Juzuu
وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٧٠﴾
170. Na wale wanaoshikilia imara Kitabu na wakasimamisha Swalaah, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa Muswlihiyn (watendao mema).وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧١﴾
171. Na (taja) Tulipoling’oa jabali (Tukalinyanyua na kulining’iniza) juu yao, kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kwamba litawaangukia. (Tukawaambia): “Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu, na kumbukeni yale yaliyomo humo ili mpate kuwa na taqwa.وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ ﴿١٧٢﴾
172. Na (taja) pale Mola wako Alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, (Akawuliza): “Je, Mimi siye Mola wenu?” (Wakajibu kwa) kusema: “Ndiye, tunashuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah (kwamba) hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.”أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ ﴿١٧٣﴾
173. Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?”وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٧٤﴾
174. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayah na ili wapate kurejea (katika utiifu).وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿١٧٥﴾
175. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule ambaye Tulimpa (ujuzi wa) Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, n.k.) akajivua nazo (asizifuate), na shaytwaan akamfuata na akawa miongoni mwa waliopotoka.وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿١٧٦﴾
176. Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayah), lakini aligandamana na dunia (kutaka anasa na ukubwa) na akafuata hawaa yake. Basi mithali yake ni kama mithali ya mbwa, ukimhujumu atahema (na kuning’iniza ulimi nje) na ukimwacha pia atahema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza.) Basi simulia visa huenda wakatafakari.سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٧٧﴾
177. Uovu ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza) na wakawa wanajidhulumu nafsi zao (wanapigiwa mfano na mbwa).مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِي ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٧٨﴾
178. Anayeongozwa na Allaah, basi ndiye aliyeongoka. Na Anayempotoa, basi hao ndio wenye kukhasirika.وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Kwa yakini Tumeuumbia (Moto wa) Jahannam wengi katika majini na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚسَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾
180. Na Allaah Ana Asmaaul-Husnaa(Majina Mazuri kabisa), basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopinga (wanaoharibu utukufu) katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٨١﴾
181. Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa Haki na kwayo wanafanya uadilifu.وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٢﴾
182. Na wale ambao wamekadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.), Tutawapupuria pole pole (kuwangamiza) kwa namna wasiyoijua.وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ ﴿١٨٣﴾
183. Na Nitawapa muda. Hakika mpango Wangu (wa kuwarudishia vitimbi vyao) ni madhubuti.أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا ۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿١٨٤﴾
184. Je, hawatafakari? Swahibu yao (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hana wazimu! Hakuwa yeye ila ni mwonyaji dhahiri.أَوَلَمْ يَنظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ وَأَنْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٥﴾
185. Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi na vitu Alivyoviumba Allaah, na huenda ukawa muda wao uliopangwa umeshakaribia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?مَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ ۚ وَيَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٨٦﴾
186. Ambaye Allaah Amempotosha (kwa kuwa mwenyewe ametaka kupotea), basi hakuna wa kumuongoa. Na Atawaacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo.يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٧﴾
187. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah), lini kutokea kwake? Sema: “Hakika ujuzi wake iko kwa Mola wangu. Haidhihirishi wakati wake isipokuwa Yeye (Pekee). Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni ispokuwa kwa ghafla.” Wanakuuliza kama kwamba wewe unaijua vyema. Sema: “Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah (Pekee), lakini watu wengi hawaelewi.قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٨﴾
188. Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa naelewa ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٨٩﴾
189. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akaajaalia humo mke wake ili apate utulivu. Kisha anapomuingilia anabeba mzigo (mimba) hafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito (mimba pevu; wote wawili mke na mume) humwomba Allaah Mola wao: “Ukitupa (mtoto) mwema (mzima) bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا ۚ فَتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿١٩٠﴾
190. Lakini Anapowapa (mtoto) mwema (mzima); wanamfanyia (Allaah) washirika katika kile Alichowapa. Fata’aala-Allaahu (Ametukuka Allaah kwa Uluwwa) kutokana na yale yote wanayoshirikisha.أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ ﴿١٩١﴾
191. Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa?وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٢﴾
192. Na wala hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمْ ۚ سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنتُمْ صَامِتُونَ ﴿١٩٣﴾
193. Na mkiwaita kwenye al-Hudaa (Uongofu) hawakufuateni. Ni sawasawa kwenu, mkiwaita au mkiwanyamazia.إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٩٤﴾
194. Hakika wale mnaowaomba (mnaowaabudu) asiyekuwa Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni Swaadiqiyn (wakweli).أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۗ قُلِ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ ﴿١٩٥﴾
195. Je, kwani wana miguu wanayotembelea nayo? Au wana mikono wanayokamatia kwayo? Au wana macho wanayoonea kwayo? Au wana masikio wanayosikilizia kwayo? Sema: “Waiteni washirika wenu, kisha nifanyieni njama; wala msinipe muda.إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّـهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ ۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ ﴿١٩٦﴾
196. Hakika Walii wangu (Mlinzi, Msaidizi) ni Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu, Naye Ndiye Awalindaye Asw-Swaalihiyn (walio wema).وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٧﴾
197. Na wale mnaowaomba (mnaowaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَسْمَعُوا ۖ وَتَرَاهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ ﴿١٩٨﴾
198. Na ukiwaita katika al-Hudaa (Uongofu) hawasikii; na utawaona wanakutazama na hali wao hawaoni.خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾
199. Shikamana na usamehevu, na amrisha mema, na jiepushe na majahili.وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٠٠﴾
200. Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan; basi jikinge na Allaah (sema, A’uwdhu biLLaahi). Hakika Yeye ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِّنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُم مُّبْصِرُونَ ﴿٢٠١﴾
201. Hakika wale waliokuwa na taqwa inapowagusa pepesi za shaytwaan hukumbuka (Allaah), basi mara wao huwa wenye kumaizi (kutambua haki).وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ ﴿٢٠٢﴾
202. Na ndugu zao wanawavutia katika upotofu, kisha hawakasiri (hawahuli).وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠٣﴾
203. Na usipowaletea Aayah (wazitakazo ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) husema: “Kwanini hukuibuni?” Sema: “Hakika (mimi) nafuata yale yaliyofunuliwa Wahyi kwangu kutoka kwa Mola wangu. Hii (Qur-aan) ni umaizi (dalili wazi) kutoka kwa Mola wenu, na ni Hudan (Uongofu) na Rahmah kwa watu wanaoamini.”وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾
204. Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya (mzingatie) mpate kurehemewa.وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾
205. Na mdhukuru (mtaje) Mola wake katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara (kwa kunyanyua sauti) hadharani katika kauli yako (dhikri, du’aa zako) asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ ۩﴿٢٠٦﴾
206. Hakika walioko kwa Mola wako (Malaika) hawatakabari na kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabihi na Kwake Pekee wanasujudu.سُورَة الأَنْفَال
Al-Anfaal: 8
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١﴾
1. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira (mali iliyotekwa vitani); sema: Ngawira ni ya Allaah na Mjumbe Wake. Basi mcheni Allaah na tengenezeni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Mjumbe Wake mkiwa ni Waumini (kweli).إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٢﴾
2. Hakika Waumini (wa kweli) ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao, zinajaa khofu (hushtuka), na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia iymaan, na kwa Mola wao wanatawakali (wanategemea). الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾
3. Ambao wanasimamisha Swalaah na katika yale Tuliyowaruzuku hutoa.أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٤﴾
4. Hao ndio Waumini wa kweli! Watapata daraja (vyeo vya juu) kwa Mola wao na Maghfira na riziki karimu.كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ ﴿٥﴾
5. Kama Alivyokutoa Mola wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka nyumbani kwako kwa haki, na hakika kundi miongoni mwa Waumini bila shaka ni wenye kuchukia.يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى الْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ ﴿٦﴾
6. Wanajadiliana nawe katika Haki baada ya kubainika, kama kwamba wanasukumwa katika mauti nao huku wanatazama.وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّـهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ ﴿٧﴾
7. Na (kumbukeni enyi Waumini) pale Allaah Alipokuahidini moja kati ya makundi mawili (la msafara au la jeshi) kwamba ni lenu; nanyi mkapenda lile lisilo na nguvu (taabu yoyote) liwe lenu, na Allaah Anataka Athibitishe Haki kwa Maneno Yake, na Akate mizizi ya makafiri.لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ ﴿٨﴾
8. Ili Athibitishe Haki na Abatilishe ubatilifu japokuwa wakhalifu (watu waovu) watachukia.إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ ﴿٩﴾
9. Na (kumbukeni) pale mlipomuomba msaada Mola wenu Naye Akakujibuni kuwa: “Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo.”وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿١٠﴾
10. Na Allaah Hakujaalia haya isipokuwa ni bishara na ili zitumainike nyoyo zenu kwayo. Na hakuna nusura (ushindi) isipokuwa kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ ﴿١١﴾
11. (Kumbukeni) Pale Alipokufunikeni kwa usingizi kuwa ni amani kutoka Kwake, na Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, ili Akutwaharisheni kwayo, na Akuondosheeni rijz (wasiwasi) wa shaytwaan, na ili Atie nguvu nyoyo zenu, na Athibitishe kwayo miguu.إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ ﴿١٢﴾
12. (Kumbuka) Pale Mola wako Alipowafunulia Wahyi Malaika (Akawaambia): “Hakika Mimi Niko pamoja Nanyi; basi wathibitisheni wale walioamini. Nitavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo (zao), na wapigeni (kateni) kila ncha za vidole (vyao).”ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَمَن يُشَاقِقِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٣﴾
13. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga (kwa uadui na ukhasama) Allaah na Mjumbe Wake. Na yeyote ampingae Allaah na Mjumbe Wake basi hakika Allaah ni Shadiydul-‘Iqaab (Mkali wa Kuadhibu) .ذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابَ النَّارِ ﴿١٤﴾
14. Ndio hivyo kwenu (ni adhabu yenu), basi onjeni, na kwamba makafiri wana adhabu ya Moto.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ ﴿١٥﴾
15. Enyi mlioamini! Mtapokutana na wale waliokufuru (wakielekea) vitani, msiwageuzie migongo (kukimbia).وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٦﴾
16. Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo (atakuwa mkosa) isipokuwa akigeuka kwa kufanya mbinu za kupigana au (amegeuka) kwa kujiunga na kikosi (kingine cha Waislamu. Vinginevyo,) basi amestahiki ghadhabu ya Allaah, na makazi yake ni (moto wa) Jahannam, na ni mahali pabaya palioje pa kurejea mwishoni.فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚوَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٧﴾
17. Hamkuwaua (nyinyi makafiri), lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga uliowaingia machoni mwao), lakini Allaah Ndiye Aliyerusha; ili Awajaribu Waumini majaribio mema kutoka Kwake. Hakika Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).ذَٰلِكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ مُوهِنُ كَيْدِ الْكَافِرِينَ ﴿١٨﴾
18. Ndivyo hivyo (Amekufanyieni Allaah), na kwamba Allaah Adhoofishe mbinu (vitimbi) za makafiri.إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ وَلَن تُغْنِيَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٩﴾
19. Mkitafuta (enyi makafiri) ushindi, basi kwa yakini imeshakujieni ushindi. Na mkiacha (kupigana na kuwatesa Waislamu), basi hivyo ni kheri kwenu. Na mkirudia (kupigana nao, Nasi) Tutarudia. Na wala kikosi chenu hakitokufaeni chochote japo kikikithiri. Na kwamba Allaah Yu Pamoja na Waumini.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَوَلَّوْا عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ ﴿٢٠﴾
20. Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na Mjumbe Wake; na wala msijiepushe Naye, na hali nyinyi mnasikia (amri Zake).وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿٢١﴾
21. Na wala msiwe kama wale waliosema: “Tumesikia”; na hali wao hawasikii. إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٢٢﴾
22. Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni (wanaojifanya) viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.وَلَوْ عَلِمَ اللَّـهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na kama Allaah Angelijua (kuwa) wana kheri yoyote kwao, basi Angeliwasikilizisha; na kama Angeliwasikilizisha, wangeligeuka nao huku wakipuuza.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖوَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Enyi mlioamini! Muitikieni Allaah na Mjumbe Wake Anapokuiteni kwenye yale yenye kukuhuisheni (maisha mzuri ya dunia na Aakhirah); na eleweni kwamba Allaah Anaingilia kati baina ya mtu na moyo wake; na kwamba Kwake Pekee mtakusanywa.وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢٥﴾
25. Na ogopeni fitnah ambayo haitowasibu wale waliodhulumu (nafsi zao) pekee miongoni mwenu. Na eleweni kwamba Allaah ni Shadiydul-‘Iqaab (Mkali wa Kuadhibu) .وَاذْكُرُوا إِذْ أَنتُمْ قَلِيلٌ مُّسْتَضْعَفُونَ فِي الْأَرْضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ النَّاسُ فَآوَاكُمْ وَأَيَّدَكُم بِنَصْرِهِ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na kumbukeni (pale) mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa (mkikandamizwa) ardhini, mnakhofu watu wasikunyakueni. (Allaah) Akakupeni makazi na Akakutieni nguvu kwa Nusra Yake, na Akakuruzukuni kwa twayyibaat (halaal, vizuri) mpate kushukuru.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٧﴾
27. Enyi mlioamini! Msimfanyie khiyana Allaah na Mjumbe (kuacha kufuata mliyoamrishwa na mliyokatazwa) na (wala) msikhini amana zenu na hali nyinyi mnaelewa (matokeo yake mabaya).وَاعْلَمُوا أَنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٢٨﴾
28. Na eleweni kwamba mali zenu na watoto wenu ni fitnah (mtihani Aliokupeni Allaah kutazama mtasimamia vipi); na kwamba kwa Allaah uko ujira adhimu.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّـهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾
29. Enyi mlioamini! Mkimcha Allaah Atakupeni Furqaan (kipambanuo cha kumaizi baina ya haki na batili), na Atakufutieni maovu yenu, na Atakughufurieni. Na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu.وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٣٠﴾
30. Na (kumbuka ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) walipokufanyia njama wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakufukuze (wakutoe Makkah). Na wanafanya njama, na Allaah Anapanga mipango (Ya kuvurumisha njama zao), na Allaah ni Mbora wa kupindua njama.وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا قَالُوا قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَاءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَـٰذَا ۙ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٣١﴾
31. Na wanaposomewa Aayah Zetu, husema: “Tumekwishasikia. Lau tungelitaka tungelisema kama haya. Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.”وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٣٢﴾
32. Na (kumbuka) waliposema: “Ee Allaah! Kama haya (aliyokuja nayo Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni haki kutoka Kwako; basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni, au Tuletee adhabu iumizayo”وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao (hapo Makkah). Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa (baadhi yao wamesilimu) wanaomba maghfirah.وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّـهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na wana nini hata Allaah Asiwaadhibu na hali wao wanazuia (watu) na Al-Masjidil-Haraam, na hawakuwa walinzi wake (Msikiti huo). Hawakuwa walinzi wake isipokuwa wenye taqwa; lakini wengi wao hawajui.وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً ۚ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Na haikuwa Swalaah (‘ibaadah) zao (makafiri) kwenye Nyumba (Tukufu yaani Ka’bah) isipokuwa ni miruzi (mbinja) na kupiga makofi. Basi (wataambiwa) onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkikufuru.إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ ۗ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ ﴿٣٦﴾
36. Hakika wale waliokufuru wanatoa mali zao ili wazuie (watu) Njia ya Allaah. Basi watazitoa, kisha itakuwa ni majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye (moto wa) Jahannam.لِيَمِيزَ اللَّـهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Ili Allaah Apambanue Khabiyth (waovu) na Twayyib(wema), kisha Aweke waovu juu ya waovu wengine, kisha Awarundike pamoja Awatie katika (moto wa) Jahannam. Hao ndio waliokhasirika.قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ ﴿٣٨﴾
38. Sema (uwaambie) waliokufuru (kwamba): wakikoma (kukufuru) wataghufuriwa yaliyopita. Na wakirudi (kufanya waliyokuwa wakifanya), basi imekwishapita desturi ya watu wa awali (walioadhibiwa).وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ ۚ فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٣٩﴾
39. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na (mpaka) Dini yote iwe ni kwa ajili ya Allaah, Na wakikoma, basi hakika Allaah kwa wanayoyatenda ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima).وَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَوْلَاكُمْ ۚ نِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٤٠﴾
40. Na wakikengeuka, basi jueni kwamba Allaah ni Mawla (Mlinzi) wenu, Ni’mal-Mawlaa (Mawlaa Mzuri Alioje), na Ni’man-Naswiyr (Mwenye Kunusuru Mzuri Alioje!).