Juzuu Ya 28 – Qad Sami’a Allaahu

Juzuu Ya 28 – Qad Sami’a Allaahu

Juzuu: 28

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ

سُورَةُ الْمُجَادلَة

Al-Mujaadalah (58)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿١﴾

1. Allaah Amekwishasikia kauli ya yule (mwanamke) anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah niSamiy’um-Baswiyr (Mwenye kusikia yote daima – Mwenye kuona yote daima). 

الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ﴿٢﴾

2. Wale wanaotamka Dhwihaarmiongoni mwenu (kumwambia mke: wewe kwangu sawa na mgongo wa mama yangu) (na kuwapelekea kujitenga na kutowajimai) wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao wanasema kauli ya kuchukiza katika kauli na (katika) uongo. Na hakika Allaah bila shaka ni‘Afuwun-Ghafuwr (Mwenye kusamehe – Mwingi wa kughufuria). 

وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٣﴾

3. Na wale wanaotamka Dhwihaar kwa wake zao, kisha wakarudi katika waliyoyasema (wakaitengua kauli yao ya Dhwihaar), basi (kafara yao ni) kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hivyo kwenu mnawaidhiwa kwayo (ili msirudie jambo) hilo. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Khabiyr(Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana). 

 

فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٤﴾

4. Na yule asiyepata (mtumwa), basi (afunge) Swawm miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Mtume Wake. Na hiyo ni Mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo. 

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَقَدْ أَنزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٥﴾

5. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake wamefedheheshwa kama walivyofedheheshwa wale wa kabla yao. Na Tumekwishateremsha Aayah bayana, na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha. 

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ أَحْصَاهُ اللَّـهُ وَنَسُوهُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٦﴾

6. Siku Atakayowafufua Allaah wote, Awajulishe yale (yote) waliyoyatenda, Allaah Ameyadhibiti nao wameyasahau; na Allaah juu ya kila kitu ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia). 

أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٧﴾

7. Je, huoni kwamba Allaah Anajua yale (yote) yaliyomo mbinguni na yale (yote) yaliyomo ardhini? Hauwi mnong’ono wa (watu) watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao (kwa ujuzi Wake), na wala (hauwi mnong’ono wa) chini (kuliko) ya hivyo, na wala (wa) wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao (kwa ujuzi Wake) popote watakapokuwa; kisha Atawajulisha kwa yale (yote) waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi daima). 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٨﴾

8. Je, huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wanarudia yale waliyokatazwa nayo, na wananong’onezana kwa (mambo yanayohusu) dhambi na uadui na kumuasi Mtume? Na wanapokujia wanakuamika kwa (maamkizi) Asiyokuamkia kwayo Allaah; na wanasema katika nafsi zao: “Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema?” (Moto wa) Jahannam unawatosheleza, watauingia waungue, na pabaya mno mahali pa kuishia mwishoni. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Mnaponong’onezana, basi msinong’onezane kwa (mambo yanayohusu) dhambi na uadui na kumuasi Mtume (lakini) nong’onezaneni kwa (mambo yanayohusu) wema na taqwa; na mcheni Allaah Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa (nyote). 

إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾

10. Hakika mnong’ono ni kutoka kwa shaytwaan ili awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru chochote isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na kwa Allaah (Pekee) watawakali Waumini. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١١﴾

11. Enyi mlioamini! Mnapoambiwa: “Fanyeni nafasi katika majlisi,” basi (sogeeni) mfanye nafasi; Allaah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: “Inukeni,” basi inukeni; Allaah Anawapandisha daraja zaidi wale walioamini miongoni mwenu na wale waliopewa elimu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana). 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ۚذَٰلِكَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَأَطْهَرُ ۚ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Enyi mlioamini! Mnapotaka kunong’ona (kushauriana kwa siri na)  Mtume basi kadimisheni sadaka kabla ya mnong’ono wenu. Hivyo ni kheri kwenu na (ni) utakaso zaidi. Na msipopata, basi hakika Allaah niGhafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu). 

أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٣﴾

13. Je, mnaogopa kukadimisha swadaqah kabla ya mnong’ono wenu? Ikiwa hamjafanya na Allaah Akapokea tawbah yenu; basi simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Allaah na Mtume Wake; na Allaah niKhabiy (Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa yale myatendayo. 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤﴾

14. Je, huwaoni wale waliofanya urafiki na watu (ambao) Allaah Ameghadhibika nao, wao si miongoni mwenu (ni wanafiki), na wala si miongoni mwao (ni unafiki tu). Na wanaapia uongo, nao wanajua (kuwa ni uongo). 

 

أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾

15. Allaah Amewaandalia adhabu kali, hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu mno. 

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٦﴾

16. Wamechukua viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya vitendo vyao), (hivyo) wakazuia (watu) Njia ya Allaah, basi watapa adhabu idhalilishayo. 

 

لَّن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٧﴾

17. Hazitowafaa kitu chochote mali zao na wala watoto wao mbele ya Allaah, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. 

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ ۖ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٨﴾

18. Siku Atakayowafufua Allaah wote, watamwapia kama wanavyokuapieni nyinyi, na watadhania kwamba wamesimamia juu ya kitu (hoja). Tanabahi! Hakika wao ni waongo. 

اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٩﴾

19. Shaytwaan amewatawala, akawasahaulisha Dhikr ya Allaah, hao ndio kundi la shaytwaan. Tanabahi! Hakika kundi la shaytwaan ndio lenye kukhasirika. 

إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ ﴿٢٠﴾

20. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake hao ndio kati ya (wale) waliodhalilishwa. 

كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢١﴾

21. Allaah Amekwishaandika kwamba: “Bila shaka Nitashinda Mimi na Mitume Yangu.” Hakika Allaah niQawiyyun-‘Aziyz (Mwenye nguvu zote daima – Mwenye enzi ya nguvuAsiyeshindika daima). 

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٢٢﴾

22. Hutokuta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Aakhirah (kuwa) wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa (ni) baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao Iymaan, na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake, na Atawaingiza (kwenye) mabustani yapitayo chini yake mito (Peponi) wadumu milele humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufauluسُورَةُ الْحَشْر

Al-Hashr (59)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Allaah (vyote) vilivyomo mbinguni na (vyote) vilivyomo ardhini. Naye ndiye Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima).



هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا ۖ وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu (Mayahudi wa Banu An-Nadhwiyr) kutoka majumbani mwao katika mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhania kwamba watatoka, nao wakadhani kwamba ngome zao zitawakinga dhidi ya Allaah. (Lakini) Allaah Akawafikia (kwa Adhabu Yake) kutoka (mahali) wasipotazamia, na Akatia kiwewe (woga) katika nyoyo zao. Wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na (kwa) mikono ya Waumini, basi zingatieni, enyi wenye uoni (na kutia akilini). 

وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ ﴿٣﴾

3. Na lau kama Allaah Asingeliwaandikia kufukuzwa nchi, bila shaka Angeliwaadhibu duniani, na Aakhirah watapata adhabu ya Moto. 

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۖ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٤﴾

4. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Mtume Wake. Na yeyote (yule) anayempinga Allaah, basi hakika Allaah ni Shadiydul-‘Iqaab (Mkali wa kuadhibu). 

مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Hamkukata mtende wowote (ule, katika mitende yao mliyoikata) au mliouacha umesimama juu ya shina lake, basi ni kwa Idhini ya Allaah na ili Awahizi mafasiki. 

وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾

6. Na ngawira yeyote ile Aliyoleta Allaah kwa Mtume Wake kutoka kwao; basi hamkuyaendea mbio kwa farasi na wala ngamia (vitani), lakini Allaah Huwasalitishia Mitume Yake kwa Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu niQadiyr (Mweza daima). 

مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ ۚوَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٧﴾

7. Ngawira Aliyoyatoa Allaah kwa Mtume Wake kutoka kwa watu wa vijiji, basi ni za Allaah na Mtume(Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili yasiwe yanarudiarudia (kinyang’anyiro) baina ya matajiri miongoni mwenu. Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)basi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah niShadiydul-‘Iqaab (Mkali wa kuadhibu). 

 

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿٨﴾

8. (Na pia liweko fungu la ngawira) Kwa masikini Muhaajiriyn (waliohajiri) ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na (wakaacha au zikataifishwa) mali zao wanatafuta fadhila kutoka kwa Allaah na Radhi na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake; hao ndio wakweli. 

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٩﴾

9. Na (pia wapewe) wale waliokuwa na makazi (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao, na wala hawapatikuhisi hajayoyote (choyo, wivu, husda) vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiriyn), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wana ufukara. Na yeyote (yule) anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. 

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Na (pia wapewe) wale waliokuja baada yao (wenye) kusema: “Mola wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.) kwa wale walioamini; Mola wetu! Hakika Wewe ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma na upole mno – Mwenye kurehemu). 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١١﴾

11. Je, huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu (Mayahudi): “Mkitolewa (mkifukuzwa kutoka Madiynah), bila shaka nasi tutatoka pamoja nanyi, na wala hatutomtii yeyote abadan dhidi yenu. Na mkipigwa vita, bila shaka tutakunusuruni.” Na Allaah Anashuhudia kwamba wao bila shaka ni waongo. 

لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١٢﴾

12. Wakitolewa, hawatotoka pamoja nao, na wakipigwa vita, hawatowanusuru, na hata wakiwanusuru, bila shaka watageukia mbali migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa. 

لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِم مِّنَ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ﴿١٣﴾

13. Bila shaka nyinyi (Waumini) ni tisho kubwa katika vifua vyao kuliko (wanavyomuogopa) Allaah. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiofahamu. 

لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿١٤﴾

14. Hawatopigana nanyi wote (kwa mkusanyiko) isipokuwa katika vijiji vilivyohifadhiwa kwa ngome, au kutoka nyuma ya kuta. Vita vyao baina yao ni vikali. Utawadhania wako pamoja, kumbe nyoyo zao ziko mbalimbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini. 

كَمَثَلِ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٥﴾

15. (Hali yao hawa Mayahudi wa Banu Nadhwiyr) Ni kama mfano wa wale (Mayahudi wa Banu Qaynuqaa) walio kabla yao hivi karibuni tu walionja matokeo ya ubaya wa mambo yao, na watapata adhabu iumizayo. 

كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾

16. (Wanafiki ni) Kama mfano wa shaytwaan anapomwambia mtu: “Kufuru!” Alipokufuru; (shaytwaan) husema: “Hakika mimi siko pamoja nawe! Mimi namuogopa Allaah Mola wa walimwengu.” 

فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿١٧﴾

17. Basi yakawa matokeo yao wote wawili ni kwamba watakuwa Motoni wote wawili wadumu humo milele. Na hiyo ndio jazaa ya madhalimu. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚإِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨﴾

18. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho (Siku ya Qiyaamah), na mcheni Allaah. Hakika Allaah niKhabiyr (Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa yale (yote) myatendayo. 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿١٩﴾

19. Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki. 

لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾

20. Hawalingani sawa watu wa Motoni na watu wa Jannah, watu wa Jannah ndio wenye kufuzu. 

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۚوَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾

21. Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya jabali, bila shaka ungeliliona linanyenyekea (na) lenye kupasukapasuka kutokana na khofu ya Allaah. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu ili wapate kutafakari. 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾

22. Yeye ni Allaah, Ambaye hapana ilaaha ila Yeye. ‘Aalimul-Ghaybi wash-Shahaadah (Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri), Yeye Ndiye Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah – Mwenye kurehemu). 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾

23. Yeye Ndiye Allaah Ambaye hapana ilaaha ila Yeye, Al-Malik (Mfalme), Al-Qudduws (Mtakatifu, Ametakasika na Sifa zote Hasi), As-Salaam (Mwenye amani na kusalimika na kasoro zote),Al-Muumin (Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha), Al-Muhaymin (Mwenye kutawalia na kuendesha), Al-‘Aziyz(Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima), Al-Jabbaar (Asiyeshindwa kufanya Atakalo), Al-Mutakabbir(Mkubwa, Aliye na nguvu dhidi ya kila shari, ovu na dhulma), Subhaana Allaah! (Ametakasika Allaah) kwa yale yote wanayomshirikisha (nayo). 

هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

24. Yeye Ndiye Allaah, Al-Khaaliq(Muumbaji), Al-Baariu (Mwanzishi viumbe bila kasoro), Al-Muswawwir(Muundaji sura na umbile), AnaAsmaaul-Husnaa (Majina Mazuri kabisa), vinamsabihi (vyote) vilivyomo katika mbingu na ardhi; Naye NdiyeAl-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima).سُورَةُ الْمُمْتُحِنَة

Al-Mumtahinah (60)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي ۚتُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١﴾

1. Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu (kuwa) marafiki wandani mkiwapelekea (siri za mikakati) kwa mapenzi, na hali wamekwishakanusha Haki iliyokujieni (Qur-aan). Wanamtoa kwa kumfukuza Mtume (pamoja) na nyinyi kwa vile mmemuamini Allaah Mola wenu; ikiwa mmetoka (kwa ajili ya) jihaad katika Njia Yangu na kutafuta radhi Zangu. Mnawapa siri kwa mapenzi, na (hali) Mimi Najua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Na yeyote (yule) atakayefanya hivyo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia ya sawa. 

إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ ﴿٢﴾

2. Wakikudhibitini (wakakushindeni) watakuwa ni maadui kwenu, na watakunyosheeni mikono yao na ndimi zao kwa uovu, na watatamani lau mngekufuru. 

لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٣﴾

3. Hawatokufaeni (kitu) jamaa zenu wa uhusiano wa damu, na wala watoto wenu Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atapambanua baina yenu; na Allaah kwa yale myatendayo ni Baswiyr(Mwenye kuona). 

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٤﴾

4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale (yote) mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya daima mpaka mumuamini Allaah Pekee.” Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: “Nitakuombea maghfirah, na wala similiki kitu chochote kwako mbele ya Allaah. Mola wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia mwishoni. 

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٥﴾

5. “Mola wetu! Usitujaalie (kuwa) fitnah kwa wale waliokufuru, na Tughufurie Mola wetu; hakika Wewe ni Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvuAsiyeshindika daima  – Mwenye hikmah wa yote daima).” 

لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٦﴾

6. Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika (mwenendo) wao kwa aliyekuwa ana matarajio Allaah na Siku ya Aakhirah Na yeyote atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Al-Ghaniyyul-Hamiyd (Mkwasi, Hahitaji lolote – Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima). 

عَسَى اللَّـهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَاللَّـهُ قَدِيرٌ ۚوَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧﴾

7. Huenda Allaah Akajaalia mapenzi baina yenu na baina ya wale mlio na uaduwi nao; na Allaah ni Qadiyr(Muweza wa yote daima), na Allaah niGhafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria – Mwenye kurehemu). 

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٨﴾

8. Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu. 

إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٩﴾

9. Hakika Allaah Anakukatazeni tu kuhusu wale waliokupigeni vita katika Dini, na wakakuoteni kutoka majumbani mwenu, na wakasadiana (kwenye) kukutoeni (ndio Anakataza) kufanya urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya (hao) marafiki, basi hao ndio madhalimu. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike Muhaajiraat(waliohajiri), basi wajaribuni. Allaah Anajua zaidi iymaan zao. Na mkiwatambua kuwa ni Waumini (wa kike), basi msiwarejeshe (Makkah) kwa makafiri. Wao si (wake) halali kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halali kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa; na takeni (kurudishiwa) mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio Hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu, na Allaah ni ‘Aliymun-Hakim (Mjuzi daima wa yote – Mwenye hikmah wa yote daima). 

وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا أَنفَقُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾

11. Na kama mkimpoteza yeyote kati ya wake zenu (akitoroka na) kurejea kwa makafiri (bila ya kurudisha mahari), ikatokea kuwa (mmekwenda vitani dhidi yao na mkapata ngawira), basi wapeni wale walioondokewa na wake zao mfano wa walichotoa (mahari); na mcheni Allaah Ambaye nyinyi Kwake mnamuamini. 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Ee Nabii! Wakikujia Waumini wa kike wanafungamana nawe ahadi kwamba hawatamshirikisha Allaah na chochote, na wala hawataiba, na wala hawatazini, na wala hawataua watoto wao, na wala hawataleta kashfa wanayoizusha baina ya mikono yao na miguu yao, na wala hawatakuasi katika (jambo) jema; basi fungamana nao ahadi, na waombee maghfira kwa Allaah. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria – Mwenye kurehemu). 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ ﴿١٣﴾

13. Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki watu ambao Allaah Ameghadhibika nao, wamekwishakata tamaa na Aakhirah kama walivyokwishakata tamaa makafiri kati ya watu wa makaburini. سُورَةُ الصَّف

Asw-Swaff (61)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Allaah (vyote) vilivyomo mbinguni na (vyote) vilivyomo ardhini. Naye ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima). 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٢﴾

2. Enyi mlioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? 

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ ﴿٣﴾

3. Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. 

إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ ﴿٤﴾

4. Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika Njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo linalokamatana barabara. 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٥﴾

5. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Muwsaa alipowaambia watu wake: “Enyi watu wangu! Kwanini mnaniudhi na hali mmekwishajua kwamba hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu?” Basi walipopotoka, Allaah Akapotosha nyoyo zao; na Allaah Haongoi watu mafasiki. 

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖفَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٦﴾

6. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposema ‘Iysaa mwana wa Maryam: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nnayesadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake: Ahmad.” Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: “Hii ni sihiri bayana.” 

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Allaah uongo na (hali) yeye analinganiwa katika Uislamu? Na Allaah Haongoi watu madhalimu. 

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ ﴿٨﴾

8. Wanataka kuizima Nuru ya Allaah kwa midomo yao, (lakini) Allaah ni Mwenye kuitimiza Nuru Yake japo makafiri watachukia. 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٩﴾

9. Yeye Ndiye Aliyemtuma Mtume Wake (Nabii Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Hidaayah na Dini ya haki (ya Kiislamu) ili Aidhihirishe (Aishindishe) juu ya Dini zote, japo washirikina watachukia. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿١٠﴾

10. Enyi mlioamini! Nikujulisheni tijara (biashara) itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? 

 

تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١﴾

11. Mumuamini Allaah na Mtume Wake, na mfanye Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua. 

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾

12. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni mabustanini yapitayo chini yake mito (Peponi) na masikani mazuri katika mabustaniya ‘Adn. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 

وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣﴾

13. Na (Atakupeni neema) nyinginezo mzipendazo; nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ ۖفَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Kuweni Answaar(wenye kunusuru Dini ya) Allaah kama (vile alivyosema) ‘Iysa mwana wa Maryam kuwaambia Al-Hawariyyiyn(wafuasi): “Nani Answaar wangu kwa (ajili ya) Allaah?” Al-Hawariyyuwnwakasema: “Sisi ni Answaaru Allaah.” Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israaiyl na likakufuru kundi. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi.سُورَةُ الْجُمُعَة

Al-Jumu’ah (62)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Allaah (vyote) vilivyomo mbinguni na (vyote) vilivyomo ardhini,Al-Malik (Mfalme) Al-Qudduws(Mtakatifu, Ametakasika na Sifa zote Hasi) Al-‘Aziyzil-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima). 

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Aliyepeleka Mtume kwaAl-Ummiyyiyn (watu wasioelewa kusoma wala kuandika) miongoni mwao anawasomea Aayah Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu (Qur-aan) na Hikmah (Sunnah), na japo walikuwa kabla katika upotofu bayana. 

وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٣﴾

3. Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye NdiyeAl-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima). 

ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٤﴾

4. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu. 

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚبِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥﴾

5. Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe (kwa kutotekeleza amri zake) ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayah za Allaah, na Allaah Haongoi watu madhalimu. 

قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّـهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦﴾

6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Enyi Mayahudi! Mkidai kuwa nyinyi ni awliyaa (vipenzi) wa Allaah pasina watu wengine, basi tamaneni mauti, mkiwa ni wasemao kweli. 

وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٧﴾

7. Na wala hawatayatamani (hayo mauti) abadan kwa sababu ya yale (maovu) yaliyotanguliza mikono yao, na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi daima) wa madhalimu. 

قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika (hayo) mauti mnayoyakimbia, hakika yatakukuteni tu! Kisha mtarudishwa kwa ‘Aalimul-Ghaybi Wash-Shahaadah (Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri) Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Inaponadiwa (adhana ya) Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kwenye dhikri ya Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.


Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈


https://t.me/Furqanbot




Report Page