Juzuu

Juzuu



95. Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyuma kutokwenda vitani) wasiokuwa na dharura na Mujaahiduwna katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo Mujaahidiyna kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (thawabu na Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha Mujaahidiyna kwa ujira mkubwa kuliko wanaokaa (nyuma).

دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾

 

96. Ni vyeo (vya juu kabisa) kutoka Kwake na maghfirah na Rahmah. Na Allaah ni Ghafuwrar-Rahiymaa(Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu). 

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَاۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

 

97. Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao; (Malaika) watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni (moto wa) Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kurejea.

إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾

 

98. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata (mpango wa) hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia.

فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٩٩﴾

 

99. Basi hao huenda Allaah Akawasamehe. Na Allaah ni ‘Afuwwan-Ghafuwraa (Mwingi wa Kusamehe – Mwingi wa Kughufiria).

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

 

100. Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia na wasaa. Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umeshatokea kwa Allaah. Na Allaah ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).

وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿١٠١﴾

101. Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah (hasa) mkikhofu kwamba waliokufuru watakufitinisheni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri.

وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖوَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾

 

102. Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu (watakapomaliza sijda zao), basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jengine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike tahadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na chukueni tahadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.

فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

 

103. Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na ubavuni mwenu (mlalapo). Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi). Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu.

وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖوَتَرْجُونَ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٠٤﴾

 

104. Wala msilegee kuwafuatia (kuwaandama) watu. Mkiwa manaumia basi nao (pia) wanaumia kama mnavyoumia. Na mnataraji kutoka kwa Allaah wasiyoyataraji wao. Na Allaah ni ‘Aliyman-Hakiymaa(Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima).

إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾

105. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini. 

وَاسْتَغْفِرِ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٦﴾

 

106. Na muombe Allaah maghfira. Hakika Allaah daima ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).

وَلَا تُجَادِلْ عَنِ الَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا ﴿١٠٧﴾

 

107. Wala usijadili (usiwatetee) kuhusu wanaokhini nafsi zao. Hakika Allaah Hampendi aliye khaini mtendaji dhambi kwa wingi.

يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ﴿١٠٨﴾

 

108. Wanaficha kwa watu (niyyah na vitendo wala hawafichi (hawawezi kuficha) kwa Allaah, Naye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) pale wanapokesha kupanga njama kwa zile kauli Asizoziridhia. Na Allaah kwa wayatendayo ni Muhiytwaa (Mwenye Kuzunguka vyote kwaUjuzi).

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ جَادَلْتُمْ عَنْهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَمَن يُجَادِلُ اللَّـهَ عَنْهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿١٠٩﴾

 

109. Ha! Nyinyi ndio hawa mliojadili kwa niaba yao (mmewatetea) katika maisha ya dunia. Basi nani atakayemjadili Allaah kuhusu wao Siku ya Qiyaamah au nani atakayekuwa mdhamini wao?

وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾

 

110. Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake; kisha akamwomba Allaah maghfira; atamkuta Allaah ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).

وَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١١﴾

 

111. Na atakayechuma dhambi, basi hakika anaichumia nafsi yake. Na Allaah ni ‘Aliyman Hakiymaa (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima).

وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿١١٢﴾

 

112. Na atakayechuma hatia (kosa) au dhambi kisha akamtupia (akamsingizia) asiye na hatia; basi kwa yakini atajitweka buhtaanan (usingiziaji) na dhambi zilizo bayana.

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُ لَهَمَّت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ ۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيْءٍ ۚ وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا ﴿١١٣﴾

113. Na lau kuwa si fadhila ya Allaah juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na Rahmah Yake; bila shaka kundi miongoni mwao lingefanya hima (kudhamiria) kukupoteza. Na hawazipotezi ila nafsi zao, na hawakudhuru kwa chochote. Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na fadhila za Allaah juu yako ni kubwa. 

لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾

 

114. Hakuna kheri katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha kutoa swadaqah, au (kumarisha) ma’aruwf (Uislamu, mema), au kusuhulisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka Radhi za Allaah, basi Tutampa ujira mkubwa.

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾

 

115. Na atakayempinga Mtume baada ya kuwa umeshambainikia Al-Hudaa (Uuongofu) na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini; Tutamgeuza alikogeukia (mwenyewe upotofuni) na Tutamuingiza (moto wa) Jahannam. Na uovu ulioje mahali pa kurejea.

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾

 

116. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria (mengineyo) yasiyokuwa hayo (ya shirki) kwa Amtakaye. Na atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾

 

117. Hawaombi (katika ‘ibaadah zao) ghairi Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi (hakika) isipokuwa shaytwaan muasi.

لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾

 

118. Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: “Kwa hakika nitachukua (nitashika) katika waja Wako sehemu maalumu.

وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾

 

119. Na hakika nitawapoteza, na nitawatumainisha na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawafanye kuwa hao ni wanyama watukufu), na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa ni walii (rafiki mwandani) badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara iliyo bayana.

يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢٠﴾

 

120. Anawaahidi na anawatumainisha. Na shaytwaan hawaahidi isipokuwa ghuruwr (udanganyifu).

أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾

121. Hao makaazi yao ni (moto wa) Jahannam, na wala hawatopata makimbilio ya kutoka humo.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا ﴿١٢٢﴾

 

122. Na wale walioamini na wakatenda mema, Tutawaingiza Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo (Peponi) milele. Ahadi ya Allaah ni iliyo haki. Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?

لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾

 

123. Si kwa matamanio yenu (Waumini) wala si matamanio ya Ahlil-Kitaab (Mayahudi na Manaswaara) (kutakaswa, kuokoka na moto na kuipata Pepo). Atakayefanya uovu atalipwa kwayo, na wala hatapata pasi na Allaah walii wala mwenye kunusuru.

وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا ﴿١٢٤﴾

 

124. Na atakayefanya katika mema akiwa mwanamume au mwanamke hali yeye ni Muumin; basi hao wataingia Jannah (Peponi) na wala hawatodhulumiwa watu hata kitone (tundu) cha kokwa ya tende. 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

 

125. Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyeuelekeza uso wake kwa Allaah naye ni Muhsin(mwema) na akafuata mila ya Ibraahiym haniyfaa(aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki). Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni khaliyl (kipenzi).

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطًا ﴿١٢٦﴾

 

126. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Allaah kwa kila kitu ni Muhiytwaa(Mwenye Kuzunguka vyote kwa Ujuzi).

وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾

127. Na wanatafuta kwako fatwa (hukmu ya Shari’ah ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: “Allaah Atakupeni hukmu kuhusu wao na yale mnayosomewa kwenu katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari yao) waliyoandikiwa; na mnapenda kuwaoa. Na juu ya walio dhaifu katika watoto. Na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la kheri basi hakika Allaah kwa hilo ni ‘Aliymaa (Mjuzi wa yote daima).

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

 

128. Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe nushuwzaa (uonevu wa ndoa) au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa sulhu Na sulhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo mbele (ya macho yake) Na mkifanya wema na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa mfanyao ni Khabiyraa (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾

 

129. Na wala hamtaweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msielemee muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mke mwengine msiyempenda) kama kining’inio (aliyetundikwa). Na mkisuluhisha na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah ni  Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴿١٣٠﴾

 

130. Na wakifarikiana (wakiachana kwa talaka) basi Allaah Atamkwasisha kila mmoja katika wasaa Wake. Na Allaah ni Waasi‘an-Hakiymaa (Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mwenye Hikma wa yote daima).

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَنِيًّا حَمِيدًا ﴿١٣١﴾

 

131. Na ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na kwa yakini Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na (Tumewausia) nanyi (pia), kwamba: “Mcheni Allaah.” Na mkikufuru basi hakika ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na Allaah ni Ghaniyyan-Hamiydaa (Mkwasi, Hahitaji Lolote – Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa na Kushukuriwa).

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٣٢﴾

 

132. Na ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na inatosheleza Allaah kuwa ni Wakiylaa(Wakili, Mtegemewa Kwa Yote). 

إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا النَّاسُ وَيَأْتِ بِآخَرِينَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا ﴿١٣٣﴾

 

133. Akitaka, Atakuondoeni mbali enyi watu, na Ataleta wengine. Na Allaah kwa hayo ni Qadiyraa (Muweza wa yote daima).

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿١٣٤﴾

134. Anayetaka thawabu za dunia basi kwa Allaah kuna thawabu za dunia na Aakhirah. Na Allaah ni Samiy’an-Baswiyraa (Mwenye Kusikia yote daima – Mwenye Kuona yote daima).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾

 

135. Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini Allaah Anawastahiki zaidi (kuliko wewe). Basi msifuate hawaa (matamanio) mkaacha kufanya uadilifu. Na mkipotoa (ushahidi wenu) au mkijitenga (kuepuka au kukataa kutoa ushahidi), basi hakika Allaah kwa myatendayo ni Khabiyraa(Mjuzi wa undani na ukina wa mambo). 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٣٦﴾

 

136. Enyi mlioamini! Mwaminini Allaah na Mtume Wake na Kitabu Alichokiteremsha kwa Mtume Wake na Kitabu Alichokiteremsha kabla. Na atakayemkanusha Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ya ‘Aakhirah, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًا ﴿١٣٧﴾

 

137. Hakika wale ambao wameamini kisha wakakufuru kisha wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi kufru, Allaah Hatowaghufiria na wala Hatowaongoa njia (ya haki).

بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣٨﴾

 

138. Wabashirie wanafiki kwamba watapata adhabu iumizayo.

الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ﴿١٣٩﴾

 

139. Wale ambao wanafanya makafiri kuwa ni mawalii (marafiki wapenzi) badala ya Waumini. Je wanatafuta utukufu (wa nguvu) kutoka kwao? Basi hakika utukufu wote ni wa Allaah Pekee.

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗإِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا ﴿١٤٠﴾

 

140. Naye Amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Au sivyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah Atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika (moto wa) Jahannam.

الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّـهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا ﴿١٤١﴾

 

141. Wale ambao wanakungojeeni na kuangaza (mpate msiba). Inapokuwa ni ushindi kwenu kutoka kwa Allaah; husema: “Je, hatukuwa pamoja nanyi?” Na inapokuwa kwa makafiri sehemu (ya ushindi); husema: “Hatukukudhibitini (tulipokuwa katika jeshi la Waislamu) na tukakuzuilieni (tukakukingeni) na Waumini?” Basi Allaah Atawahakumu baina yenu Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Hatojaalia kwa makafiri njia (ya kuwashinda).

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾

 

145. Hakika wanafiki wanamhadaa Allaah. Na Yeye (Allaah) Atawaadhibu kwa hadaa zao. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wanajionyesha kwa watu (riyaa) na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.

مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿١٤٣﴾

 

143. Wanayumbayumba baina ya huko (kwa Waislamu na huko kwa makafiri). Huku hawako wala huko hawako. Na ambaye Allaah Amempotoa huwezi kumpatia njia (ya kumuongoa).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚأَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّـهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٤٤﴾

 

144. Enyi mlioamini! Msiwafanye makafiri kuwa mawalii (marafiki wapenzi) badala ya Waumini. Je, mnataka Allaah Awe na hoja bayana dhidi yenu? (iwe sababu ya kukuadhibuni?).

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾

 

145. Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto; na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru (yeyote).

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾

 

146. Isipokuwa wale ambao wametubu na wakatengenea na wakashikamana na Allaah na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah; basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira mkuu.

مَّا يَفْعَلُ اللَّـهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَآمَنتُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ شَاكِرًا عَلِيمًا ﴿١٤٧

147. Allaah Hatokuadhibuni ikiwa mtashukuru na mtaamini. Na Allaah ni Shaakiran ‘Aliymaa (Mwenye Kupokea Shukurani – Mjuzi wa yote daima)


Report Page