Juzuu Ya 12 – Wa Maa Min Daabbatin

Juzuu Ya 12 – Wa Maa Min Daabbatin

Juzuu: 12

وَمَا مِن دَابَّةٍ

 

 

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَاۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٦﴾

6. Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah; na (Allaah) Anajua mahali pa kustakiri (pa kutulia na kukaa milele) na pa bohari (pa kuwekwa muda mdogo). Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha.وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِن بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾

 

7. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita; na ikawa ‘Arshi Yake juu ya maji; (kakuumbeni) ili Akujaribuni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Na lau ukisema: “Nyinyi mtafufuliwa baada ya mauti”; bila shaka watasema wale waliokufuru: “Hakika haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.”وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٨﴾

 

8. Na lau Tukiwaakhirishia adhabu mpaka muda uliokwishahesabiwa; bila shaka watasema: “Ni nini kinachoizuia (hiyo adhabu)? Tanabahi! Siku itakayowafikia (hiyo adhabu) haitaondoshwa kwao, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ ﴿٩﴾

 

9. Na Tunapomuonjesha binaadamu Rahmah kutoka Kwetu, kisha Tukaiondoa kwake; hakika yeye huwa ni mwenye kukata tamaa sana asiye na shukurani.وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي ۚ إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ ﴿١٠﴾

 

10. Na Tunapomuonjesha neema baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: “Maovu yemeniondokea.” Bila shaka yeye ni mwenye kufurahi sana kwa kujigamba na kujifaharisha.إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿١١﴾

 

11. Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema, hao watapata maghfirah na ujira mkubwa.فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٢﴾

12. Pengine utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa Wahyi kwako na kifua chako kitaona dhiki kwa hayo kwa sababu wanasema (kama kweli ni Mtume, basi): “Mbona hakuteremshiwa hazina au hakuja pamoja naye Malaika?” Hakika wewe ni mwonyaji tu, na Allaah juu ya kila kitu ni Wakiyl (Wakili, Mdhamini, Mtegemewa kwa yote).أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٣﴾

 

13. Je, wanasema ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasi na Allaah mkiwa ni Swaadiqiyn (wakweli).فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللَّـهِ وَأَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٤﴾

 

14. Wasipokujibuni, basi eleweni kwamba hakika (hii Qur-aan) imeteremshwa kwa elimu ya Allaah, na kwamba laa ilaaha illa Huwa  (hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye); basi je, nyinyi hamtokuwa Waislamu (wanaojisalimisha katika Uislamu)?مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ ﴿١٥﴾

 

15. Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu ‘amali zao humo, nao hawatopunjwa humo.أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٦﴾

 

16. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Na yataporomoka (zitaharibika) yale (yote) waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale (yote) waliyokuwa wakiyatenda.أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٧﴾

 

17. Je, basi yule aliyekuwa na hoja bayana (Qur-aan) kutoka kwa Mola wake, na anaisoma shahidi (Jibriyl) kutoka Kwake (je, huyu anaweza kuwa kama makafiri?); na kabla yake (kilikuwa) Kitabu cha Muwsaa kilichokuwa kiongozi na Rahmah. Hao ndio wanaoiamini (Qur-aan). Na atakayeikanusha kati ya makundi, basi Moto ndio miadi yake. Basi usiwe katika shaka nacho. Hakika hiyo ni haki kutoka kwa Mola wako, lakini watu wengi hawaamini.وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۚ أُولَـٰئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٨﴾

 

18. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Allaah. Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao, na mashahidi watasema: “Hawa ndio wale waliomzulia Mola wao!” Tanabahi! Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu.الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿١٩﴾

 

19. Wale wanaozuia (watu) Njia ya Allaah na wainatakia upogo, nao wanaikanusha Aakhirah.أُولَـٰئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ۘ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ ﴿٢٠﴾

 

20. Hao hawawezi kushinda(kukimbia adhabu ya Allaah) katika ardhi na hawana awliyaa (walinzi, wasaidizi) badala ya Allaah. Watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia na hawakuwa wakiona (haki kwa sababu ya kukengeuka kwako kwa ujeuri japokuwa walikuwa wana macho na masikio)أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢١﴾

 

21. Hao ndio wale waliokhasirika nafsi zao, na yakawapotea yale (yote) waliyokuwa wakiyazua.لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ ﴿٢٢﴾

 

22. Hapana shaka kwamba wao watakuwa wenye kukhasirika (kweli) huko Aakhirah.إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٣﴾

 

23. Hakika wale walioamini na wakatenda memo na wakanyenyekea kwa Mola wao, hao ndio watu wa Jannah, watadumu humo (Peponi) milele.مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ ۚ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚأَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٢٤﴾

 

24. Mfano wa makundi mawili (wenye mashaka waovu, na wenye furaha watu wema) ni kama (mfano wa) kipofu na kiziwi na mwenye kuona na kusikia. Je, wanakuwa sawa (wanalingana katika hali zao)? Basi je, hamkumbuki (mkazingatia)?وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٢٥﴾

 

25. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh kwa Qawm yake (akawaambia): “Hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana.”أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ أَلِيمٍ ﴿٢٦﴾

 

26. “Ya kwamba msiabudu (yeyote wala chochote) isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku inayoumiza.”فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ ﴿٢٧﴾

 

27. Wakasema wakuu (wa) wale waliokufuru katika Qawm yake: “Hatukuoni isipokuwa ni binaadamu kama sisi, na hatukuoni wanaokufuata isipokuwa wale ambao ni duni wetu, (wamekufuata) kwa fikra ya mwanzo tu; na hatukuoneni (kuwa) mna fadhila yoyote (ile) juu yetu, bali tunakudhanieni ni waongo.”قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا كَارِهُونَ ﴿٢٨﴾

28. (Nuwh) Akasema: “Enyi Qawm yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Mola wangu, na (Mola wangu) Amenipa Rahmah kutoka Kwake (ya Utume), kisha ikakufichikieni, je, tukulazimisheni kuikubali (hiyo Rahmah kutoka kwa Mola) kwayo na hali nyinyi mnaichukia?”وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۚ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ إِنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ ﴿٢٩﴾

 

29. “Na enyi Qawm yangu! Sikuombeni mali juu ya (jambo) hili. Sina ujira isipokuwa kwa Allaah. Nami sitowafukuza wale walioamini (kama mnavyotaka). Hakika wao watakutana na Mola wao, lakini nakuoneni (nyinyi) ni watu majahili.”وَيَا قَوْمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٣٠﴾

 

30. “Na enyi Qawm yangu! Nani atakayeninusuru kutokana na (mbele ya) Allaah nikiwafukuza? Je, hamkumbuki (mkazingatia)?”وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ اللَّـهُ خَيْرًا ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّي إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣١﴾

 

31. “Na wala sikuambieni kwamba mimi nina Hazina za Allaah, na wala sijui (ya) ghayb; na wala sikuambieni kwamba mimi ni Malaika, na wala siwaambii wale ambao yamewadharau macho yenu kwamba Allaah hatowapa kheri. Allaah Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zao. Hakika mimi (nikifanya hivyo) hapo bila shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu.”قَالُوا يَا نُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٣٢﴾

 

32. Wakasema: “Ee Nuwh, kwa yakini umejadiliana nasi na umekithirisha majadiliano nasi, basi tuletee (hayo) unayotutishia nayo ukiwa (kweli wewe) ni miongoni mwa wa Swaadiqiyn.” (wasemao kweli).قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ اللَّـهُ إِن شَاءَ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿٣٣﴾

 

33. (Nuwh) Akasema: “Hakika hayo Atakuleteeni Allaah Akitaka, nanyi si wenye kushinda (kuikwepa adhabu ya Allaah).”وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللَّـهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٣٤﴾

 

34. “Na wala haitokufaeni nasaha yangu nikitaka kukunasihini ikiwa Allaah Anataka kukuacheni kupotea. Yeye ndio Mola wenu, na Kwake mtarejeshwa.”أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ ﴿٣٥﴾

 

35. Je, wanasema (kuwa) ameitunga (Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ikiwa nimeitunga, basi ni juu yangu ukhalifu wangu, nami sina jukumu na ukhalifu mnaoufanya.”وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

 

36. Na akafunuliwa Wahyi Nuwh kwamba: “Hatoamini (mwengine yeyote) katika watu wako isipokuwa wale waliokwishaamini. Basi usisononeke kwa yale wanayoyafanya.”وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ ﴿٣٧﴾

37. “Na unda jahazi mbele ya Macho Yetu na Ufunuzi wa Wahyi Wetu, na wala usinisemeze kuhusu (kuwasamehe) wale waliodhulumu; hakika wao ni wenye kuzamishwa.”وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِّن قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ ۚ قَالَ إِن تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ ﴿٣٨﴾

 

38. (Nuwh) Akawa anaunda jahazi; basi kila walipompitia wakuu katika Qawm yake walimfanyia kejeli. (Nuwh) Akasema: “Ikiwa (nyinyi) mnatufanyia kejeli, basi nasi tunakufanyieni kejeli (vile vile) kama mnavyotufanyia kejeli.فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٣٩﴾

 

39. “Mtakuja kujua nani itakayemfikia adhabu itakayomhizi, na itakayemwangukia adhabu ya kudumu”.حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ ﴿٤٠﴾

 

40. Mpaka ilipokuja Amri Yetu na tanuri likafoka (maji kutoka ardhini kama chemchemu) Tukasema: “Beba humo (jahazini) jozi moja (dume na jike) katika kila (kiumbe), na ahli zako; isipokuwa yule ambaye imemtangulia kauli (ya hukmu ya kuangamizwa; na pia wachukue) na walioamaini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.”وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّـهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٤١﴾

 

41. Na (Nuwh) akasema: “Pandeni humo ‘BismiLlaah’(kwa Jina la Allaah) kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Mola wangu bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).”وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ الْكَافِرِينَ ﴿٤٢﴾

 

42. Nayo (jahazi) likawa linakwenda nao katika mawimbi (urefu wake) kama jabali. Na Nuwh akamwita mwanawe naye alikuwa kandoni: “Ee mwanangu! Panda pamoja nasi, na wala usiwe pamoja na makafiri.”قَالَ سَآوِي إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ ﴿٤٣﴾

 

43. (Mtoto wa Nuwh) Akasema: “Nitakimbilia jabali litanilinda na maji.” (Nuwh) Akasema: “Hapana wa kulindwa leo na Amri ya Allaah isipokuwa Aliyemrehemu.” Tahamaki! Mawimbi yakaingia kati baina yao, akawa miongoni mwa waliogharikishwa.وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَا سَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾

 

44. Na (baada ya kugharikishwa waovu) pakasemwa: “Ee ardhi! Meza maji yako na ee mbingu, zuia (mvua),” na maji yakadidimia (chini); na amri ikakidhiwa; na (jahazi) likatua juu ya (mlima wa) Al-Juwdiyy. Na pakasemwa: “Wametokomelea mbali watu madhalimu.”وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na Nuwh akamwita (kumwomba) Mola wake, akasema: “Mola wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu, na hakika Ahadi Yako ni haki, Nawe ni Ahkamul-Haakimiyn (Mbora zaidi wa Kuhukumu kuliko mahakimu wote).”قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٤٦﴾

46. Pakasemwa: “Ee Nuwh! Hakika huyo si miongoni mwa ahli zako. Hakika yeye ni (mwenye) ‘amali zisizokuwa njema. Basi usiniulize (usiniombe) yale usiyokuwa na elimu nayo. Hakika Mimi nakuwaidhi usijekuwa miongoni mwa majahili.”قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٤٧﴾

 

47. (Nuwh) Akasema: “Ee Mola wangu! Hakika mimi najikinga Kwako kukuuliza (kukuomba) yale nisiyo na elimu nayo. Na Usiponighufuria na Ukanirehemu, nitakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٤٨﴾

 

48. Pakasemwa: “Ee Nuwh! Teremka (jahazini) kwa Amani kutoka Kwetu na Baraka nyingi juu yako, na juu za umati zilio pamoja na wewe. Na (zitakuweko) umati Tutakazozistarehesha, kisha itawagusa kutoka Kwetu adhabu iumizayo.”تِلْكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَا أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٤٩﴾

 

49. Hizo ni katika habari za ghayb Tunakufunuliwa Wahyi kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hukuwa unazielewa wewe na wala watu wako kabla ya hii (Qur-aan). Basi subiri, hakika mwisho (mwema) ni kwa Muttaqiyn (wenye taqwa).وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ ﴿٥٠﴾

 

50. Na kwa kina ‘Aad (Tulimpeleka) ndugu yao Huwd. Akasema: “Ee Qawm yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ghairi Yake. Nyinyi si chochote isipokuwa wazushi.”يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٥١﴾

 

51. “Enyi Qawm yangu! Sikuombeni ujira juu ya huu (ujumbe). Haukuwa ujira wangu isipokuwa kwa Yule Aliyeniumba. Je, basi hamtii akilini?”وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ ﴿٥٢﴾

 

52. “Na enyi Qawm yangu! Mwombeni maghfirah Mola wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni (kutoka) mbinguni mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wakhalifu.”قَالُوا يَا هُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿٥٣﴾

53. (Watu wake) Wakasema: “Ee Huwd! Hukutuletea hoja bayana, nasi hatutoacha miungu yetu kwa (kuamini na kufuata) kauli yako, nasi hatutokuwa wenye kukuamini.إِن نَّقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ ۗ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ اللَّـهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٥٤﴾

 

54. “Hatusemi ila kuwa baadhi ya miungu yetu imekusibu kwa uovu.” (Huwd) Akasema: “Hakika mimi namshuhudisha Allaah, na shuhudieni kwamba mimi sina dhima na mnaowashirikisha.مِن دُونِهِ ۖ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ ﴿٥٥﴾

 

55. “Pasi Naye, basi nifanyieni njama nyote (ya kunidhuru au kuniua), kisha msinipe muhula (wa kungojea).إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّـهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٦﴾

 

56. “Hakika mimi nimetawakali kwa Allaah, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Anamkamata kwa kipaji chake (Anamsarifu Atakavyo). Hakika Mola wangu Yuko juu ya Swiraatwil-Mustaqiym (njia iliyonyooka).فَإِن تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ ﴿٥٧﴾

 

57. “Mkikengeuka basi nimekwishakubalighishieni (ujumbe) niliyotumwa nao kwenu. Na Mola wangu Atawafanya makhalifa watu wengineo wasiokuwa nyinyi, na wala hamtaweza kumdhuru chochote. Hakika Mola wangu juu ya kila kitu ni Hafiydhw(Mwenye Kuhifadhi, Kulinda daima).” 

وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَنَجَّيْنَاهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٥٨﴾

 

58. Na ilipokuja Amri Yetu (ya kuangamizwa), Tulimuokoa Huwd na wale walioamini pamoja naye kwa Rahmah kutoka Kwetu, na Tukawaokoa kutokana na adhabu (ngumu).وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ ﴿٥٩﴾

 

59. Na hao ni kina ‘Aad. Wamezikanusha kwa ushupavu Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza) za Mola wao, na wakawaasi Mitume Wake, na wakaufata amri ya kila jabari mkaidi.وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ ﴿٦٠﴾

 

60. Na wakafuatishwa na laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hakika kina ‘Aad walimkufuru Mola wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina ‘Aad; Qawm ya Huwd.وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖهُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ ﴿٦١﴾

 

61. Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: “Ee Qawm yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni (Amekuumbeni) katika ardhi, na Akakufanyieni makazi humo; basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Mola wangu ni Qariybum-Mujiyb (Yu Karibu daima kwa Elimu Yake – Mwenye Kuitikia daima).”قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ ﴿٦٢﴾

62. (Watu wake) Wakasema: “Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa miongoni mwetu (mwenye) kutarajiwa (kuwa na kheri) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaowaabudu baba zetu; na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia.”قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ ﴿٦٣﴾

63. (Swaalih) Akasema: “Enyi Qawm yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Mola wangu, na (Mola wangu) Amenipa Rahmah kutoka Kwake (ya Utume); basi nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ ﴿٦٤﴾

 

64. “Enyi Qawm yangu! Huyu ni ngamia jike wa Allaah, ni Aayah (ishara, dalili, muujiza) kwenu (kama mlivyotaka), basi mwacheni ale katika ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu (wowote; kwani mkimgusa kwa uovu) itakuchukueni adhabu iliyo karibu.”فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ ﴿٦٥﴾

 

65. Basi wakamkata ukano wa mvungu wa goti (wakamchinja ngamia); (Swaalih) akasema: “Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.”فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ ﴿٦٦﴾

 

66. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa Rahmah kutoka Kwetu, na (Tuliwaokoa pia) kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Mola wako Yeye Ndiye Al Qawiyyul-‘Aziyz(Mwenye Nguvu daima – Mwenye Nguvu – Mshindi Asiyeshindika daima).وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٦٧﴾

 

67. Na wale waliodhulumu iliwateka swayhah (ukelele wa mshindo kutoka mbinguni unaoangamiza), wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ ﴿٦٨﴾

 

68. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Mola wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd.وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ ﴿٦٩﴾

 

69. Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu (Malaika) kwa bishara, wakasema: “Salaam (Amani! – Ibraahiym naye akaitikia kwa) kusema: “Salaam”. Basi hakubakia (haukupita muda) ila alikuja na ndama aliyebanikwa.فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ ﴿٧٠﴾

 

70. Alipoona mikono yao haifikii (chakula) aliwashangaa na ikamuuingia dhana moyoni kutokana na khofu nao kutokana nao. Wakasema: “Usiogope! Hakika Sisi Tumetumwa kwa watu wa Luwtw” (Tukawaangamize).وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ ﴿٧١﴾

71. Na mkewe amesimama wima, akacheka; Tukambashiria (huyo mkewe kuwa atazaa mtoto amwite) Is-haaq na baada ya Is-haaq (watapata mjukuu wamwite) Ya’quwb.قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ ﴿٧٢﴾

 

72. (Mkewe) Akasema (kwa mshangao): “Ole wangu! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!”قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ ۖ رَحْمَتُ اللَّـهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ ۚ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ ﴿٧٣﴾

 

73. (Malaika) Wakasema: “Je, unastaajabia Amri ya Allaah? Rahmah ya Allaah na Baraka Zake ziko juu yenu enyi Ahlul-Bayt(watu wa nyumba). Hakika Yeye ni Hamiydun-Majiyd.” (Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa, Msifiwa, Mwenye Kushukuriwa kwa yote daima – Mtukufu, Mwingi mno wa vipawa, Fadhila na Ukarimu)فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَىٰ يُجَادِلُنَا فِي قَوْمِ لُوطٍ ﴿٧٤﴾

 

74. Basi kiwewe cha tisho la moyo kilipomuondoka Ibraahiym, na ikamjia bishara; (akaanza) kujadiliana Nasi kuhusu Qawm ya Luwtw.إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُّنِيبٌ ﴿٧٥﴾

 

75. Hakika Ibraahiym bila shaka ni mpole (na mvumilivu), Awwaah; (mwenye huruma, unyenyekevu), mwenye kurejea kutubia kila mara kwa Allaah.يَا إِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۖ إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ ﴿٧٦﴾

 

76. (Malaika wakamwambia): “Ee Ibraahiym! Achilia mbali haya! Hakika imekwishakuja Amri ya Mola wako (ya kuangamizwa hawo watu wa Luwtw), na kwamba wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.”وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ ﴿٧٧﴾

 

77. Na wajumbe (Malaika) Wetu walipomjia Luwtw alisononeka kwa ajili yao (kudhania kwamba watu wake watawakurubia kutaka kufanya uliwati nao) na akadhikika na kushindwa (la kufanya); akasema: “Hii ni siku ngumu.”وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ ﴿٧٨﴾

 

78. Wakamjia watu wake wakimkimbilia na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luwtw) Akasema: “Enyi Qawm yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (mkiwaoa kihalali). Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu aliyeongoka?قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ ﴿٧٩﴾

 

79. Wakasema: “Kwa yakini umekwishaelewa kwamba hatuna haki katika mabinti zako, na kwamba hakika wewe unaelewa tunalolitaka.”قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ ﴿٨٠﴾

 

80. (Luwtw) Akasema: Lau ningelikuwa nina nguvu dhidi yenu, au nikimbilie katika nguzo madhubuti.”قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ ﴿٨١﴾

81. (Malaika) Wakasema: “Ee Luutw! Hakika sisi ni Wajumbe wa Mola wako; (hivyo usiwe na wasiwasi hawawezi kutufanya chochote; na hawa) hawatoweza kukufika (kwa baya lolote). Basi toka usiku na ahli zako katika pande la (nyakati ya) usiku, na wala asitazame nyuma yeyote miongoni mwenu, isipokuwa mke wako; kwani yeye itamsibu yatakayowasibu wao; hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu?فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ ﴿٨٢﴾

 

82. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tuliupindua (mji wao huo) juu chini, na Tukaunyeshea (mvua ya) mawe ya udongo (wa Motoni) yaliookwa yaliyo na tabaka na kuandamana.مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ ﴿٨٣﴾

 

83. Yametiwa alama (mawe hayo) kutoka kwa Mola wako (kila moja na jina la mtu wake). Na adhabu hiyo haiko mbali na madhalimu.وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖوَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ ﴿٨٤﴾

 

84. Na kwa (watu wa) Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb.  Akasema: “Enyi Qawm yangu! Mwabuduni Allaah (kwani nyinyi) hamna ilaah (mungu apasaye kuabudiwa kwa haki) ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani; hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu siku ya kuzunguka (watu).وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٨٥﴾

 

85. “Na Enyi Qawm yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi.بَقِيَّتُ اللَّـهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿٨٦﴾

 

86. “Mabaki (ya halali) ya Allaah ni bora kwenu, mkiwa ni wenye kuamini. Nami si mlinzi kwenu.”قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ ﴿٨٧﴾

 

87. Wakasema: “Ee Shu’ayb! Je, Swalaah zako (ndio) zinakuamrisha kuwa sisi tuache wale wanaowaabudu baba zetu, au (tuache) kufanya tunavyotaka katika mali zetu? Hakika wewe bila shaka ni mtu mpole na muongofu.” (Wakamsifu kwa istihizai na kejeli).قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚوَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ ﴿٨٨﴾

88. (Shu’ayb) Akasema: Enyi Qawm yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Mola wangu (ya Utume), na Amenirukuzuku humo riziki njema. Nami sitaki kukukhalifuni (kwa) kufanya ninayokukatazeni. Sitaki lolote ila kutengeneza niwezavyo. Na sipati tawfiyq (ya kuyawezesha haya) ila kwa Allaah. Kwake natawakali na Kwake narejea.”وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم بِبَعِيدٍ ﴿٨٩﴾

 

89. “Enyi Qawm yangu! Kupingana nami (kwa uadui na kufarikiana) kusikupelekeni (kufikia) kusibiwa (na) yale yaliyowasibu Qawm ya Nuwh au Qawm ya Huwd, au Qawm ya Swaalih. Na Qawm ya Luwtw hawako mbali nanyi.”وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ ﴿٩٠﴾

 

90. “Na ombeni maghfirah kwa Mola wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Mola wangu ni Rahiymuw-Waduwd (Mwenye Kurehemu – Mwenye mapenzi khalisi).”قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ ﴿٩١﴾

 

91. Wakasema: “Ee Shu’ayb! Hatufahamu mengi unayoyasema, na hakika sisi tunakuona ni dhaifu kati yetu. Na lau si familia yako tungelikupiga mawe (ufe). Nawe si mwenye utukufu (au nguvu) kwetu.قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿٩٢﴾

 

92. (Shu’ayb) Akasema: “Enyi Qawm yangu! Je, familia yangu kwenu ina utukufu zaidi kwenu kuliko Allaah, na mmemuweka nyuma ya migongo yenu? Hakika Mola wangu kwa yale (yote) myatendayo ni Muhiytw(Mwenye kuyazunguka kwa Ujuzi Wake).”وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖ وَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ ﴿٩٣﴾

93. “Na enyi Qawm yangu! Tendeni (‘amali) kwa tamkini yenu (mtakavyo) nami pia natenda (‘amali zangu kwa tamkini yangu). Mtakuja kujua nani itamfika adhabu itakayomhizi, na ni nani yeye muongo. Na ngojeeni mchunge. Hakika mimi niko pamoja nanyi nikingojea na kuchunga.”وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩٤﴾

 

94. Na ilipokuja Amri Yetu; Tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa Rahmah kutoka Kwetu. Na ukawachukuwa wale waliodhulumu Swayhah (ukelele wa mishindo kutoka mbinguni unaoangamiza), wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ ﴿٩٥﴾

 

95. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali (watu wa) Madyan kama walivyotokomea Thamuwd.وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٩٦﴾

 

96. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayah Zetu; (Wahyi, ishara, miujiza) na dalili bayana.إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ ﴿٩٧﴾

97. Kwa Fir’awn na wakuu wake, (lakini wao) walifuata amri ya Fir’awn. Na amri ya Fira’wn haikuwa yenye uongofu.يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ ﴿٩٨﴾

98. (Fira’wn) Atawatangulia watu wake Siku ya Qiyaamah, na atawaingiza Motoni. Na ubaya ulioje (mahali pa) muingio wa maingizo.وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ ﴿٩٩﴾

99. Na wamefuatishwa na laana katika (dunia) hii na Siku ya Qiyaamah (pia). Uovu ulioje zawadi ya kutunukiwa. (Laana ya dunia na kufuatiliwa na ya Aakhirah). ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ ﴿١٠٠﴾

 

100. Hizo ni baadhi ya habari za vijiji (miji), Tunakusimulia kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); miongoni mwayo ingalipo bado, na (mengineyo) imefekwa.وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ ﴿١٠١﴾

 

101. Na hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu nafsi zao wenyewe. Basi hawakuwafaa kitu chochote miungu yao waliyokuwa wakiyaomba badala ya Allaah ilipokuja Amri ya Mola wako. Na wala hawakuwazidishia (lolote) isipokuwa mateketezo.وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ ﴿١٠٢﴾

 

102. Na hivyo ndivyo kuchukua (kuangamiza) kwa Mola wako kunavyokuwa Anapochukua vijiji (watu wa miji) inapodhulumu. Hakika Uchukuaji Wake ni uumizao vikali.إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ ﴿١٠٣﴾

 

103. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ ﴿١٠٤﴾

 

104. Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda unaohesabiwa (Umeshapangwa na Allaah).يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ ﴿١٠٥﴾

 

105. Siku (hiyo) itakapofika; haitosema nafsi (kiumbe) yeyote isipokuwa kwa Idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao ni shaqiyyu (wenye mashaka waovu) na (wengine ni) sa’iyd (wenye furaha watu wema).فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ ﴿١٠٦﴾

 

106. Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa Motoni, watapata humo kuvuta pumzi na kutoa pumzi (kwa mngurumo kutokana na mateso ya kupapatika na adhabu ya Moto).خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٠٧﴾

 

107. Watadumu humo milele (sawa na) muda wa kudumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Mola wako. Hakika Mola wako Anafanya Atakavyo.وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ ﴿١٠٨﴾

108. Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, watadumu humo (Peponi) milele (sawa na) muda wa kudumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Mola wako. Ni zawadi isiyokatizwa (neema ya kuendelea moja kwa moja).فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰؤُلَاءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ ﴿١٠٩﴾

 

109. Basi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usiwe katika shaka kutokana na wanayoyaabudu hao (washirikina). Hawaabudu ila kama walivyoabudu baba zao kabla. Na bila shaka Tutawalipa kikamilifu fungu(sehemu ya adhabu) yao bila ya kupunguzwa.وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ ﴿١١٠﴾

 

110. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu (Tawraat), zikatiwa ikhtilaafu ndani yake. Na lau si neno lilotangulia kutoka kwa Mola wako, (la hukumu ya kutokuwaadhibu sasa) bila shaka ingelikidhiwa baina yao. Na hakika wao wako katika shaka juu yake (hii Qur-aan) inayowatia wasiwasi.وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١١١﴾

 


https://t.me/Furqanbot



Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈





Report Page