Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 14 - Septemba 9, 1922🖋📃📖📔

Yesu kwa Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA Binti Mdogo wa Utashi wa Mungu - KITABU cha MBINGU - Juzuu na. 14 - Septemba 9, 1922🖋📃📖📔


Yesu Wangu Mtamu wa daima anaendelea kuzungumzia juu ya Utashi Wake Mtukufu. Alinionyesha Moyo Wake ukiwa umefunguliwa na wazi. Kutoka humo vilikuwa vikitoka vijito vidogovidogo vya mwanga uliokuwa ukiwajeruhi wanadamu wote. Na kwa vile ulitengeneza mtandao, ule mwanga ulienea na kufunika kila kitu. Na Yesu, alipoanza kuzungumza, akawa ameniambia:

“Binti Yangu, katika kumwumba yule binadamu wa kwanza ndivyo nilivyoweka mwanzo kwa Uumbaji wa kizazi cha binadamu. Na baada ya kuumba mwili, Mimi, kwa pumzi Yangu yenye enzi, nilimvuvia roho, na naweza nikasema kuwa, kwa pumzi Yangu nyingine, nilivuvia Nafsi Yangu Mwenyewe ndani ya kina cha binadamu ili niweze kumtawala, kumwamrisha na kumlinda. Kwa jinsi hiyo, yule binadamu akawa ametengeneza ufalme kwa ajili Yangu, na kwake yeye, Mimi nilipasika kuipanua, kuieneza na kuifikisha kwake mipaka Yangu. Furaha Yangu kubwa na iliyofikia kilele ilikuwa ni kuona uzalishwaji wa viumbe vingine vingi kabisa ndani ya binadamu huyo. Uzalishwaji huo ulikuwa ukiendelea karibu bila ukomo wowote, na ulitakiwa uniletee Mimi himaya nyingine nyingi kulingana na idadi ya wanadamu ambao wangepasika kuzaliwa na kujitokeza kwenye mwanga wa jua. Na katika himaya hizo Mimi nilipasika tena kutawala na kuendelea kueneza na kupanua mipaka Yangu ya kimungu. Na mema yote ya hizo himaya nyingine yalitakiwa yafurike, na yatoe na kuongeza, utukufu na heshima ya ule ufalme wa kwanza, ambao, ulitakiwa uwe ndiyo kichwa kiongozi, na pia, kama ndiyo tendo la kwanza la Uumbwa. Kwa bahati mbaya, kwa lile tendo la binadamu kujiondoa kutoka Utashi Wangu, ule ufalme Wangu na ufalme wa binadamu vilikwisha. Na siyo hilo tu, bali binadamu alinikanyaga, na katika ile nafasi Yangu, alijiweka atawale yeye mwenyewe, na kwa kujifanya mwenyewe kuwa mungu, alitengeneza ufalme wa madhambi, wa matatizo, ufalme wa madhila na wa mabomoko na maporomoko. Furaha Yangu ikawa imekufa wakati wa kuzaliwa kwake, na iligeuka kuwa ni maumivu. Angalia, ubaya wote haukuwa kitu kingine, isipokuwa ilikuwa ni lile tendo la kujiondoa toka kwenye Utashi Wangu.

Hata hivyo, Pendo Letu halikukoma pale. Mimi sikupenda niwe Mungu ninayejitenga peke Yangu, hapana, na kwa hiyo, nikapenda kuteremka kutoka Mbinguni na kuja kuchukua Ubinadamu ulio sawa na ule wa binadamu wa kwanza. Ndani ya Ubinadamu huo nilifungilia Uumbwa wote.  Halafu niliuchomelea utashi wa kibinadamu wa huo Ubinadamu Wangu na kuuunga kwenye Utashi wa Mungu, ili kusudi, huo utashi wa kibinadamu, ukiwa unakumbatia na kubeba Uumbwa wote pamoja na matendo yao yote, ndani ya huo Utashi wa Mungu, upate kuniletea Mimi pale mbele ya Kiti Changu cha Ufalme, kama ndiyo mshindi wa matendo yote ya kibinadamu, ambayo, sasa yamegeuzwa na Utashi Wangu, na kuwa ni matendo ya Utashi Wangu wenyewe. Kwa hatua hiyo, utashi wa kibinadamu ulikuwa unaanza kuubeba na kuumiliki Utashi wa Mungu, na Utashi wa Mungu ulianza kuumiliki utashi wa kibinadamu. Utashi moja ulikuwa unaumiliki utashi mwingine. Ni kwa vile, pale ambapo nafsi moja pamoja na nafsi nyingine zinapounganika na kutengeneza kitu kimoja pekee, na endapo moja ya nafsi hizo ni mmiliki, basi na ile nafsi ya pili, kwa mujibu wa asilia-shirikishi, itakuwa nayo ni mmiliki pia.  Hiyo ndiyo ilikuwa hoja Yangu pekee, iliyonifanya nitoe amri na agizo kwa binadamu ya kutogusa lile tunda lililokatazwa Nami: Nilikuwa nimetaka, kwa upande wa utashi wake binadamu, afanye tendo la sadaka ndani ya Utashi Wangu, ili, sadaka hiyo, itakapochomelea na kuunganisha utashi wake na Utashi Wangu, basi utashi wake umilikishwe Utashi Wangu, na Mimi ningemilikishwa ule wa kwake, na hivyo tashi zote mbili, zingetawala kwa Maweza yale yale, kwa Hekima ile ile, na kwa Wema ule ule. Mimi sikumtaka binadamu mwenye tofauti yoyote kutoka Kwangu Mimi: yeye alikuwa ni mzao Wangu, alikuwa ni mwana Wangu. Kwani ni baba gani asiyependa mwana wake awe tajiri na mwenye furaha kama yeye mwenyewe? Mimi ni zaidi kabisa, niliye ni Baba wa Mbinguni, na wala nisingepoteza chochote kile kwa tendo la kumfanya huyo mwanangu awe tajiri, mwenye furaha na mtawala sawa kama Mimi!

Toka hapo, baada ya binadamu kuvunja na kutenganisha utashi wake kutoka Utashi wa Kwangu, Pendo Langu halikutulia bali liliwaka moto zaidi na kupandisha juu zaidi miali yake. Kwa gharama yoyote ile Mimi nilitamani kuzalisha Mimi Mwingine, na ndipo nikawa nimechagua Ubinadamu Wangu, ambao, kwa kujitolea kila kitu, na kukabidhi yote, kwa Utashi Wangu, ulitwaa milki juu ya Utashi Wangu, na hivyo kunifanya Mimi nitimize ndani yake lile lengo la Uumbwa wa binadamu. Kwa vile Mimi nimezoea kutekeleza mipango Yangu mikuu kabisa kwa kutumia mtu mmoja tu, na hatimaye huwa ninaisambaza hiyo mipango, sasa je si ndiyo mtu mmoja tu ndiye aliyeharibu mipango Yangu yote? Halafu, ni Ubinadamu Wangu pekee ndio uliopasika kunirekebishia uharibifu wote huo. Maweza ya Utashi Wangu, uliofungilia, ndani ya Ubinadamu Wangu, ule Uumbwa wote, yalipasika kunifanya Mimi nirejeshe aina zote za Mapendo, nirejeshe na mabusu, na mipapaso, vyote ambavyo yule binadamu wa kwanza alikuwa amevikatalia na kuvisukumia mbali. Pendo Langu, naweza nikasema, likivua mavazi yake ya mateso na ya machozi, lilijivika hatimaye vazi la sherehe, na kama mshindi liliingia katika raha za kupindukia, na katika wendawazimu wa Pendo. Kwa jinsi hiyo, ninapotaka kutekeleza kazi fulani pamoja na mwanadamu, huwa ninaanza daima na uhusiano wa ana kwa ana, yaani uhusiano wa wewe kwa wewe, kana kwamba pasingekuwepo na mwingine. Kishapo huwa ninaipanua hiyo kazi kwa upana kabisa hata kuweza kujaza Mbingu na dunia.

Basi, Binti Yangu, Pendo Langu linataka kuzalisha kwa mara nyingine. Kwa vile huwa linatoa kwa kiwango cha kupindukia, lenyewe linatoka nje na kungojea, linatamani kutoa washirika wengine wapya. Na kile ambacho lilitenda ndani ya Ubinadamu Wangu, yaani tendo la kuufungilia Uumbwa wote ndanimo, ili kusudi kila kitu kiweze kutoa kwa Mungu Baba, kile ambacho Yeye alikitamani na alikitegemea kutoka kwa huo Uumbwa, na papo hapo, ili kusudi Ubinadamu Wangu uwezeshe kuteremsha kila kitu kwa manufaa ya Wanadamu Wote. Pendo Langu linatamani kulirudia tendo hilo. Basi, kwa kuchomelea na kuunganisha utashi wako kwenye Utashi Wangu, Mimi nanuia kufungilia ndani yako ule Uumbwa wote, na kwa kukumilikisha Utashi Wangu, ninataka niwe ninaonja kurudiwa kwa yale matendo Yangu, kurudiwa kwa Pendo Langu, na kwa maumivu Yangu. Ninataka uwe ni kioo Changu cha kujitazamia hapa duniani. Ninapokitazama kioo hicho, Mimi niwe ninauona Uumbwa ule niliokuwa nimeuumba pale Mbinguni, na ambao, Ubinadamu Wangu ukawa umeufungilia ndani yako wewe kama ndani ya kioo. Na Mimi, ninapojitazama na kujiona niweze kuutambua huo Uumbwa ndani yako wewe. Wewe na Mimi tutakuwa katika uhusiano endelevu wa kuonana mithili ya kwenye kioo: Nitafanya kuwa, Mimi niwe ninaonekana ndani yako, na wewe uwe unaonekana ndani Yangu. Mimi nitakuwa nikionekana toka Mbinguni na wewe utakuwa unaonekana toka duniani. Basi, Pendo Langu litakuwa likiridhika pale nitakapokuwa nikiona, ndani ya kiumbe kimoja, siyo tu sura ya Ubinadamu Wangu, bali pale, nitakuwa nikiona pia, kila kitu ambacho Umungu Wangu ulikuwa umetenda ndani ya Ubinadamu Wangu. Basi uwe makini na uwe unafuata Utashi Wangu”.

Juzuu na. 14 ku download - click here

Kila siku, hatua kwa hatua, jisomee hapa, ili upate kukua katika Paji la Uhai, ndani ya UTASHI WA MUNGU, kulingana na Mafundisho aliyoyatoa YESU kwake Mtumishi wa Mungu LUISA PICCARRETA

Swahili - Telegram Channel: Utashi Wa Mungu Na Upendo Wa Mungu

Swahili - Telegram Channel: Saa 24 Za Mateso Ya Bwana Weto Yesu Kristo

English - Telegram Channel: Divine Will Divine Love

English - Telegram Channel: The Virgin Mary in the Kingdom of the Divine Will

Français - Chaine de Telegram: Divine Volonte Divin Amour

Français - Chaîne de Telegram: Lettres de Luisa Piccarreta

Lingala - Chaine de Telegram: Mpo Elingi Nzambe Bolingi bwa Nzambe

Website all languages: www.divinewilldivinelove.com

Vitabu yote vilivyo katika faili za PDF vinaweza kupakuliwa bila gharama yoyote ile wakati wote ule. Pia, upo huru kabisa kuchapisha VITABU hivyo wewe mwenyewe binafsi au kuchapisha kwenye kiwanda chochote kile. Lakini vitabu hivyo ni kwa matumizi binafsi tu na siyo kwa ajili ya biashara! Hata hivyo una ruhusa ya kuwashirikisha na kuwapatia watu wengine vitabu hivyo kadiri unavyopenda!!

Swahili landing page: click here

English landing page: click here

Lingala landing page: click here

Kikongo landing page: click here

French landing page: click here

Italian landing page: click here


Report Page