JUZUU
وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini walikadhibishwa Mitume kabla yako, wakasubiri juu ya yale waliyokadhibishwa; na wakaudhiwa hata ilipowafikia Nusura Yetu. Na hakuna abadilishaye Maneno ya Allaah. Kwa yakini imekujia khabari za Mitume (waliopita).وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥﴾
35. Na ikiwa kukengeuka kwao ni makubwa kwako, basi ukiweza kutafuta upenyo chini kwa chini katika ardhi au ngazi ya (kwendea) mbinguni ili uwaletee Aayah (muujiza wanaotaka basi fanya). Na lau Angetaka Allaah Angeliwakusanya katika Al-Hudaa(Uongofu); basi usiwe miongoni mwa majahili.إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦﴾
36. Hakika wanaokubali ni wale wanaosikia. Na wafu Allaah Atawafufua, kisha Kwake Pekee watarejeshwa.وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na walisema: “Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (ishara, dalili, hoja, muujiza) kutoka kwa Mola wake?” Sema: “Hakika Allaah ni Qaadir (Muweza) wa kuteremsha Aayah (ishara, dalili, hoja, muujiza) lakini wengi wao hawaelewi.”وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨﴾
38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotambaa katika ardhi na wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umati mfano wenu. Hatukupuuza katika Kitabu (Qur-aan) kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Pekee watakusanywa.وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٣٩﴾
39. Na wale waliokadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) ni viziwi na mabubu katika viza. Yeyote Allaah Amtakaye Humpotoa na yeyote Allaah Amtakaye Humjaalia katika Swiraatwim-Mustaqiym (njia iliyonyooka).قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠﴾
40. Sema: “Je mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa (ya Qiyaamah); je, mtamwomba ghairi ya Allaah (akuepusheni) mkiwa ni wakweli?”بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ﴿٤١﴾
41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Atakuondoleeni yale mliyomwomba (Atakuondoleeni) Akitaka; na mtasahau yale mnayoyashirikisha (pamoja Naye).وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na kwa yakini Tulipeleka (Mitume) kwa umati (zilizokuwa) kabla yako; Tukawatia katika dhiki na madhara ili wapate kunyenyekea.فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakitenda.فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤﴾
44. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwafungulia milango ya kila kitu (walichotaka), mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; Tukawachukua ghafla (tukawaadhibu), basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥﴾
45. Basi ikakatwa mizizi ya watu wale waliodhulumu; na AlhamduliLlaahi Rabbil-‘Aalamiyna (Himdi zote ni za Allaah Pekee, Mola wa walimwengu).قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ ﴿٤٦﴾
46. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni masikio yenu (kusikia kwenu) na macho yenu (kuona kwenu) na Akapiga muhuri juu ya nyoyo zenu (zisiinge kheri yoyote); je, ni ilaahu(mungu) gani ghairi ya Allaah Atakuleteeni tena (Aliyoyachukua kwenu Allaah)?” Tazama namna Tunavyozisarifu Aayah, kisha wao wanakengeuka. قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧﴾
47. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah ghafla au kwa dhahiri; je, (nani) wataangamia isipokuwa watu madhalimu?”وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na Hatupeleki Mitume isipokuwa ni wbashiriaji (khabari njema) na waonyaji. Basi yeyote atakayeamini na kutengenea; haitakuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na wale waliokadhibisha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) itawagusa adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki. قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala (sikuambieni) kwamba naelewa (mambo ya) ghayb; na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale (pekee) yaliyofunuliwa Wahyi kwangu”. Sema: “Je, wanalingana sawasawa kipofu na mwenye kuona? Basi hamtafakari?”وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١﴾
51. Na waonye kwayo (yaliyofunuliwa kwako Wahyi) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Mola wao; hawana ghairi Yake walii (mlinzi, msaidizi) wala mwombezi ili wapate kuwa na taqwa.وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾
52. Na wala usiwafukuze wale ambao wanamwomba Mola wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze (kwani ukiwafukuza) utakuwa miongoni mwa madhalimu.وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗأَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: “Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu?” Je, kwani Allaah si A’lam (Mjuzi) zaidi kwa wanaoshukuru?”وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤﴾
54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) basi sema: “Salaamun ‘Alaykum (amani iwe juu yenu). Mola wenu Amekidhia juu ya Nafsi Yake Rahmah; kwamba yeyote miongoni mwenu atayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye (Allaah) ni Ghafuwrur-Rahiym(Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥﴾
55. Na hivyo ndivyo Tunavyofafanua Aayah na ili idhihirike njia ya wakhalifu.قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙقَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Sema: “Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale ambao mnawaomba ghairi ya Allaah.” Sema: “Sifuati hawaa zenu (kwani nikifanya hivyo) hakika nitakuwa nimepotoka, hapo nami sitokuwa miongoni mwa walioongoka.”قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾
57. Sema: “Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Mola wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anahadithia Haki; Naye ni Khayrul-Faaswiliyn (Mbora wa Kuhukumu.”)قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨﴾
58. Sema: “Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka ingelikidhiwa Amri baina yangu na baina yenu. Na Allaah ni A’lam(Mjuzi)zaidi kwa madhalimu.”وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾
59. Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua (kuwa limeanguka kutoka tawi la mti kadhaa na kuangukia mahali kadhaa). Na wala (haianguki) punje katika viza vya ardhi, na wala (hakianguki) kilichorutubika na wala (hakianguki) kikavu isipokuwa (kimeandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuwdhw).وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliopangwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kasha Atakujulisheni kuhusu yale yote mliyokuwa mkiyatenda.وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١﴾
61. Naye ni Al-Qaahir (Mwenye Kuteza Nguvu, Mwenye Kudhibiti) juu ya waja Wake, na Anakutumieni (Malaika) wanaohifadhi hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢﴾
62. Kisha hurudishwa kwa Allaah Mola wao wa haki. Tanabahi! Bila shaka! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Asra’ul-Haasibiyn (Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu).قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣﴾
63. Sema: “Nani Anakuokoeni kutoka dhwulumaat(viza) vya bara na bahari? (Pale) mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri” (Mnamuomba kwa kusema): “Akituokoa kutokana na (balaa) hili; bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.”قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤﴾
64. Sema: “Allaah Anakuokoeni katika hayo na katika kila janga; kisha nyinyi mnashirikisha.”قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥﴾
65. Sema: “Yeye ni Al-Qaadir (Muweza daima) wa Kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu ujeuri wa wengineo. Tazama namna Tunavyozisarifu Aayah wapate kufahamu.”وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦﴾
66. Na wakaikadhibisha (Qur-aan) watu wako na hali ni Haki. Sema: “Mimi si mdhamini juu yenu.”لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٦٧﴾
67. Kwa kila khabari ina wakati (wake) maalumu, na mtakuja kujua.وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾
68. Na unapowaona wale wanaotumbukia kwenye mazungumzo (ya kukadhibisha) Aayah Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka (kutanabahi), usikae pamoja na watu madhalimu.وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٦٩﴾
69. Na wala si juu ya wale wenye taqwa hisabu yao chochote (si jukumu lao juu ya makafiri), lakini ni dhkiraa (ukumbusho) huenda wapate kuwa na taqwa.وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na waachilie mbali wale walioichukua dini yao mchezo na pumbao, na yakawaghuri maisha ya dunia, basi wakumbushe kwayo (Qur-aan watahadhari) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma. Nayo haina pasi na Allaah walii (mlinzi, msaidizi) wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa yale waliyoyachuma; watapata kinywaji cha maji ya moto yachemkayo na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakiyakanusha.قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾
71. Sema: “Je, tuombe ghairi ya Allaah ambaye (hawezi) kutunufaisha wala (hawezi) kutudhuru, na tuje kurudishwa nyuma juu ya visigino vyetu baada ya kuwa Ameshatuongoa Allaah? Kama (mfano wa) yule ambaye amezubaishwa (kutangatanga) na mashaytwaan katika ardhi akibabaika?” (Huku) Anao marafiki wanamwita katika Al-Hudaa (Uongofu) (wakimwambia) “Njoo.” Sema: Hakika Huda-Allaahi(Uongofu wa Allaah) ndio Al-Hudaa, na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Mola wa Al-‘Aalamiyna(walimwengu).وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na (tumeamrishwa): “Simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa.”وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾
73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: “Kun” (Kuwa) basi (jambo) litakuwa. Kauli Yake ni Haki. Naye Pekee Ana ufalme Siku itakapopulizwa baragumu. ‘Aalimul-Ghayrbi wash-Shahaadah (Mjuzi wa ya ghayb na dhahiri) Naye ni Hakiymul-Khabiyr (Mwenye Hikmah wa yote daima – Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤﴾
74. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: “Je unawafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona (wewe) na watu wako katika upotofu ulio dhahiri.”وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥﴾
75. Na hivyo ndivyo Tulivyomwonyesha Ibraahiym ufalme wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦﴾
76. Na ulipomwingilia usiku akaona nyota (sayari ing’aayo). Akasema: “Huyu ni mola wangu.” Ilipotoweka akasema: “Hakika mimi sipendi (mola) wanaotoweka.”فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧﴾
77. (Na) Alipoona mwezi umechomoza akasema: “Huyu ni mola wangu”. Ulipotoweka akasema: “Asiponiongoa Mola wangu; bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.”فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨﴾
78. (Na) Alipoliona jua limechomoza akasema: “Huyu ni mola wangu, (kwani) huyu ni mkubwa zaidi.” Lilipotoweka akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi niko huru (niko mbali) na yale yote mnayoyashirikisha (na Allaah).”إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩﴾
79. “Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameumba mbingu na ardhi nimeelemea haki; nami si katika washirikina.”وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na watu wake wakamhoji (kwa kumwambia unaacha kuabudu walivyokuwa wakiviabudu wazee! Utadhurika!) Akasema: “Je, mnanihoji kuhusu Allaah na hali Ameniongoa? Na wala sikhofu mnayomshirikisha Naye (na hakuna kitachonisibu) isipokuwa Mola wangu Akitaka lolote (linifike, basi litanifika). Mola wangu Amezunguka kila kitu kwa Ujuzi (Anaelewa vyema). Je, basi hamuwaidhiki?”وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١﴾
81. “Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, na wala (nyinyi) hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia kwenu dalili. Je, basi kundi gani kati ya mawili (nyinyi au mimi) linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnaelewa?”الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾
82. Wale ambao wameamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma (ya kumshirikisha Allaah). Hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka.وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾
83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Mola wako ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye Hikmah wa yote daima – Mjuzi wa yote daima).وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Tukamtunukia (Ibraahiym mwana anayeitwa) Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb. Wote Tukawaongoa. Na Nuwh Tulimuongoa kabla (zamani kabla ya Nabii Ibraahiym). Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo Muhsiniyn (watenda wema).وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swaalihiyna (waja wema).وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya Al-‘Aalamiyna(walimwengu).وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾
87. Na katika baba zao, na vizazi vyao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoa katika Swiraatwim-Mustaqiym (njia iliyonyooka).ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
88. Hiyo ndiyo Huda-Allaahi (Uongofu wa Allaah), Anamhidi kwayo Amtakaye kati ya waja Wake. Na lau wangemshirikisha bila shaka ingewaharibikia yale waliyokuwa wakitenda.أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾
89. Hao ndio wale ambao Tuliwapa Kitabu na Hukumu na Unabii. Wakiyakanusha hawa (makafari) basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠﴾
90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo uongofu wao. Sema: “Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni dhikraa (ukumbusho) kwa Al-‘Aalamiyna (walimwengu).وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖقُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾
91. Na hawakumkadiria (hawakumthamini) Allaah kama inavyostahiki kukadiriwa Kwake, (pale Mayahudi) waliposema: “Allaah Hakuteremsha kwa binaadamu chochote.” Sema: (uwaulize): “Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) Nuru na Hudan (Uongofu) kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizidhihirisha na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyaelewi nyinyi na wala baba zenu.” Sema: “Allaah” (Ndiye Aliyeteremsha hii Qur-aan na Vitabu vilivyoitangulia). Kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na hiki Kitabu Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale ambayo yaliyokitangulia na ili uwaonye (watu wa) mama wa vijiji (Makkah) na (watu wa nchi) ziloizunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia uongo Allaah au akasema: “Nimefunuliwa Wahyi” na hali hakufunuliwa chochote. Na yule asemaye: “Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.” Na lau ungeliwaona madhalimu pale wakiwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): “Zitoeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na (kwa vile) mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Aayah Zake; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.).”وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na (Siku ya Qiyaamah Tutakwambieni): “Kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao kwenu ni washirika (wa Allaah). Kwa yakini yamekatika (mahusiano yaliyokuwa) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.”إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥﴾
95. Hakika Allaah ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa aliye hai kutokana na maiti na Mtoaji maiti kutokana na aliyehai. Huyo Ndiye kwenu Allaah. Basi wapi mnageuzwa (mnaghilibiwa katika haki)?فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦﴾
96. Mpasuaji wa asubuhi (kukapambazuka); na Akajaalia usiku kuwa ni mapumziko ya utulivu; na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hivyo ndio ukadiriaji wa ‘Aziyzil-Hakiym (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾
97. Na Yeye Ndiye Ambaye Aliyekufanyieni nyota ili muongozwe kwazo (njia) katika dhwulumaati (viza) vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili Aayah kwa watu wanaojua.وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨﴾
98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri (pa kutulia na kukaa milele) na (pako) pa bohari (pa kuwekwa muda mdogo). Kwa yakini Tumezifasili Aayah kwa watu wanaofahamu.وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo mbegu zinazopandana; na katika mitende (vinatoka) katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na (Anakuotesheeni) mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Tazameni matunda yake yanapozaa na na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) kwenu kwa watu wanaoamini.وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚسُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Na (juu ya hivyo) wamemfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake; na hali (Yeye Ndiye) Aliyewaumba. Na wakamsingizia bila ya ujuzi wowote kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhaanahu wa Ta’aala (Utakaso ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomsifu (wanayompachika) nayo.بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾
101. Mwanzishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima).ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾
102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Mola wenu. Laa ilaaha illa Huwa (Hapana ilaah -mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye). Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Wakiyl (Wakili, Mtegemewa kwa yote).لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾
103. Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho; Naye Al-Latwiyful-Khabiyr(Mwenye Kudabiri mambo kwa utuvu, Mjuzi – Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤﴾
104. Kwa yakini umekujieni utambuzi kutoka kwa Mola wenu. Basi aliyefunua macho (yakampelekea kutambua) ni kwa (faida ya) nafsi yake; na aliyepofoka basi ni kwa dhara yake mwenyewe, (sema ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “nami si mlinzi kwenu.”وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu Aayah na wao (makafiri) waseme (kukuambia): “Umesoma” (Kutoka Vitabu vya Mayahudi na Manaswara na ukaleta hii Qur-aan kutoka humo) na ili Tuibainishe kwa watu wenye kujua.تَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahyi kwako kutoka Mola wako: Laa ilaaha illa Huwa (Hapana ilaah – mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye); na jitenge na washirikina.اوَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧﴾
107. Na lau Allaah Angetaka wasingelishirikisha. Na Hatukukufanya wewe uwe mlinzi juu yao, na wewe siye mdhamini juu yao.وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗكَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨﴾
108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba ghairi ya Allaah; wasije (nao) kumtukana Allaah kwa uadui bila ya kujua. Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah ‘amali zao, kisha kwa Mola wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakitenda.وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩﴾
109. Na (makafiri) waliapa kwa (jina la) Allaah kwa viapo vya nguvu; kwamba ikiwafikia Aayah (Ishara, dalili, muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: “Hakika Aayah iko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba itakapokuja (hiyo Aayah) hawataamini?” وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠﴾
110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika maasi yao wanatangatanga ovyo