@Ribbiyyuwna

@Ribbiyyuwna


 

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠﴾

50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala kwamba najua ya ghayb; na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale nilofunuliwa Wahy.” Sema: “Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona? Basi hamtafakari?”

 

 

 

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١﴾

51. Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb wao; hawana badala Yake mlinzi wala mwombezi - huenda wapate kuwa na taqwa.

 

 

 

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾

52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata ukawafukuza; utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu.[3] 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗأَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣﴾

53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: “Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu?” Je, kwani Allaah Hajui zaidi wanaoshukuru?

 

 

 

وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤﴾

54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayaat Zetu basi sema: “Salaamun ‘alaykum! Rabb wenu Ameandika juu ya Nafsi Yake rahmah; kwamba yeyote miongoni mwenu atakayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥﴾

55. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat na ili idhihirike njia ya wakhalifu.

 

 

 

قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙقَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ﴿٥٦﴾

56. Sema: “Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale mnaowaomba asiyekuwa Allaah.” Sema: “Sifuati hawaa zenu (kwani nikifuata,) kwa yakini nitakuwa nimepotoka, hapo nami sitokuwa miongoni mwa walioongoka.”

 

 

 

قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾

57. Sema: “Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki; Naye ni Mbora wa wenye kuamua hukumu.”

 

 

 

قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨﴾

58. Sema: “Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka lingehukumiwa jambo baina yangu na baina yenu. Na Allaah Anawajua zaidi madhalimu.”

 

 

 

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

59. Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٦٠﴾

60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni kuhusu yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ﴿٦١﴾

61. Naye ni Mwenye kudhibiti juu ya waja Wake, na Anakutumieni Malaika wanaohifadhi hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.

 

    

  

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ﴿٦٢﴾

62. Kisha hurudishwa kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu.

 

 

 

قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣﴾

63. Sema: “Nani Anakuokoeni kutoka viza vya bara na bahari mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri” (mkisema): “Akituokoa kutokana na (janga) hili; bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.”

 

 

 

قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤﴾

64. Sema: “Allaah Anakuokoeni katika hayo na katika kila janga; kisha nyinyi mnamshirikisha.”

 

 

 

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥﴾

65. Sema: “Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu (vurugu la) nguvu za wengineo.” Tazama jinsi Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat wapate kufahamu.

 

 

 

وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦﴾

66. Na wakaikadhibisha (Qur-aan) watu wako na hali ni haki. Sema: “Mimi si mdhamini wenu.”

 

 

 

 

لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٦٧﴾

67. Kwa kila khabari ina wakati maalumu, na mtakuja kujua.

 

 

 

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾

68. Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika Aayaat Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.

 

 

 

وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ﴿٦٩﴾

69. Wala si juu wale wenye taqwa, kuwa wana jukumu nao (makafiri) kwa lolote, lakini ni ukumbusho ili huenda wapate kuwa na taqwa. 

 

 

 

وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٧٠﴾

70. Na waachilie mbali wale walioichukua Dini yao mchezo na pumbao, na ukawaghuri uhai wa dunia, basi wakumbushe kwayo (Qur-aan) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma, haina pasi na Allaah mlinzi wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma; watapata kinywaji cha maji ya kutokota na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakiyakufuru.

 

 

 

قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

71. Sema: “Je, tumwombe asiyekuwa Allaah ambaye hawezi kutunufaisha wala kutudhuru na tuje kurudishwa nyuma juu ya visigino vyetu baada ya kuwa Ameshatuongoza Allaah? Kama yule ambaye ameshawishiwa na mashaytwaan akikanganyika katika ardhi, anao marafiki wanamwita katika mwongozo: Njoo kwetu!” Sema: “Hakika Mwongozo wa Allaah ndio Mwongozo na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.”

 

 

 

وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na kuwa simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake mtakusanywa.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾

73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: “Kun!” basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki. Naye Atakuwa na ufalme Siku itakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghayb na dhahiri. Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

 

 

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤﴾

74. Na pindi Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: “Je, unachukua masanamu kuwa ni waabudiwa? Hakika mimi nakuona na watu wako katika upotofu wa bayana.”

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥﴾

75. Na hivyo ndivyo Tulivyomwonyesha Ibraahiym ufalme wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.

 

 

 

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦﴾

76. Na ulipomwingilia usiku akaona sayari ing’aayo. Akasema: “Huyu ni Rabb wangu.” Ilipotoweka akasema: “Hakika mimi sipendi wanaotoweka.” 

 

 

 

فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖفَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧﴾

77. Kisha alipoona mwezi umechomoza akasema: “Huyu ni Rabb wangu.” Ulipotoweka akasema: “Asiponiongoza Rabb wangu; bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.”

 

 

 

فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨﴾

78. Kisha alipoliona jua limechomoza akasema: “Huyu ni Rabb wangu, huyu ni mkubwa zaidi.” Lilipotoweka akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi simo katika yale mnayoyashirikisha (na Allaah).”

 

 

 

إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩﴾

79. “Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi nimeelemea haki, nami si katika washirikina.”

 

 

 

وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗوَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: “Je, mnahojiana nami kuhusu Allaah na hali Amenihidi? Na wala sikhofu mnayomshirikisha Naye (kwani sitodhurika) isipokuwa Rabb wangu Akitaka jambo. Rabb wangu Amezunguka kila kitu (kwa Ujuzi). Je, basi hamkumbuki?”

 

 

 

وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١﴾

81. “Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, na wala hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?”

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ﴿٨٢﴾

82. Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.

 

 

 

وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾

83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾

84. Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚوَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.

 

 

وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖوَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾

87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

 

ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

88. Hiyo ndiyo hidaaya ya Allaah, kwa hiyo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾

89. Hao ndio wale Tuliowapa Kitabu na hikma na Unabiy. Wakiyakanusha hawa (makafiri) basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠﴾

90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo mwongozo wao. Sema: “Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu.”

 

 

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖوَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾

91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: “Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu.” Sema: “Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na wala baba zenu.” Sema: “Allaah” (Ameiteremsha); kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.

 

 

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢﴾

92. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale ambayo yaliyokitangulia na ili uonye Mama wa miji, na ambao wameuzunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.

 

 

 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾

93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: “Nimefunuliwa Wahy” na hali hakufunuliwa Wahy wowote.  Na yule asemaye: “Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.” Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti, na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): “Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari kuhusu Aayaat Zake.”

 

 

 

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٩٥﴾

95. Hakika Allaah ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Mtoaji kilicho mfu kutokana na kilicho hai. Huyo Ndiye kwenu Allaah. Basi vipi mnaghilibiwa?

 

 

 

فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦﴾

96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni   mapumziko; na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hivyo ndio ukadiriaji wa Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote. 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾

97. Na Yeye Ndiye Ambaye Aliyekufanyieni nyota ili muongozwe kwazo katika viza vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua.

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨﴾

98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri na pa kuhifadhiwa. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaofahamu.[4]

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩﴾

99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana; na katika mitende, katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (ishara, zingatio) kwenu kwa watu wanaoamini.



Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈

Report Page