Juzuu Ya 11 – Ya’tadhiruwna Ilaykum
Juzuu: 11يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ
يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٤﴾
94. (Wanafiki) Watakutoleeeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema: “Msitoe udhuru, hatutokuaminini! Allaah Amekwishatujulisha kuhusu khabari zenu. Na hivi karibuni Allaah Ataona ‘amali zenu na Mjumbe Wake (pia ataona). Kisha mtarudishwa kwa ‘Aalimil-Ghaybi wash-Shahaadah(Mjuzi wa ghayb na dhahiri), Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖإِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٥﴾
95. Watakuapieni kwa Jina la Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao ni rijs(najsi, uchafu), na makazi yao ni (moto wa) Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٩٦﴾
96. Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.
الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٩٧﴾
97. Mabedui wamezidi zaidi kufuru na unafiki, na wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya yale Aliyoyateremsha Allaah (katika Shari’ah) juu ya Mjumbe Wake. Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٩٨﴾
98. Na katika Mabedui, wako wanaochukulia yale wanayoyatoa (ya mchango katika Njia ya Allaah) kuwa ni gharama (za bure), na wanakungojeleeni misiba. Misiba mibaya itawafika wao. Na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ ۚ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٩﴾
99. Na katika Mabedui, wako wanaomwamini Allaah na Siku ya Aakhirah, na wanachukulia yale wanayoyatoa kuwa ni njia ya makurubisho (yao) mbele ya Allaah, na kupata du’aa ya Mtume. Tanabahi! Hakika hayo ni njia ya kikurubisho kwao. Allaah Atawaingiza katika Rahmah Yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu)
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٠٠﴾
100. Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn katika wakaazi wa Madiynah), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Mabustani yapitayo chini yake mito, watadumu huko (Peponi) milele. Huko ndiko kufuzu kukuu.
وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Na katika Mabedui wanaokaa pembezoni mwenu (katika vijiji vilivyo jirani nanyi; wako) wanafiki. Na katika watu wa Madiynah (pia wako wanafiki) walibobea katika unafiki. Huwajui (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sisi Tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili; kisha watarudishwa katika adhabu kubwa.
وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٠٢﴾
102. Na wengineo wamekiri madhambi yao; wamechanganya ‘amali njema na nyinginezo ovu; huenda Allaah Apokee tawbah zao. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٣﴾
103. Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mali zao Swadaqah, uwatwaharishe (makosa na akhlaaq zao) na uwatakase kwazo (kuwaongezea katika taqwa), na waombee (du’aa na maghfirah). Hakika du’aa yako ni utulivu kwao. Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Je hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayepokea tawbah ya waja Wake, na Anapokea Swadaqah; na kwamba Allaah Ndiye Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye Kurehemu).
وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Na sema (uwaambie): Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona ‘amali zenu na Mjumbe Wake, na Waumini (pia wataona). Na mtarudishwa kwa ‘Aalimil-Ghaybi wash-Shahaadah (Mjuzi wa ghayb na dhahiri); kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٠٦﴾
106. Na wengineo wamengojeshewa kwa Amri ya Allaah. Ama Atawaadhibu au Atawapokelea tawbah zao. Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٠٧﴾
107. Na wale (wanafiki) waliojenga Msikiti kwa ajili ya kuleta madhara na kufuru na kufarikisha baina ya Waumini na (kuufanya ni (mahali) pa kuvizia waliompiga vita Allaah na Mjumbe Wake (hapo) kabla. Na bila shaka wanaapa (kwa kusema): “Hatukukusudia ila wema.” Na Allaah Anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo.
لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Usisimame (Msikitini) humo Abadan. Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa (Masjid Qubaa) tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha (madhambi yao) Na Allaah Anapenda wanaojitwaharisha (madhambi, uchafu, najsi, n.k.).
أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٩﴾
109. Je, ambaye ameasisi jengo lake katika taqwa ya Allaah na radhi, ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa lenye kuburugunyika likaporomoka pamoja naye katika moto wa Jahannam? Na Allaah Haongoi watu madhalimu.
لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١١٠﴾
110. Halitoacha (litaendelea) jengo lao hilo walolijenga kuwa ni sababu ya kuwatia shaka katika nyoyo zao (siku zote), mpaka nyoyo zao zikatikatike; na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).
إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚوَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١١﴾
111. Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata (badala yake) Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea (Allaah kuitimiza) katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah? Basi furahieni kwa biashara yenu mliyouziana Naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾
112. (Waumini ambao Allaah Amenunua mali zao na nafsi zao ni wale) At-Taaibuwn (wanaotubia pindi wakikosa), Al-‘Aabiduwn (wanaofanya ibada, Al-Haamiduwn (wanaoshukuru), As-Saaihuwn (wanaotembea huku na kule kwa ajili ya Njia ya Allaah au wanaofunga Swawm), Ar-Raaki’uwn (wanaorukuu), As-Saajiduwn (wanaosujudu), wanaoamrisha ma’aruwf (Uislamu, mema) na wanaokataza munkari, na wanohifadhi mipaka ya Allaah. Na wabashirie Waumini.
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١١٣﴾
113. Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa (moto wa) Jahiym.
وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾
114. Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya miadi aliyofanya naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye (huyo baba yake) ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni Awwaah (mwenye kumrejelea Allaah kwa maghfira na mambo yote, mwingi mno wa kumdhukuru, kumtukuza kwa unyenyekevu), na mwenye kuvumilia.
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾
115. Na haiwi kwa Allaah Awapotoze watu baada ya kuwa Amewaongoa mpaka Awabainishie ya kujikinga nayo. (Wakikataa kujiepusha nayo ndipo Anapowahesabu kuwa ni waovu). Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima).
إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١١٦﴾
116. Hakika Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na Anafisha. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi wala msadizi yeyote.
لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١١٧﴾
117. Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabii na Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah) na Answaar (waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn katika wakaazi wa Madiynah) ambao wamemfuata (Mtume صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (walipokwenda katika vita vya Tabuwk pamoja na Warumi) baada ya nyoyo za kundi (moja) miongoni mwao zilikaribia kupotoka (kutoka njia iliyonyooka), kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye Huruma, Mpole Mno – Mwenye Kurehemu).
وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١١٨﴾
118. Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu walioabaki nyuma (kwa kutokwenda katika vita vya Tabuwk; watatu hawa walihisi vibaya wa kosa lao kwa kutoitikia wito wa Jihaad, hali zao walizielewa wao wenyewe na Mjuzi wa yaliyomo ndani ya nyoyo; kwani zilikuwa ni mbaya) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana. Pia na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa (kuelekea) Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie (kuwa na wao waombe tawbah). Hakika Allaah Yeye Ndiye Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye Kurehemu).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ ﴿١١٩﴾
119. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na As-Swaadiqiyn (wakweli).
مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Haikuwapasa watu wa Madiynah na Mabedui walio pembezoni mwao kwamba wabakie nyuma ya Mtume wa Allaah (kwa kutokwenda katika vita pamoja na Mtume), wala (haipasi) wajipendelee nafasi zao kuliko nafsi yake (Mtume). Hivyo ni kwa kuwa wao haiwasibu kiu wala machofu, wala njaa kali katika Njia ya Allaah, na wala hawakanyagi njia inayowaghadhibisha makafiri, na wala hawawasibu maadui msiba wowote ila wanaadikiwa kwayo ‘amali njema. Hakika Allaah Hapotezi ujira wa Al-Muhsiniyn(watendao wema).
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢١﴾
121. Na wala hawatoi mchango wowote mdogo au mkubwa (kwa ajili ya Dini ya Allaah) na wala hawavuki bonde (wakiwa vitani) isipokuwa wameandikiwa ili Allaah Awalipe mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wanayatenda.
وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja kwenda (kupigana vita vya Jihaad). Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze (Dini); na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujitahadharisha (na wao na mabaya).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚوَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Enyi Mlioamini! Piganeni (Jihaad) na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na eleweni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Na inapoteremshwa Suwrah (mpya yoyote ile katika Qur-aan), basi miongoni mwao (wanafiki) wako wanaosema: “Nani kati yenu (Suwrah) hii imemzidishia iymaan?” Basi ama wale walioamini huwazidishia iymaan nao wanafurahia.
وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ ﴿١٢٥﴾
125. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (uchafu) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.
أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾
126. Je, hawaoni kwamba wao wanafitiniwa (wanatahiniwa) katika kila mwaka mara moja au mara mbili; kisha hawatubii na wala wao hawawaidhiki?
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Na inapoteremshwa Suwrah (wanafiki) wanatazamana wenyewe kwa wenyewe, (kisha hunong’onezana): “Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni?” Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah Amewagezua nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾
128. Kwa yakini amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumu juu yake (yanamhuzunisha) yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni (kwa kukujalini), ni mpole (na mwenye mapenzi) kwa Waumini, na mwenye huruma.
فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ﴿١٢٩﴾
129. Na wakikengeuka, basi sema: “Hasbiya-Allaah!” (Amenitosheleza Allaah); Laa ilaaha illaa Huwa(hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye), Kwake nimetawakali. Naye ni Mola wa ‘Arsh adhimu.
سُورَةُ يُونُس
Yunus: 10
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Hizo ni Aayah za Kitabu chenye hikmah.
أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ ﴿٢﴾
2. Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahyi mtu miongoni mwao kwamba: “Waonye watu (kuhusu adhabu ya Moto) na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Mola wao.” Wakasema makafiri: “Hakika huyu bila shaka ni mchawi dhahiri.”
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾
3. Hakika Mola wenu ni (Yule) Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa(Akalingamana inavyolingana na Utukufu Wake) katika ‘Arsh. Anadabiri amri (ya kila Alichokiumba). Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya Idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Mola Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?
إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٤﴾
4. Kwake ni marejeo yenu nyote. Ni ahadi ya Allaah iliyo ya kweli. Hakika Yeye Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha ili Awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda (‘amali) njema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka, na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakikufuru.
هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥﴾
5. Yeye (Allaah) Aliyejaalia jua kuwa ni mwanga na mwezi kuwa ni nuru; na Akaukadiria vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyingine). Allaah Hakuumba hivyo ila kwa haki. Anafasili Aayah kwa watu wanaoelewa.
إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ ﴿٦﴾
7. Hakika katika mabadiliko (ya mfuatano) ya usiku na mchana na Alivyoviumba Allaah katika mbingu na ardhi, bila shaka ni Aayaat(Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, mafunzo, maonyo n.k) kwa watu walio na taqwa.
إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ ﴿٧﴾
7. Hakika wale wasiotaraji kukutana Nasi, na wakaridhika na maisha ya dunia na wakakinaika nayo, na wale ambao wanaghafilika na Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.)
أولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٨﴾
8. Hao makazi yao ni Moto, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٩﴾
9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Mola wao Atawaongoa kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Mabustani ya neema (Peponi).
دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
10. Wito wao humo (utakuwa) ni: “Subhaanaka-Allaahumma” (Umetakasika ee Allaah). Na maamkizi yao humo ni “Salaam” (Amani). Na wito wao wa mwisho ni ‘AlhamduliLLaahi Rabbil-‘Aalamiyn” (Himdi Zote ni za Allaah Mola wa walimwengu).
وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖفَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١﴾
11. Na lau Allaah Angeliwaharakizia watu shari (wanayoihimiza iwafike) kama wanavyojihimizia kheri, basi bila shaka ingelikidhiwa ajali yao (ya adhabu). Basi Tunawaacha wale wasiotarajia kukutana Nasi katika upotofu wao wakitangatanga ovyo.
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢﴾
12. Na inapomgusa binaadamu dhara hutuomba (katika kila hali), anapolala ubavu, au anapokaa au kusimama. Tunapomuondolea dhara, hupita (kuendelea na maasi) kama kwamba hakutuomba (Tumuondoshee) dhara iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapindukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini Tulihiliki watu kabla yenu walipodhulumu, na wakawajia Mitume yao kwa hoja bayana, na hawakuwa wa kuamini. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa watu wakhalifu.
ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٤﴾
14. Kisha Tukakufanyeni makhalifa katika ardhi baada yao, ili Tutazame vipi mtatenda.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾
15. Na wanaposomewa Aayah Zetu bayana, wale wasiotarajai kukutana Nasi husema: “Lete Qur-aan isiyokuwa hii au ibadilishe.” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hainipasii mimi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu. Mimi sifuati ila tu yale yanayofunuliwa kwangu Wahyi. Hakika mimi nahofi nikimuasi Mola wangu (Atanisibu) adhabu kuu.
قُل لَّوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٦﴾
16. Sema: “Lau Angetaka Allaah nisingelikusomeeni (hii Qur-aan) na wala Asingelikujulisheni nayo. Kwani nimekwishaishi nanyi umri (mwingi) kabla yake. Je, basi hamtii akilini?”
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi nani dhalimu zaidi kuliko (yule) ambaye anamzulia Allaah uongo au amekadhibisha Aayah Zake; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo?) Hakika wakhalifu hawatofaulu.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿١٨﴾
18. Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao (hawawezi) kuwadhuru na wala (hawawezi) kuwanufaisha, na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Subhaanahu wa Ta’ala! (Utakaso ni Wake Na Ametukuka kwa Uluwa) kwa yale yote wanayomshirikisha.
وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١٩﴾
19. Na wala watu hawakuwa (huko nyuma katika zama za Nabii Aadam) ila ni Ummah mmoja (wote wanampwekesha Allaah), kisha wakakhitilafiana. Na lau si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako; bila shaka ingelikidhiwa baina yao (hapa hapa) katika yale waliyokuwa kwayo wakikhitilafiana.
وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema: “Kwanini haikuteremshwa juu yake Aayah (ishara, dalili, hoja, muujiza) kutoka kwa Mola wake?” Basi sema: “Hakika (‘ilm) ya ghayb ni ya Allaah Pekee. Basi ngojeeni; hakika mimi niko pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.”
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na Tunapowaonjesha watu Rahmah baada ya dhara iliyowagusa; tahamaki wanafanyia hila katika Aayah Zetu (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza n.k.). Sema: “Allaah ni Mwepesi zaidi wa kuvurumisha hila. Hakika Wajumbe wetu (Malaika) wanaandika yale (yote) wanayofanya hila.”
هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٢٢﴾
22. Yeye Ndiye Anayekuendesheni katika bara (nchi kavu) na bahari. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upepo mzuri, na wakafurahia; mara ukawajia upepo wa dhoruba, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakadhani kwamba wameshazungukwa. Hapo humwomba Allaah kwa kumtakasia Dini Yake; (wakisema): “Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٢٣﴾
23. Lakini Anapowaokoa, tahamaki wao wanafanya jeuri (kumuasi Allaah) katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri yenu ni dhidi ya nafsi zenu (itakudhuruni nyinyi wenyewe). Ni starehe ya maisha ya dunia. Kisha Kwetu marejeo yenu; Tutakujulisheni kwa yale (yote) mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uweza juu yake (ya kuivuna); tahamaki Amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayah kwa watu wanaotafakari.
وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢٥﴾
25. Na Allaah Anaitia kwenye Daarus-Salaam (nyumba ya amani, Peponi), na Anamhidi Amtakaye kwenye Swiraatwim-Mustaqiym (Njia iliyonyooka).
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٦﴾
26. Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah). Na wala vumbi halitowafunika nyuso zao na wala (hawatopatikana na) udhalilifu. Hao ni watu wa Jannah Wao watadumu humo milele.
وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧﴾
27. Na wale waliochuma maovu, jazaa ya uovu ni mfano wake vile vile, na udhalilifu utawafunika. Hawatopata atakayewaepusha na (adhabu ya) Allaah. Zitakuwa nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wenye giza kubwa. Hao ni watu wa Motoni, wao watadumu humo milele.
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚفَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na (wakumbushe): Siku Tutakayowakusanya wote, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “(Bakieni) mahali penu nyinyi na washirika wenu (mliokuwa mkiwashirikisha na Allaah duniani).” Kisha Tutawatenganisha baina yao. Na washirika wao watasema: “Hamkuwa mkituabudu sisi.”
فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ ﴿٢٩﴾
29. “Basi Allaah Anatosheleza kuwa Shahidi baina yetu na baina yenu kwamba sisi tulikuwa hatuna khabari na ‘ibaadahzenu.”
هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٣٠﴾
30. Huko (Siku hiyo ya Qiyaamah) kila nafsi itatiwa mtihanini kwa iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Allaah, Mola wao wa haki. Na yatawapotea yale yote waliyokuwa wakiyazua.
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚفَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣١﴾
31. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa (aliye) hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka (aliye) uhai; na nani anayedabiri mambo (yote)? Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na taqwa?”
فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٣٢﴾
32. Basi Huyo Ndiye Allaah, Mola wenu wa haki. Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? Basi vipi mnageuzwa (kutoka kumwabudu Yeye kuelekea kumwabudu mwengine)?
كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo Neno la Mola wako litakavyothibiti juu ya wale waliofanya ufasiki kwamba hawatoamini.
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣٤﴾
34. Sema: “Je, yuko kati ya washirika wenu (mnaowafanya miungu) anayeanzisha uumbaji (wa viumbe) kisha anaurudisha?” Sema: “Allaah Anaanzisha uumbaji (wa viumbe) kisha Anaurudisha. Basi vipi mnaghilibiwa (kugeuzwa kutoka njia ya uongofu kuelekea ya batili)?”
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿٣٥﴾
35. Sema: “Je, yuko kati ya (hao) washirika wenu (mnaowafanya miungu) anayeongoza kwenye haki?” Sema: “Allaah Anaongoza kwenye haki. Je, basi anayeongoza kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au (anastahiki) ambaye asiyeongoza isipokuwa tu yeye (mwenyewe) aongozwe? Basi mna nini, vipi mnahukumuje?”
وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Hakika dhana haifai kitu (chochote) mbele ya haki. Hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa yale yote myatendayo.
وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٧﴾
37. Na haiwezekani hii Qur-aan kuwa imetungwa pasi na Allaah, lakini inasadikisha yale yaliyokuja kabla yake (Tawraat, Injiyl, Zabuwr), na ni tafsili ya Kitabu ambayo haina shaka ndani yake imetoka kwa Mola wa Al-‘Aalamiyna (walimwengu).
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾
38. Je, (ndio) wanasema (kuwa Qur-aan) ameitunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)? Sema: “Hebu basi leteni Suwrah (yoyote ile) ya mfano wake, na waiteni mnaoweza (kuwaita ili wakusaidieni katika hilo) pasi na Allaah mkiwa ni Swaadiqiyn.” (wakweli)
بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٣٩﴾
39. Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema elimu yake, na wala taawiyl (uhakika wake halisi) haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao. Basi tazama vipi ulikuwa mwisho wa madhalimu.
وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٤٠﴾
40. Na miongoni mwao wako wanaoiamini, na miongoni mwao wako wasioiamini. Na Mola wako Anawajua vyema mafisadi.وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٤١﴾
41. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: “Mimi nina ‘amali yangu, nanyi mna ‘amali zenu. Nyinyi hamna dhima na yale niyatendayo, na wala mimi sina dhima na yale myatendayo.وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na miongoni mwao (wako) wanaokusikiliza. Je, kwani wewe unasikilizisha viziwi japokuwa hawatii akilini?وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na miongoni mwao (wako) wanaokutazama. Je, kwani wewe unaongoa kipofu japokuwa hawaoni?إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٤﴾