Juzuu
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾
156. Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kwa ndugu zao; waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: “Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa,” ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima).وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Na kama mtauliwa katika njia ya Allaah au mtakufa; bila shaka Maghfira kutoka kwa Allaah na Rahmah ni bora kuliko yale wanayoyakusanya (duniani). وَلَئِن مُّتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى اللَّـهِ تُحْشَرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Na kama mtakufa au mtauliwa; bila shaka kwa Allaah mtakusanywa.فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
159. Basi ni kwa Rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa laini kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelikukimbia. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anawapenda wanaomtegemea. إِن يَنصُرْكُمُ اللَّـهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Akikunusuruni Allaah, basi hakuna wa kukushindeni. Na Akikutelekezeni, basi nani atakunusuruni baada Yake? Na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini. وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾
161. Na haipasi kwa Nabii yeyote (kuwa na kosa la) kukhini (kwa hali yoyote; kutimiza amana, ghanima n.k.); na yeyote atakayekhini atakuja kwa kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa. أَفَمَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَ اللَّـهِ كَمَن بَاءَ بِسَخَطٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٦٢﴾
162. Je aliyefuata radhi za Allaah ni kama aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah?! Na makazi yake ni (moto wa) Jahannam; na ni mahali pabaya mno pa kurejea.هُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٣﴾
163. Wao wana vyeo (mbali mbali) mbele ya Allaah. Na Allaah ni Baswiyr (Mwenye Kuona yote daima) kwa wayatendayo.لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾
164. Kwa yakini Allaah Amewafadhilisha Waumini pale Alipomtuma miongoni mwao Mtume kutokana na nafsi zao; anawasomea Aayah Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah; japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾
165. Ulipokusibuni msiba (siku ya vita vya Uhud) bila shaka mliwasibu mara mbili yake (maadui siku ya vita vya Badr); mlisema: “Umetoka wapi huu?” Sema: “Huo ni kutoka kwenu wenyewe”. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Mweza wa yote daima).وَمَا أَصَابَكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيَعْلَمَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٦٦﴾
166. Na yale yaliyokusibuni siku yalipokutana (kwa kupambana) makundi mawili, basi ni kwa idhini ya Allaah; na ili Awapambanue Waumini (wa kweli). وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ نَافَقُوا ۚ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا قَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوِ ادْفَعُوا ۖقَالُوا لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّاتَّبَعْنَاكُمْ ۗ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَانِ ۚيَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ ﴿١٦٧﴾
167. Na ili Awapambanue wale ambao wamenafiki na kuambiwa: “Njooni mpigane katika njia ya Allaah au (angalau) lindeni” (waambiapo hivyo) Husema: “Lau tungelijua (kuwa kuna) kupigana bila shaka tungelikufuateni”. Wao siku hiyo kwa ukafiri (walikuwa wako) karibu zaidi kuliko iymaan. Wanasema kwa midomo yao, yale yasiyokuwemo katika nyoyo zao. Na Allaah ni A‘lam (Mjuzi zaidi wa yote) wanayoyaficha.الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Wale ambao waliwaambia ndugu zao nao wakakaa (hawakwenda vitani): “Lau wangelitutii basi wasingeliuawa.” Sema: “Basi ziondoleeni (jiepusheni) nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli. وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Na wala usiwadhanie kabisa wale ambao wameuawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Mola wao wanaruzukiwa.فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾
170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa Fadhila Zake na wanawabashiria (wanawashangilia watakaokufa mashahidi) ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.” يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾
171. Wanawabashiria kwa Neema za Allaah na Fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾
172. Wale (Waumini) waliomwitikia Allaah na Mtume baada ya kuwasibu majeraha. Kwa wale waliofanya ihsaan (wema) miongoni mwao na wakawa na taqwa watapa ujira mkuu.الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾
173. Wale ambao waliwaambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan; na wakasema: “Hasbuna-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl (Allaah Anatutosheleza Naye ni Mbora wa kumtegemea) فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗوَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi wakarudi na Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila; halijawagusa ovu lolote; na wakafuata radhi za Allaah. Na Allaah ni Mwenye fadhila kuu. إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٥﴾
175. Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha mawalii (marafiki) zake. Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini (wa kweli).وَلَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ ۚ إِنَّهُمْ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٦﴾
176. Wala wasikuhuzunishe kabisa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale ambao wanakimbilia katika ukafiri. Hakika wao hawamdhuru Allaah kitu chochote. Allaah Anataka Asiwawekee sehemu (fungu) yoyote Aakhirah; na watapa adhabu kuu.إِنَّ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٧﴾
177. Hakika wale ambao wamenunua ukafiri badala ya iymaan, hawatomdhuru kitu chochote Allaah; nao watapata adhabu iumizayo.وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٧٨﴾
178. Na wala wasidhanie kabisa wale ambao wamekufuru kwamba muhula Tunaowapa (wa kustarehe) ni kheri kwa nafsi zao. Hakika Tunawapa muhula ili wazidi (kufanya) dhambi. Nao watapata adhabu ya kudhalilisha. مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَجْتَبِي مِن رُّسُلِهِ مَن يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٩﴾
179. Haiwi kwa Allaah kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka Apambanue khabiyth (mbaya) kutoka kwa twayyib (mwema). Na haiwi kwa Allaah Akujulisheni (mambo ya) ghayb; lakini Allaah Humteua katika Wajumbe Wake Amtakaye (Akamjulisha baadhi ya hayo mambo ya ghayb). Basi mwaminini Allaah na Mitume Wake. Na mkiamini na mkawa na taqwa mtapaa ujira mkuu. وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٨٠﴾
180. Wala wasidhani kabisa wale ambao wanafanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. Na ni Wake Allaah Pekee urithi wa mbingu na ardhi. Na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa undani na ukina wa mambo).
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾
181. Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli wa wale (Mayahudi) ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.” Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: “Onjeni adhabu ya kuungua.”ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿١٨٢﴾
182. Hivyo ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao na kwamba Allaah si dhalimu kabisa kwa waja. الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٨٣﴾
183. (Hao ndio) Wale waliosema: “Hakika Allaah Ametuahidi kwamba tusimwamini Mtume yeyote mpaka atuletee qurbaan (kafara kutoka mbinguni) iliwe na moto. Sema: “Kwa yakini walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja bayana na (hata) kwa yale ambayo mmesema; basi kwa nini mliwaua mkiwa ni wakweli?”فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ ﴿١٨٤﴾
184. Basi wakikukanusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa yakini wamekanushwa Mitume kabla yako. Walikuja kwa hoja bayana na Az-Zubur (vitabu vya waadhi) na Kitabu chenye Nuru. كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾
185. Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na maisha ya dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾
186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu; na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale ambao wamepewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale ambao wameshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni mambo (mazito) ya kuazimia. وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾
187. (Na taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Alipochukua Allaah fungamano la wale ambao wamepewa Kitabu (Allaah Akaawambia): “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.” Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakainunua kwayo thamani ndogo. Basi ubaya ulioje yale wanayoyanunua.لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾
188. Na wala usidhanie kabisa wale ambao wanafurahia kwa waliyopewa na wanapenda washukuriwe (wasifiwe) kwa wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٨٩﴾
189. Ni Wake Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Mweza wa yote daima).إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾
190. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na kukhitilafiana (kubadilika) usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (Ishara, dalili, miujiza, mazingatio, maonyo n.k.) kwa wenye akili.الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾
191. Ambao wanaomdhukuru Allaah kwa kusimama, na kukaa na kwa kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Mola wetu, Hukuumba haya bure. Subhaanak! (Utakaso ni Wako!) Tukinge na adhabu ya Moto.رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾
192. Mola wetu, hakika Umuingizaye motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru.رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾
193. Mola wetu, hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye iymaan kwamba ‘mwaminini Mola wenu’ basi tukaamini. Mola wetu Tughufurie madhambi yetu na Tufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na Al-Abraar(waja wema). رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾
194. Mola wetu na Tupe Uliyotuahidi kupitia Mitume Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah; hakika Wewe Huendi kinyume na miadi (Yako).”فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖبَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾
195. Basi Mola wao Akawaitikia (maombi yao kwa kusema) “Hakika Mimi Sipotezi amali za mtendaji miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale ambao wamehajiri (walohama kwa ajili ya dini) na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika njia Yangu, wakapigana na wakauliwa; bila shaka Nitawafutia makosa yao na bila shaka Nitawaingiza katika Bustani (Peponi) zipitazo mito chini yake; ni thawabu kutoka kwa Allaah. Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa.” لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ ﴿١٩٦﴾
196. Isikudanganye kabisa kutangatanga kwa wale ambao wamekufuru katika nchi.مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٩٧﴾
197. Ni starehe ndogo, kisha makazi yao ni (moto wa) Jahannam. Na ni mahala pabaya mno pa kupumzikia. لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّلْأَبْرَارِ ﴿١٩٨﴾
198. Lakini wale ambao wamemcha Mola wao watapata Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo (Peponi) milele, mapokezi mema kutoka kwa Allaah. Na vilioko kwa Allaah ni bora kabisa kwa ajili ya Al-Abraar (watu wema).وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾
199. Na miongoni mwa Ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswaara), wamo wanaomwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah hawauzi Aayah za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Mola wao. Hakika Allaah ni Sariy’ul-Hisaab (Mwepesi wa kuhesabu).يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾
200. Enyi mlioamini! Subirini na zidini kuvuta subira (washindeni makafiri katika kusubiri), na unganeni na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.سُورَةُ النِّسَاء
An-Nisaa: 4
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾
1. Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah Amekuwa juu yenu Raqiybaa (Mwenye Kuchunga).وَآتُوا الْيَتَامَىٰ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا الْخَبِيثَ بِالطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَهُمْ إِلَىٰ أَمْوَالِكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا ﴿٢﴾
2. Na wapeni mayatima mali zao, na wala msibadilishe khabiytha (kibaya chenu) kwa twayyib(kizuri chao). Na wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika hilo limekuwa ni dhambi kubwa.وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾
3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima; basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne. Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki (masuriya). Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea (kudhulumu). وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا ﴿٤﴾
4. Na wapeni wanawake sadaqa (mahari) zao kwa maridhawa. Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa raha na muruwa.وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٥﴾
5. Wala msiwape masafihi mali zenu ambazo Allaah Amekujaalieni kuwa ni msingi wa kujipatia riziki, na walisheni humo na wavisheni na waambieni maneno mazuri.وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾
6. Na wajaribuni mayatima (uwezo wao wa kufahamu na kusimamia mambo) mpaka wakifikia kuoa (kubalegehe). Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa (kukhofu) kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na (mlezi) aliyekuwa tajiri basi ajizuie (kuchukua ujira kuwahudumia hao mayatima); na aliyekuwa fakiri basi ale kwa ma’aruwf (kadiri ya kukubalika kishari’ah). Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Hasiybaa (Mwenye Kutosheleza).لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿٧﴾
7. Wanaume wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake (pia) wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu, ikiwa ni kidogo au kingi; fungu iliyofaridhishwa. وَإِذَا حَضَرَ الْقِسْمَةَ أُولُو الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينُ فَارْزُقُوهُم مِّنْهُ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٨﴾
8. Na wakati wa kugawa, wakihudhuria jamaa wa karibu na mayatima na masikini, basi wapeni kitu katika hayo na wasemezeni kauli njema.وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّـهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٩﴾
9. Na waogope (hao walezi au wasimamizi kukhini) wale ambao lau (nao) wangeliacha nyuma yao dhuriya dhaifu wangeliwakhofia; basi wamche Allaah na waseme kauli iliyo sawa (ya haki). إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖوَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾
10. Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uwakao. يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾
11. Allaah Anakuusieni katika watoto wenu. Mwanamume apate (atastahiki) mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi wapate (watastahiki) thuluthi mbili za alichoacha (maiti). Na akiwa mwanamke ni mmoja pekee basi apate (atastahiki) nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao apate (atastahiki) sudusi (sehemu ya sita) katika alichoacha (maiti) ikiwa maiti huyo anaye mtoto wa kiume. Na ikiwa hakuwa na mtoto wa kiume na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake apate (atastahiki) thuluthi (sehemu ya tatu). Na ikiwa maiti huyo anao ndugu basi mama yake apate (atastahiki) sudusi (sehemu ya sita); baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au (kulipa) deni (aloliacha). Baba zenu na watoto wenu hamjui ni yupi miongoni mwao aliyekaribu zaidi kwenu kwa manufaa. (Ugawaji huu wa mirathi) Ni shari’ah kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah ni ‘Aliyman-Hakiymaa (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima). وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾
12. Nanyi mpate (mtastahiki) nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mpate (mtastahiki) robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au (kulipa) deni (waloliacha). Nao (wake zenu) wapate (watastahiki) robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi (wake zenu) wapate (watastahiki) thumuni (sehemu ya nane) katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao apate (atastahiki) sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hiyvo basi watashirikiana katika thuluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara. Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah ni ‘Aliymun-Haliym (Mjuzi wa yote daima – Mpole wa kuwavumilia waja). تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٣﴾
13. Hiyo ni mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayemtii Allaah na Mtume Wake Atamuingiza katika Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo (Peponi) milele, na huko ndiko kufuzu kukubwa. وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾
14. Na yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake na akapindukia mipaka Yake Atamuingiza motoni adumu humo milele na atapata adhabu inayodhalilisha. وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖفَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾
15. Na wale ambao wanafanya faahishah (machafu) miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni (mashahidi) wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine).وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾
16. Na wawili wanaofanya haya (faahishah) waadhibuni. Wakitubu na kutengenea basi waacheni. Hakika Allaah ni Tawwabar-Rahiymaa (Mwingi wa kupokea tawbah baada ya tawbah – Mwenye Kurehemu). إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾
17. Hakika tawbah inayopokelewa na Allaah ni ya wale ambao wanafanya uovu kwa ujahili (ujinga) kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah ni ‘Aliyman-Hakiymaa (Mjuzi wa yote daima – Mwenye Hikma wa yote daima). وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾
18. Hawana (haikubaliwi) tawbah wale ambao wanafanya maovu mpaka mauti yanapohudhuria kwa mmoja wao husema: “Hakika mimi sasa nimetubu.” Na wala wale ambao wanakufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo. يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾
19. Enyi mlioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwakirihisha. Na Wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya faahishah (zinaa) bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi huenda ikiwa mnachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye kheri nyingi. وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا ۚ أَتَأْخُذُونَهُ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٢٠﴾
20. Na mkitaka kubadlisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao (zawadi ya) mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote. Je, mnakichukua kwa kusingizia (dhuluma) na dhambi iliyo bayana? وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٢١﴾
21. Na mtachukuaje na hali nyinyi kwa nyinyi mmeingiliana, na (wao wanawake) wakapokea kwenu fungamano thabiti?وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾
22. Na wala msiwaoe (wake) waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni faahishah (uchafu) na chukizo na njia ovu.حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٣﴾
23. Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati (mama wakubwa na wadogo) zenu, na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na ndugu zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishiwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishwa) kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah ni Ghafuwrar-Rahiymaa (Mwingi wa Kughufiria – Mwenye Kurehemu).