Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Novemba 19, 1926🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 20 - Novemba 19, 1926🖋📃📖📔


Yesu Wangu Mpendevu wa daima, huku akinivutia mimi ndani ya Utashi Wake mwabudiwa, alinionyesha na kunifanya nionje zile hali Zake za maumivu makali kabisa ambamo utovu wa shukrani wa wanadamu huwa unamwingiza. 

Alitweta kwa uchungu sana akaniambia:

“Maumivu ya Utashi Wangu wa Kimungu hayasemekani, na hayawezi yakaeleweka katika hali ya kibinadamu.

Utashi Wangu upo ndani ya wanadamu wote, lakini sasa hivi upo katika jinamizi la maumivu makali mno na ya kutisha ajabu kwa vile, badala ya wanadamu kuupokea na kuruhusu utawale, na badala ya kuruhusu uendeshe uhai wake ndani yao, wao wanausukumia mbali, wanaukandamiza na wanaunyima uhuru wake wa kutenda chochote, uhuru wa kupumua na uhuru wa kuendesha mapigo yake ya moyo.

Kwa hiyo, ni utashi wa kibinadamu ndio unaotenda mambo, ndio unaopumua kwa uhuru, ndio unaoendesha mapigo ya moyo kadiri unavyotaka.

Kumbe Utashi Wangu upo pale kwa ajili ya kuutumikia utashi wa kibinadamu, upo pale tu kwa ajili ya kuchangia kwenye matendo yao wanadamu, na upo pale kubaki daima ndani ya hayo matendo yao, upo pale ukiteseka kweli, na ukiwa umekabwa pumzi yake na ukereketo wa umivu kali kabisa la tangu karne nyingi.

Utashi Wangu unahema na kugaagaa ndani ya wanadamu, katika jinamizi la kutisha namna hiyo.

Kugaagaa kwake na mihemuko yake ni ile mifadhaiko ya dhamiri, ni kule kudangayika, kukabiliana na vikwazo mbalimbali, misalaba mbalimbali, kuchoka na maisha, na mambo yale yote yanayowahangaisha masikini wanadamu.

Ni kwa vile, Utashi Wangu, kwa njia ya hiyo mihemuko yake, unayo haki ya kuwaita wanadamu wanaoendelea kuusulibisha daima na kuuacha katika huo ukereketo wa umivu.

Utashi Wangu hauna jinsi nyingine ya kutenda kwa vile hauna mamlaka yoyote.

Sijui labda, kama wanadamu watakapojirudi wenyewe, na watakapogundua karaha zinazoletwa kwao na utashi wao mbaya, iwapo wataweza, angalau, kuupatia Utashi Wangu pumzi kidogo na kuupumzisha kutoka hayo maumivu yake makali na ya kutisha. 

Maumivu makali hayo ya Utashi Wangu, yanaleta mateso makali mno, hivi kwamba, hata Ubinadamu Wangu, uliotaka wenyewe uyakabili pale Bustanini Getsemani, ulifikia mahali pa kuomba msaada toka kwa wale Mitume Wangu wenyewe - na ingawa kama huo msaada sikuupata.

Na kutweta Kwangu kulinipelekea kutoka jasho la damu iliyo hai.

Nilipoonja kuwa ninatetereka na kuzimia pale chini ya uzito ulionielemea wa yale maumivu makali mno ya Utashi Wangu, maumivu yaliyodumu kitambo kirefu vile na ya kutisha vile, Mimi niliita na kulilia msaada wa Baba Yangu wa Mbinguni nikimwambia: ‘Baba Yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke’. Katika maumivu mengine yote ya Mateso Yangu, hata kama yalikuwa makali vile, Mimi sikuwahi kusema: ‘Ikiwezekana, maumivu haya yaniepuke’.

Kumbe lakini, pale Msalabani niliweza kulia kwa sauti: ‘Naona kiu’ - Mimi ninaona kiu kutokana na maumivu.

Lakini, katika maumivu haya ya mateso makali ya Utashi Mkuu wa Juu, nilikuwa nikionja ule uzito wote wa yale maumivu ya muda huu wote mrefu, yaani umivu zima la Utashi wa Mungu unaoteseka mno - Utashi wa Mungu unaotweta na kugaagaa katika vizazi vya binadamu. 

Uchungu gani huo! Hakuna teso linaloweza likalingana na hili.

Basi sasa, FIAT Kuu ya Juu inataka kuondokana na hilo.

Imekwisha kuchoka, na kwa gharama yoyote ile inataka sasa kuondokana na umivu hilo lililoendelea na kudumu kwa muda mrefu kiasi hicho.

Na kama unasikia juu ya mapigo ya adhabu, juu ya miji inayoanguka, juu ya uharibifu na mabomoko, hilo si kitu kingine isipokuwa ni mhemko na kugaagaa kunakotokana na umivu lake kali. Kwa vile FIAT haiwezi kuvumilia zaidi, sasa inataka kuifanya familia ya binadamu ionje hiyo hali yake ya maumivu na jinsi yenyewe inavyohema na kugaagaa kwa nguvu ndani yao wenyewe, bila hata mmoja wao kushituka na kuionea huruma.

Kwa kutumia nguvu, pamoja na mhemko wake na kugaagaa kwake, FIAT inataka wanadamu waonje kwamba ipo ndani yao, lakini haitaki tena kuwa katika hali ya maumivu makali - kwamba, inataka uhuru na mamlaka.

Inataka kuendesha uhai wake ndani yao.

Binti Yangu, kwa Utashi Wangu kutotawala, ni vurugu jinsi gani katika jamii! Roho zao huwa kama nyumba zisizokuwa na taratibu - mambo yote yamepinduka juu chini. Harufu ni chafu mno - mbaya zaidi kuliko ile ya mwili unaooza.

Na Utashi Wangu, katika ule ukuu wake, ukuu usioruhusu uweze kujiondoa kutoka hata pigo moja la moyo wa mwanadamu, unaendelea kuteseka kati ya hayo maovu mengi mno. Na hilo linatokea katika mpangilio wa jumla wa watu wote.

Na katika mpangilio wa pekee, hali ni mbaya zaidi: ndani ya watawa, ndani ya wakleri, ndani ya wale wanaojiiti wakatoliki, Utashi Wangu siyo tu unateseka mno, bali unaachwa katika hali ya kupooza kana kwamba hauna uhai wowote.

Oh! Jinsi gani hali hii ilivyo ngumu zaidi.

Na kwa kweli, katika lile teso kali, ninaweza angalau kuhema na kugaagaa, ninaweza kutenda kitu fulani, angalau hapo ninaweza kujifanya nisikike kuwa nipo ndani yao, hata kama nipo katika hali ya teso kali mno.

Kumbe lakini, katika hali ile ya kupooza tu, hapo ninakosa ujimudu wowote ule - inakuwa ni hali ile endelevu ya kifo.

Na kwa hiyo, huwa ni sura ya nje tu ndiyo inaweza kuonekana bado, yaani yale mavazi ya kitawa, kwa vile wanaendelea kuuweka Utashi Wangu katika hali ya kupooza. Na kwa vile wanaendelea kuuweka katika hali ya kupooza, ule undani wa watu hao una hali ya kusinzia tu, kana kwamba mwanga na mema si kwa ajili yao. Na kama wanajaribu kutenda chochote kile kwa nje, hicho huwa ni tupu kabisa bila Uhai wa Kimungu, na mwishowe humalizikia kuwa ni moshi wa majigambo, wa kujikweza wenyewe, na moshi wa kuwapendeza wanadamu wengine. 

Na Mimi, pamoja na Utashi Wangu Mkuu wa Juu, wakati nikiwa bado ndani yao, ninaondoka na kuziacha kazi zao.

Binti Yangu, ni upinzani gani huo.

Ni jinsi gani ningetamani kila mmoja wao aweze kuonja hayo maumivu Yangu ya ajabu kabisa, aweze kuonja ule ukereketo endelevu, aweze kuonja lile pooza ambamo wameuweka Utashi Wangu.

Ni kwa vile wao wanataka kutekeleza utashi wao na siyo Utashi wa Kwangu. Hawataki kabisa kuruhusu Utashi Wangu utawale. 

Hawataki kabisa kuufahamu.

Na hiyo ndiyo hoja kwa nini Utashi Wangu, kwa kule kugaagaa kwake na kwa mhemko wake, unataka kupasua kuta za mipaka yake, ili kusudi, kama wao hawataki kuujua na kuupokea kwa njia za Pendo, basi wafikie kuujua kupitia njia ya Hukumu ya Haki.

Utashi Wangu, ukiwa umekwisha kuchoka na teso kali la karne na karne, sasa unataka kuondoka na kutoka nje, na kwa hiyo, upo ukiandaa njia mbili: ile njia ya sherehe ya ushindi, yaani yale maarifa yake mbalimbali, ile miujiza yake, na yale mema yote yatakayoletwa na Ufalme wa FIAT Kuu ya Juu.

Njia ya pili ni ile njia ya Hukumu ya Haki kwa watu wale wasiotaka kuujua Utashi Wangu kama unafanya sherehe yake ya ushindi. 

Ni juu ya mwanadamu mwenyewe, kuchagua njia atakamoupokea Utashi Wangu”.

Juzuu na. 20 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page