viumbe kupata Heshima na Utukufu kama siku hiyo vilipomwona Mfalme Wao na Muumba Wao akiwa kati yao. Viumbe vyote vilionja kuheshimika mno, kwa vile sasa vingekuwa vinaanza kumtumikia Yule ambaye tokea Kwake viliupata uwepo wao. Ndipo viumbe wote walianza kusherehekea. Kwa hiyo, kwa upande wa Mama Yangu na Uumbwa wote, tendo la kuzaliwa Kwangu lilileta furaha kubwa na Utukufu juu Yangu. Lakini kwa upande Wangu nilipata uchungu sana mintarafu wanadamu. Ni kwa minajili hiyo, Mimi leo nimekuja kwako – ili ndani yako niweze kuzionja zile furaha za Mama Yangu zikiwa zinajirudia ndani Yangu, na ili niweze kuweka ndani yako lile tunda la kuzaliwa Kwangu”.

Baada ya hapo, nikawa ninawaza jinsi Pango lile alipozaliwa Mtoto Yesu lilivyokosa kuwa na furaha! Jinsi Pango lile lilivyokuwa linapigwa na pepo zote na baridi muda wote, kiasi kwamba mtu aliweza kupata ganzi kwa baridi kali! Halafu, badala ya kuwepo watu, palikuwepo wanyama tu kukesha Naye! Ndipo nikawaza: ‘Ni gereza gani lililoleta uchungu na masikitiko zaidi – gereza lile la usiku wa Mateso Yake au gereza la Pango lile la Belehemu?’. Ndipo Kichanga Wangu Mtamu alinijibu akisema:

“Binti Yangu, uchungu niliopata katika gereza lile la usiku wa Mateso haliwezi likalinganishwa na uchungu niliopata pale Pangoni Betlehemu.

Pale penye Pango nilikuwa na Mama Yangu kando Yangu katika mwili wake na roho yake. Alikuwa pamoja Nami, na hivyo nilipata furaha zote za kutoka kwa Mama Mpenzi na yeye alikuwa na furaha za Kwangu Mimi Mtoto Wake na hizo furaha zetu zilitengeneza Paradisi Yetu. Furaha za Mama anayemshika Mtoto Wake ni kubwa kweli. Hata hivyo, furaha za Mtoto kumshika Mama Yake ni kubwa zaidi. Mimi nilikiona kila kitu ndani yake na yeye alikiona kila kitu ndani Yangu. Zaidi ya hilo, kulikuwepo na Mpenzi Baba Yangu Mtakatifu Yosefu ambaye alikuwa Kwangu ni badala ya Baba Yangu, na nilikuwa nazionja furaha zote alizokuwa akizionja yeye kwa ajili Yangu.

Kinyume chake, lakini, wakati ule wa Mateso Yangu[1], furaha zetu ziliingiliwa na kukatishwa kwani ilitupasa tukaribishe uchungu. Kati ya Mama na Mtoto, tulikuwa tukionja uchungu mkubwa wa kuachana na kutengana, walau kimwili, utengano ambao ulikuwa ukikaribia kutokana na Kifo Changu.

Pale Pangoni, wanyama walinitambua, na kwa kuniheshimu, walijitahidi kunipasha joto angalau kwa njia ya pumzi zao. Lakini kule gerezani, wakati wa Mateso Yangu, hata mtu mmoja hakunijali na badala yake, kwa kutaka kunidhalilisha waliujaza Uso Wangu kwa kunitemea mate na kunidhihaki. Kwa hiyo, huwezi ukalinganisha uchungu wa magereza hayo mawili”.

[1] Vinapatikana na unaweza ku download✍🏼📚: Kitabu: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Wetu Yesu Kristo

Juzuu na. 20 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page