Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Desemba 22, 1921🖋📄📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 13 - Desemba 22, 1921🖋📄📖📔


Wakati nikiendelea kuwa katika ile hali yangu ya daima, Yesu Mpendwa Wangu wa daima alijitokeza akiwa ndani ya mwanga mkali kabisa unaochoma. Mwanga huo, pindi ukiyeyuka kuwa mvua ya mwanga, ukawa unawanyeshea watu. Hata hivyo watu wengi hawakuupokea huo mkondo wa mwanga kwa vile walikuwa kama vile wamefunga mioyo yao. Na ndipo ule mkondo ulitiririka kwenda kule ambako uliwakuta watu waliokuwa wazi na tayari kuupokea. Ndipo hapo Yesu Wangu Mtamu aliniambia:

“Binti Yangu, ule mkondo wa neema Yangu huwa unaingia kwa watu wale ambao wanatenda kufuata pendo lililo safi. Peke yake, lengo la kunipenda Mimi, ndilo linawafanya watu wawe na moyo wazi wa kuupokea mkondo wa neema Zangu zote. Pendo ni Mimi - pendo ni wao. Kwa hiyo wao wapo katika mikondo endelevu kwa ajili ya Mimi, na Mimi kwa ajili yao. 

Kinyume chake, wale ambao hutenda mambo kwa nia ya kibinadamu tu, hao wana mioyo iliyofungwa dhidi ya Mimi. Mkondo wao umefunguka wazi kwa mambo yote yaliyo ya kibinadamu, na wanapokea mkondo wa mambo yale yaliyo ya kibinadamu. Mtu anayetenda mambo kwa nia ya kutenda dhambi, huyo anapokea mkondo wa kosa. Na yule atendaye kwa nia ya ibilisi, huyo anapokea mkondo wa motoni. Nia ya kutenda kitu ndiyo inayompa mtu rangi na madoa tofauti tofauti. Nia huwa inamgeuza mtu, au kufanya mzuri au kumfanya mchafu. Au awe mwanga au awe giza. Au katika utakatifu au katika dhambi. Namna yoyote ile ya lengo la kutenda jambo ndiyo hiyo ni aina ya binadamu. Ndiyo maana mkondo Wangu Mimi hauingii ndani ya kila mmoja. Na kwa vile huwa unakataliwa na watu wale waliofunga mioyo yao dhidi ya Mimi, mkondo Wangu huo hutua mzigo wake wa neema, kwa nguvu na kwa utele zaidi, kwa watu wale ambao wana moyo wazi Kwangu”.

Baada ya kusema hayo, Yesu alififia. Lakini punde tu baadaye alirejea akaongeza kusema:

“Je wewe unaweza ukanieleza kwa nini jua huwa linaiangaza dunia nzima? Ni kwa sababu lenyewe ni kubwa zaidi kuliko dunia.  Na kwa vile ni kubwa zaidi, linao uwezo wa kumeza, ndani ya mwanga wake, ile duara yote ya dunia.

Kama lingekuwa ni dogo zaidi, lingekuwa linaangaza sehemu tu ya dunia, lakini siyo dunia nzima. Kwa hiyo, mambo madogo ndiyo yanazungukwa na yanamezwa na yale yaliyo makubwa zaidi. Sasa, Utashi Wangu ni mkubwa kabisa kupita fadhila zote. Kwa hiyo fadhila zote hubakia zimenyaukia na kufifia ndani ya Utashi Wangu. Aidha, mbele ya fadhila ya utakatifu wa Utashi Wangu, fadhila nyingine huwa zinatetemeka zikitoa heshima kwa Utashi Wangu. Na ikitokea kwamba, bila ya Utashi Wangu, fadhila zikadhani kwamba zenyewe zinatenda jambo fulani kubwa, mara zitakapokutana na utakatifu pamoja na nguvu ya fadhila ya Utashi Wangu, fadhila hizo zitatambua kwamba zenyewe hazijatenda lolote. Na ili kuweza kuzipatia tabia au alama ya fadhila, Mimi huwa ninalazimika kuzitumbukiza ndani ya bahari kuu ya Utashi Wangu. Utashi Wangu sio tu unazishinda na kuzipita fadhila zote, bali ndio unaoleta zile tofauti tofauti za uzuri zilizopo ndani ya fadhila mbalimbali. Utashi Wangu ndio huwa unazitilia zile rangi, na yale mapambo mbalimbali ya Kimungu, ule mng’ao wa kimbingu, na ule mwanga unaoangaza na kuchoma. Basi, kama fadhila hazijafunikwa kwa Utashi Wangu, zinaweza zikawa ni njema, lakini haziwezi zikawa na ule uzuri upendezao na unaozivuta, unaoziteka na unazozilewesha Mbingu na dunia”.

Basi, baada ya muda, Yesu Wangu Mtamu alinichukua na kunipeleka nje ya nafsi yangu. Alinieleza kuwa mifereji ya maji ilikuwa ikifunguka pale chini ya bahari. Mifereji hiyo, kwa kuelekea chini ya ardhi, ilikuwa inajaa na kupita kuosha misingi ya miji - na kwa hiyo katika sehemu fulani fulani, majengo yalikuwa yakibomoka na kuanguka, na mahali pengine zaidi, mifereji hiyo ilisababisha majengo kufifia kabisa. Wakati mifereji hiyo ya maji ilipofunguka, maji yaliyazoa majengo hayo na kuyafukia ardhini. Yesu, akiwa katika masikitiko makubwa alisema:

“Binadamu hataki kusitisha jambo hili. Hukumu Yangu ya haki inalazimika kumpiga. Ni miji mingi itakayopigwa na maji, itakayokabiliwa na moto, na itakayokabiliwa na matetemeko ya ardhi”.

Ndipo mimi nilijibu: ‘Ewe Pendo Langu, unasema kitu gani? Utatekeleza hilo’. Na mimi nilipokuwa nataka kumwomba, Yeye alififia.

Juzuu na. 13 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page