Juzuu Ya 20 – Famaa Kaana Jawaaba Qawmihi

Juzuu Ya 20 – Famaa Kaana Jawaaba Qawmihi


Juzuu: 20

فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ

Juzuu Ya 20 – Famaa Kaana Jawaaba Qawmihi


فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوا آلَ لُوطٍ مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٥٦﴾

56. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Watoeni watu wa Luwtw kutoka mji wenu, hakika wao ni watu wanaojiweka katika utakaso. 

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَاهَا مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٥٧﴾

57. Basi Tulimuokoa na ahli yake isipokuwa mke wake Tumekadiria (yeye awe) miongoni mwa watakaobakia nyuma (kuangamizwa).” 

وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na Tukawanyeshea mvua. Basi uovu ulioje mvua ya walioonywa. 

قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَىٰ ۗ آللَّـهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٥٩﴾

59. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): AlhamduliLlaah (Himdi zote ni za Allaah) na amani kwa Waja Wake ambao Amewachagua. Je, Allaah ni Bora au wanaowashirikisha? 

أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا شَجَرَهَا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ ﴿٦٠﴾

60. (Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Aliyeumba mbingu na ardhi na Akakuteremshieni kutoka mbinguni maji, kisha Tukaotesha kwayo mabustani yenye uzuri mno (ya kupendeza). Nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko ilaah (mungu mwengine) pamoja na Allaah? (Hapana!) Bali wao ni watu wanaolinganisha (miungu wengine na Allaah). 

أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾

61. (Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Aliyeijaalia ardhi kuwa makazi ya kutulia (thabiti), na Akajaalia baina yake mito, na Akaiwekea milima, na Akajaalia baina ya bahari mbili (ya maji ya chumvi na tamu) kizuizi. Je, yuko ilaah (mungu mwengine) pamoja na Allaah? (Hapana!) Bali wengi wao hawaelewi. 

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗأَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

62. (Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Anayemuitika mwenye dhiki anapomwomba, na Akamuondoshea uovu (dhiki), na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko ilaah (mungu mwengine) pamoja na Allaah? (Hapana!) Ni machache (mno) mnayokumbuka (na mkapata kuzingatia). 

أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ تَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٣﴾

63. (Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari; na nani anayetuma pepo za bishara kabla ya Rahmah Yake. Je, yuko ilaah (mungu mwengine) pamoja na Allaah?  Ta’aala-Allaah (Ametukuka Allaah) kutokana na yale (yote) wanayomshirikisha. 

أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦٤﴾

64. (Wanaowashirikisha ni bora) Au Yule Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha; na nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je, yuko ilaah (mungu mwengine) pamoja na Allaah? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.” 

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

65. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakuna (yeyote yule miongoni mwa) waliomo katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah (Pekee). Na wala hawatambui (ni) lini watafufuliwa.” 

بَلِ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الْآخِرَةِ ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّنْهَا ۖ بَلْ هُم مِّنْهَا عَمُونَ﴿٦٦﴾

66. Bali umefikia kikomo ujuzi wao kuhusu Aakhirah. Bali wao wamo katika shaka nayo. Bali wao ni vipofu nayo. 

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ ﴿٦٧﴾

67. Na wakasema wale waliokufuru: “Je, tukiwa mchanga na baba zetu; hivi sisi (kweli) tutatolewa (kutoka makubirini mwetu tuwe hai tena)?” 

لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٦٨﴾

68. “Tumekwishaahidiwa haya sisi na baba zetu (hapo) kabla. Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za (watu) wa kale. 

قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٦٩﴾

69. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Tembeeni katika ardhi mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wakhalifu.”  

وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ ﴿٧٠﴾

70. Na wala usihuzunike juu yao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na wala usiwe katika dhiki kutokana na wanayofanya hila. 

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٧١﴾

71. Na wanasema (kukuuliza): “Ni lini hiyo ahadi (ya adhabu au Qiyaamah itatimizwa) mkiwa ni wakweli?”‏.‏ 

قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٧٢﴾

72. Sema: “Huenda yakawa yamekaribia nyuma yenu baadhi ya mnayoyahimiza.” 

وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾

73. Na hakika Mola wako ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru. 

وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٤﴾

74. Na hakika Mola wako bila shaka Anajua yale (yote) yanayoficha vifua vyao (ya siri) na yale (yote) wanayoyatangaza 

وَمَا مِنْ غَائِبَةٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٧٥﴾

75. Na hakuna ghayb yoyote (ile) katika mbingu na ardhi isipokuwa yamo katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuudhw-Ubao uliohifadhiwa). 

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٧٦﴾

76. Hakika hii Qur-aan inawasimulia wana wa Israaiyl mengi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.  

وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٧٧﴾

77. Na hakika hii (Qur-aan) ni Uongofu na Rahmah kwa Waumini. 

إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُم بِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ ﴿٧٨﴾

78. Hakika Mola wako Atahukumu baina yao kwa Hukumu Yake. NayeAl-’Aziyzul-‘Aliym (Mwenye Nguvu,Mshindi Asiyeshindika daima – Mjuzi wa yote daima). 

فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ ﴿٧٩﴾

79. Basi tawakali kwa Allaah. Hakika wewe uko kwenye haki bayana. 

إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٨٠﴾

80. Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapogeuka nyuma (kwenda zao). 

وَمَا أَنتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨١﴾

81. Na wala wewe huwezi kuwahidi vipofu katika upotofu wao; huwasikilizishi isipokuwa yule anayeamini Aayah Zetu nao ndio Waislamu (wanaojisalimisha kwa Allaah سبحانه وتعالى ). 

وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na itakapowaangukia kauli (ya kufika Qiyaamah); Tutawatolea  mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha (aseme): kwamba watu walikuwa hawana yakini na Aayah Zetu. 

وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾

83. Na Siku Tutakayokusanya katika kila Uummah makundi miongoni mwa wale wanaokadhibisha Aayah Zetu nao watagawanywa. 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُم بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾

84. Mpaka watakapokuja, Allaah Atasema: “Je, mmekadhibisha Aayah Zangu na wala hamkuwa na elimu nazo vyema? Au nini mlikuwa mnafanya?”  

وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ ﴿٨٥﴾

85. Na itawaangukia kauli juu yao kwa yale waliyodhulumu, nao hawatoweza kutamka (lolote kujipigania nafsi zao). 

أَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٨٦﴾

86. Je, hawaoni kwamba Tumejaalia usiku ili wapate utulivu humo, na mchana wenye kuangaza? Hakika katika hayo (kuna) Aayah kwa watu wanaoamini. 

وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na (tahadharisha) Siku itakayopulizwa baragumu, atafazaika kila alioko mbinguni na aliyoko ardhini isipokuwa Amtakaye Allaah. Na wote watamfikia wakiwa duni (wanyenyekevu). 

وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ ۚ صُنْعَ اللَّـهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ ۚ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na utaona majabali ukiyadhania yametulia thabiti (hayataharuki) nayo yanapita mpito wa mawingu. Ufundi wa Allaah Ambaye Ametengeneza kwa umahiri kila kitu. Hakika Yeye niKhabiyr (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo) kwa yale (yote) myafanyayo. 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ آمِنُونَ ﴿٨٩﴾ ﴾

89. (Yeyote yule) Atakayekuja (Siku ya Qiyamah) na jema, basi atapata (yaliyo) bora zaidi kuliko hilo; nao watakuwa katika amani na mafazaiko ya Siku hiyo. 

وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٠﴾

90. Na (yeyote yule) atakayekuja na ovu, basi zitatupwa gubigubi nyuso zao katika Moto; (wataambiwa): “Je, mnalipwa (mengine) isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda?” 

إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾

91. (Sema ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika nimeamrishwa nimwabudu Mola wa huu mji (Makkah) Ambaye Ameuharamisha (Ameufanya mtakatifu kwa Amri Yake). Naye ni Vyake Pekee kila kitu. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu (wanaojisalimisha). 

وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَا أَنَا مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿٩٢﴾

92. “Na kwamba nisome Qur-aan.” Hivyo anayehidika, basi anahidika kwa ajili ya (manufaa ya) nafsi yake. Na anayepotoka, basi sema: “Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.” 

 وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ سَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾

93. Na sema: “AlhamduliLLaahi (Himdi Zote ni za Allaah); Atakuonyesheni Aayah Zake na mtazitambua.” Na Mola wako si Mwenye kughafilika kutokana na yale (yote) wanayoyatenda.”سُورَةُ الْقَصَص

Al-Qaswasw: 28

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

طسم ﴿١﴾

1. Twaa Siyn Miym.  

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Hizi ni Aayah za Kitabu kinachobainisha. 

نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾

3. Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari za Muwsaa na Fir’awn kwa haki kwa watu wanaoamini. 

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾

4. Hakika Fir’awn alijitukuza (kwa kutakabari) katika ardhi, na akawafanya watu wake makundi mbali mbali, akilidhoofisha (kwa kulikandamiza) kundi (la wana Israaiyl) miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume (wanaozaliwa), na akiacha hai wanawake wao. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa mafisadi. 

وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾

5. Na Tunataka Tuwafanyia ihsani wale waliodhoofishwa (kwa kukandamizwa) katika ardhi; na Tuwafanye (kuwa) viongozi na Tuwafanye (kuwa) wenye kurithi. 

وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾

6. Na Tuwamakinishe (kwa uwezo) katika ardhi, na Tumwonyeshe Fir’awn na (waziri wake) Haamaan na majeshi yao miongoni mwao yale waliyokuwa wakitahadhari. 

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾

7. Na Tukamfunulia (kwa kumtia ilhamu) mama yake Muwsaa kwamba: “Mnyonyeshe (Muwsaa); na utakapomkhofia, basi mtupe katika mto (wa Nile), na wala usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi Tutamrudisha kwako, na Tutamjaalia miongoni mwa Mitume”. 

فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾

8. Basi wakamwokota watu wa Fir’awn ili awe adui kwao na (sababu ya) huzuni. Hakika Fir’awn na Haamaan na majeshi yao walikuwa wenye makosa. 

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. Na akasema mke wa Fir’awn (kumwambia Fir’awn), “Kiburudisho cha macho kwangu na kwako; usimuue, huenda akatufaa, au tumfanye mtoto.” Nao hawatambui. 

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾

10. Na moyo wa mama yake Muwsaa ukawa mtupu (kutokana na kila wazo isipokuwa kumwaza Muwsaa tu!) Alikaribia kumdhihirisha (kuwa huyo mtoto ni mwanawe) lau kama Tusingeutia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini. 

وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾

11. (Mama yake Muwsaa) Akamwambia dada yake (Muwsaa): “Mfuatilie!” Akamtazama kwa mbali nao hawatambui.  

وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ ﴿١٢﴾

12. Na Tukamharamishia (akatae kabisa) wanyonyeshaji tokea awali. (Mpaka akaja dada yake Muwsaa) akasema: “Je, nikuelekezeni kwa watu wa nyumba watakaomlea kwa ajili yenu, nao kwake watakuwa wenye kumnasihi (katika kumlea kwa wema)? 

فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Basi Tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na wala asihuzunike, na ili aelewe kwamba ahadi ya Allaah ni haki, lakini wengi wao hawajui. 

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٤﴾

14. Na (Muswsaa) alipofikia umri wa kupevuka na (akaimarika), Tulimpa hukumu na elimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa Al-Muhsiniyn(watendao wema). 

وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. (Siku moja) Akaingia mjini wakati watu wake wako katika ghaflah (wameshughulika); akakuta humo watu wawili wanapigana; huyu (mmoja) ni miongoni mwa kundi lake, na huyu (mmoja mwengine) miongoni mwa adui wake. Akamsaidia yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake, Muwsaa akampiga ngumi, akammaliza (kumuua pale pale). (Muwsaa) Akasema: “Hiki (nilichofanya) ni katika amali za shaytwaan. Hakika yeye (shaytwaan) ni adui mpotezaji dhahiri.”  

قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٦﴾

16. (Muwsaa) Akasema: “Mola wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie; Akamghufuria. Hakika Yeye ni Al-Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa Kughufuria – Mwenye Kurehemu). 

قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾

17. (Muwsaa) Akasema: “Mola wangu! Kwa Uliyonineemesha; sitokuwa kamwe msadizi wa makhalifu.” 

فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ ۚ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾

18. Akapambaukiwa kuwa mwenye khofu katika mji ule anaangaza kwa tahadhari (akingojea matokeo ya kitendo chake cha kumuua mtu). Basi mara yule aliyemuomba amnusuru jana (kupigana na adui yake) anampigia kelele (amsaidie tena kupigana na adui mwingine). Muwsaa akamwambia: “Hakika wewe ni mpotofu dhahiri”. 

فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ ۖ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾

19. Basi alipotaka kumtia mkononi (amshike) yule aliye ni adui wao wote wawili, (yule mtu) akasema: “Ee Muwsaa! Je, unataka kuniua kama ulivyoiua nafsi (mtu) jana? Hutaki lolote isipokuwa unataka uwe jabari katika ardhi, na wala hutaki kuwa miongoni mwa wasuluhishaji.” 

وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾

20. Akaja mtu kutoka pande ya mbali ya mji ule akiwa anakimbia; akasema: “Ee Muwsaa! Hakika wakuu (wa Fir’awn) wanashauriana kuhusu wewe katika kikao ili wakuue; basi toka (nchini haraka), hakika mimi kwako ni miongoni mwa wanaonasihi.”



فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾

21. Basi (Muwsaa) akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari. Akasema: “Mola wangu! Niokoe na watu madhalimu.” 

وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾

22. Na alipoelekea upande wa (mji) wa Madyan, (Muwsaa) akasema: “Huenda Mola wangu Akaniongoza njia iliyo sawa.” 

وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖوَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾

23. Alipofikia maji (kisimani) ya Madyan; alikuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao); (Muwsaa) akasema: “Mna nini?” (Wale wanawake wawili) Wakasema: “Hatunyweshi mpaka wachungaji waondoshe (wanyama wao); (na sababu ya sisi kuwepo hapa nje, ni kuwa) baba yetu ni mtu mzima sana (hawezi kuja kunywesha wanyama wetu).” 

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾

24. Basi (Muwsaa) akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: “Mola wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri Utakayoniteremshia.”  

فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾

25. Basi akaja mmoja wao (katika wale wanawake wawili) akitembea kwa kuona hayaa; akasema: “Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea.” Basi (Muwsaa) alipomfikia (baba yao) na akamsimulia visa (vyake); (yule baba) akasema: “Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.” 

قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ﴿٢٦﴾

26. Akasema mmoja wao (katika wale wanawake wawili): “Ee baba yangu, muajiri! Hakika mbora wa kuajiri ni mwenye nguvu mwaminifu.” 

قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾

27. (Yule baba) Akasema: “Mimi nataka nikuozeshe mmoja wapo wa binti zangu hawa wawili kwa (sharti) kuwa unitumikie miaka minane; ukitimiza (miaka) kumi, basi ni (khiari) kutoka kwako. Na wala sitaki kukutia mashakani; utanikuta In Shaa Allaahmiongoni mwa As-Swaalihiyn (watu wema).” 

قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾

28. (Muwsaa) Akasema: “Hayo ni (makubaliano) baina yangu na baina yako. Muda wowote kati ya miwili nitakaoutimiza basi hakuna uadui dhidi yangu. Na Allaah juu ya yale tunayoyasema ni Wakiyl (Mtegemewa kwa yote).”  

فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾

29. Basi alipotimiza Muwsaa muda, akasafiri pamoja na ahli zake, akaona moto upande wa (jabali) Twuwr. Akawaambia ahli zake: “Bakieni; hakika mimi nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo khabari, au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.” 

فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٠﴾

30. Basi alipoufikia (ule moto), akaitwa kutoka ng’ambo ya bonde la kulia katika eneo lililobarikiwa kutoka mtini kwamba: “Ee Muwsaa! Hakika Mimi ni Allaah, Mola wa walimwengu.” 

وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ الْآمِنِينَ ﴿٣١﴾

31. (Akaambiwa): “Tupa fimbo yako!” Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka (mwembamba anayekimbia mbio) akageuka nyuma kukimbia na wala hakugeuka. (Allaah Akamwita): “Ee Muwsaa! Njoo mbele, na wala usikhofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliokuwa katika amani.”


https://t.me/Furqanbot


Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈


Report Page