JUZUU
قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: “Tuombee Mola wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah tutakuwa wenye kuongoka.”
قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾
71. Akasema: (Muwsaa): ”Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa; kwa kulima ardhi wala kwa kumwagilia (maji) shamba; ni kamilifu (yu safi) hana dosari.” Wakasema: “Sasa umekuja na haki”. Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo (kuchinja).
وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na (kumbukeni) mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah ni Mtoaji (Mfichuaji) wa hayo mliyokuwa mkiyaficha.
فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾
73. Tukasema: “Mpigeni (huyo maiti) kwa baadhi ya sehemu yake (huyo ng’ombe).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayah Zake; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) huenda mkatia akilini.
ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾
74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, (zikawa) kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna yanayobubujika ndani yake mito. Na hakika katika hayo (mawe) kuna yanayopasuka yakatoka ndani yake maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na hofu ya Allaah. Na Allaah si Mwenye kughafilika na myatendayo.
أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾
75. Je, mnatumai (enyi Waumini) kwamba watakuamininina hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha wakayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?
وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾
76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: “Tumeamini”. Na wanapokuwa peke yao; wao kwa wao; husema: “Mnawasimulia Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Mola wenu; hamtii akilini?”
أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾
77. Je, hawaelewi kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?
وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾
78. Na miongoni mwao wako ummiyyuwn (wasioelewa kusoma wala kuandika); hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhani tu.
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾
79. Basi ole wao wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Haya ni kutoka kwa Allaah” ili wachume kwayo thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa wanayoyachuma.
وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na walisema: “Hautatugusa Moto ila siku chache tu”. Sema: “Je, mmechukua ahadi kwa Allaah?” Basi Allaah Hakhalifu Ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?
بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾
81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa Motoni, wao humo watadumu milele.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na wale ambao wameamini na wakatenda mema; hao ni watu wa Jannah, wao humo (Peponi) watadumu milele.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾
83. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi (fungamano) ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie wema wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾
84. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (Tukawaambia): “Msimwage damu zenu, wala msitoe nafsi zenu kutoka miji yenu;” kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.
ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾
85. Kisha nyinyi ndio hao mnaua nafsi zenu na mnalitoa kundi miongoni mwenu kutoka miji (majumbani) yao, mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui; na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo limeharamishwa kwenu kuwatoa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye (katika) adhabu kali zaidi, na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾
86. Hao ndio wale ambao wamenunua uhai wa dunia kwa Aakhirah, basi haitopunguzwa kwao adhabu wala hawatanusuriwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾
87. Na kwa hakika Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Mitume baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Je basi kila anapokujieni Mtume (enyi wana wa Israaiyl) kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; basi kundi (la Mitume) mlikadhibisha na kundi (jengine) mnawaua.
وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na wakasema: “Nyoyo zetu zimefunikwa.” Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao; basi machache tu wanayoyaamini.
وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾
89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yaliyo pamoja nao, na (japokuwa) kabla ya (hapo) walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale ambao wamekufuru; basi yalipowajia waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah juu ya wakanushaji.
بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾
90. Ubaya ulioje wa yale waliyojichumia nafsi zao kwamba wakanushe Aliyoyateremsha Allaah kwa ajili ya chuki kwa kuwa Allaah Kateremsha katika fadhila Zake juu ya Amtakae katika waja Wake. Basi wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾
91. Na wanapoambiwa: “Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah”, husema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yaliyokuja nyuma (baada) yake, na hali ya kuwa hayo (wanayoyakanusha) ni haki yenye kusadikisha yaliyo pamoja nao. Sema: “Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah toka hapo kabla kama kweli mlikuwa waumini (wa kweli)?
وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na kwa hakika alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamchukua ndama baada yake na hali ya kuwa nyinyi ni madhalimu.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾
93. Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi yenu (mtekeleze Tawraat) na Tukaunyanyua juu yenu at-Twuwr (mlima au mlima wa at-Twuwr). (Tukasema): “Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni”. Wakasema: ”Tumesikia na tumeasi.” Wakanyweshwa katika nyoyo zao ndama (mapenzi ya kumuabudu) kwa kufuru yao. Sema: “Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imani yenu mkiwa ni waumini (wa kweli).”
قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾
94. Sema (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): ”Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine; basi tamanini mauti mkiwa ni Swaadiqyn (wakweli).
وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾
95. Na hawatoyatamani kamwe (hayo mauti) kutokana na yaliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah ni ‘Aliymun (Mjuzi wa yote daima) wa madhalimu.
وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa mno kuliko yeyote juu ya uhai na kuliko wale ambao wameshirikisha. Anapenda mmoja wao lau angelipewa umri mrefu wa miaka elfu. Na wala huko hakutamuondoshea adhabu kwa kupewa umri mrefu. Na Allaah ni Baswiyrun (Mwenye kuona yote daima) wanayoyatenda.
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾
97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na Hudan (Uongofu), na bishara kwa Waumini.
مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾
98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Mitume Wake, na Jibriyl, na Mikaaiyl, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.
وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na kwa hakika Tumeteremsha kwako Aayah bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.
أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je, ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja? Bali wengi wao hawaamini.
وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾
101. Na alipowajia Mtume kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao kundi miongoni mwa wale ambao wamepewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui (yaliyomo humo).
وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Na wakafuata yale waliyoyasoma shayaatwiyn (mashetani) juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru walakini shayaatwiyn ndio waliokufuru; wanafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili (katika mji wa) Baabil Haaruwt na Maaruwt. Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni fitnah (mtihani), basi usikufuru (kufanya uchawi).” Basi wakajifunza kutoka kwa hao (Malaika) wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao si wenye kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa hakika walielewa kwamba atakayenunua (atayefanya biashara ya uchawi) hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichouzia kwayo nafsi zao, lau wangelikuwa wanaelewa.
وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Na lau wangeliamini na wakawa na taqwa, basi malipo kutoka kwa Allaah yangekuwa ni kheri (kwao), lau wangekuwa wanajua.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٠٤﴾
104. Enyi mlioamini, msiseme (kumwambia Mtume wa Allaah) “raa’inaa” lakini semeni “un-dhwur-naa” na sikilizeni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.
مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿١٠٥﴾
105. Hawapendi wale ambao wamekufuru miongoni mwa Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara), wala washirikina kwamba iteremshwe kwenu kheri yoyote ile kutoka kwa Mola wenu. Na Allaah Humkhusisha kwa Rahmah Yake Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye fadhila kuu.
مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾
106. Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake. Je, huelewi kwamba Allaah ni Qadiyr (Muweza Daima) wa kila kitu?
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٠٧﴾
107. Je, huelewi kwamba Allaah Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru (na msaidizi).
أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٠٨﴾
108. Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Muwsaa hapo kabla? Na yeyote atakayebadilisha iymaan kwa kufru, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.
وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾
109. Wengi katika Ahlil-Kitaab (Mayahudi na Manaswaara) wametamani lau wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri (kutokana na) husuda iliyomo katika nafsi zao; baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na achilieni mbali (puuzeni); mpaka Allaah Alete Amri Yake. Hakika Allaah ni Qadiyr (Muweza Daima) wa kila kitu.
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾
110. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na lolote mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu katika kheri mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa myafanyao ni Baswiyr (Mwenye kuona yote daima).
وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾
111. Na walisema: “Hatoingia Peponi isipokuwa aliyekuwa Yahudi au Naswaara.” Hilo ni tamanio lao. Sema: “Leteni burhaan (ushahidi wa wazi) wenu mkiwa ni Swaadiqiyn (wasemao kweli).”
بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١١٢﴾
112. Naam! Yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali ni Muhsin, (mtenda mema) basi atapata ujira wake kwa Mola wake, na wala haitokuwa khofu juu yao wala hawatohuzunika.
وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١١٣﴾
113. Na Mayahudi wakasema: “Manaswaara hawana lao jambo.” Na Manaswaara wakasema: “Mayahudi hawana lao jambo,” na hali wao wanasoma Kitabu. Hivyo hivyo ndivyo walivyosema wale ambao hawaelewi mfano wa kauli yao. Basi Allaah Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾
114. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayezuia Misikiti ya Allaah kutajwa Jina Lake na akajitahidi katika kuiharibu? Hao haitokuwa kuingia kwako humo isipokuwa wakiwa ni wenye khofu; watapata duniani hizaya na Aakhirah watapata adhabu kubwa.
وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾
115. Na ni (milki) ya Allaah Mashariki na Magharibi; basi popote mnapogeuka kuna Wajhu Allaah. Hakika Allaah ni Waasi’un-‘Aliym (Mwenye Wasaa, Mkunjufu – Mjuzi wa yote daima).
وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾
116. Na wakasema: “Allaah Amejichukulia mwana.” Subhaanah! (Ametakasika!) Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.
بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾
117. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia “Kun” (kuwa) basi nalo huwa.
وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿١١٨﴾
118. Na wakasema wale ambao hawaelewi: “Lau Angetusemesha Allaah au ingetujia Aayah (muujiza);” kadhalika walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimeshabihiana nyoyo zao. Kwa yakini Tumekwisha bainisha Aayah kwa watu wenye yakini.
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ ﴿١١٩﴾
119. Hakika Tumekutuma kwa Haki ukiwa mwenye kutoa bishara njema na mwonyaji wala hutaulizwa kuhusu watu wa Jahiym (motoni).
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾
120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswaara mpaka ufuate mila zao. Sema: “Hakika Hudaa (Uongofu) wa Allaah ndio Al-Hudaa (Uongofu pekee)”. Na ukifuata matamanio yao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾
121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ya kukisoma kwake (ipasavyo); hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٢٢﴾
122. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya Al–‘aalamiyn (walimwengu wote).
وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa lolote, wala haitokubaliwa kutoka kwake kikomboleo wala haitamfaa shafaa’ah (maombezi) wala hawatonusuriwa.
وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾
124. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Alipojaribiwa Ibraahiym na Mola wake kwa kalimaat (maneno), naye akazitimiza. Akasema (Allaah): “Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam (kiongozi) kwa watu.” Akasema (Ibraahiym): “Na katika dhurriyah (kizazi) wangu.” Akasema (Allaah): “Haiwafikii Ahadi Yangu madhalimu.”
وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾
125. Na (taja) Tulipoifanya Nyumba kuwa ni mahali pa kurejewa (kuendewa) na watu na (mahali pa) amani, na chukueni kutoka mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni muswallaa (pahala pa kuswalia). Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itwaharisheni (itakaseni) Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٢٦﴾
126. Na (taja) aliposema Ibraahiym: “Mola wangu Ufanye mji huu kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Aakhirah.” Akasema (Allaah): “Na atakayekufuru pia Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya moto, na ubaya ulioje wa mahali pa mwisho kurejea.”
وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾
127. Na (taja) aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’abah); (wakaomba): “Mola wetu, Takabali kutoka kwetu, hakika Wewe ni as-Samiy’ul-’Aliym (Mwenye kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾
128. “Mola wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na dhurriyah (kizazi) wetu wawe Ummah wenye kujisalimisha Kwako na Tuonyeshe manaasik (taratibu za ‘ibaadah) zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe ni at-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye kurehemu).
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾
129. “Mola wetu, Peleka kwao Mtume miongoni mwao ataewasomea Aayah Zako na ataewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikma wa yote daima).”
وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Na nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayejitia usafihi nafsi yake? Na kwa yakini Tumemchagua duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa Asw–Swaalihiyn (waja wema).
إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾
131. Mola wake Alipomwambia: “Jisalimishe.” Akasema (Ibraahiym): “Nimejisalimisha kwa Mola wa Al-‘aalamiyna (walimwengu wote)”
وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na (kadhalika) Ya’quwb (akawaambia): “Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekuchagulieni nyinyi Dini; basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.”
أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾
133. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: “Mtaabudu nini baada yangu?” Wakasema: “Tutamwabudu Ilaah wako (Allaah: Mungu Anayestahiki kuabudiwa kwa haki) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja nasi Kwake tunajisalimisha.”
تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٤﴾
134. Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, una uliyoyachuma nanyi mna mliyoyachuma; na wala hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakitenda.
وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾
135. Na wakasema: “Kuweni Mayahudi au Manaswaara mtaongoka.” Sema: “Bali (Sisi hatuna haja ya kuwa Mayahudi wala Manaswaara kama mnavyotulingania kuwafuata) mila ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki) na wala hakuwa katika washirikina.”
قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾
136. Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatufarikishi (hatutofautishi) baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.”
فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾
137. Basi wakiamini kama vile mlivyoyaamini nyinyi (Swahaba), basi kwa hakika watakuwa kweli wameongoka; na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao, Naye ni As-Samiy’ul-’Aliym (Mwenye kusikia yote daima – Mjuzi wa yote daima).
صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ ﴿١٣٨﴾
138. (Swib-ghah yetu; Dini yetu ni) Swib-ghata Allaahi (Dini ya Allaah) na Swib-ghah gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Swib-ghah ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye pekee.
قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّـهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ ﴿١٣٩﴾
139. Sema: “Je mnahojiana nasi kuhusu Allaah na hali Yeye ni Mola wetu na Mola wenu; nasi tuna ‘amali zetu nanyi mna ‘amali zenu, na sisi Kwake ni mukhliswuwn (wenye ikhlaas kwa nia na vitendo).“
أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ قُلْ أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّـهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾
140. Je, mnasema (mnadai) kwamba Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (vizazi) walikuwa Mayahudi au Manaswaara? Sema: “Je nyinyi mnajua zaidi au Allaah?” Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao kutoka kwa Allaah? Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa wayatendayo.
تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤١﴾
141. Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, una uliyoyachuma nanyi mna mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.