Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 32 – Septemba 24, 1933🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 32 – Septemba 24, 1933🖋📄📖📔


Ujikabidhi wangu mikononi mwa FIAT ulikuwa unaendelea. Siwezi nikafanya chochote bila kusikia moyoni ule mlio wa FIAT, ulio ni mvumo wa chini chini wa Uhai Wake; kwangu ingekuwa ni sawa na kukosa uhai kabisa. Ni mlio unaovuma na papo hapo unaleta mwanga, unavuma na kutia nguvu, unavuma na huku unakufanya uonje Uhai Wake ambao unakupasha joto, na halafu unakugeuza na kukuingiza katika Uhai Wake huo. Ni namna gani ewe Utashi wa Mungu ulivyokuwa mpendevu na wa kustaajabisha! Itakuwaje tusiweze kukupenda?

Halafu, nikawa nafuatilia kazi Zake. Kadiri nilivyozidi kuzifuatilia ndivyo nazo zikawa zinamiminika kuja ndani yangu, ili kunionyesha pendo lao na kunisimulia zikisema: ‘Sisi ni kazi zako wewe mwenyewe, na tumewekwa tuwe kwa ajili yako – ebu utuchukue, utubebe na kutufanya tuwe mali yako kabisa, ili katika kila kitu unachotenda uweze kuwa tayari na sisi tuwe daima ni kama kielelezo na mfano’. Na halafu wakati nikifuatilia kazi za Ukombozi, Yesu wangu Mtamu alinipa mapumziko kwa kipindi kifupi na halafu akaniambia:

“Binti Yangu Mwema, katika kazi Zetu zote, kulikuwa daima na Pendo Letu la ziada kwa binadamu. Na kila ziada niliyoitoa ikawa inanisukuma nitengeneze ziada nyingine zaidi. Kwa hiyo, haikuwa imetosha kwa Mimi kushuka toka Mbinguni na kuja duniani ili kumtengeneza upya mwanadamu, bali kila tendo nililofanya, kila Teso, na hata naweza nikasema, na kila pumzi niliyoitoa, vikawa vyote vimeelekezwa kwake. Katika yale Maweza Yangu ya kuona yote, nilimwita, nilimshika Mikononi Mwangu, nilimfinyanga upya, ili kumrejeshea kwenye umbo mpya, na ili kumpatia ule Uhai mpya ambao nilikuwa nimemletea toka Mbinguni. Nilimfanya awe ndugu Yangu halisi, ili nimwingize katika ukoo wa wana wa Baba Yangu wa Mbinguni. Lakini hata hilo peke yake, halikutosha kwa upande Wangu Mimi. Ili kumweka katika usalama zaidi, niliufanya Ubinadamu Wangu uwe ndiyo hifadhi ya kazi zote, hifadhi ya sadaka zote na hata ya hatua zote za mwanadamu. Ebu sasa unitazame ili uone namna ninavyobeba kila kitu ndani Yangu. Ndilo hilo linalonifanya nimpende mwanadamu daima mara dufu zaidi katika kila tendo afanyalo.

Kwa hatu Yangu ya kujimwilisha tumboni mwa Malkia Immakulata, nilitengeneza huu Ubinadamu Wangu, na ndivyo nikajiweka kuwa Kichwa cha familia yote ya binadamu, ili kusudi niwaunganishe wanadamu wote ndani Yangu na hivyo nikawafanye wawe ni viungo vyangu vya mwili. Kwa hiyo, kila wanachotenda ni Changu, na ni ndani ya kaburi moja takatifu la Ubinadamu Wangu Mtakatifu; ninafungilia kila kitu na ninahifadhi hapo ndani kila jema, liwe dogo au kubwa. Lakini je wewe wajua ni kwa nini? Ni kwa sababu kazi zote zinapopita pale ndani Yangu, huwa ninazitilia thamani na tunu sawa kana kwamba zingekuwa ni kazi Zangu Mimi, kana kwamba ni sala Zangu, na sadaka za Kwangu Mimi. Nguvu ya Kichwa huteremkia hadi ndani ya viungo vya mwili wake wote, nguvu hiyo inaviunganisha viungo vyote pamoja, na ninavitilia thamani na tunu ya mastahili Yangu Mwenyewe. Kwa hiyo, Mwanadamu anajikuta akiwa ndani Yangu, na Mimi nikiwa kama Kichwa, najikuta nikiwa ndani yao.

Lakini hata hivyo, unadhani Pendo Langu linafikia kusema ‘inatosha’? La hasha! Sivyo. Haliwezi kufikia kusema ‘basi’. Ni tabia asilia ya Pendo la Kimungu kutafuta daima uvumbuzi mpya wa Pendo, tabia yake ni kuendelea kutoa Pendo na kuendelea kupokea pendo. Kama isingekuwa hivyo, ina maana kwamba tungekuwa tunajenga mpaka na kulifungilia Pendo Letu ndani ya ulimwengu Wetu wa kimungu basi. Lakini kumbe mambo sivyo hivyo. Pendo Letu Sisi ni bahari kuu, na kwa tabia yake asilia, ni lazima liwe linapenda daima. Na hapo unaona hoja kwa nini ninataka Ubinadamu Wangu uwe unafuatwa daima na ule uwanja mpana wa Utashi Wangu wa Kimungu, ambao utakuwa ukitenda mambo ya ajabu kwa ajili ya kuwapenda wanadamu. Ndiyo maana unaweza kuelewa kwa nini kuna hitaji la kuwa na uelewa fika juu yake, na unaona hoja kwa nini Utashi unataka kutawala. Kama hautatawala, utawezaje kuenea na kujaa hata uweze kuonyesha wazi maajabu yake ya Pendo? Basi, angalia uwe makini, na ndipo utaona mambo ambayo Utashi Wangu utayatenda.

"FIAT" - Sahihi halisi ya mkono wa Luisa mwenyewe


Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page