@Ribbiyyuwna

@Ribbiyyuwna


وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖوَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚسُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Na wakamfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake; na hali Amewaumba. Na wakampachikia uongo bila ya ujuzi wowote kuwa Ana wana wa kiume na wa kike. Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na ambayo wanavumisha.

 

 

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١٠١﴾

101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

 

 

 

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖوَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.[5]

 

 

 

قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚوَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤﴾

104. Kwa yakini imekujieni nuru za elimu kutoka kwa Rabb wenu. Basi aliyeona akatambua ni kwa faida ya nafsi yake; na aliyepofuka basi ni dhidi yake, (sema) “nami si mwenye kuwahifadhi.”

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat na (makafiri) waseme: “Umedurusu” (kutoka Ahlil-Kitaab) na ili Tuibainishe kwa watu wenye kujua.

 

 

 

اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿١٠٦﴾

106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy kutokana na Rabb wako: Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na jitenge na washirikina.

 

 

 

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧﴾

107. Na lau Allaah Angetaka wasingelifanya shirki. Na Hatukukufanya wewe mwenye kuwahifadhi, na wala wewe si mdhamini wao.

 

 

 

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗكَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨﴾

108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah; wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi. Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah ‘amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakitenda.

 

 

 

وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩﴾

109. Na waliapa kwa Allaah kwa viapo vya nguvu; kwamba ikiwafikia Aayah (muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: “Hakika Aayaat ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?”

 

 

 

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠﴾

110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.

 

 

 

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾

111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika na wakasemeshwa na wafu na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili. 

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖفَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui - mashaytwaan katika wana Aadam na majini wakidokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga.

 

 

 

وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾

113. Na ili zielemee katika (udanganyifu) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah na ili waridhike nayo na ili wachume (madhambi) wanayoyachumia.

 

 

 

أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ﴿١١٤﴾

114. (Sema): “Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Ambaye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa?” Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka. 

 

 

 

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿١١٥﴾

115. Na limetimia neno la Rabb wako kwa kweli na uadilifu. Hakuna mwenye kuyabadilisha maneno Yake. Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿١١٦﴾

116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.

 

 

 

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾

117. Hakika Rabb wako Anajua zaidi mwenye kupotea na njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuhidika.

 

 

 

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

118. Basi kuleni katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na hukmu) Zake.

 

 

 

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾

119. Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya elimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua Zaidi wenye kutaadi.

 

 

 

وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾

120. Na acheni dhambi zilizodhihirika na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖوَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ﴿١٢١﴾

121. Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ufasiki. Na hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.[6] 

 

 

 

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢٢﴾

122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo? Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wakhalifu wao wakuu kabisa ili wafanyie njama humo. Na hawafanyii njama ila nafsi zao, na wala hawahisi.

 

 

 

وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘاللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗسَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾

124. Na inapowajia Aayah (muujiza, hoja) husema: “Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rusuli wa Allaah. Allaah Anajua zaidi wapi Aweke risala Yake. Itawasibu wale waliokhalifu, udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa yale waliyokuwa wakifanya makri. 

 

 

 

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ﴿١٢٥﴾

125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavojaalia unajisi (na adhabu) juu ya wale wasioamini. 

 

 

 

وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾

126. Na hii ni njia ya Rabb wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaokumbuka.

 

 

 

لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾

127. Watapata Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah) kwa Rabb wao. Naye Ndiye Mlinzi wao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. 

 

 

 

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾

128. Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema): Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmetafuta kwa wingi (kuwapotoa) katika wana Aadam. Na watasema marafiki wao wandani katika wana Aadam: “Rabb wetu! Tulinufaishana baadhi yetu na wengineo, na tumefikia muda wetu ambao Umetupangia.” (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, ni wenye kudumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾

129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wandani wao kwa wao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾

130. Enyi hadhara ya majini na wana Aadam! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na Wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: “Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu.” Na uliwaghuri uhai wa dunia; na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.

 

 

 

ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾

131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb wako Hakuwa Mwenye kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe wameghafilika.

 

 

 

وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na wote wana daraja mbalimbali kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb wako si Mwenye kughafilika na yale waliyoyatenda.

 

 

 

وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾

133. Na Rabb wako ni Mkwasi Mwenye rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine watakaofuatia baada yenu kwa Atakao, kama vile Alivyokuzalisheni kutokana na vizazi vya watu wengine.

 

 

 

إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾

134. Hakika mnayoahidiwa bila shaka yatakuja tu! Nanyi si wenye kuweza kukwepa.

 

 

 

قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ﴿١٣٥﴾

135. Sema: “Enyi kaumu yangu! Tendeni kwa tamkini yenu, nami pia natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah. Hakika madhalimu hawatofaulu.”

 

 

 

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗسَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾

136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: “Hili ni la Allaah” kwa madai yao, “na hili ni kwa ajili ya washirika wetu.” Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao havimfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ﴿١٣٧﴾

137. Na hivyo ndivyo washirikina wengi walivyopambiwa na washirika wao (wanaowaabudu) kuua watoto wao ili wawateketeze na wawatatanishe dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga.

 

 

 

وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚسَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾

138. Na wakasema kwa madai yao: “Hawa wanyama wa mifugo na mazao ni marufuku; hawatowala ila wale tuwatakao, na wanyama imeharamishwa migongo yao (kuwapanda).” Na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia uongo (Allaah). Atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyatunga.

 

 

 

وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚسَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ﴿١٣٩﴾

139. Na wakasema: “Vilivyokuwemo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi kwa wanaume wetu na wameharamishiwa kwa wake zetu.” Lakini wanapokuwa ni nyamafu (wanapozaliwa), basi katika hao huwa wanashirikiana (na wanawake kula). Hakika Atawalipa uvumishi wao. Hakika Yeye ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾

140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia Allaah. Kwa yakini wamepotea wala hawakuwa wenye kuhidika. 

 

 

 

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾

141. Naye (Allaah) Ndiye Ambaye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yakitofautiana kwa ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.

 

 

وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾

142. Na katika wanyama wa mifugo (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.

 

 

 

ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾

143. Jozi nane: (za dume na jike) katika kondoo wawili na katika mbuzi wawili. Sema: “Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au viliomo fukoni la uzazi mwa majike yote mawili? Nijulisheni kwa elimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.”

 

 

 

وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗقُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚفَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Na katika ngamia, wawili na katika ng’ombe wawili. Sema: “Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo fukoni la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya?” Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila elimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.

 

 

 

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚفَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾

145. Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe; kwani hiyo ni najisi au ufasiki; kimetajiwa asiyekuwa Allaah (katika kuchinjwa).” Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

 

وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ﴿١٤٦﴾

146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa. Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa udhalimu wao. Na bila shaka Sisi ni Wakweli.

 

 

 

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); basi sema: “Rabb wenu ni Mwenye rahmah iliyoenea. Na wala haizuiliwi adhabu Yake kwa watu wakhalifu.”

 

 

 

سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾

148. Watasema wale walioshirikisha: “Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote.” Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja adhabu Yetu. Sema: “Je, mna elimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.”

 

 

قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Sema: “Basi ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.”

 

 

 

قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾

150. Sema: “Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa.” Wakishuhudia; basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanawasawazisha wengine na Rabb wao. 

 

 

 

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖأَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

151. Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kutia akilini.”

 

 

 

وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿١٥٢﴾

152. “Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka.”

 

 

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖوَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ﴿١٥٣﴾

153. “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.”[7] 

 

 

 

ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٤﴾

154. Kisha Tukampa Muwsaa Kitabu kutimiza (neema) juu ya yule aliyefanya ihsaan kuwa ni fasili ya kila kitu na ni mwongozo na rahmah wapate kuamini kukutana na Rabb wao.

 

 

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾

155. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa.

 

 

 

أَن تَقُولُوا إِنَّمَا أُنزِلَ الْكِتَابُ عَلَىٰ طَائِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ ﴿١٥٦﴾

156. Msije kusema: “Hakika Kitabu kimeteremshwa juu ya makundi mawili kabla yetu; lakini tulikuwa bila ya shaka tumeghafilika kuhusu waliyokuwa wakiyasoma.”

 

 

أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗسَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ﴿١٥٧﴾

157. Au mkaseme: “Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi, bila shaka tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao.” Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu na mwongozo na rahmah. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa yale waliyokuwa wakijitenga nayo.

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Je, wanangojea (lolote) isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au awafikie Rabb wako (kuwahukumu) au ziwajie baadhi za Aayaat za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi za Aayaat (alama za Qiyaamah) za Rabb wako haitoifaa nafsi iymaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika iymaan yake khayr yoyote. Sema: “Ngojeeni hakika nasi tunangojea.”

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴿١٥٩﴾

159. Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna (uhusiano) wa lolote nao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.

 

 

 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖوَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾

160. Atakayekuja kwa ‘amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo. Na Atakayekuja kwa ovu basi hatolipwa ila mfano wake, nao hawatodhulumiwa.

 

 

قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٦١﴾

161. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi, Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.”

 

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

162. Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.”[8]

 

 

لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

163. “Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.” 

 

 

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚوَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

164. Sema “Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.”

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾

165. Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni makhalifa wa duniani na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbali mbali ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

Kuendelea kusoma Gusa HAPA





Report Page