Juzuu Ya 5 – Wal-Muhswanaatu
Juzuu: 5وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ
وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾
24. Na (Mmeharamishiwa pia) muhswanaatu katika wanawake (waliomo katika ndoa) isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shari’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalalishiwa (wengineo) wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao (katika ndoa) wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah ni ‘Aliyman-Hakiymaa(Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima).
وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۚ فَانكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٥﴾
25. Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea muhswanaat (wanawake waungwana waliohuru) Waumini, basi (aoe) katika wale iliyomiliki mikono yenu ya kulia miongoni mwa wajakazi wenu Waumini. Na Allaah ni Mjuzi wa iymaan yenu. (Waumini) Nyinyi kwa nyinyi. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na wapeni mahari yao kwa ma’aruwf; (waoeni na hali ya kuwa ni) muhswanaat (wanawake wanaojistiri na machafu) si makahaba na wala si wenye kuchukua hawara. Na watakapohifadhiwa (katika ndoa), kisha wakafanya faahishah (zinaa) basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu ya waliyowekewa wanawake waungwana (wasioolewa). Hayo ni kwa yule anayeogopa zinaa miongoni mwenu. Na mkisubiri ni kheri kwenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria, – Mwenye Kurehemu).
يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗوَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦﴾
26. Allaah Anataka kukubainishieni (yaliyo halaal na haraam) na kukuongozeni nyendo (nzuri) za wale walio kabla yenu, na Apokee tawbah kwenu. Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote daima, – Mwenye Hikma wa yote daima).
وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُوا مَيْلًا عَظِيمًا ﴿٢٧﴾
27. Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu; na wale ambao wanafuata matamanio (yao) wanataka mkengeuke mkengeuko mkuu.
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾
28. Allaah Anataka kukukhafifishieni (tabu zenu); kwani mwanaadam ameumbwa dhaifu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾
29. Enyi mlioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatilifu, isipokuwa iwe biashara (ya halaal) kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue (au kuuana). Hakika Allaah kwenu ni Rahiymaa (Mwenye Kurehemu).
وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni sahali (daima).
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
31. Mkijiepusha na kabaaira (madhambi makubwa) mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu (Peponi).
وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚ وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾
32. Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliymaa (Mjuzi wa yote daima).
وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَالِيَ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ ۚ وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٣٣﴾
33. Na kila mmoja Tumemuwekea jamaa (zake) wa kurithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale ambao mmefungamana nao ahadi, basi wapeni sehemu yao. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Shahiydaa (Shahidi, Mwenye Kushuhudia yote daima).
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚوَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ﴿٣٤﴾
34. Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao. Basi wanawake swaalihaatu (wema), watiifu, wenye kuhifadhi (hata) wanapokuwa hawapo (waume zao) kwa Aliyoyahifadhi Allaah. Na wale ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Yuko juu ya vyote, Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa).
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾
35. Na mkikhofu mafarikiano baina yao (mke na mume), basi pelekeni hakimu (mwamuzi) kutoka watu wake (mume) na hakimu kutoka watu wake (mke). Wakitaka sulhu (mapatano) Allaah Atawawafikisha baina yao. Hakika Allaah ni ‘Aliyman Khabiyraa (Mjuzi wa yote daima – (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).
وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾
36. Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na majirani wa karibu na majirani wa walio mbali, na rafiki wa ubavuni na msafiri na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye kiburi mwenye kujifakharisha.
الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٣٧﴾
37. Wale ambao wanafanya ubakhili na wanawaamrisha watu ubakhili na wanaficha Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗوَمَن يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا ﴿٣٨﴾
38. Na (pia) wale ambao wanatoa mali zao kwa ajili ya riyaa (kuonyesha watu) na wala hawamwamini Allaah wala Siku ya ‘Aakhirah. Na yule ambaye shaytwaan amekuwa ni rafiki yake mwandani, basi mbaya aliyoje rafiki mwandani (huyo).
وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِهِمْ عَلِيمًا ﴿٣٩﴾
39. Na ingekuwa nini juu yao lau wangelimwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wakatoa katika yale Aliyowaruzuku Allaah. Na Allaah kwao ni ‘Aliymaa(Mjuzi wa yote daima).
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Hakika Allaah Hadhulumu (viumbe Vyake hata) uzito wa atomu. Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu.
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
41. Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?
يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا ﴿٤٢﴾
42. Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Mtume watatamani lau ardhi isawazishwe juu yao. Na wala hawatoweza kumficha Allaah kauli yoyote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾
43. Enyi mloamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala (msikaribie) hali mna janaba isipokuwa wapita njia (ya mahali pa kuswali) mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa (mmekatazwa kutumia maji) au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa (mmewaingilia) wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammamu (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah ni ‘Afuwwan Ghafuwraa(Mwingi wa Kusamehe – Mwingi wa Kughufiria).
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلَالَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ ﴿٤٤﴾
44. Je, huoni (huzingatii) wale waliopewa sehemu ya Kitabu wananunua upotofu na wanataka mpotee njia?
وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَائِكُمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَلِيًّا وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ نَصِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Na Allaah Anawajua vyema maadui zenu, na Allaah Anatosha kuwa Walii na Allaah Anatosha kuwa Naswiyraa (Mwenye Kunusuru, Msaidizi).
مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٤٦﴾
46. Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema (midomoni mwao): “Tumesikia” na (nyoyoni mwao husema): “Tumeasi”; na (wanasema kumwambia Mtume): “Sikia bila kusikilizwa.” Na (hulitamka tamko la): “Raa’inaa” kwa kuzipotoa ndimi zao (hata igeuke maana yake) na kutukana dini. Na lau wangesema: “Tumesikia na tumetii na sikia na utuangalie” (kwa tamko la “Undhwurnaa” badala ya tamko la “Raa’inaa”) ingelikuwa kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Allaah Amewalaani kwa kufru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ آمِنُوا بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰ أَدْبَارِهَا أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّا أَصْحَابَ السَّبْتِ ۚوَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٤٧﴾
47. Enyi mliopewa Kitabu! Aminini yale Tuliyoyateremsha (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yanayosadikisha yale mliyonayo kabla hatujabadilisha nyuso Tukazirudisha kisogoni, au Tukawalaani kama Tulivyowalaani watu wa Sabato (walovunja shari’a ya Jumamosi). Na amri ya Allaah ni ya kufanyika tu.
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
48. Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; na Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amebuni dhambi kuu.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ اللَّـهُ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٤٩﴾
49. Je, huoni (huzingatii) wale ambao wanajitakasa nafsi zao? Bali Allaah Humtakasa Amtakaye; na wala hawatodhulumiwa hata kadiri ya uzi uliomo ndani ya kokwa ya tende.
انظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِ إِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٠﴾
50. Tazama vipi wanavyomzulia uongo Allaah; na yatosha haya kuwa dhambi za dhahiri.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾
51. Je, huoni (huzingatii) wale ambao wamepewa sehemu ya Kitabu wanaamini mazimwi na twaaghuwt(miungu ya uongo) na wanasema juu ya wale ambao wamekufuru kuwa: “Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale ambao wameamini.”
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾
52. Hao ndio wale ambao Allaah Amewalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani basi hatopata wa kumnusuru.
أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ الْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيرًا ﴿٥٣﴾
53. Au wanayo sehemu ya ufalme? Basi, (ingelikuwa ni hivyo) wasingeliwapa watu hata kitone (tundu) cha kokwa ya tende.
أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَآتَيْنَاهُم مُّلْكًا عَظِيمًا ﴿٥٤﴾
54. Au wanawahusudu watu kwa yale Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake? Basi kwa yakini Tuliwapa familia ya Ibraahiym; Kitabu na Hikima na Tukawapa ufalme mkuu.
فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ بِهِ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا ﴿٥٥﴾
55. Basi miongoni mwao wako waliyoyaamini haya, na miongoni mwao wako waliyoyapinga. Na Jahannam yatosheleza kuwa ni moto wa kuunguza.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿٥٦﴾
56. Hakika wale waliozikanusha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) Tutawaingiza motoni. Kila ngozi zao zitakapowiva Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje adhabu. Hakika Allaah ni ‘Aziyzan-Hakiymaa (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika Daima – Mwenye Hikma wa yote daima).
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا ﴿٥٧﴾
57. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Bustani zipitazo chini yake mito, watadumu humo (Peponi) milele. Watapata humo wake waliotakasika na Tutawaingiza katika vivuli vizuri mno.
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾
58. Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika (mawaidha) Anayokuwaidhini nayo Allaah ni mazuri kabisa; hakika Allaah ni Samiy’an-Baswiyraa (Mwenye Kusikia yote daima – Mwenye Kuona yote daima).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖفَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
59. Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya ‘Aakhirah. Hivyo ni (njia) bora na matokeo mazuri zaidi.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾
60. Je, huoni (huzingatii) wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiwe kwa twaaghuwtna hali wameamrishwa wakanushe hiyo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾
61. Na wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume; utawaona wanafiki wanakugeuka kwa upinzani.
فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾
62. Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa: “Wa-Allaahi hatukutaka ila wema na mapatano.”
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَعْلَمُ اللَّـهُ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلًا بَلِيغًا ﴿٦٣﴾
63. Hao ndio ambao Allaah Anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali na wape mawaidha na uwaambie maneno yatakayowaathiri na kuingia katika nafsi zao.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿٦٤﴾
64. Na Hatukutuma Mtume yeyote ila atiiwe kwa idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwomba Allaah maghfirah na Mtume akawaombea maghfirah, basi wangelimkuta Allaah ni Tawwaabar-Rahiymaa (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye Kurehemu).
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
65. Basi Naapa kwa Mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu (mwamuzi) katika yale wanayotofautiana baina yao, kisha wasione katika nyoyo zao uzito katika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.
وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ اقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ أَوِ اخْرُجُوا مِن دِيَارِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا ﴿٦٦﴾
66. Na lau Tungeliwawekea shari’ah (kuwaamrisha): “Jiueni nafsi zenu na tokeni katika majumba yenu”; wasingelifanya hayo ila wachache miongoni mwao. Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa nayo ingelikuwa kheri kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi.
وَإِذًا لَّآتَيْنَاهُم مِّن لَّدُنَّا أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٦٧﴾
67. Na hapo Tungeliwapa kutoka Kwetu ujira mkubwa.
وَلَهَدَيْنَاهُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٦٨﴾
68. Na Tungewaongoza Swiraatwan Mustaqiymaa(njia iliyonyooka).
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
69. Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii, na Maswiddiqiyna (waliosadikisha haki), na Mashahidi na Swaalihiyna (waja wema). Na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki (zake).
ذَٰلِكَ الْفَضْلُ مِنَ اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ عَلِيمًا ﴿٧٠﴾
70. Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa ni ‘Aliymaa (Mjuzi wa yote daima).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا ﴿٧١﴾
71. Enyi mlioamini! Chukueni tahadhari yenu; tokeni kwa vikosi vikosi au tokeni kwa pamoja.
وَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا ﴿٧٢﴾
72. Na hakika miongoni mwenu wako wanaobakia nyuma (wakati wa kwenda vitani); inapokusibuni msiba husema: “Kwa yakini Allaah Amenineemesha nilivyokuwa sikuhudhuria pamoja nao.”
وَلَئِنْ أَصَابَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ اللَّـهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُن بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُ مَوَدَّةٌ يَا لَيْتَنِي كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧٣﴾
73. Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Allaah kwa hakika husema; kama kwamba hakukuwa baina yenu na yake mawaddah (mapenzi): (husema) “Laiti ningelikuwa pamoja nao nikapata kufuzu mafanikio makubwa.”
فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٧٤﴾
74. Basi wapigane katika njia ya Allaah wale ambao wanaouza (wanaochagua) maisha ya dunia kwa Aakhirah. Na atakayepigana katika Njia ya Allaah akauliwa au akashinda basi Tutampa ujira mkubwa.
وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا ﴿٧٥﴾
75. Na mna nini (mpaka mkawa) hampigani katika Njia ya Allaah, na walio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao husema: “Mola wetu Tutoe kutoka katika mji huu ambao watu wake ni dhalimu, na Tujaalie kutoka kwako mlinzi na Tujaalie kutoka Kwako mwenye kunusuru.
الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا ﴿٧٦﴾
76. Wale walioamini hupigana katika Njia ya Allaah. Na wale waliokufuru hupigana katika njia ya twaaghuwt. Basi wapiganeni marafiki wa shaytwaan. Hakika hila za shaytwaan ni dhaifu.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧٧﴾
77. Je, huoni (huzingatii) wale walioambiwa: “Zuieni mikono yenu (msipigane) na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah.” Basi walipoandikiwa kupigana (vita), mara kundi miongoni mwao linakhofu watu kama kumkhofu Allaah au khofu zaidi (ya hiyo). Na husema: “Mola wetu! Kwa nini Umetuandikia kupigana? Lau Ungelituakhirishia hadi muda kidogo hivi!” Sema: “Starehe za dunia ni chache; na Aakhirah ni bora zaidi kwa mwenye kuwa na taqwa; wala hamtodhulumiwa hata uzi uliomo ndani ya kokwa ya tende.”
أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا ﴿٧٨﴾
78. Popote mtakapokuwa yatakufukieni mauti, japo mkiwa katika ngome madhubuti. Na ikiwafikia jema husema: “Hili ni kutoka kwa Allaah.” Na ikiwasibu ovu husema: “Hili kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).” Sema: “Yote ni kutoka kwa Allaah.” Basi wana nini hawa watu hawakaribii kufahamu kauli?
مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚوَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾
79. Wema uliokufikia ni kutoka kwa Allaah. Na ubaya uliokusibu (ee binaadamu) ni kutokana na nafsi yako. Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Mtume na inatosheleza Allaah kuwa ni Shahiydaa (Shahidi, Mwenye Kushuhudia yote daima).
مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾
80. Atakayemtii Mtume basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.
وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَائِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ الَّذِي تَقُولُ ۖوَاللَّـهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾
81. Na husema: “Tunatii.” Lakini wanapotoka kutoka kwako, kundi miongoni mwao hukesha kushauriana kinyume na unayoyasema. Na Allaah Anayaandika yale wanayokeshea. Basi waachilie mbali na tawakali kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Wakiylaa(Wakili, Mtegemewa kwa yote).
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾
82. Je hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka ghairi ya Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake ikhtilafu nyingi.
وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾
83. Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Mtume na kwa wenye madaraka kati yao, wale (Wanavyuoni) wanaotafiti miongoni mwao wangelilijua. Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan (nyote) ila wachache tu.
فَقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَاللَّـهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا ﴿٨٤﴾
84. Basi pigana katika Njia ya Allaah, hukalifishwi ila nafsi yako. Na wahimize Waumini. Huenda Allaah Akazuia mashambulizi ya nguvu ya waliokufuru. Na Allaah ni Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu (adhabu ya funzo).
مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾
85. Atakayeombea shafa’ah njema, atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombea shafa’ah ovu atapata sehemu katika hayo. Na Allaah juu ya kila kitu ni Muqiytaa (Mwenye Uwezo, Kudhibiti, Kuhifadhi, Mwangalizi).
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴿٨٦﴾
86. Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo (kama mlivyoamkiwa). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Hasiybaa(Mwenye Kuhesabu, Kutosheleza).
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾
87. Allaah; laa ilaaha illaa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye). Bila shaka Atakukusanyeni (kukuhesabuni) Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?
فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾
88. Basi mna nini (hata) mkawa makundi mawili kuhusu wanafiki; na Allaah Amewageuza (katika makosa na kufru) kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Je, mnataka kumhidi ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumwongoza).
وَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا فَتَكُونُونَ سَوَاءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ أَوْلِيَاءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٨٩﴾
89. Wanatamani kama mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msichukue miongoni mwao mawalii (marafiki wapenzi) mpaka wahajiri (wahame) katika Njia ya Allaah. Wakikengeuka basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Wala msichukue miongoni mwao walii wala mwenye kunusuru (msaidizi).
إِلَّا الَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ أَوْ جَاءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَاتِلُوكُمْ أَوْ يُقَاتِلُوا قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَاتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ﴿٩٠﴾
90. Isipokuwa wale ambao wanafungamana na watu ambao baina yenu na baina yao mna mkataba au wamekujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao. Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasaliti juu yenu, wakapigana nanyi. Basi wakijitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia juu yao (ya kuwapiga vita).
سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَـٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿٩١﴾
91. Mtawakuta wengine wanaotaka kupata amani kwenu na kupata amani kwa watu wao; kila wanaporudishwa katika fitnah huangushwa humo. Wasipokuachilieni mbali na wakakuleteeni amani na wakazuia mikono yao (kukupigeni), basi wachukuweni na wauweni popote muwapatapo. Na hao Tumekufanyieni dhidi yao mamlaka yaliyo bayana.
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٩٢﴾
92. Na haiwi kwa Muumin amuue Muumin ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumin kwa kukosea basi aachilie huru mtumwa Muumin na atoe diya kwa kuisalimisha kwa watu wake (ahli wa maiti) isipokuwa watolee swadaqah (wasamehe haki yao). Na ikiwa ni miongoni mwa watu wa maadui zenu naye ni Muumin, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumin. Na ikiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao; basi wapewe diya kuisalimisha kwa watu wake na aachiliwe huru mtumwa Muumin. Asiyepata (asiyekuwa na uwezo), afunge Swawm (badala yake) miezi miwili mfululizo; kuwa ni tawbah kwa Allaah. Na Allaah ni ‘Aliyman Hakiymaa (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima).
وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾
93. Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni (moto wa) Jahannam, atadumu humo milele na Allaah Atamghadhibikia na Atamlaani na Atamuandalia adhabu kuu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾
94. Enyi mlioamini! Mnaposafiri (kupigana Jihaad) katika Njia ya Allaah hakikisheni. Wala msimwambie anayekutoleeni (maamkizi ya) salamu (kwamba): “Wewe si Muumin” kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan basi hakikisheni. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Khabiyraa(Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).
لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ