Juzuu
وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na miongoni mwao (wako) wanaokutazama. Je, kwani wewe unaongoa kipofu japokuwa hawaoni?إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٤﴾
44. Hakika Allaah Hadhulumu watu chochote, lakini watu nafsi zao wenyewe (ndio) wenye kujidhulumu.وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿٤٥﴾
45. Na (wakumbushe) Siku Atakayowakusanya (wataona) kama kwamba hawakuishi (duniani) isipokuwa saa moja ya mchana, watajuana (wenyewe kwa wenyewe). Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah, na hawakuwa wenye kuongoka.وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na kama Tutakuonyesha (katika uhai wako ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya yale Tunayowaahidi (ya adhabu) au Tukikufisha, basi Kwetu (ndio) marejeo yao; kisha Allaah ni Shahiydi juu ya yale wanayoyatenda.وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na kila ummah kuna Mtume. Basi anapokuja Mtume wao (wakimkanusha) inakidhiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: “Lini (itafika) hiyo ahadi (adhabu ya Qiyaamah), mkiwa ni Swaadiqiyn?” (wakweli)قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Sema: “Similiki kwa ajili ya nafsi yangu dhara na wala manufaa isipokuwa Aliyotaka Allaah. Kwa kila Ummah una muda (wake) maalumu. Utakapofika muda wao, basi hawatoweza kuakhirisha saa moja wala hawatoweza kukadimisha.”قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٥٠﴾
50. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu Yake usiku au mchana, sehemu gani (ya adhabu) wanaihimiza wakhalifu?”أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ ۚ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٥١﴾
51. Kisha tena! Itakapotokea ndio mtaiamini? (Wataambiwa): “Je, sasa? (Ndio mnaamini)? Na hali mlikuwa mnaihimiza?”ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٥٢﴾
52. Kisha wataambiwa wale waliodhulumu: “Onjeni adhabu ya kudumu. Kwani je, mtalipwa (vingine) isipokuwa kwa yale mliyokuwa mkiyachuma?”وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuuliza je, hiyo (adhabu ya Qiyaamah) ni kweli? Sema: “Ndio! Naapa kwa Mola wangu. Hakika hiyo bila shaka ni kweli! Nanyi hamuwezi kushinda (Qudra ya Allaah ya kukufufueni).”وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ ۗ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٥٤﴾
54. Na lau ingelikuwa kila nafsi iliyodhulumu, inamiliki yote yaliyomo katika ardhi, bila shaka ingeliyatolea fidia kwayo (lakini haitopokelewa), na wataficha (au watadhihirisha) majuto watakapoona adhabu. Na itakidhiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٥﴾
55. Tanabahi! Hakika ni vya Allaah (Pekee) vilivyomo katika mbingu na ardhi. Tanabahi! Hakika Ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawaelewi.هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٥٦﴾
56. Yeye Ndiye Anayehuisha na Anayefisha, na Kwake (Yeye Pekee) mtarejeshwa.يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾
57. Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni Mawaidha (Qur-aan inayoamrisha mema na kukataza maovu) kutoka kwa Mola wenu, na Shifaa (poza) ya yale (maradhi) yote yaliyomo vifuani, na Hudan (Uongofu) na Rahmah kwa Waumini.قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿٥٨﴾
58. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Kwa Fadhila za Allaah na kwa Rahmah Yake (Qur-aan, Uislamu, Iymaan), basi kwa hayo wafurahi.” Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya (mali na starehe za dunia).قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ ﴿٥٩﴾
59. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo (nyingine kuwa) ni haraam na halaal.” Sema: “Je, Allaah Amekupeni idhini (kuzifanya hivyo?) Au mnamzulia uongo Allaah?”وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na nini dhana ya wale wanaomzulia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah? (Yaani wanadhani hawatoadhibiwa kwa yale waliyoyazua? Hapana! Bali watatiwa Motoni). Hakika Allaah Ana fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٦١﴾
61. Na hushughuliki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika jambo lolote, na wala husomi humo (chochote) katika Qur-aan, na wala (enyi Watu) hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Mola wako (kitu chochote hata) cha uzito wa atomu ndogo katika ardhi wala mbinguni na (hata) kidogo kuliko hicho na (hata) kikubwa zaidi ya hicho isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho bayana (kimerekodiwa kinaganaga).أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾
62. Tanabahi! Hakika awliyaa wa Allaah (wanaoamini Tawhiyd ya Allaah, na kujiepusha madhambi na maovu yote yaliyokatazwa) hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾
63. Wale walioamini na wakawa wana taqwa (wanafuata amri za Allaah na wanajiepusha na makatazo Yake).لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٤﴾
64. Watapata bishara katika maisha ya dunia na ya Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukuu.وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦٥﴾
65. Na wala isikuhuzushie kauli yao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hakika taadhima zote (kutokana na nguvu) ni za Allaah Pekee. Yeye Ndiye As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ شُرَكَاءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿٦٦﴾
66. Tanabahi! Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na wale wanaoomba (wanaoabudu) ghairi ya Allaah, hawafuati washirika (wanaodaiwa kuwa ni) wa Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana, nao hawasemi isipokuwa uongo tu.هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٦٧﴾
67. Yeye Ndiye Ambaye Amekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana ung’aao (mpate kuonea). Hakika katika hayo ni Aayaat (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, mafunzo n.k) kwa watu wanaosikia (wakatafakari na kuzingatia).قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَـٰذَا ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٨﴾
68. (Mayahudi na Manaswara) Wanasema: “(Allaah) Amejifanyia mtoto.” Subhaanah! (Utakaso ni Wake). Yeye Ni Al-Ghaniyyu(Mkwasi, Hahitaji lolote) Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Hamna nyinyi dalili kwa hayo (mnayodai). Je, mnasema juu ya Allaah msiyoyajua? قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾
69. Sema: “Hakika wale wanaomzulia uongo Allaah hawatofaulu.”مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. (Watapata) Starehe (chache tu) katika dunia, kisha Kwetu ndio marejeo yao, kisha Tutawaonjesha adhabu shadidi kwa yale waliyokuwa wakiyakanusha.وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللَّـهِ فَعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ ﴿٧١﴾
71. Na wasomee khabari za Nuwh, alipoiambia Qawm yake: “Enyi Qawm yangu! Ikiwa kukaa kwangu na kukumbusha kwangu Aayah za Allaah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, mafunzo n.k) kumekuwa ni mashaka juu yenu (kinakuchukizeni); basi kwa Allaah nategemea. (Hivyo basi) Jumuisheni amri yenu na washirika wenu (mnidhuru). Kisha amri yenu (hiyo) isiwe ya kufichika; kisha nihukumuni wala msinipe muda wa kungojea.”فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٧٢﴾
72. “Mkikengeuka, (khiyari yenu). Kwani mimi sikukuombeni ujira wowote. Sitaki ujira isipokuwa kwa Allaah na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.”فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾
73. Walimkadhibisha; Tukamuokoa (Nuwh) pamoja na waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawafanya makhalifa, na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayah Zetu. (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, n.k) Basi tazama vipi ulikuwa mwisho wa (watu) walioonywa (wasisikie na kufuata).ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ ﴿٧٤﴾
74. Kisha Tukapeleka baada yake Mitume kwa Qawm zao, wakawajia kwa hoja bayana; lakini hawakuwa wenye kuyaaamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Hivyo ndivyo Tunavyopiga muhuri juu ya nyoyo za wapindukao mipaka.ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿٧٥﴾
75. Kisha baada ya hao, Tukamtuma Muwsaa na Haaruwn kwa Fir’awn na wakuu wake kwa Aayah Zetu (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza n.k); walitakabari na wakawa watu wakhalifu.فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧٦﴾
76. Ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: “Huu bila shaka ni uchawi dhahiri.”قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُونَ ﴿٧٧﴾
77. Muwsaa akasema: “Je, mnasema (hivyo) kuhusu haki ilipokujeni? Huu ni uchawi? Na wachawi hawafaulu.”قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ ﴿٧٨﴾
78. Wakasema: “Je, umetujia ili utugeuze (Dini yetu) kutokana na yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ili ukubwa uwe wenu (nyinyi wawili) katika ardhi? Na sisi hatutawaamini nyinyi.”وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿٧٩﴾
79. Na Fir’awn akasema: “Nileteeni kila mchawi mjuzi.”فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ ﴿٨٠﴾
80. Basi walipokuja wachawi, Muwsaa akawaambia: “Tupeni mnavyotaka kuvitupa.”فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨١﴾
81. Basi walipotupa, Muwsaa alisema: “Mliyokuja nayo ni uchawi. Hakika Allaah Atayabatilisha. Hakika Allaah Hatengenezi ‘amali za mafisadi.”وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ ﴿٨٢﴾
82. “Na Allaah Atathibitisha haki kwa Maneno Yake; japokuwa watakirihika wakhalifu.”فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ ﴿٨٣﴾
83. Basi hawakumwamini Muwsaa isipokuwa (baadhi tu ya) dhuria katika Qawm yake kwa kumkhofu Fir’awn na wakuu wao wasiwafitinishe (asiwatese). Na hakika Fir’awn ni jeuri katika ardhi, na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wapindukao mipaka.وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Muwsaa akasema: “Enyi watu wangu! Ikiwa mmemwamini Allaah; basi Kwake mtawakali, mkiwa ni Waislamu.”فَقَالُوا عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٨٥﴾
85. Wakasema: “Tumetawakali kwa Allaah. Ee Mola wetu! Usitujaalie kuwa ni fitnah kwa watu madhalimu.”وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾
86. “Na Tuokoe kwa Rahmah Yako dhidi ya watu makafiri.”وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na Tukamfunulia Muwsaa Wahyi na kaka yake kwamba: “Watengenezeeni watu wenu katika mji nyumba na zifanyeni nyumba zenu Qiblah (Misikiti; sehemu za kufanyia ‘ibaadah kuelekea Al-Ka’abah), na simamisheni Swalaah. Na wabashirie Waumini. وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ ۖ رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٨٨﴾
88. Na Muwsaa akasema: “Ee Mola Wetu! Hakika Wewe Umempa Fir’awn na wakuu wake mapambo na mali katika maisha ya dunia. Ee Mola wetu! Ili wapoteze (watu) Njia Yako. Mola wetu! Ondoshelea mbali mali zao na fanya nyoyo zao ziwe ngumu kwani hawatoamini mpaka waone adhabu iumizayo.”قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٨٩﴾
89. (Allaah) Akasema: “Imekwishaitikiwa du’aa yenu nyinyi wawili, basi nyookeni (kuweni na istiqaamah katika kutenda mema na kulingania ujumbe wa Allaah kwa subira) na wala msifuate njia ya wale wasiojua (haki).”وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩٠﴾
90. Na Tukawavukisha wana wa Israaiyl bahari, basi Fir’awn akawafuata (pamoja) na jeshi lake kwa dhulma na uadui; mpaka ilipomfikia (Fir’awn) gharka akasema: “Nimeamini kwamba hapana ilaah (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Yule waliyemwamini wana wa Israaiyl, na mimi ni miongoni mwa Waislamu (wanaojisalimisha kwa Allaah).”آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٩١﴾
91. (Malaika wakamwambia): “Sasa ndio unaamini, na hali umeasi kabla, na ulikuwa miongoni mwa mafisadi?”فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ ﴿٩٢﴾
92. Basi leo Tunakuokoa kwa (kuuweka) mwili wako ili uwe Aayah (Ishara, dalili, muujiza, mazingatio, mafunzo, maonyo n.k) kwa wa (watakaokuja) nyuma yako (wajue kuwa hukuwa mungu). Na hakika watu wengi wameghafilika na Aayah Zetu (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, mafunzo, maonyo n.k)وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na kwa yakini Tuliwapa makazi wana wa Israaiyl; makazi mema, na Tukawaruzuku katika Twayyibaat(halaal na vizuri); na hawakukhitilafiana mpaka ilipowajia elimu. Hakika Mola wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale yote waliyokuwa wakikhitilafiana. فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٩٤﴾
94. Basi ukiwa una shaka (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika yale Tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma Kitabu (cha Injiyl na Tawraat) kabla yako (Mayahudi na Manaswara waliosilimu). Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Mola wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَتَكُونَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٥﴾
95. Na wala usijekuwa miongoni mwa wale waliokadhibisha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) ukawa miongoni mwa waliokhasirika.إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٩٦﴾
96. Hakika wale ambao neno la Mola wako (ghadhabu) limewathibitikia juu yao, hawataamini.وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٩٧﴾
97. Japokuwa itawajia kila Aayah (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, maonyo n.k) mpaka waone adhabu iumizayo.فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٩٨﴾
98. Basi kwa nini usiweko mji mmoja ukaamini (kabla ya adhabu) na iymaan yake ikawafaa (kujikinga na adhabu? Hukukutokea katika tarehe mji huo) Isipokuwa watu wa Yuwnus (pekee ndio walioamini mara tu walipohisi kuwa adhabu itawafika). Walipoamini, Tuliwaondoshea adhabu ya hizaya duniani, na Tukawasterehesha mpaka wakati (tulioutaka).وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٩٩﴾
99. Na lau Angetaka Mola wako, basi wangeliamini wote pamoja walioko katika ardhi. Je, basi wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Na hakuna nafsi yoyote (inayoweza) kuamini isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Naye Hujaalia ar–rijsa(shari, upotofu) kwa wale ambao wasiotia akilini.قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠١﴾
101. Sema: “Tazameni nini yaliyoko mbinguni na ardhini.” Lakini Aayah zote (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, mafunzo, n.k) na maonyo haiwafai kitu watu wasioamini.فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Je, wanangojea jingine (la maangamizi) isipokuwa mfano wa (adhabu zilopita) siku (za) wale waliopita kabla yao? Sema: “Basi ngojeeni, hakika mimi (pia) niko ni pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.”ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Kisha (mwishowe) Tunawaokoa Mitume Wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu Kuwaokoa Waumini.قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ اللَّـهَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Sema: (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Enyi watu! Ikiwa mna shaka katika Dini yangu (ya Kiislamu); basi (mimi) siabudu ambavyo mnaviabudu badala ya Allaah; lakini namwabudu Allaah Ambaye Anakufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.”وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٥﴾
105. “Na (nimeamrishwa kwamba): Elekeza uso wako kwa Dini Haniyfaa(ya Tawhiyd – kumpwekesha Allaah), na wala usijekuwa miongoni mwa washirikina.” وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٦﴾
106. “Na (nimeamrishwa pia kwamba): Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa (ukimwabudu) na wala asiyekudhuru (usipomwabudu). Na ukifanya (hivyo), basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.”وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٧﴾
107. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na (Allaah) Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha Fadhila Yake, Anamsibu kwazo (Fadhila Zake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Al-Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٨﴾
108. Sema: “Enyi watu! Kwa yakini imekujieni haki kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan). Basi atakayeongoka, hakika anaongoka kwa ajili ya (manufaa ya) nafsi yake. Na atakayepotoka, hakika anapotoka kwa (hasara) ya nafsi yake. Nami si mdhamini juu yenu.”وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿١٠٩﴾
109. Na (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Fuata yale yaliyofunuliwa kwako Wahyi na subiri mpaka Allaah Ahukumu. Naye ni Khayrul-Haakimiyn (Mbora wa wanaohukumu).سُورَةُ هُود
Huud: 11
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa. Kitabu ambacho Aayah Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa (vyema) kutoka kwa Hakiymin-Khabiyr(Mwenye Hikmah wa yote daima – Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).
أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ ﴿٢﴾
2. (Wahyi kupitia kwa Mtume kwamba) Usiabudu (yeyote wala chochote) isipokuwa Allaah. (Na uwaambie watu kwamba): “Hakika mimi ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.”وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ ﴿٣﴾
3. Na kwamba: “Mwombeni Mola wenu maghfirah kisha tubuni Kwake. Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliopangwa; na Atampa (Aakhirah) kila mwenye fadhila, fadhila yake. Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakhofu adhabu dhidi yenu (adhabu ya) Siku kubwa (Siku ya kufufuliwa, Qiyaamah).”إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤﴾
4. Kwa Allaah ni marejeo yenu. Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Mweza wa yote daima).أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٥﴾
5. Tanabahi! Hakika wao wanageuza (wanaficha vilivyomo ndani ya) vifua vyao ili wamfiche Yeye (Allaah Asiwatambue). Tanabahi! Wanapojigubika nguo zao. Anajua wanayoyafanya siri na wanayoyatangaza. Hakika Yeye ni ‘Aliym (Mjuzi daima) kwa yaliyomo vifuani.