Juzuu Ya 1 – Alif Laam Miym Dhaalikal-Kitaab

Juzuu Ya 1 – Alif Laam Miym Dhaalikal-Kitaab



Juzuu: 1


الم ذَلِكَ الْكِتَابُ


  سُورَةُ الْبَقَرَة  


Al-Baqarah:  2


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


 الم ﴿١﴾


1. Alif Laam Miym.

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾


2. Hicho (Hiki) ni Kitabu kisicho na shakandani yake, ni Hudan (Uongofu) kwa Muttaqiyn (wamchao Allaah).

 الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾


3. Ambao huaminiya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.

 وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾


4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenyeyakini na Aakhirah.

 أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾


5. Hao wako juu ya Hudan (Uongofu) kutoka kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu.

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾


6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.

خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾


7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana kifuniko; na watapata adhabu kubwa.

 وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾


8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Aakhirah” hali ya kuwa si wenye kuamini.

يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾


9. Wanamhadaa Allaah na wale walioamini na hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi.

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾


10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.

 وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾


11. Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi”. Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”

 أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾


12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾


13. Na wanapoambiwa: “Aminini kama walivyoamini watu”. Husema: “Je, tuamini kama walivyoamini masafihi.” Tanabahi! Hakika wao ndio masafihi lakini hawajui.

 وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾


14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: “Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.”

 اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾


15. Allaah Anawadhihaki wao (kuwalipiza istihzai zao) na Atawaendeleza katika hali yao ya ukiukaji mipaka wakitangatanga ovyo.

 


 أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾


16. Hao ndio wale walionunua upotofu kwa Al-Hudaa (Uongofu). Basi haikupata tija (faida) biashara yao na wala hawakuwa wenye kuongoka.

 مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾


17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza hawaoni.

 صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾


18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea (katika njia iliyonyooka).

 أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾


19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakihofu mauti, na Allaah ni Muhiytw (Mwenye kuzunguka kwa Ujuzi Wake)makafiri.

يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾


20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) huenda ndani yake, na unapowafanyia kiza husimama; na lau Allaah Angelitaka basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah ni Qadiyr (Muweza) wa kila kitu.

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾


21. Enyi watu! mwabuduni Mola wenu Ambae Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾


22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).

 وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾


23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni Swaadiqiyn (wakweli).

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾


24. Na msipofanya, na wala hamtaweza kufanya, basi ogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, ulioandaliwa makafiri.

 وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾


25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Mabustani yapitayo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa (matunda) hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotwaharishwa, nao humo (Peponi) watadumu milele.

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾


26. Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini huelewa kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Mola wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” (Allaah) Huwapoteza kwa mfano huu wengi na Huwahidi kwa mfano huu wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki.

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾


27. Wale ambao wanavunja Ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanayakata Aliyoamrisha kwayo Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾


28. Vipi mnamkanusha Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾


29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Istawaa (Akalingamana inavyolingana na Utukufu Wake) kuzielekea mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye ni ‘Aliym (Mjuzi) wa kila kitu.

 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾


30. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Mola wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi Khaliyfah.” Wakasema: “Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabbih (tunakutakasa) kwa Himdi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako?”Akasema: “Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.”

 وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾


31. Na Akamfunza Aadam majina ya vitu vyote kisha Akayaonyesha mbele ya Malaika; Akasema: “Niambieni majina ya haya mkiwa ni Swaadiqiyn (wakweli).”

 قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾


32. Wakasema: “Sub–haanak (Utakaso ni Wako!)! Hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe ni Al-‘Aliymul-Hakiym” (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima).

 


 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾


33. Akasema: “Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao.” Basi alipowatajia majina yao; Akasema (Allaah): “Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghaibu ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha.

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾


34. Na (taja) Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾


35. Na Tukasema: “Ee Aadam, kaa wewe na mkeo Jannah na kuleni humo (Peponi) maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu.”

 فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾


36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: “Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalum.”

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾


37. Kisha Aadam akapokea maneno (fulani) kutoka kwa Mola wake; na (Mola wake) Akapokea tawbah yake, hakika Yeye Ndiye at-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye kurehemu).

 قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾


38. Tukasema: “Shukeni kutoka humo nyote. Utakapokufikieni kutoka Kwangu Hudan (Uongofu), ye yote atakayefuata Hudaa (Uongofu) Wangu hakutakuwa na khofu juu yao wala hawatahuzunika.”

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾


39. Na wale waliokufuru na wakazikanusha Aayah Zetu; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) hao ni watu wa Motoni, wao humo watadumu milele.

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾


40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na timizeni Ahadi Yangu Nikutimizie ahadi yenu na Mimi (pekee) niogopeni .

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾


41. Na aminini Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wa kuyakanusha; na wala msiuze Aayah Zangu kwa thamani ndogo na Mimi tu nicheni.

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾


42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua.

 وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾


43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika ‘ibaadah na utiifu).

أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾


44. Je, mnaamrisha watu (watende) mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu; je hamtii akilini?

 


 وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾


45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa Al-Khaashi’iyn (wanyenyekevu).

الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾


46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao watakutana na Mola wao na hakika wao Kwake watarejea.

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾


47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nikakufadhilisheni juu ya Al-‘aalamiyn (walimwengu wote).

وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾


48. Iogopeni Siku ambayo nafsi haitaifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitakubaliwa kutoka kwake shafaa’ah (maombezi), na wala hakitachukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatanusuriwa.

 وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾


49. Na (kumbukeni) Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Fir’awn walipokupeni mateso mabaya, wakiwachinja watoto wenu (wachanga wa kiume), na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Mola wenu.

 


وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾


50. Na (kumbukeni) Tulipoitenganisha bahari (ikawa sehemu mbili) kwa ajili yenu; Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Fir’awn na huku nyinyi mnatazama.

وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾


51. Na (kumbukeni) Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada ya kuondoka kwake na mkawa madhalimu.

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾


52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo mpate kushukuru.

وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾


 53. Na (kumbukeni) Tulipompa Muwsaa Kitabu na Al-Furqaan (Pambanuo baina ya haki na ubatilifu, uongofu na upotofu) huenda mpate kuongoka.

 وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾


54. Na (kumbukeni wakati) Muwsaa alipowaambia qawm yake: “Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kumchukua kwenu ndama, basi tubuni kwa Baariu (Muumbaji) wenu; (namna ya kutubu kwenyewe) ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Baariu wenu”. Akapokea tawbah yenu; hakika Yeye Ndiye At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa Kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye kurehemu).

وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾


55. Na (kumbukeni) mliposema: “Ewe Muwsaa! Hatutakuamini mpaka tumuone Allaah waziwazi”; ikakunyakueni Asw–Swaa’iqah (adhabu ya mngurumo wa mauti ya ghafla) nanyi mnatazama.

ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾


56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu mpate kushukuru.

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾


57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu (mlipokuwa mnasafiri jangwani mkitoka Misri),na Tukakuteremshieni Al-Manna na As-Salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika twayyibaat (halaal na vizuri) Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi walakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾


58. Na (kumbukeni) Tuliposema: “Ingieni mjii huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango (wake) huku mmeinama (kwa unyenyekevu) na semeni (wakati wa kuingia) “Hittwah (tuondolee uzito wa madhambi yetu)”; Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (neema na thawabu) Al-Muhsiniyn (watendao wema).

 


 فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾


59. Wakabadilisha wale ambao wamedhulumu kauli kwa kauli isiyokuwa (wakasema kauli tofauti na) ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.

 


 وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾


60. Na (kumbukeni wakati) Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya Qawm yake. Tukasema: “Piga kwa fimbo yako jiwe.” Zikachimbuka (na kububujika) kutoka kwalo chemchem kumi na mbili. Kila watu (kabila) wakaelewa kinywaji chao. Kuleni na kunyweni kutokana na riziki ya Allaah na wala msifanye uovu katika ardhi kwani mtakuwa mafisadi.

 وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾


61. Na (kumbukeni) mliposema: “Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula (cha aina) kimoja, tuombee kwa Mola Wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake.” Akasema (Muwsaa): “Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora?Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza”. Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) na wakiwaua Manabii bila ya haki; hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wanataadi (wanapindukia mipaka).

 إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾


62. Hakika wale ambao wameamini, na wale ambao ni Mayahudi, na Manaswara na Swaabiiyna; yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Aakhirah, na akatenda mema basi watapata ujira wao kutoka kwa Mola wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾


63. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (mtekeleze yaliyo katika Tawraat)na Tukaunyanyua juu yenu  at-Twuwr (Mlima au mlima wa At-Twuwr, Tukasema): “Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu (azimio la kweli) na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.”

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾


64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si fadhila za Allaah juu yenu na Rahmah Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾


65. Na kwa yakini mnaelewa (khabari za) wale ambao walikiuka mipaka miongoni mwenu katika Sabato (Shari’ah ya Jumamosi kupumzika kazi na kufanya ‘ibaadah tu) Tukawaambia: “Kuweni manyani waliotezwa (hakiri).”

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾


66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja nyuma (baada) yao na maw’idhwah (funzo) kwa Muttaqiyn (wamchao Allaah).

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾


67. Na (kumbukeni) Muwsaa alipowaambia Qawm yake: Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakasema: “Unatufanyia mzaha?” Akasema: “Najikinga kwa Allaah kuwa miongoni mwa wajinga.

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾


68. Wakasema: “Tuombee kwa Mola wako Atubainishie ni ngo’mbe wa aina gani huyo?” Akasema (Muwsaa): “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe wenyewe si mpevu (si mzee) wala si mchanga, bali ni wa (kati na kati) baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.”

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾


69. Wakasema: “Tuombee kwa Mola wako Atubainishie rangi yake?” Akasema (Muwsaa): “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.”

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾


Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈






Report Page