JUZUU

JUZUU


اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ ۖ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٣٢﴾

32. “Ingiza mkono wako mfukoni mwako (kifuani), utatoka kuwa mweupe bila ya madhara yoyote. Na ambatisha ubavuni mwako (kujikinga) na khofu. Hizo ni dalili mbili za wazi kutoka kwa Mola wako kwa Fir’awn na wakuu wake; hakika wao walikuwa watu mafasiki.” 

قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿٣٣﴾

33. (Muwsaa) Akasema: “Mola wangu! Hakika mimi nimeua nafsi (mtu) miongoni mwao, na nakhofu wataniua.” 

وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِي ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿٣٤﴾

34. “Na kaka yangu Haaruwn yeye ana ufasaha zaidi wa lugha kuliko mimi, basi mpeleke pamoja nami, kama msaidizi wangu anisadikishe; hakika mimi nakhofu wasinikadhibishe.” 

قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا ۚ بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ ﴿٣٥﴾

35. (Allaah) Akasema: “Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na Tutakupeni (nyote wawili) madaraka, basi hawatakufikilieni. Kwa sababu ya Aayah Zetu, nyinyi wawili na watakaokufuateni mtashinda. 

فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ ﴿٣٦﴾

36. Muwsaa alipowajia (kina Fir’awn na wakuu wake) kwa Aayah Zetu bayana; wakasema: “Hii si chochote isipokuwa ni uchawi uliotungwa; na hatukusikia haya kwa baba zetu wa awali.”  

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٣٧﴾

37. Muwsaa akasema: “Mola wangu Anajua zaidi yule ajaye kwa Uongofu kutoka Kwake, na yule atakayekuwa na matokeo (mazuri) ya nyumba (ya Aakhirah); hakika madhalimu hawafaulu.” 

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٣٨﴾

38. Fir’awn akasema: “Enyi wakuu! Sijui kama mnaye ilaah (mungu) badala yangu; basi niwashie (moto) ewe Haamaan juu ya (matabaka ya) udongo unifanyie mnara mrefu ili nimwangalie ilaah wa Muwsaa, na hakika mimi bila shaka namdhania ni miongoni mwa waongo.” 

وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ ﴿٣٩﴾

39. (Fir’awn) Akatakabri yeye na jeshi lake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kwamba wao Kwetu hawatorejeshwa. 

فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ﴿٤٠﴾

40. Basi Tukamchukua na jeshi lake, Tukawatupilia mbali baharini; basi tazama vipi ulikuwa mwisho wa madhalimu. 

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾

41. Na Tukawafanya viongozi wanaoita (watu) motoni; na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa. 

وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾

42. Na Tukawafuatishia laana katika dunia hii; na Siku ya Qiyaamah wao ni miongoni mwa wanaochukiwa.وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu baada ya kuwa Tumeshahiliki karne za awali (amepewa Kitabu hicho) kiwe ni kifumbuzi macho kwa watu, na Uongofu, na Rahmah ili wakumbuke (na wawaidhike). 

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٤٤﴾

44. Na wala (wewe ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hukuweko kando ya Magharibi (ya mlima) Tulipomkidhia Muwsaa amri, na wala (wewe) hukuwa miongoni mwa walioshuhudia (waliohudhuria). 

وَلَـٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٤٥﴾

45. Lakini Tulianzisha karne (baada ya Muwsaa) ukawatawilikia (ukawa mrefu) umri. Na wala (wewe) hukuwa mkaazi katika watu wa Madyan ukiwasomea Aayah Zetu, lakini Sisi Tulikuwa Watumaji (wa ujumbe na Mitume). 

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٦﴾

46. Na wala (wewe ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hukuwa kando ya (jabali) Twuwr, Tuliponadi, lakini ni Rahmah kutoka kwa Mola wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako ili wapate kuwaidhika (na kukumbuka). 

وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾

47. Na usije kuwasibu msiba kwa yale (dhambi) iliyotanguliza mikono yao, wakasema: “Mola wetu! Kwanini Hukututumia Mtume tukafuata Aayah Zako, na tuwe miongoni mwa Waumini.” 

فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ ﴿٤٨﴾

48. Basi ilipowajia Haki (Uislamu) kutoka Kwetu, walisema: “Mbona hakupewa mfano wa yale aliyopewa Muwsaa? Je, kwani hawakukufuru kwa yale aliyopewa Muwsaa kabla? Walisema: “Wachawi wawili (Muwsaa na Haaruwn) wamesaidiana.” Na wakasema: “Hakika (sisi) kwa yote (wao na kila walichokuja nacho) tunakanusha.” 

قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٩﴾

49. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Leteni Kitabu kutoka kwa Allaah ambacho ni Uongofu zaidi kuliko hivyo viwili nikifuate, mkiwa ni wakweli.  

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾

50. Na wasipokuitikia (kukuletea Kitabu au kuamini ujumbe wako), basi elewa kwamba hakika wanafuata matamanio yao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake bila ya Uongofu kutoka kwa Allaah? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu. 

وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾

51. Na kwa yakini Tumewawasilishia Kauli (Qur-aan) ili wapate kukumbuka (na kuwaidhika) 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾

52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao kwa hiyo (Qur-aan) wanaiamini. 

وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾

53. Na wanaposomewa (Qur-aan), husema: “Tumeiamini, hakika hiyo ni Haki kutoka Mola wetu, hakika Sisi tumekuwa kabla yake Waislamu (wanaojisalimisha kwa Allaah).” 

أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾

54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na (kwa sababu) wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa. 

وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ ﴿٥٥﴾

55. Na wanaposikia maneno ya upuuzi hujitenga nayo; na husema: “Sisi tuna ‘amali zetu, nanyi mna ‘amali zenu.Salaamun ‘alaykum (amani iwe juu yenu)! Hatutaki (kujibizana na) majahili.” 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye A’lam (Anajua zaidi) waongokao. 

وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾

57. Wakasema: “Tukifuata Uongofu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka ardhi yetu. Je, kwani hatukuwamakinisha mahali patakatifu, na pa amani (Makkah) ambako huletewa mazao ya kila kitu kuwa ni riziki kutoka Kwetu; lakini wengi wao hawajui.  

وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na miji mingapi Tumeihiliki, iliyopindukia mipaka mno (ya kukanusha haki na neema) katika maisha yake? Basi hayo ni masikani yao yasiyokaliwa baada yao isipokuwa kidogo tu. Na Tukawa Sisi Warithi. 

وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۚوَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ ﴿٥٩﴾

59. Na Mola wako Hakuwa Mwenye Kuhiliki miji mpaka Apeleke katika mji mkuu wake Mtume awasomee Aayah Zetu. Na Hatukuwa Wenye Kuhiliki miji isipokuwa watu wake wawe madhalimu. 

وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾

60. Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za maisha ya dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah (Aakhirah) ni bora zaidi na yakubakia zaidi. Je, basi hamtii akilini? 

أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٦١﴾

61. Je, yule Tuliyemuahidi ahadi nzuri basi atakutana nayo, ni sawa na yule Tuliyemstarehesha starehe za maisha ya dunia, kisha yeye Siku ya Qiyaamah ni miongoni mwa watakaohudhurishwa (kuadhibiwa motoni)?  

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٦٢﴾

62. Na (kumbusha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) Siku Atakayowaita; Atasema: “Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa mnadai (kuwa ni miungu na kuwalinganisha Nami)? 

قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ ۖ مَا كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ ﴿٦٣﴾

63. Watasema wale iliyowathubutukia kauli: “Mola wetu! Hawa ndio wale tuliowapoteza. Tumewapoteza kama tulivyopotea. Tunajiepusha nao mbele Yako, hawakuwa wakituabudu sisi.” 

وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا الْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ ﴿٦٤﴾

64. Na itasemwa: “Iteni washirika wenu.” Watawaita lakini hawatowaitikia; na wataiona adhabu, (watatamani hapo) lau wangelikuwa wamehidika. 

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na (kumbusha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: “Mliwajibu nini Mitume? 

فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿٦٦﴾

66. Basi zitawafichikia khabari Siku hiyo, nao hawatoweza kuulizana.  

فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ الْمُفْلِحِينَ ﴿٦٧﴾

67. Ama yule aliyetubu (kutokana na kufuru, shirki na madhambi) na akaamini (Allaah na Mitume Yake) na akatenda mema, basi ’asaa akawa miongoni mwa waliofaulu. 

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

68. Na Mola wako Anaumba Atakavyo, na Anachakugua (Atakavyo). Hawakuwa na khiari (ya jambo lolote).Subhaana Allaahi wa Ta’aala(Ametakasika Allaah na Ametukuka) kutokana na yale yote wanayomshirikisha (Nayo). 

وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٦٩﴾

69. Na Mola wako Anayajua yale (yote) yanayoficha vifua vyao, na yale (yote) wanayoyafichua. 

وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾

70. Naye ni Allaah, laa ilaaha illa Huwa(hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye), Pekee Ana Himdi zote mwanzoni na mwishoni, Na Pekee Ana Hukumu, na Kwake Pekee mtarejeshwa. 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ ﴿٧١﴾

71. Sema: “Je, mnaonaje (kama) Allaah Angelikujaalieni usiku (unaoendelea) moja kwa moja (bila ya kukoma) mpaka Siku ya Qiyaamah, nani ilaah (mungu mwengine) asiyekuwa Allaah (atayeweza) kukuleteeni mwanga? Je, basi hamsikii?” 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٧٢﴾

72. Sema: “Je, mnaonaje (kama) Allaah Angelikujaalieni mchana (unaoendelea) moja kwa moja (bila ya kukoma) mpaka Siku ya Qiyaamah, nani ilaah (mungu mwengine) asiyekuwa Allaah (ataweza) kukuleteeni usiku mpate utulivu humo? Je, basi hamuoni?” 

وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾

73. Na kutokana na Rahmah Yake, Amekujaalieni usiku na mchana ili mpate (katika usiku) utulivu humo, na ili mpate (katika mchana) kutafuta katika fadhila Zake, na ili mpate kushukuru. 

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٧٤﴾

74. Na (tahadharisha) Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: “Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa mnadai (kuwa ni miungu na kuwalinganisha Nami)?” 

وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّـهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٧٥﴾

75. Na Tutatoa (kutoka) katika kila Ummah shahidi (wao), kisha Tutasema: “Leteni ushahidi wenu wa wazi.” Basi wataelewa kwamba Haki ni ya Allaah (Pekee); na yamewapotea yale (yote) waliyokuwa wakiyazua. 

إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾

76. Hakika Qaaruwn alikuwa miongoni mwa watu wa Muwsaa akawakandamiza. Na Tulimpa katika hazina ambazo funguo zake zinalemea kuzibeba watu wenye nguvu. Walipomwambia watu wake: “Usifurahie Hakika Allaah Hapendi wanaofurahi (kwa kujigamba na kujifakharisha). 

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٧٧﴾

77. “Na tafuta katika yale Aliyokupa Allaah nyumba ya Aakhirah. Na wala usisahau fungu lako katika dunia (la starehe za halali). Na fanya wema (kwa waja wa Allaah) kama Alivyokufanyia Allaah wema, na wala usitake (kufanya) ufisadi ardhini. Hakika Allaah Hapendi mafisadi.” 

قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٧٨﴾

78. (Qaaruwn) Akasema: “Hakika nimepewa haya (mali) kwa sababu ya elimu yangu.” Je, hajui kwamba Allaah Amekwishahiliki kabla yake karne ambazo zilikuwa ni zenye nguvu zaidi kuliko yeye na zenye mkusanyo (wa mali na wafuasi) mwingi zaidi (kuliko yeye)? Na wala hawatoulizwa kuhusu dhambi zao wakhalifu (Kwani Allaah Anawajua vyema, hivyo wataadhibiwa bila ya kufanyiwa hesabu). 

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾

79. Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale wanaotaka (wanaopendelea na kufadhilisha) maisha ya dunia wakasema: “Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati  kubwa mno.” 

وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na Wakasema wale waliopewa elimu: “Ole wenu! Thawabu za Allaah (Aakhirah) ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.” 

فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ ﴿٨١﴾

81. Basi Tukamdidimiza yeye (Qaaruwn) na nyumba yake ardhini; basi hakikuweko kikosi chochote cha kumnusuru dhidi ya Allaah, na wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru (wenyewe). 

وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَا أَن مَّنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na wakapambaukiwa wale waliotamani mahali pake (Qaaruwn kwa aliyokuwa nayo) jana, wakisema: “Ee kumbe Allaah Humkunjulia riziki Amtakaye kati ya waja Wake na Anadhikisha (Amtakaye). Ingelikuwa Allaah Hakutufadhilisha Angelitudidimiza (pia). Ee kumbe makafiri hawafaulu!” 

تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚوَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾

83. Hiyo ni Nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa (ajili ya) wale wasiotaka kujitukuza (kwa cheo kikubwa) katika ardhi na wala (kutaka) ufisadi. Na mwisho (mwema) ni kwa wenye taqwa. 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾

84. Atakayekuja (Siku ya Qiyaamah) na jema, basi atapata bora kuliko hilo. Na atakayekuja na ovu, basi hawalipwi wale wanaotenda maovu isipokuwa yale waliyokuwa wanayatenda. 

إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨٥﴾

85. Hakika Yule Aliyekufaridhisha Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم, kufuata Shari’ah zake na kuilingania kwa wengineo) bila shaka Atakurudisha mahali pa marejeo. Sema: “Mola wangu Anamjua zaidi yule aliyekuja na Uongofu na yule aliyomo katika upotofu bayana.” 

وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na wala hukuwa unataraji kwamba utapewa Kitabu (Qur-aan) isipokuwa ni Rahmah kutoka kwa Mola wako. Basi usijekuwa msaidizi kwa makafiri. 

وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللَّـهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na wala wasikuzuie (kufuata) Aayah za Allaah baada ya kuteremshwa kwako; na lingania (watu) kwa Mola wako (wamwamini), na wala usiwe miongoni mwa washirikina. 

وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٨﴾

88. Na wala usiombe pamoja na Allaah ilaah (mungu) mwingine. Laa ilaaha illa Huwa (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa isipokuwa Yeye Pekee). Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi Wake. Ana Hukumu (ya mambo yote) na Kwake Pekee mtarejeshwa.سُورَةُ الْعَنْكَبُوت

Al-‘Ankabuwt: 29

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym.  

أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾

2. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa (bila ya misukosuko kwa kuwa) wanasema: “Tumeamini.” basi ndio wasijaribiwe? (Hapana!). 

وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾

3. Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao, ili Allaah Awatambulishe wale waliosadikisha na ili Awatambulishe waongo. 

أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ أَن يَسْبِقُونَا ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿٤﴾

4. Je, wanadhania wale wanaotenda maovu kwamba watatusabiki (waepukane na adhabu)? Uovu ulioje yale wanayohukumu. 

مَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّـهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ لَآتٍ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٥﴾

5. Anayetaraji kukutana na Allaah basi (aelewe kuwa) hakika muda uliopangwana Allaah utafika (tu) Naye ni As Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye Kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima). 

وَمَن جَاهَدَ فَإِنَّمَا يُجَاهِدُ لِنَفْسِهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾

6. Na anayefanya juhudi basi (aelewe kuwa) hakika anafanyia juhudi (kwa manufaa ya) nafsi yake. Hakika Allaah bila shaka ni Ghaniyyu (Mkwasi, Hahitaji lolote) kutokana na walimwengu. 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٧﴾

7. Na wale walioamini na wakatenda mema bila shaka Tutawafutia maovu yao, na bila shaka Tutawalipa mazuri zaidi kuliko yale waliyokuwa wakitenda. 

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۚ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

8. Na Tumemuusia binaadamu (kuwafanyia) wema wazazi wake wawili. Lakini wakikufanyia juhudi (kukulazimisha) kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii; Kwangu ni marejeo yenu, Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. 

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُدْخِلَنَّهُمْ فِي الصَّالِحِينَ ﴿٩﴾

9. Na wale walioamini na wakatenda mema bila shaka Tutawaingiza katikaAs-Swaalihiyn (watu wema). 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾

10. Na katika watu (wako) wasemao: “Tumemwamini Allaah;” lakini wanapofanyia maudhi katika (njia ya) Allaah, hufanya fitnah (mitihani ya mateso au maudhi, vituko n.k.) ya watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah. Na inapowajia nusura kutoka kwa Mola wako, bila shaka husema: “Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi.” Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifua vya walimwengu? 

وَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْمُنَافِقِينَ ﴿١١﴾

11. Na bila shaka Allaah Atatambulisha wale walioamini, na bila shaka Atawatambulisha wanafiki. 

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا اتَّبِعُوا سَبِيلَنَا وَلْنَحْمِلْ خَطَايَاكُمْ وَمَا هُم بِحَامِلِينَ مِنْ خَطَايَاهُم مِّن شَيْءٍ ۖ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٢﴾

12. Na wakasema wale waliokufuru kuwaambia walo walioamini: “Fuateni njia yetu, nasi tutabeba madhambi yenu.” Na wala wao hawatokuwa wenye kubeba chochote kile katika makosa yao. Hakika wao bila shaka ni waongo. 

وَلَيَحْمِلُنَّ أَثْقَالَهُمْ وَأَثْقَالًا مَّعَ أَثْقَالِهِمْ ۖ وَلَيُسْأَلُنَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَمَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣﴾

13. Na bila shaka watabeba mizigo yao (ya dhambi) na mizigo ya (dhambi ya kuwapoteza wengineo) pamoja na mizigo yao; na bila shaka wataulizwa Siku ya Qiyaamah kuhusu yale (yote) waliyokuwa wakiyazua. 

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٤﴾

14. Na kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa watu wake akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi ikawachukua Tufani nao ni madhalimu. 

فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٥﴾

15. Basi Tukamuokoa na watu wa jahazi, na Tukaifanya kuwa ni Aayah kwa walimwengu. 

وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾

16. Na (kumbusha pale) Ibraahiym alipowaambia watu wake: “Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua. 

إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ ۖ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١٧﴾

17. “Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah (hawana uwezo) wa kukumilikiini riziki; basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni (Yeye) na mshukuruni, Kwake mtarejeshwa. 

وَإِن تُكَذِّبُوا فَقَدْ كَذَّبَ أُمَمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ۖ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿١٨﴾

18. Na mkikadhibisha (ujumbe enyi watu), basi umati za kabla yenu zilikwishakadhibisha. Na si juu ya Mtume (jukumu lolote lile) isipokuwa ubalighisho bayana (wa ujumbe).” 

أَوَلَمْ يَرَوْا كَيْفَ يُبْدِئُ اللَّـهُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴿١٩﴾

19. Je, hawaoni jinsi Allaah Anavyoanzisha uumbaji kisha Anaurudisha? Hakika hayo kwa Allaah ni sahali. 

قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ ۚ ثُمَّ اللَّـهُ يُنشِئُ النَّشْأَةَ الْآخِرَةَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾

20. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Nendeni katika ardhi, na mtazame jinsi (Allaah) Alivyoanzisha uumbaji; kisha Allaah Ataanzisha umbo la Aakhirah. Hakika Allaah daima juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza). 

يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَن يَشَاءُ ۖ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ ﴿٢١﴾

21. “Anamuadhibu Amtakaye, na Anamrehemu Amtakaye; na Kwake mtarudishwa. 

وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿٢٢﴾

22. “Nanyi si wenye kushinda ardhini (kuzuia adhabu ya Allaah) na wala (si wenye kushinda pia) mbinguni Na hamna badala ya Allaah walii yeyote wala mwenye kunusuru yeyote.” 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَلِقَائِهِ أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٣﴾

23. Na wale waliozikanusha Aayah za Allaah na (pia wakakanusha) kukutana Naye, hao wamekata tamaa na Rahmah Yangu, na hao watapata adhabu iumizayo. 

فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا اقْتُلُوهُ أَوْ حَرِّقُوهُ فَأَنجَاهُ اللَّـهُ مِنَ النَّارِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٤﴾

24. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Muuweni, au muunguzeni.” Basi Allaah Akamuokoa na Moto. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaoamini. 

وَقَالَ إِنَّمَا اتَّخَذْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا مَّوَدَّةَ بَيْنِكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُ بَعْضُكُم بِبَعْضٍ وَيَلْعَنُ بَعْضُكُم بَعْضًا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٥﴾

25. Na (Ibraahiym) akasema: “Hakika mmefanya badala ya Allaah masanamu kuwa ni mapenzi makubwa baina yenu katika maisha ya dunia, kisha Siku ya Qiyaamah mtakanushana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana wenyewe kwa wenyewe; na makazi yenu ni Moto, na hamtokua na mwenye kunusuru.” 

فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ ۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٦﴾

26. Basi Luwtw akamwamini; na (Ibraahiym) akasema: “Hakika mimi nahajiri kwa Mola wangu; hakika Yeye Ndiye Al-’Aziyzul-Hakiym  (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima). 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ وَآتَيْنَاهُ أَجْرَهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾

27. Tukamtunukia (mtoto) Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb, na Tukajaalia katika dhuria wake Unabii na Kitabu; na Tukampa ujira wake duniani, na hakika yeye katika Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa waja wema. 

وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾

28. Na Luwtw alipowaambia watu wake: “Hakika nyinyi mnaendea uchafu (wa liwati) ambao hakuna yeyote aliyekutangulieni (kufanya) hayo katika walimwengu. 

أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ وَتَقْطَعُونَ السَّبِيلَ وَتَأْتُونَ فِي نَادِيكُمُ الْمُنكَرَ ۖ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتِنَا بِعَذَابِ اللَّـهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٢٩﴾

29. Je, nyinyi mnawaendea wanaume na mnakata njia (za wasafiri kwa kuwaua na kuwaibia), na mnafanya katika vilabu vyenu (mikusanyiko yenu) munkari? Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: “Tuletee adhabu ya Allaah ukiwa ni miongoni mwa wakweli.” 

قَالَ رَبِّ انصُرْنِي عَلَى الْقَوْمِ الْمُفْسِدِينَ ﴿٣٠﴾

30. (Luwtw) Akasema: “Mola wangu! Ninusuru dhidi ya watu mafisadi.” 

وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا إِنَّا مُهْلِكُو أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ ۖ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا ظَالِمِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Wajumbe Wetu (Malaika) walipomjia Ibraahiym kwa bishara (kuwa atamzaa Is-haaq); walisema: “Hakika sisi tutawahiliki watu wa mji huu. Hakika watu wake wamekuwa madhalimu.” 

قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٢﴾

32. (Ibraahiym) Akasema: “Hakika humo yumo Luwtw.” (Malaika) Wakasema: “Sisi tunajua zaidi waliokuwemo humo; tutamuokoa na ahli zake isipokuwa mke wake amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.” 

وَلَمَّا أَن جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ ۖ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا امْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luwtw aliwasikitikia, na akadhikika na kukosa raha kwa ajili yao; (Malaika) wakasema: “Usikhofu na wala usihuzunike; hakika sisi tutakuokoa na ahli zako isipokuwa mke wako amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.” 

إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰ أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٣٤﴾

34. Hakika Sisi Tutawateremshia juu ya watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya ule ufasiki waliokuwa wanafanya. 

وَلَقَد تَّرَكْنَا مِنْهَا آيَةً بَيِّنَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٣٥﴾

35. Na kwa yakini Tuliacha humo Aayah bayana kwa watu wanaotia akilini. 

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَارْجُوا الْيَوْمَ الْآخِرَ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٣٦﴾

36. Na kwa (watu wa mji wa) Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb, akasema: “Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, na tarajieni Siku ya Aakhirah, na wala msifanye uovu katika ardhi kuwa mafisadi.” 

فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٣٧﴾

37. Wakamkadhibisha, likawachukuwaAr-Rajfah (tetemeko kali la ardhi) wakapambaukiwa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi (wamekufa). 

وَعَادًا وَثَمُودَ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَاكِنِهِمْ ۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَكَانُوا مُسْتَبْصِرِينَ ﴿٣٨﴾

38. Na (Tuliwaangamiza pia kina) ‘Aad na Thamuwd; na yamekwishakubainikieni masikani yao; na shaytwaan aliwapambia ‘amali zao (mbovu na chafu), akawazuia na njia (ya haki na kheri), na walikuwa ni wenye kumaizi (na kutambua vizuri). 

وَقَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانُوا سَابِقِينَ ﴿٣٩﴾

39. Na (Tuliwaangamiza pia kina) Qaaruwn, na Fir’awn, na Haamaan; na kwa yakini aliwajia Muwsaa kwa hoja bayana wakatakabari katika ardhi, lakini hawakuwa wenye kushinda. 

فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ وَمِنْهُم مَّنْ أَغْرَقْنَا ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٠﴾

40. Basi kila mmoja Tulimchukua kwa (sababu ya) dhambi yake; miongoni mwao (wako) wale Tuliowapelekea tufani; na miongoni mwao (wako) wale waliochukuliwa Asw-Swayhah (ukelele wa kishindo unaoangamiza kutoka mbinguni); na miongoni mwao (wako) wale Tuliowadidimizia ardhi; na miongoni mwao (wako) wale Tuliowagharikisha. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe. 

مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا ۖوَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ ۖ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾

41. Mfano wa wale waliochukua badala ya Allaah awliyaa (walinzi, wasaidizi) ni kama mfano wa buibui alivyojichukulia (alivyojitandia) nyumba (yake ili imhifadhi nayo haimhifadhi lolote), na bila shaka nyumba iliyo dhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui, lau wangelikuwa wanajua! 

إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤٢﴾

42. Hakika Allaah Anavijua vitu (vyote) vile wanavyoviomba badala Yake, Naye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikmah wa yote daima).  

وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ﴿٤٣﴾

43. Na hiyo (ni) mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye elimu. 

خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٤﴾

44. Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Hakika katika hayo ni (kuna) Aayah kwa Waumini.  

اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾

45. Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahyi kwako katika Kitabu (Qur-aan) na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka dhikri ya Allaah ni (jambo) kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale (yote) mnayoyatenda. 

Report Page