Juzuu Ya 7 – Waidhaa Sami’uw
Juzuu 7 وَإِذَا سَمِعُوا
وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾
83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: “Mola wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.”
وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾
84. “Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Mola wetu Atuingize (Peponi) pamoja na Swaalihiyn (waja wema)?”
فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Basi Allaah Akawalipa kwa yale waliyoyasema, Mabustani zipitizao chini yake mito, watadumu humo (Peponi) milele. Na hayo ndio jazaa ya Muhsiniyn(watendao wema).
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) hao ni watu wa Jahiym (motoni).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾
87. Enyi mlioamini! Msiharamishe twayyibaat (halaal, vizuri) Aliyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka.
وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzuku Allaah vya halaal na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini.
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖفَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾
89. Allaah Hatokuhisabuni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuhisabuni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake (ya kuvunja viapo hivi) ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahlizenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (moja katika hayo), basi afunge Swawm siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini viapo vyenu (msiape kisha hamtimizi). Hivyo ndivyo Allaah Anavokubainishieni Aayah Zake mpate kushukuru.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾
90. Enyi mlioamini! Hakika ulevi na kamari na (kuabudu) masanamu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli; (yote hayo) ni rjisun (uchafu, chukizo) katika amali ya shaytwaan; basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu.
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika ulevi na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na (akuzuieni pia) Swalaah; basi je mtaacha (maovu hayo)?
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾
92. Na mtiini Allaah na mtiini Mtume na tahadharini! (kwenda kinyume na amri Zao). Mkikengeuka, basi eleweni kuwa juu ya Mjumbe Wetu ni kufikisha (ujumbe tu) waziwazi.
لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾
93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (awali vya haraam) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema; kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan Na Allaah Anapenda Muhsiniyn (watendao wema).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾
94. Enyi mlioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah Ajue mwenye kumkhofu kwa ghayb (japo hamwoni). Na atakayepindukia mipaka baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾
95. Enyi mlioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam. Na atakayemuua miongoni mwenu kwa kusudi, basi jazaa yake itakuwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wanaofugwa (ngamia, ng’ombe, mbuzi, kondoo). Ahukumu kwacho (watu) wawili walio waadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah (akachinjwe), au kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, kufunga ili aonje maovu ya jambo lake. Allaah Amesamehe kwa yaliyopita; na yeyote atakayerudia (kufanya) tena, basi Allaah Atamlipizia (adhabu). Na Allaah ni ‘Aziyz (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima) wa kulipiza.
أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾
96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa.
جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾
97. Allaah Amejaalia Ka’bah Nyumba Takatifu kuwa simamio (tegemeo) la watu, na (pia Ameijaalia) miezi mitukufu na wanyama wa kafara (dhabihu) na vigwe (alama ya waliokusudiwa kafara). Hivyo ili mpate kuelewa kuwa Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah ni kwa kila kitu ni ‘Aliym(Mjuzi wa yote daima).
اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾
98. Eleweni kuwa Allaah ni Shadiydul-‘Iqaabi (Mkali wa kuadhibu), na kwamba Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).
مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾
99. Hapana (jukumu) juu ya Mtume ila kufikisha tu (ujumbe). Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.
قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Sema: “Haviwi sawasawa Khabiyth (watu waovu, vitu, amali ovu; kufru, shirki, maasi, vyakula na mali ya haraam n.k.) na Twayyib (watu wema, iymaan, amali njema na vyote vya halaal na vizuri, n.k.) japokuwa utakupendekezea wingi wa Khabiyth.” Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾
101. Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtadhihirishiwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa Kughufiria – Mpole wa Kuwavumilia waja).
قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Bila shaka walikwishayauliza (mambo) hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa kwayo ni makafiri.
مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Allaah Hakujaalia (uharaam wowote wa) Bahiyrah(ngamia aliyezaa matumbo matano), wala (wa) Saaibah (ngamia aliyeachiliwa kwa nadhiri), wala (wa) Waswiylah (kondoo aliyezaa matumbo saba), wala (wa) Haam (fahali lililozalisha matumbo kumi), lakini wale waliokufuru wanamzulia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Na wanapoambiwa: “Njooni (katika) yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume” Husema: “Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu”. Je, japokuwa walikuwa baba zao hawaelewi chochote na wala hawakuongoka?
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Enyi mlioamini! Ni juu yenu (majukumu ya) nafsi zenu. Hawatokudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah Pekee ni marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Enyi mlioamini! Ushahidi (uweko kushuhudiwa) baina yenu yanapohudhuria mauti (kwa) mmoja wenu wakati anapousia. Waweko mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu; au wawili wengine wasiokuwa katika nyinyi (wasio Waislamu) mnapokuwa safarini (pakawa hakuna Waislamu), basi ukakufikeni msiba wa mauti, Muwazuie (wawili hao) baada ya Swalaah, basi waape kwa (jina la) Allaah mkitilia shaka (ushahidi wao waseme): “Hatutobadilisha kwayo (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah. (Kwani tukifanya hivyo) hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.”
فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾
107. Ikigundilikana kwamba hao wawili wamestahiki dhambi (kwa kusema uongo katika waliyoyashuhudia); basi wawili wengine wasimame (wachukue) mahali pao kutoka katika wale wanaotokana na warithi (wenye kudai haki); basi waape kwa (jina la) Allaah (kwa kusema): “Bila shaka ushahidi wetu ni wa haki (ni kweli) zaidi kuliko ushahidi (wa wawili) wao; nasi hatukuvuka mipaka; (ikiwa tumefanya hivyo), hakika hapo tutakuwa miongoni mwa madhalimu.
ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo vingine baada ya (kurudishwa) viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki.
يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾
109. (Tahadhari) Siku Allaah Atakayowakusanya Mitume na Kuwaambia: “Mlijibiwa (mliitikiwa) nini?” (Mitume) Watasema: “Hatuna ujuzi nalo; hakika Wewe Ndiye ‘Allaamul-Ghuyuwb (Mjuzi wa mambo ya ghayb).
إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾
110. (Siku) Allaah Ataposema: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka Neema Yangu juu yako na juu ya mama yako; Nilipokusaidia kwa Roho Takatifu; unasemesha watu katika utoto na utuuzimani; na (kumbuka) Nilipokufunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl; na (kumbuka pale) ulipotengeneza kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa Idhini Yangu; ukapulizia likawa ndege kwa Idhini Yangu; na ulipowaponyesha vipofu na ubarasi kwa Idhini Yangu; na ulipowatoa wafu (kutoka makaburini mwao) kwa Idhini Yangu; na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako (kutaka kuua) ulipowajia kwa hoja bayana; wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: “Haya si chochote ila ni uchawi bayana.”
وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾
111. Na (kumbuka pale) Nilipowafunulia (ilhamu) Hawariyyiyna (wafuasi wako) kwamba: “Niaminini Mimi na Mtume Wangu.” Wakasema: “Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.”
إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾
112. (Kumbuka pale) waliposema Hawariyyiyna: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je Anaweza Mola wako Kututeremshia Maaidah (meza iliyotandazwa chakula) kutoka mbinguni?” (‘Iysaa) Akasema: “Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini (wa kweli).”
قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾
113. (Hawariyyiyna) Wakasema: “Tunataka kula katika hicho; na (ili) nyoyo zetu zitulie; na tujue kwamba kwa yakini umetuambia kweli; na kwayo tuwe miongoni wa wanaoshuhudia.”
قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾
114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: “Ee Allaah Mola wetu, Tuteremshie Maaidah kutoka mbinguni (ili) iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, muujiza, dalili) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Khayrur-Raaziqiyn (Mbora wa wanaoruzuku.”)
قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾
115. Akasema Allaah: “Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu; (lakini) atakayekufuru baada ya hapo miongoni mwenu; basi hakika Nitamuadhibu adhabu (ambayo) Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.”
وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾
116. Na (Tahadhari) Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu (hivi): “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili ghairi ya Allaah?” (‘Iysaa) Akasema: “Subhaanak(Utakaso ni Wako)! Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema (hayo), basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu; na wala (mimi) sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako; hakika Wewe ni ‘Allaamul-Ghuyuwb (Mjuzi wa mambo ya ghayb).
مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾
117. “Sijawaambia (lolote) ila yale Uliyoniamrisha kwayo kwamba: Mwabuduni Allaah Mola wangu na Mola wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi nilipokuwa nao. Uliponichukua (Uliponitimizia muda wa kuishi duniani) Ulikuwa Wewe Ar-Raqiyba (Mwenye Kuchunga) juu yao. Na Wewe juu ya kila kitu ni Shahiyd” (Shahidi, Mwenye Kushuhudia yote daima).
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
118. “Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym” (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).
قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾
119. Akasema Allaah: “Hii ndiyo Siku itakayowafaa As-Swaadiqiyna (wakweli) ukweli wao; watapata Mabustani (Peponi) zipitazo chini yake mito; watadumu humo milele. Allaah Amewawia radhi, nao wawe radhi Naye. Huko ni kufuzu kukubwa.”
لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾
120. Ni wa Allaah (Pekee) ufalme wa mbingu na ardhi na yale yote yaliyomo humo. Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza wa yote daima).
سُورَةُ الأنْعَام
Al-An’aam: 6
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾
1. AlhamduliLlaahi (Himdi zote ni za Allaah Pekee) Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia adhw-dhwulumaati (viza) na Nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanamsawazisha Mola wao (na wengine).
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akakidhia muda (wa ajali ya kila kiumbe); na muda maalumu (uliowekwa kuondoka ulimwengu) uko Kwake; kisha (juu ya haya) nyinyi mnafanya shaka.
وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾
3. Naye Ndiye Allaah (Anayestahiki kuabudiwa) katika mbingu na ardhi; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma.
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤﴾
4. Na haiwafikii Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) yoyote ile katika Aayaat za Mola wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.
فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥﴾
5. Kwa yakini wameikadhibisha Haki ilipowajia; basi zitawafikia khabari za yale waliyokuwa kwayo wakiyafanyia istihzai.
أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦﴾
6. Je, hawaoni (hawazingatii) ni ummah ngapi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi yale ambayo Hatujapata kuwamakinisha (nayo) nyinyi; na Tukawapelekea mvua iendeleayo; na Tukajaalia mito ipitayo chini kwao. Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao ummah nyingine.
وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾
7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu katika karatasi, wakakigusa kwa mikono yao; bila shaka wangelisema wale waliokufuru hii si chochote isipokuwa ni sihri bayana.
وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨﴾
8. Na wakasema: “Mbona hakuteremshiwa Malaika?” Na lau Tungeliteremsha Malaika; basi ingepitishwa Amri (ya kuwaangamiza), kisha wasingelipewa muhula wa kuakhirishwa adhabu.
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩﴾
9. Na lau Tungelimjaalia (Mtume) Malaika, bila shaka Tungelimjaalia mtu (kama binaadamu) na Tungeliwatatanishia yale wanayoyatatanisha.
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Mitume kabla yako, lakini mwisho yakawazunguka wale waliofanya kejeli miongoni mwao yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
11. Sema: “Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa mwisho wa waliokadhibisha.”
قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚلَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾
12. Sema: “Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini?” Sema: “Ni vya Allaah (Pekee).” Ameandika juu ya Nafsi Yake Rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, (Siku hiyo) haina shaka ndani yake; wale ambao wamekhasiri nafsi zao wao hawaamini.
وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣﴾
13. Na ni Vyake Pekee (Allaah) vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye ni As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).
قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗقُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾
14. Sema: “Je, nimchukue (kuwa) walii (mlinzi, msaidizi) ghairi ya Allaah; (Ambaye Ndiye) Muumbaji mbingu na ardhi; Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza mwenye kusilimu.” Na (nimeamrishwa): “Wala usijekuwa miongoni mwa washirikina.”
قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾
15. Sema: “Hakika mimi nakhofu adhabu ya Siku kubwa kama nitamuasi Mola wangu.”
مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾
16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo; basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kuliko dhahiri.
وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾
17. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye; na Akikugusisha kheri, basi Yeye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza wa yote daima).
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨﴾
18. Naye ni Al-Qaahir (Mwenye Kuteza Nguvu, Mwenye Kudhibiti) juu ya waja Wake; Naye ni Al-Hakiymul-Khabiyr(Mwenye Hikmah wa yote daima – Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).
قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚقُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩﴾
19. Sema (uwaulize): “Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema (ujibu): “Allaah; ni Shahiyd(Shahidi, Mwenye Kushuhudia yote daima) baina yangu na baina yenu. Na imefunuliwa Wahyi kwangu hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itayomfikia. Je, kwa yakini nyinyi mnashuhudia kwamba wako miungu wengine pamoja na Allaah?” Sema: “Mimi sishuhudii (pamoja nanyi).” Sema: “Hakika Yeye ni Ilaahun Waahid (Mungu Mmoje Pekee Anayestahiki kuabudiwa kwa haki). Na kwamba hakika mimi niko mbali na hao mnaowashirikisha (Naye).”
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾
20. Wale ambao Tumewapa Kitabu (Mayahudi Na Manaswara) wanamuelewa kama wanavyowaelewa watoto wao. Wale ambao wamekhasirika nafsi zao (Aakhirah) hawaamini.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١﴾
21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayah Zake?; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.). Hakika madhalimu hawatofaulu.
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwa hao ni miungu)?
ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣﴾
23. Kisha haitokuwa fitnah (udhuru) yao isipokuwa kusema: “Wa-Allaahi Mola wetu hatukuwa washirikina.”
انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Tazama namna walivyokadhibisha juu ya nafsi zao; na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥﴾
25. Na miongoni mwao (wako) wanaotega sikio kukusikiliza. Na Tumejaalia juu ya nyoyo zao vifuniko wasifahamu (wanayoyasikia); na katika masikio yao (kama kwamba pana) uziwi. Na wanapoona kila Aayah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) hawaiamini; hata wanapokujia kukujadili husema wale waliokufuru: “Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.”
وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٦﴾
26. Nao wanazuia (wengine) dhidi yake; nao (wenyewe) wanajiweka mbali naye. Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao (tu) na hali hawatambui.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na lau ungeliona (Siku ya Qiyaamah) watakaposimamishwa kwenye Moto; kisha wakasema: “Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) za Mola wetu, na tutakuwa katika wanaoamini.”
بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨﴾
28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa; kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa nayo; na bila shaka wao ni waongo.
وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na walisema: “Haya si chochote isipokuwa ni maisha yetu ya dunia tu; na wala sisi hatutofufuliwa.”
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚقَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠﴾
30. Na lau ungeliona (Siku ya Qiyaamah) watakaposimamishwa mbele ya Mola wao. Atasema (Allaah): “Je, haya si ya kweli?” Watasema: “Ndio, tunaapa kwa Mola wetu”. Atasema (Allaah): “Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha”.
قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١﴾
31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah (Aakhirah); hata itakapowajia Saa (ya Qiyaamah) kwa ghafla; watasema: “Ole khasara yetu kwa yale tuliyoyapuuza humo, na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi! Ubaya ulioje wanayobeba!
وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtumii akili?
قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣﴾
33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha kwa ujeuri Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) za Allaah.