Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 23 – Desemba 18, 1927🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 23 – Desemba 18, 1927🖋📄📖📔


Nilikuwa nikiwazia juu ya lile Pendo Kuu lililotokea wakati Yesu, Chema Changu Kikuu, alipojimwilisha ndani ya tumbo la kimo cha juu kabisa cha yule Bibi Mwenye mamlaka Makuu. Nilikuwa nawaza pia: inawezekanaje kiumbe, hata kama hakina doa lolote lile, kikathubutu kumshika Mungu ndani yake? Na hapo Yesu Wangu mpendevu, akijimudu ndani yangu aliniambia hivi:

“Binti Yangu, Mama Yangu wa Mbinguni alikuwa tayari anao Utashi Wangu. Alikuwa amejaa kabisa na Utashi Wangu hata akawa amejazwa mwanga mkubwa hadi ukawa unafurikia nje. Mafuriko ya huo mwanga nayo yalitengeneza mawimbi zaidi ya mwanga, ambayo nayo yalivimba na kupanda hadi yakawa yanafika kule ndani ya Kifua cha Umungu Wetu. Ndipo Mama wa Mbinguni, kwa nguvu ya ule Utashi Wetu aliokuwa anao tayari, alijifanya Mshindi kiasi cha kufaulu kumshinda Baba wa Mbinguni. Pia aliuteka Mwanga wa Neno na kuuingiza ndani ya mwanga wake kiasi kwamba akamfanya Neno ashuke na kuingia katika tumbo lake na ndani ya mwanga ule ule aliokuwa ameutengeneza kwa nguvu ya ule Utashi Wangu. Mimi nisingeweza kuwa nimeteremka kutoka Mbinguni kama nisingeuona ule Mwanga wa Sisi Wenyewe katika huyu Mama, na kama nisingeuona Utashi wetu ukitawala pale ndani yake. Na kama hali isingekuwa hivyo, tangu dakika ile ya awali, ingekuwa sawa na kuteremkia ndani ya nyumba ya kigeni. Lakini kumbe sasa ilinipasa nishuke na kuingia ndani ya nyumba Yangu. Ilinipasa nipate mahali pa kuteremshia Mwanga Wangu, mahali pa kuteremshia Mbingu Yangu, na pa kuteremshia furaha Zangu tele tele. Huyu Bibi Mwenye mamlaka wa Mbinguni, kwa vile alikuwa anao tayari Utashi Wangu, ndiye kaniandalia Mimi makao haya, yaani, Mbingu hii ambayo haikuwa na tofauti yoyote na Makao Yangu ya Mbinguni. Je wewe hudhani kwamba Utashi Wangu, ndio ambao huwa unatengeneza Paradisi ya Wenyeheri wote?

Basi, ule Mwanga wa FIAT Yangu uliponivutia Mimi niingie ndani ya tumbo lake Mama, na ule Mwanga wa Neno ulipoteremka, Mianga ile ikawa yote inapiga mbizi kwa pamoja na ndipo Bikira Safi, Malkia na Mama, kwa matone machache tu ya damu aliyotoa na kuitiririsha kutoka Moyo wake uliokuwa unawaka, akatengeneza pazia la Ubinadamu Wangu, na ndanimo akauzungushia ule Mwanga wa Neno, na ndani ya huo Mwanga wa Neno alimzungushia Neno Mwenyewe. Lakini kumbe, Mwanga Wangu ukawa mkubwa ajabu, kiasi kwamba Mama Yangu wa kimungu alipokuwa anafunika lile tufe la Mwanga huo ndani ya pazia la Ubinadamu Wangu alilokuwa amenitengenezea, hakufanikiwa kufunika mionzi yote. Kwa hiyo mionzi ikawa inafurikia nje. Jua linapopambazuka, kutoka pale juu penye tufe lake lile, huwa linasambaza mionzi yake ya mwanga juu ya dunia nzima. Linaisambaza ili mionzi hiyo ikafuatilie na kuifikia mimea, maua, bahari, na viumbe vingine vyote, ili ikazipeleke pale kwa vitu hivyo vyote, zile faida zote na yale matunda yote yatokanayo na mwanga. Halafu hilo jua, kutoka pale juu kabisa ya tufe lake, huku likijifanya kana kwamba linajivunia ushindi wake, huwa linajitokeza nje na kuyaangalia yale mema na mazuri ambayo linafanikisha, na linaangalia pia, ule uhai ambao linafaulu kuuleta, na kuuingiza ndani ya kila kitu kilichoangaziwa nalo. Ndiyo kadhalika na Mimi, nilifanya hivyo mithili ya jua: Lakini, zaidi ya hicho ambacho jua linalopambazuka huwa linatenda, ile mionzi ya Mwanga Wangu, ilipofurika nje ya pazia la Ubinadamu Wangu, ilizidi kuendelea kuwafuatilia wanadamu wote, ili kuweza kufikisha, kwa kila mmoja wao, Uhai Wangu, na kila Chema nilichofika kukileta duniani.

Mionzi hiyo ya Mwanga Wangu, toka ndani ya tufe langu, ilimgonga na kumvamia kila mwanadamu. Ilimgonga kwa nguvu kabisa na kumwambia: ‘Nifungulie mlango – ebu chukua sasa Uhai huu niliokuja kukuletea!’. Hili Jua la kwangu huwa halizami, na bado linaendelea kufuata lengo Lake la kusambaza mionzi yake, huendelea kugonga na kugonga kwa nguvu juu ya mioyo, juu ya utashi, juu ya akili za wanadamu, huendelea kugonga tena na tena na tena ili tu niwapatie Uzima Wangu. Lakini kwa sikitiko, ni watu wengi ilioje, wanaonifungia milango yao, wala wasinifungulie kunikaribisha? Na ni wengine wangapi ilioje, wanaothubutu hata kudharau na kuchezea Mwanga Wangu? Hata hivyo, Pendo Langu ni kuu hivi, kwamba licha ya hayo yote, Mimi sifikii kughairi. Mithili ya jua ninaendeleza pambazuko Langu endelevu la kutoa Uhai kwa wanadamu”.

Baada ya hapo nikawa naendelea na matembezi yangu ndani ya Utashi wa Mungu. Yesu Wangu akaendelea kuniambia:

“Binti Yangu, kila unabii niliokuwa nimeutoa kwa Manabii Wangu mbalimbali, mintarafu Ujio Wangu duniani, ulikuwa ni kama azimio na ahadi Yangu kwa wanadamu juu ya kuja Kwangu na kufika kukaa kati yao. Na Manabii Wangu, kwa njia ya mifano yao mbalimbali, waliweza kuwaandaa watu kutamani na kutarajia Chema Kikuu cha jinsi hiyo. Na watu hawa, kwa kupokea unabii ule mbalimbali, ndio waliipokea ile hazina ya ahadi Yangu. Na jinsi nilivyoendelea kudokeza muda na mahali pa kuzaliwa Mimi, ndivyo nilizidi kuthibitisha ile ahadi niliyokuwa nimeitoa.

Ndivyo hivyo ninavyofanya mintarafu Ufalme wa Utashi Wangu. Kielezo na Mifano ninayoonyesha juu ya FIAT Yangu ya Kimungu, huwa ni ahadi ninayozidi kutoa. Kila ufahamu na uelewa juu ya FIAT ya Mungu huwa ni rehani nyingine mpya ninayoongeza. Na kama nazidi kutoa ahadi Zangu, hiyo ni ishara kwamba, kama vile Ufalme wa Ukombozi ulivyofika, na ndivyo utakavyofika Ufalme wa Utashi Wangu.

Maneno Yangu na Uhai mbalimbali ninavitoa kutoka ndani Yangu. Na uhai ni budi uwe na makao yake na budi ulete matokeo yake. Je wewe unadhani kuwa kielelezo kimoja cha ziada, au kielelezo kimoja pungufu, ni suala dogo? Hiyo ni ahadi moja ya ziada ambayo Mungu ndiye huwa anaitoa. Na Ahadi Zetu haziwezi zikapotea kamwe. Na jinsi tunavyozidi kuzitoa Ahadi zaidi, ndivyo unavyozidi kukaribia ule muda wa kuzitekeleza Ahadi Zetu hizo, na pia muda unakaribia wa kuzihifadhi mahali pa usalama.

Ni kwa sababu hiyo, nakutaka wewe uwe makini kweli kweli, na usiachilie kitu chochote kikutoroke. Vinginevyo utakuwa unaachilia Ahadi ya Mungu ikutoroke, na hilo lingeleta athari fulani”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page