JUZUU
سُورَةُ الْمَائِدَة
Al-Maaidah: 5
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ﴿١﴾
1. Enyi mlioamini! Timizeni mikataba. Mmehalalishiwa kwenu (kula) wanyama wenye miguu minne isipokuwa mnaosomewa (katika Qur-aan kuwa ni haraam). Lakini msihalalishe kuwinda mkiwa katika (Hijjah mtakapoingia) ihraam. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢﴾
2. Enyi mlioamini! Msivunje kanuni za Allaah, wala (heshima) ya mwezi mtukufu wala (kupuuza alama za) wanyama wa kafara (Makkah), wala vigwe (vyao), wala (kupuuza amani kwa) wanaoiendea Nyumba Takatifu (iliyoko Makkah); wanatafuta (huko) Fadhila kutoka kwa Mola wao na Radhi (Zake). Na mkishatoka kwenye ihraam; windeni (mkitaka). Na wala isikuchocheeni chuki ya watu kwa vile walikuzuieni (kufika) Al-Mas-jidil-Haraam (kusikupelekeeni) kuwafanyia uadui. Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni Shadiydul-‘Iqaab(Mkali wa Kuadhibu).حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾
3. Mmeharamishiwa nyamafu (mzoga), na damu, na nyama ya nguruwe, na (mnyama) aliyechinjwa si kwa ajili ya Allaah. Na (mnyama aliyeuawa) kwa kunyongwa, na (aliyekufa kwa) kupigwa, na (aliyekufa kwa) kuporomoka, na (aliyekufa kwa) kupigwa pembe (na mnyama mwengine), na aliyeliwa na mnyama mwitu (akafa) isipokuwa mliyewahi kumchinja (kabla ya kufa kwake); na (pia mmeharamishiwa) waliochinjwa kwa ajili ya mizimu, na (pia mmeharamishiwa) kupiga ramli (kutaka kuelewa ya ghayb ambayo ni muhali) kutokana na mishale. Hayo (yote) kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa (kabisa) wale ambao wamekufuru katika Dini yenu; basi msiwaogope, na Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe (ndio) Dini yenu. Basi atakayefikwa na dharura na kushurutishwa kutokana na njaa kali (ikampelekea kula vilivyoharamishwa), pasipo kuelekea dhambi; basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٤﴾
4. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa twayyibaat (halaal, vizuri) na mlichowafunza wanyama (kukiwinda) na ndege wa kuwinda; mnawafunza yale Aliyokufunzeni Allaah. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie jina la Allaah. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Sariy’ul-Hisaab(Mwepesi wa Kuhesabu).
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٥﴾
5. Leo mmehalalishiwa twayyibaat (halaa, vizuri). Na chakula cha wale ambao walipewa Kitabu ni halaal kwenu, na chakula chenu ni halaal kwao. Na (mmehalalishiwa kuwaoa) muhswanaatu (wanawake wema walioimarishwa sitara wasiozini) miongoni mwa Waumini wanawake na (pia mmehalalishiwa kuwaoa) muhswanaatu miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa mahari yao mkafunga nao ndoa bila ya kufanya uhasharati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayeikanusha Iymaan; basi kwa yakini ‘amali zake zimeporomoka (zimebatilika), naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٦﴾
6. Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka viwikoni, na pakeni (panguseni) kwa (maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa (hamuwezi kutumia maji kwa sababu ya ugonjwa) au mko safarini au mmoja wenu akitoka msalani (chooni) au mmewagusa (mmejimai na) wanawake, kisha hamkupata maji; basi mtayammamu (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni tabu (uzito), lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni Neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَاقَهُ الَّذِي وَاثَقَكُم بِهِ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٧﴾
7. Na kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu na agano (ahadi) Lake ambalo Amekufungamanisheni nalo mliposema: “Tumesikia na Tumetii.” Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa yote yaliyomo vifuani.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾
8. Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah Khabiyru(Mjuzi wa undani na ukina wa mambo) kwa myatendayo.وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٩﴾
9. Allaah Amewaahidi ambao wameamini na wakatenda mema; (kwamba) watapata maghfira na ujira mkuu.وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٠﴾
10. Na ambao wamekufuru na wakakanusha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) hao ni watu wa (moto wa) Jahiym.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾
11. Enyi mlioamini! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, (kumbukeni) pale walipopania watu kukunyosheeni mikono yao (kukushambulieni), kisha Allaah Akazuia mikono yao dhidi yenu. Na mcheni Allaah; na kwa Allaah pekee watawakali (wategemee) Waumini.وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّـهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٢﴾
12. Na kwa yakini Allaah Alichukua agano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea miongoni mwao wakuu kumi na mbili. Na Allaah Akasema: “Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; mtakaposimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kuamini Mitume Yangu, na kuwaunga mkono, na kumkopesha Allaah mkopo mzuri; bila shaka Nitakufutieni maovu yenu, na Nitakuingizeni Mabustani ipitayo mito chini yake (Peponi). Na yeyote atakayekufuru baada ya hapo miongoni mwenu; basi kwa yakini amepotoea njia iliyo sawa.”فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣﴾
13. Kwa (sababu ya) kuvunja kwao agano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka mahali pake, na wakasahu sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo. Na utaendelea kupata (khabari za) khiana kutoka kwao isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda Al–Muhsiniyn (watendao wema).وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللَّـهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿١٤﴾
15. Na kwa wale ambao wamesema: “Hakika sisi ni Naswaraa” Tulichukua agano kwao, wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo. Basi Tukapandikiza baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Atawajulisha waliyokuwa wakiyatenda.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
16. Enyi Ahlal-Kitaab! (Mayahudi na Manaswaara) Hakika amekwishakujieni Mjumbe Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu bayana.يَهْدِي بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾
16. Allaah Anamhidi kwacho yeyote atayefuata Radhi Zake katika Subulas-salaam (njia za salama); na Anawatoa kutoka adh-dhwulumaati (viza) kuingia katika Nuru kwa Idhini Yake, na Anawaongoza katika Swiraatwim-Mustaqiym (njia iliyonyooka).لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾
17. Kwa yakini, wamekufuru wale ambao wamesema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana Maryam.” Sema: “Nani anayemiliki chochote mbele ya Allaah Akitaka Kumhilikisha Al-Masiyh mwana Maryam na mama yake na walioko ardhini wote? Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo baina yake (mbingu na ardhi); Anaumba Atakacho. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza Wwa yote daima).وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّـهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚوَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾
18. Na Mayahudi na Manaswara wamesema: “Sisi ni wana wa Allaah na vipenzi Vyake.” Sema: “Kwa nini basi Anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu miongoni mwa Alioumba. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo baina yake (mbingu na ardhi); na Kwake Pekee ndio marejeo ya mwisho.يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ الرُّسُلِ أَن تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِن بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٩﴾
19. Enyi Ahlal-Kitaab! (Mayahudi na Manaswaara) Kwa yakini amekwishakujieni Mjumbe Wetu anaekubainishieni (Dini) katika kipindi cha kusita (kisichokuwa) na Mitume. Msije kusema: “Hakutujia mwenye kubashiria khabari njema yeyote wala mwonyaji yeyote.” Bila shaka (yoyote ile) amekujieni mwenye kubashiria khabari njema na mwonyaji. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza wa yote daima).وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَآتَاكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale Muwsaa alipowaambia watu wake: “Enyi watu wangu! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu Alipojaalia miongoni mwenu Manabii, na Akakufanyeni watawala, na Akakupeni yale Asiyowahi kumpa yeyote miongoni mwa walimwengu.”يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾
21. “Enyi watu wangu! Ingieni ardhi takatifu ambayo Amekuandikieni Allaah kwenu, na wala msirudi nyuma kugeuka (kukimbia kupigana katika njia ya Allaah, ikibidi); mtageuka kuwa wenye kukhasirika.”قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ﴿٢٢﴾
22. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari; nasi hatutaingia humo mpaka (majabari) watoke humo; watakapotoka humo; hapo (ndio) sisi tutaingia.”قَالَ رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾
23. Wakasema watu wawili miongoni mwa wale ambao wanakhofu (kuasi) Aliyowaneemesha Allaah, (walisema): “Waingilieni katika mlango; mkiwaingilia, basi hakika nyinyi mtashinda. Na kwa Allaah Pekee tawakalini (tegemeeni) ikiwa nyinyi ni Waumini (wa kweli).”قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا ۖ فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾
24. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika sisi hatutoingia humo kamwe madamu wamo (hao majabari); basi nenda wewe na Mola wako mkapigane, hakika sisi tutabakia hapa hapa.”قَالَ رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٥﴾
25. (Muwsaa) Akasema: “Mola wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi Tutenganishe baina yetu na watu mafasiki.”قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾
26. (Allaah) Akasema: “Basi hakika ardhi hiyo imeharamishwa kwao miaka arubaini; watatangatanga ardhini. Basi usisikitike juu ya watu mafasiki.”وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) habari za wana wawili wa Aadam; (Haabiyl na Qaabiyl) kwa haki walipotoa Qurbaan (mnyama wa kafara kwa ajili ya Allaah) ikakubaliwa ya mmoja wao, na haikukubaliwa ya mwengine; (yule asiyekubaliwa kafara yake) akasema (kumwambia nduguye): “Nitakuua.” (Yule aliyekubaliwa kafara yake) Akasema: “Hakika Allaah Anatakabalia Muttaqiyn (wamchao Allaah).”لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَا بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾
28. (Akasema aliyekubaliwa kafara yake): “Ukininyoshea mkono wako ili uniue, mimi sitokunyoshea mkono wangu kukuua; hakika mimi namkhofu Allaah Mola wa walimwengu.”إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾
29. “Hakika mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako; (na kwa hali hiyo) utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni; na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu.”فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾
30. Basi (aliyekataliwa kafara,) nafsi yake ikamuamuru kumuua ndugu yake; basi akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖفَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾
31. Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) Akasema: “Ole wangu! Nimeshindwa kuwa kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu.” Akawa miongoni mwa wajutao.
مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ ﴿٣٢﴾
32. Kwa ajili ya hivyo, Tukawaandikia wana wa Israaiyl kwamba; atakayeiua nafsi (mtu) bila ya nafsi kuua, au (bila ya) kufanya ufisadi katika ardhi; basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa (nafsi) dhidi ya mauti, basi ni kama amewaokoa watu wote. Na bila shaka walifikiwa na Mitume Yetu kwa hoja bayana; kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka (kuasi).إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٣٣﴾
33. Hakika jazaa ya wale ambao wanampiga vita Allaah na Mjumbe Wake na wanakimbilia kufanya ufisadi katika ardhi; (jazaa yao) ni kwamba wauawe au wasulubiwe au wakatwe mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho (mkono wa kulia kwa mguu wa kushoto, na mkono wa kushoto kwa mguu wa kulia) au kuhamishwa katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah watapata adhabu kubwa.إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. Isipokuwa wale waliotubia kabla ya ya kuwashinda nguvu basi eleweni kwamba hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
35. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na tafuteni Kwake Al-Wasiylah (njia za ‘ibaadah za kumkurubia); na fanyeni Jihaad katika njia Yake mpate kufaulu.إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٣٦﴾
36. Hakika wale ambao wamekufuru, lau kama watakuwa na yale yote yaliyomo ardhini na mfano wake pamoja nayo, ili wafidie kwayo kuepukana na adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatopokelewa kutoka kwao, na watapata adhabu iumizayo.يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٣٧﴾
37. Watataka kutoka katika Moto (kwa kila njia); na wao si watokaji humo, na watapata adhabu ya kudumu.وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٣٨﴾
38. Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, wakateni mikono yao; ni jazaa kwa yale waliyoyachuma ndio adhabu ya mfano kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٩﴾
39. Basi atakayetubia baada ya dhulma yake na akatengenea (kwa kutenda mema); basi Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤٠﴾
40. Je hujui ya kwamba ni Allaah Pekee Anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humwadhibu Amtakae na Humghufiria Amtakae. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza wa yote daima).يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖيَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٤١﴾
41. Ee Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kukufuru miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: “Tumeamini” na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia (wakubwa zao). Wanageuza maneno kutoka mahali pake; wanasema (kuwaambia wafuasi wao): “Mkipewa (kutoka kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) haya (tunayokuambieni) basi yachukueni, na msipopewa hayo basi tahadharini!” Na yule ambaye Allaah Anataka kumtia mtihanini, basi huwezi kumpatia mbele ya Allaah chochote. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Watapata khizaya duniani na Aakhirah watapata adhabu kubwa.سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٤٢﴾
42. (Hao) Wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji mno wa haramu. Basi wakikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatoweza kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda Muqsitwiyn(wafanyao uadilifu).وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٣﴾
43. Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu (wao) na hali wana Tawraat iliyomo ndani yake Hukumu ya Allaah; kisha baada ya hayo wanakengeuka (unapowahukumu). Na hao si wenye kuamini.إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾
44. Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna Hudan(Uongofu) na Nuru; ambayo kwayo, Manabii waliojisalimisha (kwa Allaah) waliwahukumu Mayahudi, na Ar-Rabbaniyyuwna (Wanavyouni wao watawa) na Al-Ahbaar (Makuhani – Wanavyuoni wao wa dini) pia (walihukumu kwa hiyo Tawraat) kwa sababu waliyokabidhiwa kuhifadhi Kitabu cha Allaah; na wakawa mashahidi juu yake. Basi (nyinyi Waislamu) msiwaogope watu, bali Niogopeni (Mimi), na wala msiuze Aayah Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na Tumewaandikia Shari’ah humo (katika Tawraat) kwamba (huuawa) nafsi (mtu) kwa nafsi (mtu), na jicho (hupofuliwa) kwa jicho, na pua (hukatwa) kwa pua, na sikio (humeguliwa) kwa sikio, jino (hung’olewa) kwa jino; na (katika) majaraha (kulipizana) kisasi. Lakini atakayetolea swadaqah (haki yake akasemehe) kwayo, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖوَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na Tukamfuatishia nyayo za (Mitume hao) ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl iliyomo ndani yake Hudan (Uongofu) na Nuru; na isadikishayo yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Hudan na mawaidha kwa Muttaqiyn (wamchao Allaah).وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na watu (waliopewa) Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu (hiki) kwa haki kinachosadikisha yale (yaliyokuja katika) Vitabu vilivyokuwa kabla yake na chenye kuvidhibiti (kuvishuhudia na kuvihukumu hivyo vitabu visifasiriwe vingine na visigeuzwe). Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah; na wala usifuate matamanio yao kwa kuacha yaliyokujia katika haki. Kwa kila (Ummah) katika nyinyi Tumeujaalia Shari’ah na Manhaj. Na lau Angetaka Allaah Angelikufanyeni Ummah mmoja (wenye kufuata Shari’ah na Manhaj moja); lakini (Allaah Amekufanyeni hivyo) ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Basi shindaneni katika mambo ya kheri. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote; kisha Atakujulisheni yale (yote) mliyokuwa mkikhitilafiana.وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate matamanio yao, na jihadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya yale Aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi elewa kuwa hakika Allaah Anataka kuwasibu (kuwafikishia adhabu) kwa baadhi ya madhambi yao. Na hakika wengi katika watu ni mafasiki.أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾
50. Je, wanataka (uwahukumu kwa) hukumu ya ujaahiliyyah (ujinga kabla ya Usilamu)? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu. (Yanafahamika haya) kwa watu wenye yakini.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾
51. Enyi mlioamini! Msiwachukuwe Mayahudi na Manaswara (kuwa ndio) marafiki (zenu) wapenzi. Wao kwa wao ni marafiki. Na yeyote atakayewafanya marafiki; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾
52. Basi utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi (ya shaka na unafiki) wanakimbilia kwao (kutaka kushirikiana nao Mayahudi, Manaswara na makafiri wengine huku) wakisema: “Tunakhofu isitusibu mgeuko”. Basi Huenda Allaah Akaleta ushindi au jambo (lolote jengine) litokalo Kwake; wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na wale walioamini wanasema (wakati watakapofedheheka wanafiki): “Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa (jina la) Allaah kwa viapo vyao vya nguvu, kwamba hakika wao wapo pamoja nanyi?” Zimeharibika ‘amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚوَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾
54. Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, wenye nguvu juu ya makafiri; wanafanya Jihaad (kupigana) katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya (yeyote) anayelaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mjuzi wa yote daima).إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾
55. Hakika Walii (Mlinzi, Msimamizi) wenu ni Allaah na Mtume Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na hali ya kuwa wanarukuu (katika Swalaah, wananyenyekea).وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Walii (Mlinzi, Msimamizi) na Mjumbe Wake na wale walioamini (atafuzu); kwani hakika kundi la Allaah ndio washindi.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾
57. Enyi mlioamini! Msiwafanye (kuwa ndio) warafiki (zenu) wapenzi wale ambao wameifanyia Dini yenu mzaha na mchezo miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri. Na mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini (kweli).وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na (wakati) mnapoita (mnapoadhini kwa ajili ya kuja kwenye) Swalaah; huifanyia (Swalaah) mzaha na mchezo. Hivyo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ ﴿٥٩﴾
59. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab (Mayahudi na Manaswaara) Je, mnatuchukia tu kwa vile tumemwamini Allaah na (tunaamini) yale yaliyoteremshwa kwetu na (pia tunaamini) yale yaliyoteremshwa kabla; na kwamba wengi wenu ni mafasiki?”قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٦٠﴾
60. Sema: “Je, nikujulisheni yaliyo maovu zaidi kuliko hayo kwa malipo mbele ya Allaah?” Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaaghuut (miungu ya uongo), hao wana mahali pabaya mno na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa (ya haki).وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ ﴿٦١﴾
61. Na wanapokujieni husema: “Tumeamini.” Na hali wameingia na ukafiri na wakatoka nao. Na Allaah Anayajua zaidi yale waliyokuwa wakiyaficha.وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Ubaya ulioje yale waliyokuwa wakiyatenda.لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾
63. Mbona hawawakatazi Ar-Rabbaniyyuwna(Wanavyouni watawa wa Mayahudi) na Al-Ahbaar(Makuhani, Wanavyuoni wao wa dini) kauli zao za dhambi na ulaji wao wa haraam. Bila shaka ubaya ulioje yale waliyokuwa wakitenda.وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۚ وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚكُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ ۚ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا ۚ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٦٤﴾
64. Na Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” (Siyo, bali) mikono yao ndio ilivyofumbwa; na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali Mikono Yake (Allaah) imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. Na bila shaka yatawazidisha wengi miongoni mwao (hao Mayahudi) yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako (yatawazidisha) uasi na kufuru. Na Tumewatilia baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Kila wanapouwasha moto wa vita, Allaah Huuzima. Na wanakimbilia kufanya ufisadi katika ardhi. Na Allaah Hapendi mafisadi.وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٦٥﴾
65. Na lau kama Ahlal-Kitaab (Mayahudi na Manaswaara) wangeamini na wakawa na taqwa, bila shaka Tungeliwafutia maovu yao, na bila shaka Tungeliwaingiza katika Mabustani yenye neema (Peponi).وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ ﴿٦٦﴾
66. Na lau kama wangeliisimamisha (shari’ah ya) Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Mola wao; kwa yakini wangelikula kutoka juu yao na chini ya miguu yao. Miongoni mwao (wapo watu waliokuwa) ni wastani, na (lakini) wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ee Mtume! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha Ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah Hawaongoi watu makafiri.قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾
68. Sema: “EnyiAhlal-Kitaab! (Mayahudi na Manaswaara) Hamko juu ya chochote mpaka muisimamishe Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu. Na bila shaka yatawazidisha wengi katika wao (hao Mayahudi) yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako (yatawazidisha) uasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٩﴾
69. Hakika wale walioamini na wale Mayahudi na Masabai (waabudu nyota) na Manaswara, atakayemwamini Allaah na Siku ya Aakhirah na akatenda mema, basi hawatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika.لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ ﴿٧٠﴾
70. Kwa yakini Tulichukua agano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea Mitume. Basi kila alipowajia Mtume kwa yale yasiyoyashabikia nafsi zao; kundi waliwakadhibisha (Mitume hao) na kundi wakawaua.وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٧١﴾
71. Na walidhani kwamba haitokuwa fitnah, basi wakawa vipofu na wakawa viziwi; kisha Allaah Akapokea tawbah yao; kisha (tena) wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima) kwa wayatendayo.لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٧٢﴾
72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah Mola wangu na Mola wenu. (Kwani) Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Pepo, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu. Na hali hakuna ilaah (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Ilaahun Waahid (Allaah: Mungu Mmoja Pekee). Na wasipoacha (kukufuru) wanayoyasema, kwa yakini itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾
74. Je hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfira? Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖكَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾
75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume (tu); bila shaka wamekwishapita kabla yake Mitume (wengine). Na mama yake ni swiddiyqah(mkweli). Wote wawili walikuwa wanakula chakula (na hivyo wakipata choo). Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayah, kisha tazama vipi wanavyogeuzwa (kuacha haki).قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾
76. Sema: “Vipi mnaabudu ghairi ya Allaah asiyemiliki (uwezo wa) kukudhuruni wala kukunufaisheni! Na Allaah Ndiye As-Samiy’ul- ‘Aliym” (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote Daima).قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٧٧﴾
77. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaab! (Mayahudi na Manaswaara) Msipindukie mipaka katika dini yenu bila ya haki; na wala msifuate matamanio ya watu waliokwishapotea kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.”لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾
78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa ulimi wa Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya (kuendelea) kuasi kwao na walikuwa wakipindukia mipaka.كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾
79. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ﴿٨٠﴾
80. Utawaona wengi miongoni mwao (Mayahudi) wanawafanya marafiki wale waliokufuru. Ubaya ulioje kwa yale waliyotanguliziwa na nafsi zao, (nayo ni) kuwa Allaah Amewaghadhibikia, na katika adhabu wao watadumu milele.وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٨١﴾
81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na (huyu) Nabii (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wapenzi, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Kwa yakini utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wote) kwa wale walioamini, ni Mayahudi na wale walioshirikisha (mushrikina). Na kwa yakini utawakuta walio karibu zaidi kwa mapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: “Sisi ni Manaswaara.” Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Qissiysiyna(makasisi) na Ruhbaan (Wamonaki – watawa wao) na kwamba wao hawatakabari (wakiisikia haki huifuata).