Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Desemba 3, 1921🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Desemba 3, 1921🖋📃📖📔


Nilikuwa nikitia mashaka kabisa, na nilikuwa nimehinishwa kwa yale yote ambayo Yesu Wangu anayasema mintarafu Utashi Wake wa Kimungu. Ndipo nikawa ninafikiri moyoni mwangu: ‘Iliwezekanaje kwamba aliziacha karne nyingi hivi zikapita bila kuyajulisha haya maajabu ya Utashi wa Mungu. Iliwezekanaje kwamba, kutoka Watakatifu wale wengi wa namna ile, Yeye hakuchagua mtu wa kuanzisha huu Utakatifu wa kimungu kabisa. Mbona lakini, kulikuwepo Mitume na Watakatifu wengine wengi sana ambao waliushangaza ulimwengu wote’.

Sasa, pindi mimi nikiwaza juu ya hilo, Yeye, bila kunipa wasaa wowote, na akikatisha lile wazo langu, alinijia na akaniambia: “Huyu Binti Yangu Mdogo wa Utashi Wangu, hataki kabisa kujiamini mwenyewe. Kwa nini bado unatia mashaka?”

‘Kwa vile ninajitambua mwenyewe kuwa ni mbaya, na jinsi unavyozidi kunieleza, ndivyo ninaonja ninahinishwa zaidi’

Na Yesu akasema: “Na hicho ndicho ninachotaka Mimi - upate kuhinishwa. Na kadiri ninavyozidi kukueleza mintarafu Utashi Wangu, ndivyo neno Langu, kwa vile ni neno umbaji, linaumba Utashi Wangu ndani ya utashi wako. Na utashi wako, mbele ya nguvu ya Utashi wa Kwangu, unabaki umehinishwa na unapotea - hiyo ndiyo hoja ya kuhinishwa kwako. Ujue kwamba utashi wako budi uyeyukie ndani ya Utashi Wangu, sawa kama vile barafu inavyoyeyuka mbele ya mionzi ya jua kali.

Tena, sasa ujue kwamba kadiri kazi ninayotaka kuitenda inavyozidi kuwa ni kubwa, ndivyo hutakiwa maandalizi ya ziada. Ni unabii mwingi kiasi gani, ni maandalizi mengi mangapi, na ni karne nyingi ngapi, ambazo zilipasika kuutangulia Ukombozi Wangu? Ni picha-mfano nyingi ngapi na vielelezo vingi vingapi vilivyopasika kutangulia tukio la kutungwa mimba Mama Yangu wa Mbinguni? Halafu, baada ya Ukombozi kutimia, ilinipasa nimmwimarishe binadamu katika yale mema ya Ukombozi. Na kwa hilo niliwachagua Mitume ili wawe ndio waimarishaji wa matunda ya Ukombozi ambayo ndanimo, kwa nguvu ya Sakramenti, wangemtafuta yule binadamu aliyepotea na kumrudisha kwenye usalama.

Kwa hiyo Ukombozi ni wokovu - ni tendo la kumwokoa binadamu kutoka kwenye korongo lolote lile. Ndiyo maana, katika nafasi nyingine, nilikuwa nimekuambia kuwa tendo la kumfanya mtu aishi ndani ya Utashi Wangu ni tendo kubwa zaidi kuliko hata Ukombozi wenyewe - kwa vile, kuokolewa kwa kuishi maisha ya katikati, mara mtu aanguke na mara hii asimame tena, kwa kawaida siyo ngumu sana. Na jambo hili lilikuwa limeombwa kwa njia ya Ukombozi Wangu kwani nilikuwa nimetaka, kwa gharama yoyote ile, nimwokoe binadamu. Na hiyo kazi niliikabidhi kwa Mitume Wangu wawe ndio wahifadhi wa yale matunda ya Ukombozi. Basi, kwa vile nilibakiwa na jukumu la kutenda kilicho kidogo, Mimi nilikiacha kile kilichokuwa kikubwa wakati ule, nikawa naweka akiba ya nyakati nyingine kwa ajili ya kukamilisha mipango yangu ya juu.

Halafu, huko kuishi ndani ya Utashi Wangu, siyo tendo la wokovu tu, bali ni utakatifu ambao lazima upande na uwe juu ya aina nyingine zote za utakatifu, na ni utakatifu unaobeba alama ya Utakatifu wa Muumba wake.

Kwa hiyo, aina ndogo ndogo za utakatifu zilitangulia kufika, kama wasindikizi, kama wachukuzi, kama wajumbe na kama maandalizi kwa ajili ya aina hii ya Utakatifu, yaani Utakatifu ulio ni wa kimungu kabisa. Kama vile katika Ukombozi nilikuwa nimemchagua Mama Yangu wa pekee kabisa kuwa kiunganisho kitakachounganisha wanadamu na Mimi, ambacho kwacho matunda yote ya Ukombozi ingepasa yateremke kuja kwa binadamu, ndivyo nilikuchagua wewe uwe kiunganisho cha kuunganishia na kwacho Utakatifu wa kuishi ndani ya Utashi Wangu ungekuwa unaanzia. Na Utakatifu huo, baada ya kutoka katika Utashi Wangu kuja kuniletea Mimi ule utukufu timilifu wa lile lengo ambalo kwalo binadamu alikuwa ameumbwa, Utakatifu huo ungerudi tena kupitia njia ile ile uliojia, yaani kupitia Utashi Wangu, ili kurejea kule kwa Muumba wake. Sasa wewe unastaajabu kitu gani? Hayo ni mambo yaliyokuwa yamepangwa ab aeterno na hakuna mtu atakayeweza kuyahamisha. Na kwa vile jambo hili ni kubwa kabisa - yaani, ni kwa ajili ya kujenga Ufalme Wangu ndani ya mtu hata hapa hapa duniani - Mimi nimekuwa nikitenda mambo kama Mfalme anapopasika kwenda kuchukua madaraka ya himaya yake. Yeye huwa hatangulii kwenda kule mahali isipokuwa kwanza awe ameiandaa Ikulu yake ya kifalme. Kishapo anawatuma maaskari wake kwenda kuandaa utawala wake wa kifalme na kwenda kuwaandaa watu wawe wanamtii. Halafu watafuata maaskari wa kikosi kile cha heshima, watafuata mawaziri -na wa mwisho atakuwa ni yeye mwenye Mfalme. Huo ndio utaratibu rasmi kwa Mfalme.  

Ndivyo nilivyofanya hata Mimi: Niliiandaa ikulu Yangu ya kifalme, yaani Kanisa. Maaskari wamekuwa ni wale Watakatifu kwa ajili ya kunifanya mimi nijulikane kwa watu. Halafu walifuata Watakatifu waliopanda mbegu ya miujiza, wakawa kama wahudumu wapenzi wa ndani kabisa. Sasa Mimi Mwenyewe ndiyo nakuja kutawala kama Mfalme. Ndiyo maana ilinipasa nichague mtu ambaye ndanimo nitatengeneza makao yangu ya kwanza, na ndanimo nitasimika huo Ufalme wa Utashi Wangu. Basi, uniache nitawale, na uniachie uhuru wangu kamili”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page