Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Septemba 15, 1922🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 14 - Septemba 15, 1922🖋📃📖📔


Lilikuwa likiendelea zoezi la kunakilisha, kutoka katika Makala zangu, yale mambo aliyoniambia Yesu mintarafu fadhila mbalimbali. Nilionja moyo wangu ukigoma kabisa hivi hata nikawa naonja kufa. Moyoni mwangu nikasema:

'Kwa watu wengine, orodha ya vitu na mambo huwa vinaandikwa baada ya kufa kwao. Kwangu Mimi peke yangu imeniangukia kura ya kuiandaa mimi mwenyewe hiyo orodha wakati nikiwa bado hai. Ah, Ee Bwana, nipe nguvu ya kuweza kuitekeleza hiyo sadaka!’. 

Halafu tulifikia mahali ambapo Padre Mwungamishi alinieleza namna ya kuzihifadhi hizo Makala zangu wakati zitakapokuwa zimechapishwa. Oh! Mungu Wangu, maumivu yalioje. Kweli nilionja kuchukizwa hadi kwenye kina cha uboho wa mifupa yangu. Na Yesu Mhimidiwa aliponijia na kuniona nimechukizwa kiasi kile, aliniambia:

 “Binti Yangu, kuna nini? Kwa nini unajitesa kiasi hicho? 

Ni utukufu Wangu, na heshima Yangu, ndiyo inayodai jambo hilo, na wewe budi ulifurahie neno hilo.

Kwani wadhani kuwa ni wanadamu ndio wanaolitaka hilo, au wanaolitenda hilo, au wanaokuamrisha wewe? La hasha, hapana.

Ni Mimi hapa, ndiye ninayevamia mambo yote. Ni Mimi ndiye ninayewasukuma na ninayewaangaza.

Na mara nyingi sana huwa sisikilizwi.

Vinginevyo wangekuwa wanaharikisha zaidi na wangeonyesha hamu zaidi.

Mimi huwa ninalazimika kuwasukuma kwa nguvu zaidi ili Utashi Wangu uweze kutekelezwa. Wewe unaweza pengine ukasubiri hadi baada ya kifo chako, lakini Utashi Wangu hautaki kusubiri.

Aidha, ni kweli kwamba wewe una kile kiunganisho, yaani kile kipandikizi katika Utashi Wangu, lakini hapa si suala la wewe - bali ni suala la Mimi.

Ni suala la kufanya watu wayajue matokeo, sifa, na thamani iliyopo ndani ya Utashi Wangu unaotenda kazi ndani ya mwanadamu, wakati mtu anapoishi ndani yake.

Halafu, endapo wewe hutapenda kujishughulisha na jambo hilo - wewe ujuaye ni jinsi gani ninavyolithamini, na jinsi gani ninavyotamani kwa hamu kubwa yajulikane kwa watu yale matokeo ya Utashi Wangu, matokeo ambayo kwayo Mimi nitaweza kupokea utukufu timilifu wa Uumbwa na utimilifu wa Ukombozi wenyewe...........

Oh! ni matokeo mengi mangapi ambayo bado yamesimama yakisubiriwa, matokeo ya aina zote mbili, ya Uumbaji na yale ya Ukombozi, kwa vile tu Utashi Wangu haujajulikana bado, na kwa vile bado haujapata Ufalme wake wa kweli ndani ya mwanadamu. 

Na maadam Utashi Wangu hautawali bado, utashi wa binadamu hubaki daima kama mtumwa kwake wenyewe.

Je, wewe unadhani kwamba watu wengine watapenda kushughulikia jambo hilo baada ya kifo chako? 

Oh! Ni mambo mengi mangapi, ambayo nilikuwa nimeyaeleza kwa watu, na yakabaki yamezikwa kwa kukosekana watu wenye kupendelea kufuatilia kazi Zangu! 

Hata hivyo, kama niliweza kuvumilia hayo kuhusu mambo mengine, sitaweza kuvumilia hili suala la Utashi Wangu.

Nitatoa neema nyingi kabisa kabisa kwa wale watakaojitoa kuanza kufanya kazi, kiasi kwamba, hawataweza kunigomea.

Hata hivyo, sehemu ya kufurahisha sana, na muhimu kabisa ya kazi hiyo, nataka itoke kwako wewe”.

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page