Juzuu

Juzuu


فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠﴾

10. Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah sana ili mpate kufaulu. 

وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١﴾

11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم ): “Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah ni Khayrur-Raaziqiyn(Mbora wa wanaoruzuku).سُورَةُ الْمُنَافِقُون

Al-Munaafiquwn (63)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ ﴿١﴾

1. Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: “Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Mtume wa Allaah.” Na Allaah Anajua (vyema) kuwa hakika wewe ni Mtume Wake, na Allaah Anashuhudia kuwa hakika wanafiki bila shaka ni waongo. 

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢﴾

2. Wamefanya viapo vyao (vya uongo) kuwa ni kinga (ya ‘amali zao ovu). Hivyo wakazuia (watu) Njia ya Allaah, hakika ni uovu mbaya mno waliokuwa wakitenda. 

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ ﴿٣﴾

3. Hiyo ni kwa kuwa wao waliamini, kisha wakakufuru, basi ikapigwa muhuri juu ya nyoyo zao kwa hiyo hawafahamu. 

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۖأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٤﴾

4. Na unapowaona, inakupendezesha miili yao, na wanaposema, unasikiliza kauli yao, kama kwamba magogo yaliyoegemezwa; wanadhania kuwa kila ukelele unaopigwa ni dhidi yao. Wao ndio maadui, basi tahadhari nao, Allaah Awaangamize! Namna gani wanavyogeuzwa? (mbali na Dini ya haki na kuelekea kwenye ukafiri). 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ ﴿٥﴾

5. Wanapoambiwa: “Njooni (ili) Mtume wa Allaah akuombeeni maghfirah.” Hupindisha vichwa vyao, na utawaona wanakwepa nao ni wenye kutakabari. 

سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿٦﴾

6. Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allaah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allaah Haongoi watu mafasiki. 

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗوَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ ﴿٧﴾

7. Wao ndio wale wasemao: “Msitoe (mali) kwa ajii ya walioko kwa Mtume wa Allaah mpaka watoweke.” Na ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu. 

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٨﴾

8. Wanasema: “Tutakaporudi Madiynah, mwenye utukufu (yaani ‘Abdullaah bin Ubayy bin Saluwl kichwa cha wanafiki) atamfukuza humo aliye dhalili (yaani Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)” Na hali utukufu ni wa Allaah na wa Mtume Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawaelewi. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩﴾

9. Enyi mlioamini! Yasikushughulisheni mali zenu na wala watoto wenu naDhikr ya Allaah (kumtaja na kumkumbuka). Na yeyote (yule) atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika. 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠﴾

10. Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: “Mola wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, basi ningenitoa swadaqah na ningelikuwa miongoni mwa watu wema.” 

 

وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١١﴾

11. Lakini Allaah Haiakhirishi (kamwe) nafsi yeyote inapokuja ajali yake (ya kufa) na Allaah ni Khabiyr (Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa yale (yote) mnayoyatenda. 

 

سُورَةُ التَّغَابُن

At-Taghaabun (64)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

سَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾

1. Vinamsabihi Allaah (vyote) vilivyomo mbinguni na (vyote) vilivyomo ardhini, Pekee Ana ufalme na Pekee Ana Himdi (Sifa njema, Mwenye kushukuriwa daima) Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr(Muweza daima). 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni, basi miongoni mwenu (yuko) aliye kafiri na miongoni mwenu (yuko) aliye Muumini. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona yote daima). 

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na Akakutengenezeni sura, kisha Akafanya nzuri sana sura zenu, na Kwake (Pekee) ndio marejeo ya mwisho. 

يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٤﴾

4. Anajua yale (yote) yaliyomo mbinguni na ardhini, na Anayajua yale (yote) mnayofanya siri na mnayoyatangaza. Na Allaah ni ‘Aliym(Mjuzi daima) kwa yaliyomo vifuani. 

أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٥﴾

5. Je, haijakufikieni khabari ya wale waliokufuru kabla wakaonja matokeo ya uovu wao, na watapata adhabu iumizayo. 

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا ۚ وَّاسْتَغْنَى اللَّـهُ ۚ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٦﴾

6. Hivyo kwa kuwa ilikuwa ikiwafikia Mitume yao kwa hoja bayana wakasema: “Ah! bin Aadam ndio atuongoe?” Basi wakakufuru na wakakengeuka; na Allaah Akawa hana haja nao, na Allaah ni Ghaniyyun- Hamiyd (Mkwasi, Hahitaji lolote – Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima). 

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧﴾

7. Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Bali hapana! Naapa kwa Mola wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale (yote) mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni sahali. 

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٨﴾

8. Basi muaminini Allaah na Mtume Wake na (ifuateni) Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha, na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana). 

يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٩﴾

9. Siku Atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko. Hiyo ndio Siku ya At-Taghaabun (kupata na kukosa; kupata Pepo kwa Waumini, na kukosa Pepo na kuingia Motoni wale makafiri). Basi yeyote (yule) atakayemuamini Allaah na akatenda mema Atamfutia maovu yake na Atamuingiza mabustanini yapitayo chini yake mito (Peponi) wadumu humo milele. Hayo ni mafanikio makubwa mno. 

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٠﴾

10. Na wale waliokufuru wakakadhibisha Aayah Zetu hao ndio watu wa Motoni watadumu humo milele, na mahali pabaya mno pa kuishia. 

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١١﴾

11. Hausibu msiba wowote (ule) isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na yeyote (yule) anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoa moyo wake. Na Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi daima). 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٢﴾

12. Na mtiini Allaah na mtiini Mtume na mkikengeuka, basi hakika juu ya Mtume Wetu ni ubalighisho (wa ujumbe) bayana. 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٣﴾

13. Allaah, hapana ilaaha ila YeyeNa kwa Allaah watawakali Waumini. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu (wamo) maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria – Mwenye kurehemu). 

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾

15. Hakika mali zenu na watoto wenu ni fitnah. Na kwa Allaah kuna ujira mkubwa mno. 

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٦﴾

16. Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa (ajili ya) nafsi zenu. Na yeyote (yule) anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. 

إِن تُقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ﴿١٧﴾

17. Mkimkopesha Allaah mkopo mzuri, Atakuzidishieni maradufu, na Atakughufurieni. Na Allaah niShakuwrun-Haliym (Mwenye kupokea shukurani – Mwingi wa huruma, upole wa kuwavumilia waja daima). 

 

عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. ‘Aalimul-Ghaybi Wash-Shahaadah(Mjuzi wa ghayb na dhahiri) Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvuAsiyeshindika daima – Mwenye hikmah wa yote daima).سُورَةُ الطَّلاق

Atw-Twalaaq (65)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا ﴿١﴾

1. Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahara na si katika hedhi) zao, na hesabuni (barabara siku za) eda; na mcheni Mola wenu. Msiwatoee katika nyumba (za waume) zao, na wala wao (wenyewe) wasitoke (wakati huo wa eda ya talaka) isipokuwa wakileta faahishah (uchafu) ulio bayana. Na hiyo ndio Mipaka ya Allaah. Na yeyote (yule) atakayevuka Mipaka ya Allaah basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huenda Allaah Atatokezesha jambo jingine (mapatano) baada ya haya.    

فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا ﴿٢﴾

2. Na watakapokaribia kufikia muda wao, basi (ima) wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa (ajili ya) Allaah. Hivyo ndivyo anavyowaidhiwa (yule) anayemwamini Allaah na Siku ya Aakhirah. Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamajaalia njia (ya kutoka katika matatizo). 

وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا ﴿٣﴾

3. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote (yule) anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza Amri Yake. Allaah Amejaalia kwa kila kitu kipimo chake. 

 

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا ﴿٤﴾

4. Na wale wanawake wanaokata tamaa (wanaokoma) hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa na shaka (katika muda wao wa eda), basi eda yao ni miezi mitatu, na (hiyo pia ni eda ya) wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao. Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamjaalia wepesi katika jambo lake. 

ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا ﴿٥﴾

5. Hiyo ni Amri ya Allaah Amekuteremshieni; na yeyote (yule) anayemcha Allaah, (Allaah) Atamfutia maovu yake naAtamuadhimishia ujira. 

أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚوَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَىٰ ﴿٦﴾

6. Wawekeni (hao mliowataliki) kwenye majumbani (humo humo) mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wagharamieni (matumzi yao) mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni (watoto wenu), basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkiona uzito, basi amnyonyeshee (mtoto) mwanamke mwengine. 

لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا ﴿٧﴾

7. Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi isipokuwa kwa kile Alichoipa. Atajaalia Allaah baada ya dhiki faraji. 

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُّكْرًا ﴿٨﴾

8. Na miji mingapi imeasi Amri ya Mola wake na Mitume Yake, basi Tukaihisabia hesabu kali, na Tukaiadhibu adhabu inayochukiza. 

فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا ﴿٩﴾

9. Ikaonja maovu ya mambo yake, na ikawa matokeo ya mambo yake kuwa ni khasara. 

أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ قَدْ أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا ﴿١٠﴾

10. Allaah Amewaandalia adhabu kali, basi mcheni Allaah enyi wenye akili mlioamini! Allaah Amekwishakuteremshieni Dhikraa(Qur-aan). 

رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا ﴿١١﴾

11. Mtume anakusomeeni Aayah za Allaah zinazobainisha; ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye giza kuwaingia kwenye Nuru. Na yeyote (yule) anayemwamini Allaah na akatenda mema, (Allaah) Atamuingiza mabustanini yapitayo chini yake mito (Peponi) wadumu milele humo. Allaah Amekwishampa riziki nzuri. 

 

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا ﴿١٢﴾

12. Allaah ni Yule Aliyeumba mbingu saba na katika ardhi mfano wake (mfano wa mbingu), inateremka Amri baina yake, ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza daima), na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi (Wake).سُورَةُ التَّحْرِيم

At-Tahriym (66)

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١﴾

1. Ee Nabii! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah niGhafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria – Mwenye kurehemu). 

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni (nyinyi Waislamu Shari’ah) ya kufungua viapo vyenu, na Allaah ni Mawla(Mlinzi) wenu Naye Ndiye Al-‘Aliymul-Hakiym (Mjuzi wa yote daima – Mwenye hikmah wa yote daima). 

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٣﴾

3. Na (pale) Nabii alipotoa khabari za siri kwa mmoja wa wake zake, na (huyo mke) alipoijulisha (alipoivujisha) hiyo (siri), na Allaah Akamdhihirishia (Mtume صلى الله عليه وآله وسلم), akaijulisha baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha (huyo mkewe aliyevujisha siri) akasema: “Nani aliyekujulisha haya?” (Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم), Akasema: “Amenijulisha Al-‘Aliymul-Khabiyr (Mjuzi wa yote daima – Mjuzi kwa ukina yaliyodhahiri na yaliyofichikana).” 

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ ﴿٤﴾

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kupotoka). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mawla(Mlinzi) wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia. 

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا ﴿٥﴾

5. Huenda Mola wake, ikiwa atakutalikini, Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Muslimaat(Waislamu), Muuminaat (Waumini),Qaanitaat (watiifu), Taaibaat(wanaotubia), ‘Aabidaat (wanaofanya ‘ibaadah), Saaihaat (wanaofunga Swawm au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah), Thayyibaat (wajane, waliowahi kuolewa), na Abkaar (bikra; hawajawahi kuolewa). 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

6. Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto (ambao) mafuta (kuni) yake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٧﴾

7. Enyi mliokufuru! Msitoe nyudhuru Leo! Hakika mtalipwa yake mliyokuwa mkiyafanya. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٨﴾

8. Enyi mlioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya kwelikweli; huenda Mola wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni mabustanini yapitayo chini yake mito (Peponi). Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabii na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: “Mola wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Qadiyr(Muweza daima). 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖوَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٩﴾

9. Ee Nabii! Pambana Jihaad na makafiri na wanafiki na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni (Moto wa) Jahannam, (napo ni) mahali pabaya mno pa kuishia. 

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ ﴿١٠﴾

10. Allaah Amewapigia mfano wale waliokufuru; mke wa Nuwh na mke wa Luutw. Wote wawili walikuwa chini ya waja wawili wema miongoni mwa waja Wetu; wakawafanyia khiana, basi haikuwafaa chochote mbele ya Allaah, na ikasemwa: “Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia.” 

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾

11. Na (pia) Allaah Amewapigia mfano wale walioamini; mke wa Fir’awn, aliposema: “Mola wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Jannah na niokoe na Fir’awn na vitendo vyake na niokoe na watu madhalimu.”


وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ ﴿١٢﴾

12. Na Maryam binti wa ‘Imraan ambaye amehifadhi tupu yake, Tukampulizia humo kutoka Roho Yetu, na akasadikisha Maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa Al-Qaanitiyn (watiifu).

Report Page