Juzuu

Juzuu


وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١١١﴾

 

111. Na hakika wote (kila mmoja kati ya Waumini na makafiri) bila shaka atawalipa Mola wako ‘amali zao kikamilifu. Hakika Yeye ni kwa wayatendyo ni Khabiyr (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٢﴾

 

112. Basi nyooka (thibitika imara katika Uislamu ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama ulivyoamrishwa na aliyetubia pamoja nawewe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye kwa myatendyo ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima).

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ﴿١١٣﴾

 

113. Na wala msielemee kwa wale waliodhulumu ukakuguseni Moto, na hamtokuwa na awliyaa (walinzi, wasaidizi) badala ya Allaah, kisha hamtonusuriwa.

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ ﴿١١٤﴾

 

114. Na simamisha Swalaah (katika) ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu (madhambi madogodogo). Hivyo ni dhikraa (ukumbusho, mawaidha na naswaaha) kwa wanaokumbuka.

وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٥﴾

 

115. Na subiri (vumilia) kwani hakika Allaah Hapotezi ujira wa Muhsiniyn (watendao wema).

فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ ﴿١١٦﴾

 

116. Basi kwanini hawakuweko katika watu wa karne za kabla yenu, watu wenye akili (wasaa na uwezo wa kuathiri) wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu wakafuata (anasa) walizostareheshwa nazo na wakawa wakhalifu.

وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ ﴿١١٧﴾

 

117. Na Mola wako Hakuwa Mwenye kuhilikii miji kwa dhulma na hali watu wake ni Muswlihuwn (wema).

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ ﴿١١٨﴾

 

118. Na lau Angetaka Mola wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja (wa Dini ya Kiislamu). Na hawatoacha kukhitilafiana.

إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١١٩﴾

 

119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Mola wako. Na kwa hivyo ndivyo (Mola wako) Amewaumba. Na limetimia Neno la Mola wako (kwamba): “Bila shaka Nitajaza (Moto wa) Jahannam kwa majini na watu pamoja.”

وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٠﴾

 

120. Na kila (kisa) Tunachokusimulia katika khabari za Mitume ni ambazo Tunakuthibitisha kwazo moyo wako. Na imekujia katika hii haki na mawaidha na dhikraa (utajo, ukumbusho) kwa Waumini.

وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ ﴿١٢١﴾

 

121. Na waambie wale wasioamini: “Tendeni (mtendayo na mtakavyo) kwa tamkini yenu, nasi pia tunatenda (‘amali zetu kwa tamkini zetu).

وَانتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٢٢﴾

 

122. Na ngojeeni, nasi (pia) tunangojea.”

وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٢٣﴾

 

123. Na ni ya Allaah (Pekee) ghayb (siri) ya mbingu na ardhi, na Kwake (Pekee) inarejeshwa amri yote; basi mwabudu (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na tawakali Kwake. Na Mola wako si Mwenye kughafilika na yale myatendayo.

سُورَة يُوسُفْ

Yusuf: 12

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

 

1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayah za Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢﴾

 

2. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan kwa (lugha ya) Kiarabu ili mpate kutia akilini (muifahamu vyema).

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

 

3. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usimulizi mzuri kabisa wa visa kwa kukufunulia Wahyi hii Qur-aan. Na hakika kabla ya (kufunuliwa kwako Qur-aan) ulikuwa miongoni mwa walioghafilika.

إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾

4. (Katika hivyo visa; Tunakusimulia kisa cha Yuwsuf) Pale Yuwsuf alipomwambia baba yake: “Ee baba yangu (Ya’quwb)! Hakika mimi nimeona (katika ndoto) nyota kumi na moja na jua na mwezi; nimeziona zikinisujudia.”

قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٥﴾

 

5. (Ya’quwb) Akasema: “Ee mwanangu! Usisimulie ndoto yako (hii) kwa kaka zako watakupangia njama. Hakika shaytwaan kwa binaadamu ni adui bayana.”

وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٦﴾

 

6. Na hivyo ndivyo Atakuteua Mola wako na Atakufunza tafsiri ya ndoto (uhakikisho wa matokeo) na Atakutimizia Neema Yake juu yako, na juu ya kizazi cha Ya’quwb, kama Alivyoitimiza kabla juu ya baba zako; Ibraahiym na Is-haaq. Hakika Mola wako ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).

لَّقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ ﴿٧﴾

 

7. Kwa yakini imekuwa katika (kisa cha) Yuwsuf na kaka zake Aayah (Ishara, mazingatio, mafunzo, maonyo n.k) kwa waulizao.

إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨﴾

 

8. (Kumbuka pale kaka zake) Waliposema: “Bila shaka Yuwsuf na ndugu yake (wa baba na mama mmoja) ni vipenzi zaidi kwa baba yetu kuliko sisi, na hali sisi (wa mama wengine) ni kundi lenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu bayana.”

اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ ﴿٩﴾

 

9. “Muueni Yuwsuf, au mtupilieni mbali katika nchi ya mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi (kwani atakuwa hayuko tena), na muwe baada ya hapo Swaalihiyn (wema).”

قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿١٠﴾

 

10. (Akasema msemaji miongoni wao): “Msimuue Yuwsuf, (lakini) mtupeni katika kisima kirefu watamwokota baadhi ya misafara, ikiwa nyinyi (mna ulazima kuwa) mfanye (hivyo; kumtenganisha na baba yake).”

قَالُوا يَا أَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَنَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُ لَنَاصِحُونَ ﴿١١﴾

 

11. (Baada ya kuwafikiana namna ya kumbaidisha Yuwsuf, walikwenda kwa baba yao na kumwambia): “Ee baba yetu! Una nini, hutuamini juu ya Yuwsuf, na hakika sisi ni wenye kumnasihi kidhati?”

أَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿١٢﴾

 

12. “Mpeleke pamoja nasi kesho, ale atakacho na acheze na sisi tutamhifadhi.” 

قَالَ إِنِّي لَيَحْزُنُنِي أَن تَذْهَبُوا بِهِ وَأَخَافُ أَن يَأْكُلَهُ الذِّئْبُ وَأَنتُمْ عَنْهُ غَافِلُونَ ﴿١٣﴾

 

13. (Ya’quwb) Akasema: “Hakika mimi bila shaka inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na nakhofu (kuja) kuliwa na mbwa mwitu; nanyi muwe mmeghafilika naye.”

قَالُوا لَئِنْ أَكَلَهُ الذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّا إِذًا لَّخَاسِرُونَ ﴿١٤﴾

 

14. Wakasema: “Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kundi lenye nguvu (la kumlinda); hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa wenye kukhasirika.”

فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَـٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٥﴾

 

15. Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana wamtie katika kisima kirefu. Tukamfunulia Wahyi (Tukamtia ilhamu Yuwsuf) kwamba bila shaka (iko siku) utakuja kuwajulisha jambo lao hili; na (hali) wao hawahisi.

وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَبْكُونَ ﴿١٦﴾

 

16. Wakaja kwa baba yao usiku wakilia.

قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖوَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ ﴿١٧﴾

 

17. Wakasema: “Ee baba yetu! Hakika sisi tulikwenda (tukawa) tunashindana mbio na tulimwacha Yuwsuf kwenye vitu vyetu; basi (akatokea) mbwa mwitu akamla. Nawe hutotuamini japo tukiwa ni Swaadiqiyn (wakweli).

وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّـهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ ﴿١٨﴾

 

18. Na walikuja (huku wameweka) juu ya kanzu (shati) yake damu ya uongo. (Ya’quwb) Akasema: “Bali imekushawishini nafsi zenu jambo (kumfanyia ndugu yenu). Basi subira njema, na Allaah (Pekee Ndiye) Aombwaye msaada juu ya (hayo) mnayoelezea.”

وَجَاءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُ ۖ قَالَ يَا بُشْرَىٰ هَـٰذَا غُلَامٌ ۚوَأَسَرُّوهُ بِضَاعَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾

 

19. Ukaja msafara (karibu na kisimani) wakamtuma mtekaji maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. (Alipovuta ndoo juu alimuona mtoto) akasema: “Ee bishara njema! Huyu kijana mvulana!” na (mtekaji maji na wenziwe) wakamficha (kwa wasafiri wingine, wakadai kuwa kijana huyo) ni (miongoni mwa) bidhaa (zao walizozinunua). Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa yale wanayoyatenda.

وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ الزَّاهِدِينَ ﴿٢٠﴾

 

20. Wakamuuza kwa thamani pungufu (kidogo tu) ya dirham za kuhesabika; na walikuwa ni wenye kuridhika na kidogo. (Kwani hawakuwa na haja naye).

وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِن مِّصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّـهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢١﴾

 

21. Na yule aliyemnunua huko Misri alimwamrisha mke wake (kwa kusema): “Mkirimu makazi yake, huenda akatufaa au tukamfanya mtoto.” Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi (nchi ya Misri) na ili Tumfunze tafsiri za maneno (tafsiri za ndoto na matukio). Na Allaah ni Mwenye Kushinda juu ya jambo Lake, lakini watu wengi hawajui.

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٢﴾

 

22. Na (Yuwsuf) alipobaleghe kufikia umri wa kupevuka, Tulimpa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa Muhsinyin (watendao wema).   

وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚقَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٣﴾

 

23. Na (yule mwanamke) ambaye (Yuwsuf) alikuwa katika nyumba yake akamtongoza kinyume na nafsi yake (Yuwsuf); na akafunga milango, na akasema: “Haya njoo!” (Yuwsuf) Akasema: “Najikinga kwa Allaah! Hakika yeye bwana wangu amenifanyia makazi mazuri, (basi sitomdhulumu). Hakika madhalimu hawafaulu.”

وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ ﴿٢٤﴾

 

24. Na kwa yakini (mwanamke yule) aliingiwa hima naye (kumtamani Yuwsuf) na (Yuwsuf) angeliingiwa na hima (ya kumtamani) kama asingeliona buruhani kutoka kwa Mola wake. Hivyo ndivyo Tunavyomwepusha na uovu na machafu. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Mukhlaswiyn(waliotakaswa, waliochaguliwa).

وَاسْتَبَقَا الْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَى الْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَاءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوءًا إِلَّا أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٥﴾

 

25. Wakakimbilia mlangoni wote wawili na (yule mwanamke) akalirarua kanzu (la Yuwsuf) yake kwa nyuma, na wakamkuta bwana wake (mume wake) mlangoni. (Mwanamke wa ‘Aziyz) Akasema: “Hakuna jazaa ya anayemtakia uovu ahli (mke) wako isipokuwa kufungwa jela au (apewe) adhabu iumizayo.”

قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَن نَّفْسِي ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَا إِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٢٦﴾

 

26. (Yuwsuf) Akasema: “Yeye ndiye aliyenitaka kinyume na nafsi yangu.” Na akashuhudia shahidi miongoni mwa ahli zake (mwanamke kwa kusema): “Ikiwa kanzuyake imechanwa mbele, basi mwanamke (atakuwa) amesema kweli; naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa waongo.

وَإِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٢٧﴾

 

27. Na ikiwa kanzuimechanwa nyuma, basi mwanamke (atakuwa) amesema uongo; naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa Swaadiqiyn (wakweli).”

فَلَمَّا رَأَىٰ قَمِيصَهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ ﴿٢٨﴾

 

28. Basi (yule mume) alipoona kanzuyake imechanwa nyuma; alisema: “Hakika hii ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu wanawake ni adhimu.”

يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۚ وَاسْتَغْفِرِي لِذَنبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ الْخَاطِئِينَ ﴿٢٩﴾

 

29. “Yuwsuf yaachilie mbali haya. Na (wewe mwanamke) omba maghfirah kwa dhambi lako. Hakika wewe ulikuwa miongoni mwa wakosao.” 

وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن نَّفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾

 

30. Na wanawake katika mji ule (wakapata habari ya yaliyojiri, wakawa) wakisema: “mke wa ‘Aziyz anamtaka kijana (mtumishi) wake kinyume na nafsi yake.” Kwa yakini amemuathiri kwa mapenzi (kaelemewa na mapenzi ya Yuwsuf). Hakika sisi tunamuona (mke wa ‘Aziyz) yumo katika upotofu dhahiri.”

فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ ﴿٣١﴾

 

31. Basi (mke wa ’Aziyz) aliposikia vitimbi vyao, aliwapelekea mwaliko (kuwaalika kwake) na akawaandalia karamu na akampa kila mmoja wao kisu (wamenye au wakate vya kukatwa au kumenywa). Kisha (mke wa ‘Aziyz) akasema (kumwambia Yuwsuf): “Tokeza mbele yao.” Basi walipomuona walimtukuza (kwa kushangazwa na uzuri wake), na wakajikatakata mikono yao (bila ya kujitambua kwa kushughulishwa na uzuri wake), na wakasema: “Haasha liLlaah! Huyu si binaadamu! Huyu si yeyote ila ni Malaika mtukufu.”

قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ ﴿٣٢﴾

 

32. (Mke wa ‘Aziyz) akasema: “Basi huyo ndiye (kijana) mliyekuwa mkinilaumia. Na hakika nilimtamani kinyume na nafsi yake, akajilinda. Na kama hatofanya ninalomuamrisha, basi bila shaka atafungwa jela, na bila shaka atakuwa miongoni mwa waliodunishwa (dhalili).”

قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٣﴾

 

33. (Yuwsuf) Akasema (akaomba du’aa): “Ee Mola wangu! Nastahabu zaidi (kufungwa) jela kwangu kuliko yale wanayoniitia. Na Usiponiepusha na vitimbi vyao (hawa wanawake), nitaelemea kwao na nitakuwa miongoni mwa majahili.”

فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٤﴾

 

34. Basi Mola wake Akamuitikia (du’aa yake); Akamuepusha na vitimbi vyao. Hakika Yeye ni As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّى حِينٍ ﴿٣٥﴾

 

35. Kisha ikawadhihirikia (kwa yule ‘Aziyz na watu wake) baada ya kuona Aayah nyingi (Ishara, dalili, alama za usafi wa Nabii Yuwsuf, wakashauriana kuwa la kufanya ni bora kumwondolea fedheha yule mke wa ‘Aziyz) kuwa wamfunge jela kwa muda kidogo.

وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ خَمْرًا ۖ وَقَالَ الْآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْمِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ ۖإِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٦﴾

 

36. Wakaingia pamoja naye jela vijana wawili. Mmoja wao (hao vijana wawili) akasema: “Hakika mimi nimejiona (ndotoni) kuwa nakamua ulevi.” Na mwengine akasema: “Hakika mimi nimejiona (ndotoni) nabeba juu ya kichwa changu mikate wanaila ndege humo.” (Wakasema) “Tujulishe tafsiri yake (maana yake hakika) Hakika sisi tunakuona (wewe) ni miongoni mwa Muhsiniyn (watendao wema).

قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿٣٧﴾

37. (Yuwsuf) Akasema: “Hakitakufikieni chakula chochote mtakachoruzukiwa isipokuwa nitakujulisheni tafsiri yake kabla havijakufikieni. Haya ni katika Aliyonifunza Mola wangu. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomwamini Allaah nao kwa Aakhirah ni wanakanushaji.

وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ عَلَيْنَا وَعَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٣٨﴾

 

38. “Na nimefuata mila ya baba zangu; Ibraahiym, na Is-haaq na Ya’quwb. Haikutupasa(hakiwala elimu yoyote ile) ya kumshirikisha Allaah na kitu chochote. Hiyo ni katika Fadhila za Allaah juu yetu na juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.”

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٣٩﴾

 

39. “Enyi masahibu wangu wawili wa jela (wafungwa wenzangu). Je, waungu wengi wanaofarikiana ni bora (kuabudiwa) au Allaah (ambaye ni) Al-Waahidul-Qahhaar (Mmoja, Pekee – Mwenye Kuteza, Mwenye Nguvu na Kudhibiti, Mshindi, Asiyepingika).” 

مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٠﴾

 

40. “Hamuabudu pasi Naye (Allaah) isipokuwa majina (ya masanamu) mmeyaita nyinyi na baba zenu, Hakuyateremshia Allaah kwayo mamlaka (amri) yoyote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msimwabudu (yeyote au chochote) isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawaelewi.”

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚ قُضِيَ الْأَمْرُ الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ ﴿٤١﴾

 

41. “Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake ulevi. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watakula kutoka kichwani mwake. Imeshahukumiwa jambo ambalo mkiliulizia.”

وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ ﴿٤٢﴾

 

42. (Na Yuwsuf) Akasema (kumwambia) yule aliyejua kuwa ataokoka miongoni mwa wale wawili: “Nikimbuke mbele ya bwana wako.” Lakini shaytwaan akamsahaulisha kumkumbuka kwa bwana wake (au shaytwaan alimsahaulisha Yuwsuf kumkumbuka Mola wake na kumtaka msaada Yeye badala ya wengine kama mfalme). Basi (Yuwsuf) akabakia jela miaka kadhaa. ‏

وَقَالَ الْمَلِكُ إِنِّي أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na (siku moja) mfalme akasema: “Hakika mimi naona (ndotoni) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na (pia nimeona ndotoni) mashuke saba ya kijani (mabichi) na mengineyo (saba) yabisi (makavu). Enyi wakuu (washauri wangu)! Nifutuni (nielezeni tafsiri) katika ndoto yangu, mkiwa ni wenye kuagua ndoto.”

قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ الْأَحْلَامِ بِعَالِمِينَ ﴿٤٤﴾

 

44. (Wakuu) Wakasema: “Ndoto za mparaganyiko (hizo); nasi si wenye kuelewa kufasiri (kuagua maana halisi) ya ndoto (hizi).”

وَقَالَ الَّذِي نَجَا مِنْهُمَا وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِ فَأَرْسِلُونِ ﴿٤٥﴾

 

45. (Hapo ndipo) Aliposema yule aliyeokoka kati ya wale (masahibu wawili wa Yuwsuf wa jela), na akakumbuka baada ya muda (maagizo ya Yuwsuf): “Mimi nitakujulisheni kuhusu tafsiri yake. Basi, nitumeni. (nIende kukutafutieni tafsiri yake).”

يُوسُفُ أَيُّهَا الصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِي سَبْعِ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ لَّعَلِّي أَرْجِعُ إِلَى النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٤٦﴾

 

46. (Akaenda kwa Yuwsuf kumuuliza): “Yuwsuf! Ee mkweli! Tufutu katika (ndoto ya) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani (mabichi) na mengineyo (saba) yabisi; ili nirejee kwa watu (kuwajulisha maana yake halisi) ili wapate kuelewa.”

قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ ﴿٤٧﴾

 

47. (Yuwsuf) Akasema: “Mtalima miaka saba mfululizo. Mtakachokivuna kiacheni katika mashuke yake isipokuwa kichache mtakachokula.

ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ ﴿٤٨﴾

 

48. “Kisha itakuja baada ya hapo (miaka) saba ya shida itakayokula vile mlivyovikadimisha kwa ajili yake isipokuwa kidogo katika vile mtakavyovihifadhi (kama akiba).

ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ ﴿٤٩﴾

 

49. “Kisha utakuja baada ya hapo mwaka (ambao) humo watu watasaidiwa kwa kunyweshewa mvua na na humo watakamua (vya kukamua; zaituni, zabibu n.k).”

وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ ﴿٥٠﴾

 

50. (Baada ya kutambulishwa tafsiri ya ndoto yake) Mfalme akasema:  “Nileteeni (Yuwsuf).” Basi mjumbe alipomwendea (Yuwsuf) alisema: “Rejea kwa bwana wako umuulize nini mkasa wa wanawake waliojikatakata mikono yao. Hakika Mola wangu kwa vitimbi vyao ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima).”

قَالَ مَا خَطْبُكُنَّ إِذْ رَاوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفْسِهِ ۚ قُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِن سُوءٍ ۚ قَالَتِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ الْآنَ حَصْحَصَ الْحَقُّ أَنَا رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٥١﴾

 

51. (Mfalme akawauliza wanawake): “Nini jambo lenu lilikuwa mlipomtaka Yuwsuf kinyume na nafsi yake?” Wakasema: “Haasha liLlaah! Hatukujua uovu wowote kwake.” (Hapo ndio) Mke wa ‘Aziyz (alipokiri kwa) kusema: “Hivi sasa umefichuka ukweli! Mimi nilimtongoza (Yuwsuf) kinyume na nafsi yake. Na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa Swaadiqiyn (wakweli).”

ذَٰلِكَ لِيَعْلَمَ أَنِّي لَمْ أَخُنْهُ بِالْغَيْبِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي كَيْدَ الْخَائِنِينَ ﴿٥٢﴾

52. (Yuwsuf akasema: Nimeuliza) “Hivyo ili (’Aziyz) apate kuelewa kwamba mimi sikumfanyia khiyana nyuma yake; na kwamba Allaah Haongoi hila za makhaini.”


Report Page