JUZUU

JUZUU


Juzuu 4


رَّ

لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾

92. Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe (katika njia ya Allaah) katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima). كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٣﴾

 

93. Kila chakula kilikuwa halaal kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl (Ya’quwb) juu ya nafsi yake mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa Swaadiqiyn (wakweli.”)فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩٤﴾

 

94. Na yeyote atakayemzulia Allaah uongo baada ya hayo; basi hao ndio madhalimu.قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾

 

95. Sema: “Allaah Amesema kweli.” Basi fuateni mila ya Ibraahiym haniyfaa  (aliyejiengua na dini potofu akaelemea Dini ya haki), na hakuwa miongoni mwa washirikina.إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾

 

96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye baraka na Hudan (Uongofu) kwa Al-‘aalamiyna (walimwengu).فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾

 

97. Ndani yake kuna Aayaat (Ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni Ghaniyy(Mkwasi, Hahitaji lolote) kwa Al-‘aalamiyna(walimwengu). قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٨﴾

 

98. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Kwa nini mnakanusha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) na hali Allaah ni Shahiyd (Shahidi, Mwenye Kushuhudia, Kujua vyema) kwa myatendayo?”قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾

 

99. Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! (Mayahudi na Manaswaara) Kwanini mnamzuilia aliyeamini njia ya Allaah mnaitafutia upotofu na hali nyinyi mashahidi (juu ya ukweli)? Na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.” يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا فَرِيقًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ ﴿١٠٠﴾

 

100. Enyi mlioamini! Mkitii kundi la waliopewa Kitabu watakurudisheni baada ya kuamini kwenu muwe makafiri. وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّـهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِاللَّـهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٠١﴾

 

101. Na vipi mkufuru na hali mnasomewa Aayah za Allaah na hali Mtume yuko kati yenu? Na atakayeshikamana na Allaah basi kwa yakini ameongozwa kwenye Swiraatwil-Mustaqiym (njia iliyonyooka).يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Enyi mlioamini! Muogopeni Allaah kama apasavyo kuogopwa wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu (mliojisalamisha Kwake).وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾

 

103. Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni Neema ya Allaah kwenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa Neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayah Zake mpate kuongoka.وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

 

104. Na uweko (watokeze) kutoka kwenu Ummah unaolingania kheri na unaoamrisha ma’aruwf(Uislamu, mema) na unaokataza munkari (maovu). Na hao ndio waliofaulu.وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾

 

105. Na wala msiwe kama wale ambao walifarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu. يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾

 

106. Siku nyuso zitanawiri na zitasawajika nyuso. Basi wale ambao nyuso zao zitasawijika (wataambiwa): “Je mlikufuru baada ya kuamini kwenu?! Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkikufuru.” وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾

 

107. Na wale ambao nyuso zao zitanawiri; watakuwa katika Rahmah ya Allaah (Peponi), wao humo watadumu.تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۗ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٨﴾

 

108. Hizi ni Aayah za Allaah Tunakusomea kwa haki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Hataki dhulma kwa Al-‘Aalamiyna (walimwengu). وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿١٠٩﴾

 

109. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na kwa Allaah Pekee mambo yote yatarejeshwa. كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

 

110. Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha ma’aruwf (Uislamu, mema) na mnakataza munkari (maovu) na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara) ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao ni Waumini na wengi wao ni mafasiki. لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى ۖ وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١١١﴾

 

111. Hawatokudhuruni isipokuwa udhia tu, na wakikupigeni vita watakupeni migongo, kisha hawatonusuriwa.ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾

 

112. Wamepigwa na udhalili (kutoka kwa Allaah), popote wanapopatikana isipokuwa kamba (mapatano) ya Allaah na kamba ya watu na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, na wakapigwa na umasikini. Hivyo kwa kuwa walikuwa wakikanusha Aayah za Allaah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) na wakiua Manabii pasi na haki. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi (wakipindukia mipaka).لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

 

113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara, wako) watu wenye kusimama (kama itakiwavyo) wanasoma Aayah za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

 

114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Aakhirah na wanaamrisha ma’aruwf (Uislamu, mema) na wanakataza munkari (maovu) na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Asw-Swaalihiyn (watu wema). وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

 

115. Na kheri yoyote waifanyayo hawatakanushwa nayo (hawatanyimwa thawabu yake). Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa Al-Muttaqiyn(wamchao Allaah).إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖوَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١٦﴾

 

116. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao na wala watoto wao mbele ya Allaah; na hao ni watu wa motoni watadumu humo milele.مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١١٧﴾

 

117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai wao huu wa duniani ni kama mfano wa upepo ndani yake mna baridi ya barafu, ukalisibu shamba la watu waliojidhulumu nafsi zao ukaliteketeza. Na Allaah Hakuwadhulumu lakini wamejidhulumu nafsi zao. يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

 

118. Enyi mlioamini! Msichukue rafiki mwandani (msiri wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayah; (Wahyi, Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) mkiwa mtatia akilini.هَا أَنتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١١٩﴾

 

119. Hivi nyinyi ndio wale mnaowapenda na wala wao hawakupendeni, na mnaamini Kitabu chote; na wanapokukuteni husema: “Tumeamini” na wanapokuwa peke yao wanakutafunieni ncha za vidole kutokana na chuki. Sema: “Kufeni kwa chuki zenu.” Hakika Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa yaliyomo vifuani.إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾

 

120. Ikikuguseni zuri (kheri) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia; na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao. Hakika Allaah kwa wayatendayo ni Muhiytw (Mwenye Kuzunguka vyote kwa ujuzi Wake).وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٢١﴾

 

121. Na (kumbuka ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) pale ulipotoka asubuhi mapema ukaacha ahli zako uwapange Waumini vituo vya kupigana (vita vya Uhud). Na Allaah ni Samiy‘un-‘Aliym(Mwenye Kuona yote daima – Mjuzi wa yote daima). إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾

 

122. Pale walipofanya wasiwasi makundi mawili miongoni mwenu kwamba watashindwa na Allaah ni Walii wao; basi kwa Allaah pekee na watawakali Waumini. وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾

 

123. Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika (vita vya) Badr na hali nyinyi mlikuwa dhalili. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru. إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَن يَكْفِيَكُمْ أَن يُمِدَّكُمْ رَبُّكُم بِثَلَاثَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُنزَلِينَ ﴿١٢٤﴾

 

124. (Kumbuka) Pale ulipowaambia Waumini: “Je, haikutosheni ikiwa Mola wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?” بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴿١٢٥﴾

 

125. Ndio! Mkisubiri mkawa na taqwa na wakakujieni kwa ghafla hivi (kukutekeni); Mola wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tano waliotiwa alama (ya ubora). وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِ ۗ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١٢٦﴾

 

126. Na hakujaalia hayo Allaah isipokuwa ni bishara kwenu na ili zitue nyote zenu kwayo. Na hakuna naswr(ushindi) isipokuwa kutoka kwa Allaah ‘Aziyzil-Hakiym(Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika daima – Mwenye Hikma wa yote daima).لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا خَائِبِينَ ﴿١٢٧﴾

 

127. Ili ikate sehemu ya waliokufuru (Awaue) au awatahayarishe, warudi nyuma wakiwa wamevunjika moyo. لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

128. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika jambo kuamua lolote; (bali ni juu ya Allaah) au Apokee tawbah yao, au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٩﴾

 

129. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi Wa Kughufiri – Mwenye Kurehemu)يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٣٠﴾

 

130. Enyi mlioamini! Msile ribaa mkizidisha maradufu juu ya maradufu. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿١٣١﴾

 

131. Na uogopeni moto ambao umeandaliwa kwa makafiri. وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

 

132. Na mtiini Allaah na Mtume mpate kurehemewa.وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٣﴾

 

133. Na kimbilieni maghfira kutoka kwa Mola wenu na Pepo upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa Al-Muttaqiyn (wamchao Allaah).الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾

 

134. Ambao wanaotoa katika (hali ya) wasaa na katika (hali ya) shida, na wanaozuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda Al-Muhsiniyn (watendao wema).وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wale ambao wanapofanya faahishah (kila aina ya machafu na dhambi) au wakajidhulumu nafsi zao (kwa kupindukia mipaka); humkumbuka Allaah wakaomba maghfira kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua. أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

 

136. Hao jazaa yao ni maghfira kutoka kwa Mola wao na Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu milele humo (Peponi). Uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema).قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١٣٧﴾

 

137. Kwa hakika zimekwishaptia kabla yenu nyendo (kama zenu), basi tembeeni katika ardhi na mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wakadhibishaji.هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٨﴾

 

138. Hii (Qur-aan) ni ubainisho kwa watu (wote) na ni Hudan (Uongofu) na ni mawaidha kwa Al-Muttaqiyn(wamchao Allaah). وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾

 

139. Na wala msilegee na wala msihuzunike na ilhali nyinyi mko juu mkiwa Waumini (wa kweli). إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ ۚ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاءَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٠﴾

 

140. Inapoguseni majeraha basi yamekwisha wagusa watu (walio dhidi yenu) majeraha kama hayo. Na hizo ni siku (za mabadiliko ya hali) Tunazizungusha zamu baina ya watu na ili Allaah Awatambue waloamini na Afanye miongoni mwenu mashahidi. Na Allaah Hapendi madhalimu.وَلِيُمَحِّصَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ ﴿١٤١﴾

 

141. Na ili Allaah Awatakase walioamini (kutokana na mitihani) na Awafute (Awaangamize) makafiri. أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٢﴾

 

142. Je! Mnadhani kwamba mtaingia Peponi na hali Allaah Hakuwapambanua wale ambao wamepigana Jihaad miongoni mwenu na Akapambanua wenye kusubiri?وَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿١٤٣﴾

 

143. Na kwa yakini mlikuwa mnatamani mauti kabla hamjakutana nayo, basi mmekwishayaona na huku mnayatazama.وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّـهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّـهُ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

 

144. Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi katika ukafiri)? Na atakayegeuka nyuma ya visigino vyake, basi hatomdhuru Allaah kitu chochote. Na Allaah Atawalipa wenye kushukuru. وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٥﴾

 

145. Na haiwi kwa nafsi yeyote kufa isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, imeandikwa muda wake maalumu. Na yeyote anayetaka thawabu za dunia Tutampa katika hizo. Na yeyote anayetaka thawabu za Aakhirah Tutampa katika hizo; na Tutawalipa wanaoshukuru. وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَمَا ضَعُفُوا وَمَا اسْتَكَانُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾

 

146. Na Nabii wangapi (miongoni mwa Manabii) waja watiifu wengi. Basi hawakulegea kwa yaliyowasibu katika njia ya Allaah, wala hawakudhoofika na wala hawakunyong’onyea. Na Allaah Anawapenda wanaosubiri.وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿١٤٧﴾

 

147. Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: “Mola wetu Tughufurie madhambi yetu na upindukiaji mipaka katika mambo yetu, na Ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.” فَآتَاهُمُ اللَّـهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤٨﴾

 

148. Basi Allaah Akawalipa thawabu za dunia na thawabu nzuri za Aakhirah. Na Allaah Anawapenda Al-Muhsiniyn(watendao wema). يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾

 

149. Enyi mlioamini! Mkiwatii wale ambao wamekufuru watakurudisheni juu ya visigino vyenu, kisha mtageuka mkiwa wenye kukhasirika.بَلِ اللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ ﴿١٥٠﴾

 

150. Bali Allaah ndio Mawlaa (Mlinzi, Msaidizi, Mlezi) wenu. Naye ni Khayrun-Naaswiriyn (Mbora wa kunusuru). سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾

 

151. Tutatia katika nyoyo za waliokufuru kizaazaa (khofu) kwa sababu ya kumshirikisha Allaah ambayo Hakuyateremshia mamlaka. Na makazi yao ni moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu.وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ اللَّـهُ وَعْدَهُ إِذْ تَحُسُّونَهُم بِإِذْنِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَعَصَيْتُم مِّن بَعْدِ مَا أَرَاكُم مَّا تُحِبُّونَ ۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۚ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ ۖ وَلَقَدْ عَفَا عَنكُمْ ۗوَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٥٢﴾

152. Na Allaah Amekwisha kusadikishieni Ahadi Yake mlipowaua vikali kwa Idhini Yake; mpaka mliposhindwa na mkazozana katika amri (aliyokupeni Mtume) na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni yale mnayoyapenda. Miongoni mwenu (wako) wenye kutaka dunia, na miongoni mwenu (wako) wenye kutaka Aakhirah. Kisha Akakuepusheni nao (maadui zenu) ili Akujaribuni. Na kwa yakini Amekwisha kusameheni. Na Allaah ni Mwenye fadhila kwa Waumini.إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُونَ عَلَىٰ أَحَدٍ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِي أُخْرَاكُمْ فَأَثَابَكُمْ غَمًّا بِغَمٍّ لِّكَيْلَا تَحْزَنُوا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَا أَصَابَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٥٣﴾

153. (Kumbuka) Pale mlipopanda (mlima na kukimbia) na wala hamgeuki nyuma kumtazama yeyote, na Mtume anakuiteni nyuma yenu, kisha Akakulipeni dhiki juu ya dhiki ili msihuzunike kwa yaliyokupiteni (ngawira za vita) na wala kwa yaliyokusibuni (majeraha na vifo). Na Allaah ni Khabiyr(Mjuzi wa undani na ukina wa mambo) kwa myatendayo.ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

 

154. Kisha Akakuteremshieni baada ya dhiki, amani (utulivu kwa) usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah” Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa”. Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale ambao wameandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi wa yote daima) kwa yaliyomo vifuani.إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا ۖ وَلَقَدْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٥٥﴾

 

155. Hakika wale waliokengeuka miongoni mwenu siku yalipokutana (kwa kupambana) makundi mawili, shaytwaan ndiye aliyewatelezesha kwa baadhi ya yale waliyoyachuma. Na kwa yakini Allaah Aliwasamehe. Hakika Allaah ni Ghafuwrun-Haliym(Mwingi wa Kughufuria – Mpole wa Kuwavumilia waja). يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾

 




Endelea Kusoma Kwa Kugusa Hapa 👈



Report Page