Juzuu Ya 6 – Laa Yuhibbu-Allaahu

Juzuu Ya 6 – Laa Yuhibbu-Allaahu

Juzuu 6

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ﴿١٤٨﴾

 

148. Allaah Hapendi kutajwa hadharani uovu katika maneno isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah ni Samiy’an-‘Aliymaa (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا ﴿١٤٩﴾

 

149. Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah ni ‘Afuwwan-Qadiyraa (Mwingi wa Kusamehe – Muweza wa yote daima).إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١٥٠﴾

 

150. Hakika wale waliomkanusha Allaah na Mitume Yake; na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Mitume Yake; na wanasema: “Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi”; na wanataka kuchukua njia iliyo baina (kati kati) ya hayo.أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٥١﴾

 

151. Hao ndio makafiri wa kweli. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٥٢﴾

 

152. Na wale waliomwamini Allaah na Mitume Yake na hawakumfarikisha yeyote baina yao; hao Atawapa ujira wao. Na Allaah ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).يَسْأَلُكَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَابًا مِّنَ السَّمَاءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَآتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٥٣﴾

 

153. Wanakuuliza Ahlul-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara) uwateremshie Kitabu juu yao kutoka mbinguni. Kwa yakini walimuuliza Muwsaa makubwa kulio hayo. Walisema: “Tuonyeshe Allaah waziwazi”. Basi iliwachukuwa Asw-swaa’iqah (mngurumo angamizi) kwa dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama (kumwabudu) baada ya kwisha kuwajia hoja bayana. Tukawasamehe hayo; na Tukampa Muwsaa mamlaka bayana. 

وَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ الطُّورَ بِمِيثَاقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا فِي السَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿١٥٤﴾

 

154. Na Tukaunyanyua juu yao Atw-Twuwr (mlima au mlima wa Atw-Twuwr kwa sababu ya kukanusha kwao) kwa fungamano lao; na Tukawaambia: “Ingieni mlangoni hali mkiwa mmesujudu (mmeinama kwa kunyenyekea)”; na Tukawaambia: “Msivunje mipaka (kuhusu) Sabato (Shari’ah ya Jumamosi kupumzika kazi na kufanya ‘ibaadah tu)”. Na Tukachukua kutoka kwao fungamano madhubuti.فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَلْ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٥٥﴾

 

155. Na (Tukawaalani na kuwaadhibu) kwa kuvunja kwao fungamano lao, na kukanusha kwao Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.), na kuua kwao Manabii bila ya haki, na kauli yao: “Nyoyo zetu zimefumbwa” (haziwezi kuingia kitu yakiwemo hayo unayoyasema); bali Allaah Amezipiga muhuri juu yake kwa sababu ya kufuru zao; basi hawatoamini ila kidogo.وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَانًا عَظِيمًا ﴿١٥٦﴾

 

156. Na kwa kufuru zao na kauli yao ya kumsingizia Maryam buhtaanan (usingiziaji wa kashfa) mkubwa.وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾

 

157. Na kauli yao: “Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh‘Iysaa mwana wa Maryam, Mjumbe wa Allaah.” Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa (mtu mwengine wakadhani ni ‘Iysaa). Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo (kuhusu kumuua Nabii ‘Iysaa); kwa hakika wamo katika shaka nalo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨﴾

 

158. Bali Allaah Alimnyanyua Kwake. Na Allaah ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

 

159. Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara) ila atamwamini (atakapokuja kabla ya Qiyaamah) kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.فَبِظُلْمٍ مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَاتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ كَثِيرًا ﴿١٦٠﴾

 

160. Basi kwa dhulma ya Mayahudi; Tuliwaharamishia (baadhi ya) twayyibaat (mazuri) yaliyohalalishwa kwao; na kwa kuwazuilia wengi njia ya Allaah.وَأَخْذِهِمُ الرِّبَا وَقَدْ نُهُوا عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٦١﴾

 

161. Na kuchukua kwao ribaa na hali walikatazwa kuichukua; na kula kwao mali za watu kwa ubatilifu. Na Tumeandalia kwa makafiri miongoni mwao adhabu iumizayo.لَّـٰكِنِ الرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ مِنْهُمْ وَالْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ ۚ وَالْمُقِيمِينَ الصَّلَاةَ ۚ وَالْمُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالْمُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أُولَـٰئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٦٢﴾

162. Lakini Ar-Raasikhuwn (wenye msingi madhubuti) katika elimu miongoni mwao, na Waumini wanaamini yale yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; na (khasa) wasimamishao Swalaah, na watoao Zakaah na wanaomwamini Allaah na Siku ya Aakhirah. Hao Tutawapa ujira mkubwa.إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

 

163. Hakika Tumekufunulia Wahyi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Nuwh na Mitume baada yake. Na Tumemfunulia Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (vizazi) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zaburi (vitabu vya waadhi).وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾

 

164. Na (Tuliwatuma) Mitume Tuliokwishasimulia (khabari zao) kabla; na Mitume (wengine) Hatukukusimulia (khabari zao). Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚوَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

 

165. (Tuliwatuma) Mitume wabashiriaji (khabari njema) na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Mitume. Na Allaah ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿١٦٦﴾

 

166. Lakini Allaah Anayashuhudia Aliyoyateremsha kwako; (kuwa) Ameyateremsha kwa Elimu Yake; na Malaika (pia) wanashuhudia. Na Anatosheleza Allaah kuwa Shahiydaa (Shahidi, Mwenye Kushuhudia yote daima). 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٦٧﴾

 

167. Hakika wale waliokufuru na wakazuia (watu) njia ya Allaah, kwa yakini wamekwishapotea upotofu wa mbali.إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا ﴿١٦٨﴾

 

168. Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu; haitokuwa kwa Allaah Kuwaghufuria wala Kuwaongoza njia (ya kheri).إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٦٩﴾

 

169. Isipokuwa njia ya (moto wa) Jahannam wadumu humo milele. Na hayo kwa Allaah ni sahali.يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧٠﴾

 

170. Enyi watu! Kwa yakini amekujieni Mtume kwa haki kutoka kwa Mola wenu; basi aminini; ni bora kwenu. Na mkikanusha; basi hakika ni vya Allaah Pekee viliyomo mbinguni na ardhini. Na Allaah ni ‘Aliyman-Hakiymaa (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ سُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗوَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٧١﴾

 

171. Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Allaah isipokuwa (ukweli). Hakika Al-Masiyh‘Iysaa mwana wa Maryam ni Mtume wa Allaah na ni Neno Lake Alompelekea Maryam na ni Roho kutoka Kwake. Basi mwaminini Allaah na Mitume Yake; wala msiseme: ‘watatu’. Komeni, ni kheri kwenu. Hakika Allaah ni Ilaahun Waahid (Mungu Mmoja Pekee Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) kuwa ana mwana! Ni Vyake vyote viliyomo mbinguni na vyote viliyomo ardhini. Na Anatosheleza Allaah kuwa ni Wakiylaa (Wakili, Mtegemewa kwa yote).لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا ﴿١٧٢﴾

 

172. Al-Masiyh hatokataa (kwa kiburi wala kwa dharau) kuwa mja wa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa (Kwake). Na atakayekataa (kwa beza au dharau)ibaadah Yake na kutakabari, basi Atawakusanya wote Kwake (Siku ya Qiyaamah).فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ اسْتَنكَفُوا وَاسْتَكْبَرُوا فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧٣﴾

 

173. Ama wale ambao waliamini na wakatenda mema; Atawalipa kwa ukamilifu ujira wao; na Atawazidishia kwa Fadhila Zake. Na ama waliokataa (kwa kudunisha, au kubeua au dharau) na wakatakabari; Atawaadhibu adhabu iumizayo; na wala hawatopata pasi na Allaah walii (mlinzi) wala mwenye kunusuru.يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾

 

174. Enyi watu! Kwa yakini imekujieni burhaan (dalili bayana) kutoka kwa Mola wenu na Tumekuteremshieni Nuru (iliyo) bayana.فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿١٧٥﴾

 

175. Basi wale ambao wamemwamini Allaah, na wakashikamana Naye; Atawaingiza katika Rahmah kutoka Kwake na Fadhila, na Atawaongoza Kwake (katika) Swiraatwam-Mustaqiymaa (njia iliyonyooka).يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾

 

176. Wanakufutu (kutoa Fatwa ya Shari’ah juu ya masuala au tatizo), Sema: Allaah Atakufutuni kuhusu mkiwa. Ikiwa mwanamume amekufa, hana mtoto lakini ana dada; basi (huyo dada) atapata nusu ya yale (mali) aliyoyaacha (na maiti). Na yeye (huyo mwanamume akiwa yu hai) atamrithi (huyo dada ikiwa amekufa) kama hana mtoto. Na ikiwa wao (madada) ni wawili; basi (wote wawili) watapata thuluthi mbili ya yale (mali) aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake; basi (kila) mwanamme atapata sehemu iliyo sawa na (sehemu) ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni (Shari’ah Yake) ili msipotee; na Allaah kwa kila kitu ni‘Aliym (Mjuzi wa yote daima).



Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈




Report Page