Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 19 - Agosti 1, 1926🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu Na. 19 - Agosti 1, 1926🖋📃📖📔


Nilikuwa nikimtamani sana Yule aliye ni Chema Changu Mtamu, aliye ni Uhai wa uhai wangu. Kwa vile hakuwa anafika, basi nikawa ninawaza moyoni mwangu: ‘Ni jinsi gani ilivyo ngumu kumkosa Yeye. Ah! Yesu hanipendi tena. Siyo tu kwamba yamekwisha yale mapapaso, yale mabusu, na hata vile vitendo Vyake, vilivyokuwa ni ishara kubwa za pendo alilokuwa akinipatia kwa uwingi kabisa pale mwanzoni, bali hata ule uwepo Wake mpendevu na wenye kuniteka mimi sasa ni kitu cha kungojea kwa muda mrefu sana”. Ee Mungu, ni masikitiko yalioje! Ni kifodini endelevu kilioje.....! Ni maisha yaliyoje bila uhai, bila hewa, na bila pumzi....! Ewe Yesu Wangu, unihurumie mimi, mie niliye mhanga mdogo wa uhamishoni. Lakini nilipokuwa nikiwaza hilo na mengineyo, Yesu Wangu Mpendevu wa daima alijitokeza kutoka ndani mwangu, na huku akiegemeza mikono Yake juu ya kifua changu, aliniambia:

“Binti Yangu, wewe unajidanganya sana unaposema kwamba Mimi sikupendi kama pale mwanzoni. Kwa kweli inakupasa kujua kwamba yale mabusu Yangu, mapapaso, na vile viashiria vya mapendo nilivyokuwa nikikutendea, vyote hivyo vilikuwa ni namna ya kujimwaga kwa Pendo Langu ambalo, kwa Mimi kutoweza kulizuia na kulivumilia ndani Mwangu, nikawa ninalionyesha kwako wewe kwa njia ya ishara nyingi sana za upenzi. Na kwa vile, kati ya wewe na Mimi hapakuwepo kazi kubwa ya kutenda, Mimi nikawa ninajiburudisha na wewe kwa njia ya ishara nyingi sana na mbinu nyingi sana za Pendo. Lakini, hiyo yote ilikuwa ni njia ya kukuandaa wewe kwa ile kazi kuu ambayo ilitakiwa itekelezwe kati ya wewe na Mimi. Na wakati wa kufanya kazi, huwa hatuna nafasi ya kujiburudisha. Lakini licha ya hayo, Pendo halikomi, bali linarudufiwa mara mia na mia, linathibitishwa na linafungwa kwa kugongwa mhuri juu yake.

Sasa, ewe Binti Yangu, baada ya kukuonyesha wewe jinsi ya kujimwaga kwa Pendo Langu lililokuwa ndani Mwangu, nimependa nichukue hatua nyingine ya kukupatia kile nilichokuwa nimekibeba ndani Yangu, nimependa nikushirikishe ile siri kuu ya Ufalme wa Utashi Wangu, kwa njia ya kukupatia yale mema yaliyopo ndani ya huo Ufalme. Na wakati tunaposhirikisha siri zilizo ni muhimu kabisa - na kwa vile hiyo ndiyo siri kuu kupita zote katika historia ya Uumbwa - kwa kawaida huwa tunaweka kando mambo ya burudani, mambo ya mabusu, mambo ya mipapaso. Na hasa hasa, kwa vile ile kazi ya Ufalme wa Utashi Mkuu wa Juu ni tukufu mno, na ndiyo kazi kuu kabisa inayoweza kupatikana katika duniani nzima. Kwa sababu hiyo, tendo la Mimi kukuonyesha ile siri Yangu, linashinda na kupita aina zote za mapendo mbalimbali ukiyajumlisha pamoja, kwa vile katika ile siri kuna kushiriki katika uhai Wangu wenyewe, na ushiriki katika mema Yangu Mwenyewe. Katika ile siri kuna kuaminiana na kuna kutegemezana. Na, je wewe unadhani ni kitu kidogo kwamba Yesu Wako anakuamini wewe na kwamba wewe ndiye mlengwa wa matumaini Yangu? Na wala si suala la bora kuaminiana na bora kutumainiana. Ni suala hasa la ile imani ya Mimi kuweza kukuaminisha na kukukabidhi Ufalme wa Utashi Wangu, na ni suala la matumaini kwamba wewe utaweza kuhifadhi haki za Utashi Wangu katika usalama, na kwamba wewe, kwa ajili Yangu Mimi, utaufanya ujulikane kwa watu.  Sasa, nikiisha kukuaminisha ile siri ya Utashi Wangu, na huu Utashi Wangu ukiwa ndiyo sehemu muhimu kabisa ya Uhai wa Mungu, Mimi nisingeweza kukifahamu kitu cha kukupatia wewe kilicho ni kikuu zaidi ya hicho. Sasa wewe unawezaje kusema eti Mimi sikupendi tena kwa kiwango kile cha awali? Kumbe lakini, ingekupasa wewe uwe unasema kuwa hiyo ni ile kazi kuu ambayo inatakiwa kwa upande wako na kwa upande Wangu katika Ufalme wa Utashi Wangu. Ni budi ukajua kuwa Mimi huwa ninakushughulikia daima na huwa nipo makini kabisa kuendelea kutenda mambo ndani yako wewe: mara ninapanua na kukuza maweza yako, mara ninakufundisha na kukuelewesha, mara nyingi huwa ninatoka na kuja kufanya kazi pamoja na wewe, na wakati mwingine ninatenda mambo badala yako wewe. Kijumla, Mimi ninakushughulikia daima, na hiyo ndiyo kusema kuwa ninakupenda zaidi na zaidi - lakini, ni kwa pendo la nguvu zaidi na lenye uhalisia zaidi”.

Juzuu na. 19 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here

Report Page