@Ribbiyyuwna

@Ribbiyyuwna



 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖوَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾

110. (Siku) Allaah Ataposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka neema Yangu juu yako na juu ya mama yako; Nilipokusaidia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام; unasemesha watu katika utoto na utu uzimani; na Nilipokufunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl; na ulipounda kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa idhini Yangu; ukapulizia likawa ndege kwa idhini Yangu; na ulipowaponyesha vipofu na ubarasi kwa idhini Yangu; na ulipowafufua wafu kwa idhini Yangu; na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako, ulipowajia kwa hoja bayana; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: ‘Haya si chochote ila ni sihiri bayana.’’

 

 

وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾

111. Na Nilipowatia ilhamu wafuasi watiifu kwamba: Niaminini Mimi na Rasuli Wangu. Wakasema: “Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.”

 

 

 

إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾

112. Pindi waliposema wafuasi watiifu: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, Anaweza Rabb wako Kututeremshia meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni?” Akasema: “Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.”

 

 

 

قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾

113. Wakasema: “Tunataka kula katika hicho; na ili nyoyo zetu zitulie; na tujue kwamba kwa yakini umetuambia kweli; na tuwe juu yake miongoni mwa wanaoshuhudia.”

 

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖوَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: “Ee Allaah, Rabb wetu, Tuteremshie meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku.”

 

 

قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾

115. Akasema Allaah: “Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu; Lakini atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo; basi hakika Nitamuadhibu adhabu ambayo Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”

 

 

 

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚإِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

116. Na pindi Allaah Atakaposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah?” (‘Iysaa) Atasema: “Utakasifu ni Wako hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu; na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako; hakika Wewe ni Mjuzi wa ghayb.”

 

 

مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚوَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

117. “Sijawaambia (lolote) ila yale Uliyoniamrisha kwayo kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponichukua kikamilifu juu Ulikuwa Wewe Mwangalizi juu yao. Na Wewe juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.”

 

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

118. “Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.”

 

 

قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١٩﴾

119. Allaah Atasema: “Hii ndiyo Siku itakayowafaa Asw-Swaadiqiyna ukweli wao; watapata Jannaat zipitazo chini yake mito; ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu adhimu.”

 

 

لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١٢٠﴾

120. Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yale yote yaliyomo humo. Naye juu ya kila kitu ni Muweza.

 

Kuendendela kusoma Gusa HAPA




Report Page