Juzuu Ya 9 – Qaalal-Malau
Juzuu: 9 قَالَ الْمَلَأُ
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ ﴿٨٨﴾
88. Wakasema Wakuu waliotakabari katika Qawm yake: “Tutakutoa ee Shua’yb na wale walioamini pamoja nawe kutoka mji wetu, au mrejee katika mila yetu.” (Shu’ayb) Akasema: “Japokuwa tumekirihika?”
قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ ﴿٨٩﴾
89. “Kwa yakini tumemzulia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Mola wetu. Mola wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali (tunategemea). Mola wetu! Hukumu baina yetu na baina ya Qawm yetu kwa Haki, Nawe ni Khayrul-Faatihiyn (Mbora wa wanaohukumu.”)
وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ ﴿٩٠﴾
90. Na wakasema Wakuu waliokufuru katika Qawm yake: “Mkimfuata Shu’ayb hakika hapo mtakuwa bila shaka wenye kukhasirika.”
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩١﴾
91. Basi ukawachukua Ar-rajfah (mtetemeko mkali wa ardhi) wakawa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa).
الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. Wale ambao wamemkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuishi humo. Waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa ndio wenye kukhasirika.
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖفَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٩٣﴾
93. Basi (Shu’ayb) akajitenga nao akasema: “Enyi Qawm yangu! Kwa yakini nimeshakubalighishieni Ujumbe wa Mola wangu na nimekunasihini, basi vipi nisikitike juu ya watu makafiri.”
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na Hatukutuma katika mji wowote Nabii yeyote (akakanushwa) isipokuwa Huwashika (kuwatesa) watu wake, kwa maafa na madhara (ufakiri, maradhi, maradhi, mateso na balaa mbalimbali) ili wapate kunyenyekea (kwa kukhofu na kutubia kwa Allaah).
ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩٥﴾
95. Kisha Tukabadilisha mahali pabaya kwa wema hata wakazidi, (na wakaneemeka na kubarikiwa); na wakasema: “Kwa yakini iliwagusa baba zetu madhara na raha.” Basi Tukawashika (kuwaadhibu) ghafla nao hawajitambui.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakawa na taqwa, kwa yakini Tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, basi Tukawashika (kuwaadhibu) kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿٩٧﴾
97. Je, watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa usiku hali wao wamelala?
أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩٨﴾
98. Au watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia adhabu Yetu wakati wa dhwuhaa (kabla ya mchana) hali wao wanacheza?
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾
99. Je, wameaminisha na mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.
أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je, haikubainika kwa wale ambao wanarithi ardhi baada ya watu (wa zamani walioangamizwa) kwamba lau Tungelitaka Tungeliwasibu kwa dhambi zao. Na Tutapiga muhuri juu ya nyoyo zao basi hawatosikia?
تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ ﴿١٠١﴾
101. Hiyo ni miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari zake. Na kwa yakini iliwajia Mitume yao kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuamini kwa yale waliyoyakadhibisha kabla. Hivyo ndivyo Allaah Anavopiga muhuri juu ya nyoyo za makafiri.
وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Na Hatukuwakuta kwa wengi wao wenye (kutekeleza) ahadi yoyote. Bali kwa yakini Tumewakuta wengi wao ni mafasiki.
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Kisha Tukamtuma baada yao Muwsaa kwa Aayah Zetu; (Ishara, dalili, miujiza) kwa Fir’awn na wakuu wake wakazifanyia dhulma. Basi tazama vipi ulikuwa mwisho wa mafisadi.
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Na Muwsaa akasema: “Ee Fir’awn! Hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola wa ‘Aalamiyna.” (walimwengu.)
حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٠٥﴾
105. “Napaswa nisiseme juu ya Allaah isipokuwa ya Haki. Kwa yakini nimekujieni kwa hoja bayana kutoka kwa Mola wengu; basi peleka pamoja nami wana wa Israaiyl (nchi waitakayo, usiwazuie hapa Misri kuwaudhi).”
قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٠٦﴾
106. (Fir’awn) Akasema: “Ikiwa umekuja na Aayah (muujiza), basi ilete, ukiwa ni miongoni mwa Swaadiqiyn.” (wakweli)
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٠٧﴾
107. Basi akaitupa fimbo yake, tahamaki (ikawa) joka la dhahiri.
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Na akatoa mkono wake; tahamaki (ukawa) mweupe (unang’ara) kwa watazamao.
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٩﴾
109. Wakasema wakuu katika Qawm ya Fir’awn: “Bila shaka huyu ni mchawi mjuzi.”
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿١١٠﴾
110. “Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu (kwa uchawi wake); basi mnaamrisha nini?”
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿١١١﴾
111. Wakasema: (kumwambia Fir’awn): “Mwache kidogo na ndugu yake (Haaruwn) na tuma katika miji wakusanyao (wakukusanyie wachawi wakubwa wakubwa).”
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿١١٢﴾
112. “Wakujie kila mchawi mjuzi.”
وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٣﴾
113. Wakaja wachawi wa Fir’awn; wakasema: “Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?”
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿١١٤﴾
114. (Fir’awn) Akasema: “Naam! Bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).”
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾
115. (Wachawi) Wakasema: “Ee Muwsaa, ima utupe (fimbo yako) au ima tuwe sisi (wa kwanza) kutupa.”
قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ ﴿١١٦﴾
116. (Muwsaa) Akasema: “Tupeni!” Basi walipotupa, waliyazuga macho ya watu na wakawatisha, na wakaja na uchawi mkubwa.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿١١٧﴾
117. Na Tukamfunulia Wahyi Muwsaa ya kwamba: “Tupa fimbo yako!” Tahamaki ikameza vyote walivovibuni.
فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١١٨﴾
118. Ukweli ukadhihiri na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ ﴿١١٩﴾
119. Wakashindwa hapo; na wakageuka kuwa wenye kudhalilika.
وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Na wachawi wakajiangusha wakisujdu (kwa Allaah).
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢١﴾
121. Wakasema: “Tumemwamini Mola wa Al-‘Aalaamiyna.” (walimwengu)
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٢﴾
122. “Mola wa Muwsaa na Haaruwn.”
قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنتُم بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Fir’awn akasema: “Je, mumemwamini kabla sijakupeni rukhsa? Hakika hii bila shaka ni njama mlizozipanga (nyinyi na Muwsaa) katika mji ili muwatoe watu wake humo. Mtakuja kujua (nini nitakufanyeni).”
لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٢٤﴾
124. “Kwa yakini nitakata mikono yenu na miguu yenu kinyume (kukata mkono wa kulia na mguu wa kushoto, au mkono wa kushoto na mguu wa kulia) kisha nitakusulubuni nyote.”
قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿١٢٥﴾
125. (Wachawi) Wakasema: “Hakika sisi kwa Mola wetu tutarudi.“
وَمَا تَنقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ ﴿١٢٦﴾
126. “Na hukuudhika nasi isipokuwa tu kwa kuwa tumeamini Aayah (Ishara, dalili, miujiza, hoja,) za Mola wetu zilipotujia. Mola wetu! Tumiminie subira na Tufishe (hali) tukiwa Waislamu.”
وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Na wakuu katika Qawm ya Fir’awn wakasema: “Je, unamwacha Muwsaa na Qawm yake (ili) wafisidi katika ardhi; na akuache (wewe) na miungu yako?” (Fir’wan) Akasema: “Tutawaua watoto wao (wachanga) wa kiume na tutaacha hai wanawake wao; na bila shaka sisi wenye nguvu juu yao.”
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّـهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّـهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿١٢٨﴾
128. Muwsaa akasema (kuwaambia) Qawm yake: “Ombeni msaada kwa Allaah na subirini. Hakika ardhi ni ya Allaah; Humrithisha Amtakaye katika wa waja Wake. Na mwisho (mwema) ni kwa wenye taqwa.”
قَالُوا أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٢٩﴾
129. (Qawm ya Muwsaa) Wakasema: “Tumeudhiwa kabla ya kutujia na baada ya kutujia.” (Muwsaa) akasema: “Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu na Akufanyeni makhalifa (watawala) katika ardhi, Atazame mtakavyotenda.”
وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٣٠﴾
130. Na kwa yakini Tuliwachukua (kwa kuwaadhibu) watu wa Fir’awn kwa miaka (ukame) na upungufu wa mazao ili wapate kukumbuka (na wawaidhike).
فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣١﴾
131. Basi ilipowajia jema, husema: “Hili letu.” Na likiwasibu ovu hunasibisha ukorofi kwa Muwsaa na walio pamoja naye. Tanabahi! Hakika ukorofi wao (huo unaowafika unatoka) kwa Allaah (kwa ajili ya ubaya wao), lakini wengi wao hawajui.
وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Na wakasema (kumwambia Muwsaa): “Chochote utachotuletea kwacho katika Aayah (muujiza) ili uturoge nacho; basi sisi hatutokuamini.”
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Basi Tuliwapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu (kuwa ni ishara) zilizofasiliwa (kuonyesha ukweli wa utume wa Mtume Muwsaa), lakini walitakabari wakawa watu makhalifu.
وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَا مُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ ۖ لَئِن كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٣٤﴾
134. Na ilipowaangukia adhabu ya kufadhaika walisema: “Ee Muwsaa! Tuombee kwa Mola wako kwa yale Aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na bila shaka tutawapeleka pamoja nawe wana Israaiyl (mnakotaka).
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَىٰ أَجَلٍ هُم بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Tulipowaondolea adhabu mpaka muda maalumu wao waufikie; tahamaki wao wanavunja ahadi.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Basi Tukawalipiza, Tukawagharikisha baharini kwa kuwa wao walikadhibisha Aayah Zetu; (Ishara, dalili, miujiza, hoja) na walikuwa kwazo ni wenye kughafilika nazo.
وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖوَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ ﴿١٣٧﴾
137. Na Tukawarithisha watu ambao walikuwa wakidhoofishwa (wakikandamizwa) Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo Tumeibariki. Na likatimia Neno la Mola wako jema kwa wana wa Israaiyl kwa kule kusubiri kwao. Na Tukadamirisha (Tukateketeza) yale waliyokuwa wakitenda Fir’awn na Qawm yake na yale waliyokuwa wakiyajenga.
وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚقَالُوا يَا مُوسَى اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na Tukawavusha wana Israaiyl bahari (wakasalimika na balaa ya Fir’awn) wakawafikia watu waliokuwa wakiabudu masanamu yao. (Wana wa Israaiyl) Wakasema: “Ee Muwsaa! Tufanyie nasi ilaaha (mungu) kama walivokwa (hawa) wana miungu. (Muwsaa) Akasema: “Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujahili.”
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٩﴾
139. “Hakika hawa (wanaoabudu sanamu) yatateketezwa waliyo nayo, na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”
قَالَ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٤٠﴾
140. (Muwsaa) Akasema: “Je, nikutafutieni ilaaha (mungu) ghairi ya Allaah, na hali Yeye Amekufadhilisheni juu ya Al-‘Aalaamiyna?” (walimwengu)
وَإِذْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿١٤١﴾
141. Na (kumbukeni enyi wana wa Israaiyl), Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokupeni mateso mabaya, wakiwakiua watoto wenu (wachanga wa kiume), na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Mola wenu.
وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةًۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾
142. Na Tukamuahidi Muwsaa misiku thelathini na Tukazitimiza kwa kumi; na ikatimia miyqaat (pahala pa miadi) ya Mola wake misiku arubaini. Muwsaa akasema (kumwambia) kaka yake Haaruwn: “Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) Qawm yangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.”
وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) yetu, na Mola wake Akamsemesha, (Muwsaa) alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” (Allaah) Akasema: “Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika; na Muwsaa akaangauka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Subhaanak! (Utakaso ni Wako!) Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini”
قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾
144. (Allaah) Akasema: “Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekuteua juu ya watu kwa Ujumbe Wangu na Maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na Tukamwandikia katika mbao katika kila kitu maw’idhah (ya kila namna), na tafsili ya kila kitu. (Tukamwambia): “Basi Yashike kwa azimio thabiti; na uwaamrishe watu wako wayashike kwa uzuri wake. Nitakuonyesheni miji (iliyoangamizwa) ya mafasiki.”
سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٤٦﴾
146. “Nitawaepusha na Aayah Zangu wale waliotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wanapoona kila Aayah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) hawaiamini. Na wanapoona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia. Na wanapoona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndio njia. Hivyo ni kwa kuwa wao walikadhibisha Aayah Zetu na walikuwa wenye kughafilika nazo.”
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na wale waliokadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) na makutano ya Aakhirah, zimeporomoka ‘amali zao. Je, watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda? (Hawatolipwa kinyume na yale matendo yao maovu).
وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ ﴿١٤٨﴾
148. Na watu wa Muwsaa walijichukulia baada ya (kuondoka kwake Muwsaa kwenda kupokea Tawraat) katika mapambo yao (ya dhahabu wakayeyusha na kujitengenezea) ndama kiwiliwili kilichokuwa na sauti (kama ya ng’ombe wakamwabudu). Je, hawakuona kwamba yeye (huyo mungu ndama) hawasemeshi na wala hawawaongozi njia? Walimfanya (kuwa mungu) na wakawa wenye kudhulumu nafsi zao.
وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Na walipojuta na wakaona kwamba kwa yakini wamepotoka; walisema: “Asipoturehemu Mola wetu na Akatughufuria, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِن بَعْدِي ۖ أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ ۖ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ ۚقَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١٥٠﴾
150. Na aliporejea Muwsaa kwa watu wake akiwa ameghadhibika na kusikitika, akasema: “Ubaya ulioje mmeniwakilisha baada yangu. Je, mmeharakiza (hamkuwa na subira ya kupokea) Amri ya Mola wenu?” (Muwsaa) Akatupa zile mbao (ziloandikwa Shari’ah za Dini) na akakamata kichwa cha kaka yake (Haaruwn) akimvuta kwake. (Haaruwn) Akasema (kumwambia Muwsaa): “Ee mwana wa mama yangu! Hakika watu (hawa) wamenikandamiza na walikaribia kuniua, basi usinifanye kifurahisho cha maadui, na wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.”
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٥١﴾
151. (Muwsaa) Akasema: “Mola wangu! Nighufurie na ndugu yangu, na Utuingize katika Rahmah Yake. Nawe ni Arhamur-Raahimiyn (Mwenye Kurehemu zaidi kuliko wenye kurehemu).”
إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ ﴿١٥٢﴾
152. Hakika wale waliomfanya ndama (kuwa mungu na kumwabudu) itawafika ghadhabu kutoka kwa Mola wao na udhalilifu katika maisha ya dunia. Na hivyo ndivyo Tunavowalipa wazushi.
وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٥٣﴾
153. Na wale waliotenda maovu kisha wakatubu baada yake na wakaamini; hakika Mola wako baada ya hayo (mema waliyoyatenda) bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi Wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).
وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ ۖ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Na ghadhabu zilipomtulia Muwsaa, alizichukuwa zile mbao. Na katika nuskha (maandiko) yake (mna) Hudan (Uongofu) na Rahmah kwa wale ambao wanamkhofu Mola wao.
وَاخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَاتِنَا ۖ فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ ۖ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا ۖ إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَاءُ وَتَهْدِي مَن تَشَاءُ ۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۖ وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ ﴿١٥٥﴾
155. Na Muwsaa akachagua wanaume sabini (katika) Qawm yake kwa Miyqaat (pahala pa miadi) Yetu (waje jabalini kuomba radhi kwa kuabudu kwao ndama). Kisha ilipowachukuwa ar-rajfah (tetemeko kali la ardh); Muwsaa alisema: “Mola wangu! Lau Ungelitaka Ungeliwaangamiza wao na mimi zamani. Je, Unatuhiliki kwa yale waliyoyafanya masafihi miongoni mwetu? Haya si chochote isipokuwa ni fitnah (majaribio) Yako. Unampotoa kwayo Umtakaye, na Unamhidi Umtakaye. Wewe Ni Walii wetu, basi Tughufurie na Turehemu; Nawe ni Khayrul-Ghaafiriyn(Mbora wa kughufuria).”
وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾
156. “Na Tuandikie katika dunia hii hasanah (mema) na katika Aakhirah (pia Tuandikie hasanah). Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako.” (Allaah) Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitaiandika (khaswa) kwa wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na wale ambao kwa Aayah Zetu wanaziamini.”
الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Wale ambao wamemfuata Mtume, an-Nabiyyi al-Ummiyy (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye wamemkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha ma’ruwf (Uislamu, mema) na anawakataza munkari (maovu), na anawahalalishia twayyibaat (halaal,. mazuri) na anawaharamishia khabaaith (maovu), na anawaondoshea mizigo (majukumu) yao na minyororo (Shari’ah ngumu) zilizokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamsaidia na wakafuata Nuru (Qur-aan) ambao imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu.
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Sema (ee Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Mjumbe wa Allaah kwenu nyinyi nyote. (Allaah) Ambaye Pekee Yake Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Laa ilaaha illa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa wa haki isipokuwa Yeye), Anahuisha na Anafisha. Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake, an-Nabiyyi al-Ummiyy (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.”
وَمِن قَوْمِ مُوسَىٰ أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Na katika Qawm ya Muwsaa (walikuweko) ummah wanaongoza kwa Haki na kwa (haki) hiyo wanafanya uadilifu.
وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۚ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Na Tukawagawanya makabila kumi na mbili, mataifa (mbali mbali). Na Tukamfunulia Wahyi Muwsaa walipomuomba maji Qawm yake kwamba: “Piga jiwe kwa fimbo yako.” Basi zikachimbuka humo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likaelewa mahali pa kinywaji chake. Na Tukawafunika kwa mawingu (walipokuwa wanasafiri jangwani wakitoka Misri), na Tukawateremshia Manna na Salwaa. (Tukawaambia): “Kuleni katika twayyibaat (halaa, vizuri) Tuliyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi walakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٦١﴾
161. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale walipoambiwa: “Kaeni katika mji huu (Quds), na kuleni humo popote mpendapo, na semeni (wakati wa kuingia), “Hittwah (ee Allaah tuondolee uzito wa madhambi yetu),” na ingieni katika mlango (wake) huku mmeinama (kwa unyenyekevu). Tutakughufurieni makosa yenu, (na) Tutawazidishia (neema na thawabu) Muhsiniyn (watendao wema).
فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٦٢﴾
162. Wakabadilisha wale ambao wamedhulumu kauli kwa kauli isiyokuwa (wakasema kauli tofauti na) ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu rijzan (adhabu ya kufadhaika) kutoka mbinguni kwa kwa yale waliyokuwa wakijidhulumu.
وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٣﴾
163. Na waulize kuhusu (khabari za watu wa) mji ambao ulikuwa kando ya bahari, waliporuka mipaka ya Sabato (Shari’ah ya kupumzika kazi Jumamosi na kufanya ‘ibaadah tu) walipowajia samaki wao juu kwa juu siku ya Jumamosi yao. Na siku isiyo? ya Jumamosi hawakuwajia. Hivyo ndivyo Tulivowajaribu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.
وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ اللَّـهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٦٤﴾
164. Na (wakumbushe) pale ummah miongoni mwao waliposema (kuwaonywa waliovunja Shari’ah ya Sabato): “Kwa nini mnawawaidhi (mnawaonya) watu ambao Allaah Atawahiliki au kuwaadhibu adhabu kali?” Wakasema (watoaji mawaidha): “Tupate kuwa na udhuru mbele ya Mola wenu (kuwa tumewaonya lakini hawakutusikiliza) na huenda wakawa na taqwa.”
فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٥﴾
165. Basi waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwaokoa wale ambao wanakataza uovu, na Tukawashika (kuwatesa) wale ambao wamedhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.
فَلَمَّا عَتَوْا عَن مَّا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿١٦٦﴾
166. Basi walipozidi kuasi (kwa kutoacha) waliyokuwa wakikatazwa nayo, Tulisema (kuwaambia): “Kuweni manyani waliotezwa.
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبْعَثَنَّ عَلَيْهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَن يَسُومُهُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۗإِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ الْعِقَابِ ۖ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٧﴾
167. Na (taja) Alipotangaza Mola wako (kwamba) kwa yakini Atawaletea (Mayahudi) mpaka siku ya Qiyaamah (watu ambao) watakaowatesa adhabu mbaya. Hakika Mola wako ni Sariy’ul-‘Iqaabi (Mwepesi wa kuadhibu), na hakika Yeye bila shaka ni Ghafuwr-Rahiym (Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu).
وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُم بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٦٨﴾
168. Na Tukawagawanya katika ardhi mataifa (mbali mbali); miongoni mwao (wako) wema na miongoni mwao ni kinyume chake. Na Tukawajaribu kwa mema na maovu ili wapate kurejea (katika utiifu).
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ أَن لَّا يَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Basi wakafuatia baada yao wafuatiaji (waovu) waliorithi Kitabu (bila ya kufuata Shari’ah zake), wanachukua anasa za hapa duniani na (huku) wanasema: “Tutaghufuriwa,” na inapowafikia (tena) anasa za kama hizo wanazichukua. Je, haikuchukuliwa kwao agano la Kitabu kwamba wasiseme juu ya Allaah isipokuwa Haki tu? Na wameshayasoma yaliyomo humo? Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale ambao wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?