Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Machi 17, 1921🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - JUZUU na. 12 - Machi 17, 1921🖋📄📖📔


Nilikuwa nikimwambia Yesu Wangu Mtamu: ‘Mimi sielewi, kadiri unavyozidi kuniambia mambo utakayonipatia kupitia huo Utashi Wako Mtakatifu, ndivyo mimi ninaonja kuwa duni zaidi na katika hali mbaya zaidi. Nilifikiri kuwa ningeweza kuonja hali bora zaidi, kuwa mwema zaidi, lakini kumbe kila kitu kinakuwa ni kinyume chake’. Hapo Yesu akaniambia:

“Binti Yangu, kadiri ngano ya Utashi Wangu inavyozidi kukua ndani yako, ndivyo utakavyozidi kuonja uduni wa nyasi zako. Ni kwa vile, pale mwanzoni wakati suke linapoanza kupachika, ngano na nyasi huwa vimeungana kuwa kitu kimoja tu; lakini kadiri suke linavyozidi kukua na kuendelea na uhai wake, na wakati ngano nayo inaanza kukua, zile nyasi huwa zinabaki zimetengwa kutoka kwa ngano na zinabaki na kazi moja tu ya kuilinda na kuitetea ile ngano. Kwa jinsi hiyo, kadiri unavyoonja uduni wako, ndivyo ngano ya Utashi Wangu inazidi kukua na kuundika ndani yako na ndivyo inavyokaribia kufikia kuiva na kukomaa kikamilifu. Zile nyasi siyo kitu kingine isipokuwa ni hiyo hali dhaifu ya maumbile yako ambayo, kadiri inavyoendelea kuishi pamoja na utakatifu na utukufu wa Utashi Wangu, ndivyo inazidi kuonja vikali zaidi huo uduni wake”. Halafu aliongeza kusema:

“Ewe Mpenzi Wangu, mpaka hivi sasa wewe ulikuwa umeshika ndani yangu lile jukumu ambalo Ubinadamu Wangu ulikuwa umelishika hapa duniani. Sasa ninapenda nikubadilishie jukumu hilo kwa kukupatia jukumu lingine lililo tukufu zaidi na lililo pana zaidi: yaani, ninapenda kukupatia jukumu lile linaloshika na Utashi Wangu ndani ya Ubinadamu Wangu. Je unaelewa jinsi jukumu hilo lilivyo ni la juu zaidi na tukufu zaidi? Ubinadamu Wangu ulikuwa na mwanzo, lakini Utashi Wangu ni wa milele. Ubinadamu Wangu umezungukwa na mduara na una mipaka, lakini Utashi Wangu hauna mwisho wala mipaka, bali ni mpana na unaenea mithili ya bahari kuu. Kwa kweli nisingeweza kukupatia wewe jukumu lililo tukufu zaidi na lililo la pekee zaidi kuliko hilo!”.

Niliposikia hilo mimi nikawa nimesema: ‘Ewe Yesu Wangu Mtamu, mimi siwezi kuelewa kwa nini Wewe una penda kunipatia mimi jukumu kama hilo, na wala sijatenda chochote kabisa ambacho kingenistahilisha kupata upendeleo huo mkubwa”. Ndipo Yesu akasema:

“Hoja yote ya neno hilo ni katika Pendo Langu, udogo wako, na kule kuishi kwako pale mikononi Mwangu kama kichanga, ambaye hafikirii chochote kile isipokuwa juu ya Yesu Wako basi, ile roho yako ya kutonigomea kamwe sadaka iwe yoyote ile ambayo nimewahi kukuomba. Mimi huwa sitekwi na mambo makubwa makubwa kwa vile katika hayo ambayo huonekana kuwa makubwa, ndanimo daima kuna kilicho cha kibinadamu. Katika mambo yaliyo madogo, yaani madogo kwa kuonekana kwa nje, lakini kwa yenyewe huwa ni makubwa. Halafu, ulipasika kulielewa hilo wewe mwenyewe, kwamba, nilipasika nikupatie wewe utume wa pekee ndani ya Utashi Wangu: nimekueleza mara zote juu ya Utashi Wangu, nimekujulisha na kukuelewesha yale matokeo ya ajabu. Na jambo hilo sijawahi kulifanya kwa mtu mwingine yeyote mpaka hivi sasa. Kwa kweli nimekutendea wewe kama mwalimu anapotaka mwanafunzi wake afanikiwe kikamilifu, iwe katika uganga, au katika historia au katika taaluma nyingine: utadhani mwalimu huyo hajui lingine la kuzungumzia kwani huwa anarudia kugonga juu ya neno lile lile daima. Ndivyo nilivyofanya hata mimi kwa wewe: Nimejitahidi kuwa Jalimu wa Utashi wa Mungu, kana kwamba ningesahau mambo mengine yote yaliyobaki. Na baada ya kukufundisha vema sana sana, nimekufunulia na nimekuonyesha utume wako, na jinsi ndani yako wewe kutakuwa ule mwanzo wa utimilifu wa Fiat Voluntas Tua kwa hapa duniani. Jipe moyo, Binti Yangu, kwani naona unakata tamaa. Usiogope, wewe utapata Utashi Wangu wote utakaokuwa ni msaada kwako na tegemeo lako”.

Na alipokuwa akisema hilo, alikuwa anapitisha mikono Yake juu ya kichwa changu, juu ya uso wangu, na juu ya moyo wangu, kama vile alitaka kuthibitisha hicho alichokuwa akizungumzia. Halafu alififia.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page